Uncategorized

WIVU WA KIMAPENZI WAMFANYA MWANAMKE HUYU,KUMUUA MUMEWE!

By  | 

NIGERIA.

Kutoka nchini Nigeria habari zinasema kuwa mwanamke mmoja amuua mumewe kwa sababu za wivu wa kimapenzi.
Mke mwenyewe ambae anashikiliwa na polisi baada ya kukiri kosa hilo alisema aliamua kumuua mumewe baada ya kugundua anataka kuoa mke mwingine.
Jina la mwanamke huyo limehifadhiwa alifanya tukio hilo usiku wa jumatano ya wiki iliyopita nyumbani kwao. Marehemu alikuwa  businessman na  contractor aliyekuwa akifanya kazi na Nigerian Agip Oil Company. 
 Mume alirudi kutoka kazini  na mke kumuandalia chakula mida ya 11:30pm baada ya kula kumbe chakula kilikuwa kimewekwa madawa ya kumlewesha.Wauaji wakulipwa walikuwa ndani wanangoja muda ufike wafanye kazi yao.Baada ya kuleweshwa ikawa rahisi kwao kuja kufanya uuaji huo.
Mmoja wa walioshiriki kumuua huyo bwana alikamatwa na police na baadae kumtaja huyo mama kuwa aliwalipa kufanya hivyo.
Mwanamke huyo alipokamatwa na polisi alikiri kosa  akasema ni kweli kwa sababu mumewe alikuwa anatarajia kuoa mke mwingine tena binti aliyempa ujauzito. 

4 Comments

 1. ELIUD SAMWEL

  March 18, 2013 at 12:32 pm

  Huo wivu sasa umekua hatari sana

 2. Mama 2 (Mrs M)

  March 18, 2013 at 2:29 pm

  Dunia sijui inakwenda wapi jamani! mbona watu wanauwana kama wanyama! huo wivu wa aina gani?

 3. Anonymous

  March 18, 2013 at 4:25 pm

  Tukio kama hili angefanya mwanaume nazan wanawake wangepaza sauti all over the world ila kafanyiwa mwanaume wala halitafumbua vichwa vya watu kna cku hiv vitendo vitaonekana sawa tu mbele ya jamii cos watasema wazoea kutuonea sheria ichukue mkondo wake

 4. emu-three

  March 19, 2013 at 5:44 am

  Wivu ukizidi sana ndio inakuwa hivyooo, !

Leave a Reply