Uncategorized

UPENDO WA MAMA UNAVYOWEZA KUVUKA MIPAKA HATA KUWEKA MAISHA HATARINI KWA AJILI YA MWANAE.

By  | 
Bibi unaemuona pichani amehukumiwa kunyongwa kwa kosa la kusafirisha madawa ya kulevya.Bibi anaitwa Lindsay Sandiford mwenye umri wa miaka 56 raia wa Uingereza alifanya hivyo kwa ajili ya kumuokoa mwanae ambae nae ni drug dealer.
Bibi Lindsay mama wa watoto wawili na mjukuu mmoja alikamatwa katika mji wa Bali Indonesia akitokea Bangkok huku  suitcaseyake kukutwa ina mzigo wa cocaine.Picha unayoiona hapo ndio siku aliyokamatwa.
Alihukumiwa kungonywa kwa kosa hilo mwezi january mwaka huu.Na rufaa yake ilikuwa wazi lakini baadae ikaja kukataliwa na mahakama kuu ya Indonesia ilikuwa ikisikiliza kesi hiyo. Bibi alijitetea kuwa hakupenda kufanya hivyo ila ilimlazimu ili kuokoa maisha ya watoto wake.Anasema aliamua kubeba huo mzigo kwa sababu mtoto wake alikuwa akitishiwa kuuwawa na hao madrug dealer wenzie.
 Human rights organisation walisema lazima kulikuwa na vitisho vilivyompelekea bibi kufanya hivyo.
 Waziri wa mambo ya nje wa Uingereza William Hague ametoa wito kwa  Indonesia wasimnyonge bibi Lindasay Sandiford.

Nchi ya Indonesia ina wafungwa zaidi ya 114 wanaongoja hukumu ya kifo.Raia wengi wakigeni hukamatwa wakisafirisha dawa za kulevya na toka 2008 washanyongwa 10.
Kina mama na huruma kwa watoto,je mama hapo ulipo unaweza kujitoa hata kuweka maisha hatarini kwa ajili ya watoto wako!?

6 Comments

 1. Anonymous

  April 8, 2013 at 1:40 pm

  DINA SJUI NISEMEJE MANA KUNA MAMBO MENGINE NI RAHISI KUYATOLEA MAJIBU HASA KM HAYAJAKUKUTA. MI BINAFSI NI MAMA ILA NISINGEWEZA KUFANYA ALIVOFANYA HUYU MWANAMKE MWENZNGU MI NAJUA POLISI WA ULAYA WAKO MAKINI SN HASA LINAPOKUJA SWALA LA DRUGS NINGEJARIBU KUOMBA USHIRIKIANO NA POLISI ILI KUMSAVE MWANANGU

 2. Suzanne

  April 8, 2013 at 2:54 pm

  Jamani anatia huruma wamsamehe tu hizi shida jamani zitatupeleka pabaya

 3. mama jaseem

  April 9, 2013 at 7:35 am

  mmh jamani inategemea na jambo lenyewe mi siwezi kusema sana kwa huyo mama huwezi jua situation aliyonayo,,ila hata mm kwa kumsevu mwanangu au wanangu naweza kujitoa kwakweli ila sio kwenye jambo zito km alofanya huyo mama,,akili ya ziada huitajika na busara zaidi tunapokutwa na majanga maishani

 4. MOJAONE

  April 9, 2013 at 9:26 am

  Ukishamlea mtoto kwa maadili mema na akakuwa vizuri tu na kuingia ktk mambo kama haya … aaa mie naona umwache tu apambane na jiwe la moto.
  Ona sasa yeye atanyongwa na mwanaye atauliwa.

 5. Anonymous

  April 9, 2013 at 11:55 am

  Haya mambo nikumwomba Mungu atuepushe na haya majaribu ila kwenye ukweli inaumiza sana hasa kwa watoto wamama tumapata maumivu sana.

 6. Anonymous

  April 9, 2013 at 3:33 pm

  watu wanasema .Huyo mama anaongopa na vilevile , she's too loud.

Leave a Reply