Uncategorized

PICHA ZAIDI ZA WOMEN CELEBRATION,NA MIMI NILIKUWEPO.

By  | 
Na mimi nilikuwepo women celebration nilipata nafasi ya kukutana na mashabiki na wasikilizaji wangu wa leo tena.
Da Sarah nilisoma nae O level alinitangulia vidato viwili.
Sare sare maua…..
 Blind tiger walikuwepo kutupa zile cocktail.Shughuli ilikwisha mapema saa moja hivi.Picha hizi nilipiga mwishoni mwishoni.
Picha za Shamim maana tuliambiwa tunyanyue nguo kuonyesha viatu kwenye hilo zulia la kijani.
Asante sana Aunty Faiza wa Beuty Point kwa seti ya acessories kama ninavyoonekana bling bling mpigie kwa namba hii kama utapenda kupata ya kwako 0713276486.Anazo za kila aina na kwa kila rangi kwenda na nguo za aina tofauti tofauti.
 Baada ya shughuli kwisha nikapita nyumbani lounge nikakutana hapo na Profesa Jay.
Gadner G,mimi na Profesa Jay
Mida ya saa tano tano nilitoka hapo kuelekea nyumbani.Hehehehehehe nilitoka kwa style ya NDUMILAKUWILI unamkumbuka wa kwenye gazeti la sani? japo macho yangu yanaonekana maana yeye anafunika macho kabisa.
Ilikuwa event nzuri sana hongera sana Shamim na team kwa ujumla sky is the limit hakuna kinachoshindikana duniani.Ukiwa na ndoto yako iamini na ifanyie kazi.Leo hii wanawake na wasichana wa Tanzania  tumehamasika kushona kanga,vitenge na kuvivaa popote kwa style yoyote kwa sababu ya Shamim Mwasha.
Kupitia blog yake ya 8020fashions kwa muda wa miaka mitatu amekuwa akituonyesha swaga za kiafrika alizozibatiza jina la BACK TO AFRICA na sasa tunashona kwa kwenda mbele.
upo juu dada kanyaga twende!

19 Comments

 1. Anonymous

  March 4, 2013 at 3:38 pm

  VAZI LAKO DINA HALINA MVUTO KBSAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAA. HUTAKIWI KUVAA NGUO ZA KUVUTIKA SN KM IYO BLAUZI UMEKUTOA SN MKONO NA MATITI,SKETI NAYO HAPANA KWAKWELI KM UNA MIAKA 40. VIATU VIZURI ILA HAVIENDI KBSAAAAAAAAA NA NGUO YA NI KWA UJUMLA HUJAVUTIA

  • Anonymous

   March 5, 2013 at 6:49 am

   WEWE NGUO YAKE INAKUHUSU NINI??KAPENDEZA HAJAPENDEZA KWANI WEWE NI JUDGE WA MAONYESHO YA MAVAZI??FANYA YAKO BIBI WEWE,UMBEA TU NAKUKOSOA WATU NDIO UJUALO mxiiiiiiiiii KWENYE SHUGHULI KAENDA NA IMEKWISHA NYIE NDIO WALE MNAENDA KUANGALIA WATU WAMEVAA NINI HOVYOOOOO

 2. Anonymous

  March 4, 2013 at 7:52 pm

  UMEPENDEZA SANA NA RANGI YAKO YA KIBANTU ENDELEA NAYO MIAKA MIA HATA ZIJE LOTION GANI MANY USISUBUTU UKO BABY FACE NA MWAAH . NA UMEPUNGUA VIZURI DIDA .AMA KWELI PENYE NIA PANA NJIA NIMEONA MATOKEO USIACHE MAZOEZ DEAR.
  WANAWAKE WA TZ MKO JUU NA MTAENDELEA KUA JUU MPAKA MWISHO
  FRM SWD

 3. emma kahere

  March 4, 2013 at 10:01 pm

  I like ua dress DINA,hasa ulivyochanganya hyo red ukachanganyia na kitenge.nimependaje sasaaa

 4. Habiba

  March 5, 2013 at 6:47 am

  WATU WENGINE BWANA MNAPENDA KUHARIBU SIKU ZA WENZENU,SASA HAPO DINA HAJAPENDEZA NINI JAMANI,ROHO MBAYA HAIJENGI NA WEWE UTAKUWA MWANAMKE TU MAANA NDO HATUPEANI MASIFA LOLEST!!! DINA UKO JUU SANA MY DEAR NIMEKUPENDAJE? SIO LAZIMA KILA UVAACHO KIMFURAHISHE KILA MTU AS LONG AS ROHO YAKO IMEPENDA WHY NOT!!!!?

 5. Anonymous

  March 5, 2013 at 10:42 am

  Dina I like ur skirt, kama hutajali tupia picha inayoonyesha mshono kwa Ukaribu mbele na nyuma, hongereni mlipendeza warembo……Naisubirije Kitchen Party Gala hapa yaaani……nikimkumbuka Mwl Geturde wa Kenya uwiiiii "Supporting Document"

 6. Anonymous

  March 5, 2013 at 2:54 pm

  Kwanini sisi binadamu tuko hivyo jamani DINA kapendeza sana tuu,tena yuko simple

 7. Anonymous

  March 5, 2013 at 3:27 pm

  ACHENI NAFKI MWAMBIENI M2 AJIFUNZE WE UKIANGALIA HAPO IVO VIATU VINAENDA NA HILO VAZI???KWA UJUMLA NGUO IMEKUWEKA KIMAMA MAMA WE MSICHANA BADO. AND YES UKIEENDA SHUGULINI LAZIMA UANGALIE WENZIO WALIVOVAA ILI KM VP UJIFUNZE KI2 WATU WANAVAA NGUO ZA MADISGNER WAKUBWA NA BADO WANACHEMKA TENA WANAAMBIWA HUAMBIWI KISA UNACHUKIWA WE M2 ELEWA BYTHE WAY KASORO YA NGUO SIO KI2 CHE KUKUKOSESHA USINGIZI AU KUHARIBU SIKU

 8. Anonymous

  March 5, 2013 at 4:30 pm

  NARUDIA DIDA UMEPENDEZA ACHANA NA HUYO HAKUWA NA KIINGILIO HATA FREE CARD HAKUPATA NI URUMA YAKE HUYO. NDO HAO HAO WANAOTUNZA ELFU 10 KTKSHEREHE HATA PAKULALA HANA MWISHO WA SHEREHE WANAOKESHA WANANDUGU TUU KASHUSHUKA ,AMEINGIA NA JEMBE MJINI MWACHE ALIME LAMI HUYO

 9. ruky

  March 5, 2013 at 7:22 pm

  umependeza mumy sana tu………angalu nimepunguza stress kwa mapicha humu ndani maana hali ilikuwa mbaya…..

 10. Anonymous

  March 6, 2013 at 6:40 am

  Tatizo letu hatupendi kuambiana ukweli, unataka umsifie mtu ndivyo sivyo ili afurahi , siku zote anaekupenda ni yule anayekwambia ukweli na sio kukusifia uongo then anakucheka pembeni.

 11. Anonymous

  March 6, 2013 at 7:35 am

  nguo imekupendeza laikini viatu ni 0+0 =O so jitahidi kuchagua viatu vinavyo endana na nguo unayovaa, sawa mammy,

 12. Anonymous

  March 6, 2013 at 8:27 am

  wewe dada sijui kaka unaesema dina ajapendeza,mimi nakuona bonge la mshamba.dina amependeza tesa sana.

 13. Anonymous

  March 6, 2013 at 8:52 am

  NAKUBALIANA na wewe mdau eti nikiambiwa sijapendeza siku imeharibika aaaaah wapi kuna vi2 vya kuharibu siku sio nguo ukizingatia hata shuhuli yenyewe ishapita haya cha kuniumiza nini??????? DINA unanifuraisha coz wewe unajua na unapenda kujifunza. Ndio kuna comment zina umiza sn tena sn ila km unaweza kuzifanyia kazi huwa unazifanyia na km ni za kupuuza unapuuza thats wat i lyk about you. KINGINE hii blog umeitengeneza km sehemu ya kujifunza na ku2funza no place 4 heaters yani humu hakunaga majungu.Aliesema hujapendeza naeza kumuunga mkono somehow ilo vazi sio baya ila halijakutoa wewe km Dina ila halina ubaya wowote na ni kweli limekuweka km kimama sn na si kidada

  • dinamariesblog

   March 6, 2013 at 10:51 am

   Sina tatizo na mtu kunipa mawazo yake na ushauri kwa nia njema.Nisichopenda ni KEJELI,DHARAU ya mtu kujifanya anakuja kunishusha mimi kwa kuninyambua ili yeye ajisikie vizuri au kuja kunishusha ili aondoe stress zake za kimaisha.Napenda ushauri na mengi nayafanyia kazi mkiniambia but sipendi kashfa.Na mimi sio malaika kusema niwe sahihi 100% ukiangalia hizo red carpet za ulaya wanachemka kina Beyonce,Halle Berry,J.LO sembuse mie hahahahahahahaha.
   Na mie wala sijaharibiwa siku maana nishazoea haya so i understand kwakweli.

 14. Anonymous

  March 6, 2013 at 2:45 pm

  UNAONA EEEEEEEH MI NDOMANA NAKUPENDA DINA MAMBO MADOGO MADOGO KM HAYA KWAKO SIYO ISHU NAKUPENDA SN

 15. Anonymous

  March 6, 2013 at 3:07 pm

  Love you D ukweli nguo haijakupendeza ila najua unapenda jifunza.

 16. Anonymous

  March 15, 2013 at 6:30 am

  Safi sana dina umemifurahisha kukubali ushauri lakini co mt akukejeli nakukuletea dharau

 17. Anonymous

  April 3, 2013 at 9:50 am

  wapo wengi dina, wanapenda kujiridhisha nafsi zao kwa kukejeli wenzao,, hahha nimeipenda hiyo wanatoa stress zao kwa kuwavunja moyo wengine, hahhah hawatapona kamweeeeeeee!!

Leave a Reply