Uncategorized

ASANTENI KWA KUJA KATIKA KITCHEN PARTY GALA JUMAMOSI ILIYOPITA.

By  | 
KWANZA NAANZA KWA KUOMBA RADHI
Najua tulitangaza shughuli kuanza mapema saa tano asubuhi lakini kwa sababu ya matatizo kadhaa ya ukumbi pale ikashindikana.Ukumbi ni mpya na una sheria kadhaa ambazo sie hatukuzijua toka awali.Usiku mpambaji alipokuja kupamba floor ya 5 walinzi walimzuia kupanda hata watu wa muziki walipokuja walizuiwa.Ikabidi tungoje asubuhi kupamba yaani hata kilichopambwa sio kilichopangwa ilibidi tuikimbize ili tuwahi kuingia ili watu mliokuwa mmefika muingie ndani.
Unapoandaa shughuli hakuna mtu anataka vitu viende kombo naandika haya nikijisikia vibaya sana japo siku ile mliniahidi mmenisamehe.
Shughuli ilichelewa kuanza na kuchelewa kuisha wengine ilibidi muondoke maana visa ilikuwa imeshaisha.
Nawashukuru sana wote mliokuja kwa uvumilivu wenu,ucheshi wenu,ushiriki wenu na kwa kupendeza mlipendeza sana.Nilikuwa na crowd nzuri sana siku ile…..kama kuna pendekezo naomba mniandikie kupitia dina_marios@yahoo.com
Kitchen party gala ya wanawake wote kufanyika tena mwezi october
RATIBA YA ZIJAZO
Singles hii kufanyika mwezi wa sita kwa wasichana ambao hawajaolewa na itashirikisha wavulana vijana ambao hawajaoa.

couples reatret hii ni ya wapenzi,wachumba,wanandoa kufanyika mwezi wa tisa nje ya mji.
Mwisho mwezi wa kumi ya wanawake wote.
Asanteni na nawapenda sana.
Dina Marios!

15 Comments

 1. Anonymous

  April 29, 2013 at 7:39 am

  dina , hiyo couples retreat ya mwezi wa tisa tupeane habari mapema na gharama zake tuanze kuzichanga mapema na kuwapa couples wetu taarifa mapema wajibook. itasaidia saana kujipanga as kuna mambo ya kazi maharusi ukiijua mapema, wajipanga mapema. asante

  • dinamariesblog

   April 29, 2013 at 11:03 am

   SAWA TUTAWEKA TANGAZO MAPEMA MWEZI UJAO!MGUSIE GUSIE NA MZEE NA MAALUMU WA WOTE.

 2. emma kahere

  April 29, 2013 at 9:03 am

  Binafsi nli enjoy sana mamii hasa wale SAMAKI walikuwa watam mpaka nkataman nichukue take away.,ila muda ndo ulikuwa tatizo but next tym hope mambo yatakuwa safii.,na ucsahau godoro uwiii

 3. Anonymous

  April 29, 2013 at 9:30 am

  Haabri Dina,
  binafsi nimekusamehe, inaeleweka kawaida katika shughuli mapungufu hayakosekani.
  Nashauri uturushie picha, na kama kuna uwezekano zile products za Bi Getrude naomba zipatikane hapa Tz maana nilipouliza walisema iwapo leo hukujaaliwa basi nilipewa namba ya simu niipige ili niagize toka Nairobi, naona kama haikukaa sawa, waonaje ukawa agent wake tununue toka kwako?
  otherwise event ilikuna bomba, ukiacha dosari ya muda ambayo wengine ilibidi tuwahi kurudi makwetu kuepuka lawama kwa tuliopewa vibali.

  Keep it up lady.

  • dinamariesblog

   April 29, 2013 at 11:25 am

   Naomba niandikie kwa email hivyo vitu unavyovihitaji nione kama naweza kumwambia avitume.Pole sana na asante kwa kuja.

  • Sophia

   April 29, 2013 at 4:38 pm

   Ok Dina,

   Kwakweli sikushika majina japo bei zilinikaa hasa kwa kile nilichopenda, naomba ulizia ile product yenye bei ta Tzs 50,000 nakumbuka Getrude alitolea mfano pale ukumbini namna ya kumsaidia Mr.Victor,kingine ni ile CD nakumbuka ilikua ni Tzs 10,000/=

   Asante Dina

 4. Anonymous

  April 29, 2013 at 10:46 am

  Mbona sikuona red carpet ya kitchen party gala clouds tv kama ulivyotuahidi.

 5. RUKY

  April 29, 2013 at 10:52 am

  JAMANI DINA POLE KWA ILO HIZO ZOTE NI CHANGA POTO ILA KUMBUKA SIKUZOTE UKITAKA KUFANYA KITU KWA NIA NZURI HUWA MUNGU LAZIMA AKULETEE CHANGA MOTO ILI UZIDI KUWA MAKINI NEXT TIME..ILA NAOMBA UTUWEKEE BASI PICHA JAMANI MBONA KILA WAKATI UNACHELEWAGA KUTUWEKEA PICHA?

 6. Anonymous

  April 29, 2013 at 12:43 pm

  kingine dina kadi zilikosewa ziliandikwa 11PM badala ya AM kuna watu walikuja mpk saa moja wakakuta watu ndo wanamalizia ilibidi waondoke na kadi zao,plzz jaribu kuangalia na hl mamii….!

 7. Anonymous

  April 29, 2013 at 1:14 pm

  Arusha lini Dina nacc tunapunjika sana cjaona ukigusia kwa ratiba umetoa ya dar tu. nasubiri picha kwa hamu kubwa

 8. Mama 2 (Mrs M)

  April 29, 2013 at 1:58 pm

  Hiyo ya couple ndo naisubiri kwa hamu! maana na wao ninaimani kuna mambo watajifunza. Pole kwa changamoto Dina, ucjali!! mi ninaimani watu walienjoy!

 9. Anonymous

  April 29, 2013 at 2:10 pm

  msosi pia mami kidogo kuna vyakula vilianza haribika kama salad nafikiri vilitengenezwa mapema . ila amarura aku kwa kwenda mbele lov uuuuuuuu.

 10. Farida Ismail

  April 29, 2013 at 5:58 pm

  Da Dina naomba hiyo kitchen party gala ije mpaka huku Iringa jamani maana tunaishia kuangalia picha tu…

 11. Anonymous

  April 30, 2013 at 7:11 am

  I am so glad umefwata ushauri kuhusiana na kushirikisha wanaume.. sasa kilichobaki ni kuwahimiza na wao pia wje kwa wingi kama mnavyohimiza wanawake.Tuache ile mentality tu ya kila kitu wanawake wanawake na tu move ku recognise role ya wanaume katika mahusiano, mapenzi na tendo la ndoa. Mahusiano ni pande zote pili na hivyo ni muhimu kuhusisha wote. You have just earned my respect hapa,ningekuwa karibu ningekuja kwenye hii ya couples. Good luck with your en devours!!

 12. Anonymous

  April 30, 2013 at 7:44 am

  Jamani Dina Arusha mbona sijaiona kwenye ratiba.. Plz usiache tena na hiyo ya couple kwa Arusha pia plz.

Leave a Reply