Uncategorized

TICKETS ZA WIB KITCHEN PARTY GALA ZIPO VITUONI TAYARI.

By  | 
TICKET ZA WOMEN IN BALANCE KITCHEN PARTY GALA KUPATIKANA VITUO VIFUATAVYO:

Shear illusion mliman city

Cassandra mikocheni kwa nyerere

Cassandra mjini jengo la golden jubilee floor ya kwanza

Born 2 shine Mwenge karibu na tra

Jackys cosmetics Kinondoni

Pata ticket yako mapema.
 MUHIMU:Ukinunua ticket hakikisha umepewa na cha kuvaa mkononi ndio kina kamilisha ticket yako.Ukija siku ya tukio mlangoni uje navyo vyote.
 Tarehe 27 April jumamosi

Kinywaji rasmi ndio hicho Amarula cream.Watu kumi watakaowahi kufika wa mwanzo kila mmoja ataondoka na chupa ya Amarula.Watu 100 wa mwanzo watapata kila mmoja glass ya Amarula cream.

DRESS CODE 

Shukrani kwa
wadhamini wetu!

U MAX MALIPO,COCACOLA,BRILIANT PRINTING,CLOUDS FM,NA KINYWAJI
RASMI CHA AMARULA CREAM
WASEMAJI… 
Getrude Mungai kutoka Nairobi Kenya atatoa somo linaitwa
Me,myself and I.
Mama Victor atakuwepo
Aunty Sadaka mwana saikolojia ya jamii
Na kutakuwa na msemaji mmoja mpya hajawahi kuzungumza kabisa.Lengo ni kumjenga msichana na mwanamke anaejiamini.
Karibuni sana Golden jubilee jumamosi hii kuanzia saa tano asubuhi.

17 Comments

 1. Anonymous

  April 24, 2013 at 2:02 pm

  Nimetoka Casandra Golden Jubilee hakuna tickets!

 2. Anonymous

  April 24, 2013 at 3:15 pm

  wanawake wasiojielewa au hawana ishu majumbani ndo wanaokuja kwanye event km izi. Wengine wanataka tu kujumuika na wanawake wenzao jus to have fun ila eti kusikiliza mnachokizungumza HAKUNA. HEBU ANDAA MAKONGAMANO YA MANA NA SI VITU MBAVYO KILA SIKU HAMNA SOLUTION YAKE.
  WANAWAKE WANGAPI WANAMATATIZO KWENYE NDOA??? MAPENZI HAYANA FORMULA HATA AJE NANI KUKUFUNDA HAISAIDII NA KM VP JIULIZE KWANINI MAKUNGWI WENGI WAMEACHIKA AU HAWAJAOLEWA????POSSIBILITY YA HAO WASEMAJI WAKUU KUWA NA MATATIZO MAJUMBANI KWAO IPO KUBWA TU ILA NDO INABAKI KUWA SIRI YA NDANI.
  DINA UNA AKILI SN HEBU TAFUTA KI2 KINGINE SIO HIKI THISI SHIT IS TOO YESTERDAY. ISHU KM ZA MWANA MAKUKA ZILE NDO MPANGO HUU UPUUZI WAKUJADILI WANAUME UWACHE MAPENZI HAYANAGA MJADALA. ITS OKEY UKIIBANIA COZ ITS 4 U AND NOT WASOMAJI WA BLOG

  • dinamariesblog

   April 25, 2013 at 12:08 pm

   Kama umesikiliza theme ya this time utaelewa.Na kama wanawake wanahisi hiki ni kibaya kwao wao wataaamua kuja au kutokuja.Watu wote tunaowatumia wameolewa hakuna aloachika.Mama Victor yupo ndoani miaka 25,Aunty sadaka yupo kwa miaka 21,Getrude yupo kwenye ndoa kwa miaka 13.
   Naamini wanawake hawa ni watu wazima na wana utashi wa kuamua jema na baya kwao kuja au kutokuja.Hakuna anaefundishwa formula ya mapenzi bali vitu kadhaa vinavyoweza kujenga.Na matatatizo ya ndoa yapo miaka nenda rudi hayajahahi kuisha.Theme ilo pita ilikuwa mwanamke wa mfano kama hili halina maana huo ni mtazamo wako wewe.Hayo makongamano mengine ya maana mbona yapo yanafanyika wakina mama naamini wanayasikia wataenda sio lazima nifanye mimi.Wanawake wanaokuja wanajielewa sana na wanaishu majumbani kwao na wapo tayari kujifunza jipya.Na wewe karibu pia!

  • mama Nasser

   April 26, 2013 at 10:46 am

   I love you Dina umemjibu vizuri sana wewe ni mwananke wa kweli mwenye busara na hekima.tuko pamoja

  • Anonymous

   April 26, 2013 at 3:52 pm

   Dina hachana na huyo asoelewa tunapoelekea. Kwanza umemjibu kwa Hekima ashukuru Mungu.
   Sio lazima yeye aje sisi tunaopenda tutajazana kibao.
   Mungu azidi kukubariki Dina na Makubwa zaidi ya haya utafanya mana nia unayo.
   NAKUPENDA SANA MAMII.
   Hao wanaokuvunja moyo achana nao.

  • Anonymous

   April 26, 2013 at 4:23 pm

   kama nimemuelewa huyo dada hapo juu, nafkiri anachojaribu kusema ni hio pressure kubwa ambayo mmewawekea wanawake kuwa wao ndo wanaotakiwa kuwa hivi au vile. Hata ukiskiliza kipindi chako.. ni kutwa habari za mwanamke usiwe hivi uwe hivi.. mwanamke usafi, sijui mambo ya huyo getrude, uvumilivu, usisema siri zako za ndani etc etc..pamoja na hayo( sikusemi wewe specifically) ila mnasahau kuwa wanaume pia ni upande wa pili wa sarafu na kama ndoa na mahusiano yanatakiwa yawe mazuri basi wote wanatakiwa waelimishwe na kila mtu atoe mchango sawa kwenye mahusiano. Yakwapi makongamano ya wanaume ? ya wana ndoa? kwanini msifanye kitu cha kuwaleta wanandoa pamoja?? ndo maana watu wanasema wekeni tu makongamano ya kuwahamasisha watu especially wanawake wafanye kazi na wajitume, waongeze bidii etc ili kupunguza huu uwazi uliopo kati ya wanawake na wanaume lakini haya makongamano yenu ya kila siku mwanamke mridhishe mumeo chumbani, mwanamke sijui awe mlezi bora etc,hayawasaidii wanaume sababu wao wanaonekana kama hawahusiki. Tafakari na chukua hatua.

  • marc

   April 26, 2013 at 4:39 pm

   yaani kuna watu wengine wana akili ndogo sana tena inabidi utuombe msamaa yaani nakushangaa wewe sijui wa wapi vile yaani unathubutu kusema wanaohudhulia hawana cha kufanya hivi una akili wewe tungekuwa atuna cha kufanya ticket tungelipia na nini,
   basi kwa taharifa yako katika maisha kila siku unatakiwa kujifunza mambo mapya yanakupa changamoto na jinsi gani ya kuhishi na watu kama nyinyi mlio na upeo mdogo,hapo sio kujifunza kuhusu mapenzi tu ni mambo mengi na refreshment pia,ndio maana kwenye hii mada unaambiwa mwanamke jiamini, kujiamini kutakusaidia kujikomboa na kufanya mambo mengi ambayo mwanzo ulikuwa uyawezi kwa kujiamini ndio maana kuna wanawake ni marais wewe na akili zako ndogo unafikili mada ni mapenzi tu kama hujui kitu bora uulize kuliko kukurupuka tu
   dina keep it up

  • Anonymous

   April 26, 2013 at 10:19 pm

   Naungana na Anony April 24, 2013 at 8:15 AM Ngoja kidogo nipoteze muda kukujibu Dina. Ujanja wa mjini nikuweka theme na kuchukua shs 40,000 kwa kila kichwa sio?Shughuli pevu mwerevu atalitambua hilo. lengo sio hawachaachika walete waume zao ndio watupe uzoefu wa kuishi pamoja kama kuna formula ndio utashangaa! Hakuna kujenga chochote ila wote tunahitaji kuelimika ili tutoke kwenye mfumo wa kutumiwa kwa manufaa ya wengine, hili lifanyie kazi wewe nasie tutafuata.Kila mtu ana mtazamo wake lakini tunatakiwa tujumuike pamoja kujenga sio tu mahusiano bali afya,elimu bora,nishati na mengine mengi sana tunahitaji ili kujikomboa na hizi fikra potofu. Watakuja wengi sio wanajielewa wanadhani ndio njia ya kutatua mapungufu yaliyopo majumbani kwao kumbe ni kuongeze.Kujifunza cha kwanza sio kuja kujumuika na nyinyi ila kukaa chini na kutafakari tupo kwenye ndoa kwa lengo lipi?Tumetoka wapi na tunaenda wapi ndio siri ya kujifunza jipa na ndoa zao zitabadilika wakitambua hilo. Huu ujumbue ni wako Dina ujifunze pia sio unajibu comment bila kufikiri. Siku moja utaingia kwenye ndoa utayakuata.

 3. Anonymous

  April 27, 2013 at 4:00 am

  nakubalina na mtoa maoni apo juu bongo kila mtu anatafuta jinsi ya kula hiii nayonibiashara kama kiashara nyingine kinamama kuweni na akili kwanini msitumie hizo pesa kufanya kitu kingine . au kuwachangia wamama wenye shida ni wengi tuu na watoto yatima.

 4. Anonymous

  April 27, 2013 at 8:49 am

  so nice of you dina yaani umemujibu vyema , kweli mungu azidi kukuongoza katika shughuli zako za kila, na we anoy pindi utoapo maoni si lazima ukashifu huwezi sema wanawake watakaoenda hawana ishu majumbani kwao wanayo mengi tena sana tu lakini penye wengi lazima utaondoka na machache ya kujifunza katika safari yetu ya hapa duniani maana naamini hata yule ambaye alikuwa anajiona amekamilika pia si mkamilifu kwa kila jambo. stay blessed anoy

 5. Anonymous

  April 27, 2013 at 2:55 pm

  Thats why I luv u dina u 'r too smart.umemjibu vzur kwa busara n hekima.co vzur kuvunjana moyo ebu tuwe na tabia apriciate n kupongezana na kutiana moyo pale mtu anapofanya jambo zuri kama halijakubariki ama kukupendeza ebu jitahidi ukae kimya basi co lazma Useme

 6. Anonymous

  April 28, 2013 at 4:32 am

  I am in love with dina marios!! Unajua sana kuongea na watu hata ambao wanakuattack! yaan jib ulilotoa ..

 7. Anonymous

  April 29, 2013 at 9:32 am

  da dina ni kweli unajitaidi kukutanisha watu katika event zako,but jaribu kuwa creative kwa maswala mengine ,majanga ni mengi sana kuliko every day and now kuwa na ishu za mapenzi,love ipo now and forever ,but umeshafikilia majanga makubwa kama ubakaji wa watoto,watoto wa mitaani,dis able person,kujikwamua kimaisha ata kwa hao hao wanawake,majority ya wanawake ni poor ata ukimfundisha mapenzi ujamsaidia,embu msaidie ki upande wa kijasiliamali,embu nitafute tutunge kitu kizuri upande wa kutokomeza poverty kwa wanawake, thanks kwa love but naona kama waitaji angalia pande nyingine my dear

  • dinamariesblog

   April 29, 2013 at 11:06 am

   NASHUKURU KWA MAWAZO NAPENDA MAWAZO KAMA HAYA…UNATOA MAWAZO,PENDEKEZO,IDEA NA NINI KIFANYIKE SIO KUKASHIFU WATU…NITAYAFANYIA KAZI,ASANTE SANA!

  • dinamariesblog

   April 29, 2013 at 11:13 am

   Sipendi kuongea sana….ila hatukukutana kumwambia mwanamke awe mnyonge kwa mwanaume bali ajenge kujiamini,kujipenda na kujisimamia mwenyewe needs zake ndio ninachokumbuka.

  • Anonymous

   April 30, 2013 at 12:15 am

   Samahani kwa kukujibu ina maana mwanamke mwenye akili timamu anahitaji kuambiwa ajiamini,kujipenda na kujisimania kwenye mahitaji yake? Tusidanganyane wote wanajua hayo ila kuwezeshwa ndio wanashidwa kutokana na kwamba tunatumika kwa manufaa ya watu wengine. Unayesema ni wewe usiyekuwa na uzoefu utafika wakati wako utayakuta tu maana we si mtoto mdogo ndio utakapokumbuka hii comment.

Leave a Reply