Uncategorized

UKUMBI UTAKAOFANYIKA WOMEN IN BALANCE..KPARTY GALA .

By  | 
Mwaka jana ile ya mwisho ya mwezi wa kumi tulifanyia Diamond jubelee VIP hall na ukumbi ulishona sana sana.Kulikuwa na mapungufu kadhaa ambayo sitapenda yajirudie this time.Najua ni mara chache shughuli kukosa upungufu fulani lakini kulirudia kosa ndio kosa zaidi.
Sasa mwaka huu tumepata ukumbi mpya kabisa upo ndani ya jengo la GOLDEN JUBELEE.Hili jengo ni jipya lipo pembeni ya jengo la PPF Tower mjini kabisaaa.
Ukumbi huo unaingiza watu 1000 tu na ndio idadi tunayoitaka siku hiyo.
Service zao ni za kihoteli kabisa na wao ndio wataserve kila kitu.Ukumbi huu uko chini ya JB Belmonte hotel hivyo wao ndio watatoa huduma za chakula.Chakula chetu kitakuwa kwenye hadhi ya starter,main course na desert.
Hivyo tumeona tuadvance ili kukidhi mahitaji yako ya kihuduma,mazungumzo yetu ya siku hiyo na burudani.
Na kwasababu tumeadvance kihuduma na shughuli kwa ujumla  kiingilio chetu this time kitapanda kitakuwa Tsh 40,000/=
Ukumbi una vyoo vingi vipya na visafi na wa hadhi ya kimataifa.Pia najua kina mama ndio waandaaji wa shughuli mbalimbali za kifamilia,marafiki,ukoo mje muone ukumbi huu mpya.Hawa wana kumbi 4 katika jengo hili hili.Unaoingiza watu 1000,600,400 na 150 mkuje muone maana tunapata taabu sana ya kumbi  hasa kama unataka maeneo ya town.
DRESS CODE:Tusisahau dress code yetu ya siku hiyo imekuwa inspired na bendera ya nchi yetu Tanzania.
TAREHE:Kparty gala itakuwa jumamosi ya tarehe 27 april 2013.Kuanzia saa tano asubuhi mpaka kumi na mbili jioni.
 Kwa lolote piga namba hii 0787583132 na 0657442255.
ASANTENI
Dina Marios!

8 Comments

 1. Anonymous

  March 26, 2013 at 11:53 am

  Thank you Dina what about Parking,Hilo eneo lina vibaka sana, mie nafanya kazi katika jengo la PPF TOWER
  Please explain tutapaki wapi?maana hapo ni balaa

 2. Anonymous

  March 27, 2013 at 6:21 am

  Sawa Dina ila nakuomba sana kuhusu mpangilio wa kukaa sio mwenyewe meza ndio mbele tusio na meza nyuma huku tumenunua tiket wa kwanza.

 3. dinamariesblog

  March 27, 2013 at 7:02 am

  UKUMBI UNA PARKING KUBWAAAA ZILE ZA JUU NA PIA KUTAKUWA NA ULINZI WA KUTOSHA!

 4. Mama 2 (Mrs M)

  March 27, 2013 at 2:18 pm

  Asante kwa taarifa nzuri!!!Naanza kujichangisha!!

 5. Anonymous

  April 4, 2013 at 7:35 am

  Wapi tunanunua tickets in advance? Maana hii ni never miss thing!!

 6. Anonymous

  April 4, 2013 at 9:40 am

  TIKETI ZINAPATIKANA WAPIIIII

 7. Mrs L

  April 12, 2013 at 11:56 am

  Dina nani ni mtoa mada mkuu ni yule dada wa kenya wa kipindi kile(Getrude).

 8. Anonymous

  April 12, 2013 at 11:59 am

  Kuhusu mpangilio wa kukaa tunaomba watu wachanganywe sio kama ile ya mara ya mwisho, nikimaanisha sio wale walio nunua meza ndio wakae mbelee tu wachanganywe wengine nyuma, kati, mwisho hata pembezone wasirundikwe mbele tu hii itasaidia kuonekana wanawake wote ni sawa sio wako kitabaka.

Leave a Reply