Uncategorized

ANGELINA JOLIE AKATWA MATITI YAKE YOTE KWA SABABU YA SARATANI.

By  | 
Kwa wale wapenzi wa movies za hollywood na mashabiki wa Angelina Jolie kuna habari yake nzito.
Angelina Jolie amesema kwamba amekatwa matiti yake yote pamoja na kuondoa mfuko wake wa uzazi.
Kwenye taarifa aliyoandika kwenye gazeti la New
York Times, Bi Jolie amesema alifanyiwa uchunguzi wa celi zake na
kugunduliwa kwamba alikuwa katika hatari kubwa sana ya kupata saratani
ya matiti. Ndipo akaamua kukatwa matiti yake mawili.
Angelina mwenye umri wa miaka 37 na mama na watoto sita, alipoteza mamake mzazi kutokana na maradhi ya saratani ya matiti.

Anasema aliandika taarifa hiyo kuwahakikishia watoto wake kwamba hakuwa kwenye hatari ya kupata saratani tena.

Kulingana na Jolie madaktari walisema kuwa
uwezekano wake kupata Saratani ya matiti ni asilimia 87 huku akiwa na
asilimia 50 uwezo wake wa kuugua Sarati ya mfuko wa uzazi.

”Niliamua kuchukua hatua mwenyewe ili kuzuia uwezekano wowote wa kuugua Saratani hiyo,” alisema Jolie.

Alisema kuwa shughuli hii ilianza mwezi Februari na kukamilika mwishoni mwa mwezi April.

Katika taarifa iliyoandikwa Jolie na yenye
kichwa, ‘Uamuzi wangu wa kimatibabu’,Jolie alieleza kuwa mamake
alipambana na Saratani kwa miaka kumi na kufariki akiwa na umri wa miaka
56.

Alisema kuwa alielewa fika kuwa siku moja
atawahi kuugua Saratani na ndio maana akachukua uamuzi wa kufanyiwa
upasuaji huo mgumu wa wiki tisa ambao ulihitaji kukatwa matiti.

Uwezekano wake wa kuugua saratani sasa umeshuka kutoka 87% hadi 5%.

Alimsifu mumewe Brad Pitt, kwa kumuunga mkono na
kumfariji kwa kila aliyopitia, na kusema kuwa ametulizwa na kuwa wanawe
hawakupata lolote katika matokeo ya uchunguzi wa madaktari tangu
kufanyiwa upasuaji.

“ninahisi kuwa na nguvu kwa uamuzi niliofanya,
na kwa kuwa ninasalia kuwa mwanamke hata baada ya kuondoa viungo
hivyo,” alisema Bi Jolie.

“kwa mwanamke yeyote anayesoma maneno haya, natumai ataweza kujua kuwa wanaweza kufanya uamuzi.”

Muigizaji huyo, ambaye ameshinda tuzo nyingi kwa
uigizaji wake, pia ni mtunzi wa filamu na mjumbe maalum wa Umoja wa
Mataifa anayehusika na harakati za kibinadamu.

Wakati alipokuwa anafanyiwa upasuaji, Bi Jolie
alizuru Jamuhuri ya Kidremokrasia ya Congo pamoja na waziri wa mambo ya
nje wa Uingereza William Hague.

Jolie pia alihudhuria mkutano wa mawaziri wa
mambo ya nchi za kigeni wa G8, kuhamasisha dunia kuhusu dhulma za
kingono katika maeneo yav ita.
 Angelina Jolie pichani na mumewe na watoto.Kama mwanamke tumuombee ashinde vita hiyo ya saratani ya matiti.Lakini hata sisi tuhamasike kupima mara kwa mara ili kujua afya ya matiti kwa upande wetu imekaaje.

17 Comments

 1. Anonymous

  May 14, 2013 at 1:11 pm

  jamani inataka maamuzi, mungu amjalie inasikitisha ila bac akuna jinsi ni katika kuokoa upande mwingine

 2. emma kahere

  May 14, 2013 at 2:48 pm

  Duu Uamuz mgumu sana huu,lakin ndo kansa tena hakuwa najinsi.,hongera kwake nakwasisi 2liobaki tuwe na uzoefu wakupima mala kwa mala 2sisubir mpaka tatizo lizid

 3. Anonymous

  May 14, 2013 at 8:14 pm

  Amefanya uamuzi mzuri na wakijasiri kama mwanamke, hakuna sababu ya kukaa na viungo vyote then ufe! Bora kupunguza then kuishi tunamuhitaji sana kwenye industry akipotea tutaumia! Its me lizzy

 4. Kivugo

  May 15, 2013 at 5:31 am

  M/Mungu amjaalie maisha marefu na kushinda katika mapambano na hilo, pia wanawake wote wahamasike na waende kuchunguza afya katika kupambana na saratani.
  Dada Dina uwe msitari wa mbele katika hilo, na wahamasishe wenzi wako kwa hilo kwani ni muhimu sana kwa afya na mapambano na saratani hiyo.

 5. Kivugo

  May 15, 2013 at 5:49 am

  “I wanted to write this to tell other women that the decision to have a mastectomy was not easy,” Jolie writes. “But it is one I am very happy that I made. My chances of developing breast cancer have dropped from 87 percent to under 5 percent. I can tell my children that they don’t need to fear they will lose me to breast cancer.”
  Jolie, who has six children with fiancé Brad Pitt, writes that her mother, actress Marcheline Bertrand, died at 56 after a long battle with ovarian cancer. That prompted Jolie to pursue genetic testing and discover she carries the BRCA1 gene, with a high likelihood of both breast and ovarian cancer. “I started with the breasts, as my risk of breast cancer is higher than my risk of ovarian cancer, and the surgery is more complex.”
  While acknowledging that the cost of genetic screening is high — as much as $3,000 — Jolie writes that she hopes more women “will be able to get gene tested” and “know that they have strong options.”

  New York Times: My Medical Choice

 6. Anonymous

  May 15, 2013 at 5:59 am

  Kweli hujafa hujaumbika mungu amjalie aweze kuyashinda

 7. Anonymous

  May 15, 2013 at 9:12 am

  kweli hujafa hujaumbika Mungu yupo anatuangalia na anatulinda. tumepata nguvu kupitia yeye jamani.

 8. Anonymous

  May 16, 2013 at 11:49 am

  bora alivyozaa haraka kabla hayajampata hayo matatizo

 9. RUKY

  May 16, 2013 at 4:12 pm

  DINA HEBU JARIBU KUTEMBELEA HOSP YA OCEN ROAD NILIWAHIKWENDA KWA AJILI YA KUMPELEKA MAMA YANGU KWA AJILI YA MIONZI YA NAE ALIKUW ANA KANSA YA MGUU ILA MOA KAMSAIDIA JAPO ALIKATWA MGUU MMOJA NAPIA ALIUGUA KWA MIAKA MINGI ILA BAADA YA KUKATWA MGUU YUPO VIZURI WA AFYA…TUNAMSHUKURU SANA MOLA KWA HILI.. SABABU NILIYOKWAMBIA UJARIBU KWENDA OCEN ROAD PIA JITAHIDI UMPATE NA DR WA KITENO CHA KANSA YA UZAZI MAANA NILIPOKUWA NA MPELEKA MAMA YANGU NILISTAAJABU SANA KUONA KINA MAMA NDIYO WANAONGOZA KWA KANSA YA UZAZI KILASIKU HUWA NAJIULIZA HILI SWALI WHAY? SIPATI JIBU LA HUWAKIKA JAPO MAJIBU MENGI YANAKUWA NI SHARI YA KUTUMIA MADAWA YA KUZUIYA UZAZI HII NDIYO KIDOGO INANIINGIA AKILINI SABABU NI WATU WENGI WANAOTUMIA MADAWA YA UZAZI YOYOTE HATA SINDANO WENGI WAO HUWA AZIWAKUBALI NA WENGINE KUWANENEPESHA BILA MPANGO, WENGINE KUWAKOSESHA SIKU ZAO AMBAYO HIYO KIAFYA NI MBAYA KWANI PERIOD INATAKIWA KUTOKA KWA MWANAMKE KILA MWEZI YANI NI KM UCHAFU FLANI KTK UZAZI..SASA KINACHOCHANGANYA WATU WANAVYOSHAURIWA KUTUMIA UZAZI WA MPANGO C BORA KUTUMIA MIPIRA KULIKO KURIZKI…MI MHH SITHUBUTU KUTUMIA DAWA Y UZAZI WAKATI MIPIRA NDIYO HAINAMADHARA…MAANA ILE PICHA YA MIAKA 6 ILIYOPITA YA HAPO OCEN ROAD BADO INANISUMBUA KABISA KICHWANI KWANGU…..HUU UGONJWA USIKE TU NA TUOMBE MUNGU SANA KWANI KWA SASA KWANCHI ZILIZOENDELEA BADO UNAWASUMBUA KULIKO HIV…

 10. Anonymous

  May 18, 2013 at 7:11 am

  Kiukweli nampa pole sana na hongera kwa maamuzi aliyoyafanya kwani TAHADHARI KABLA YA HATARI AMEIFANYA.Hili ni jambo la faraja sana na linatia moyo,tujifunze kina dada/mama kwani twaweza ongeza siku za kuishi endapo tutakua makini katika tahadhari.

  Ila nina swali na naomba nifanyie utafiti unipe jibu Dina,hawa watoto ni wakwakwe?hua nampenda sana huyu mwanadada na ningefurahi endapo ningeweza kukutana nae siku moja katika maisha yangu,namuona ni mwenye bidii na pia mimi hujifunza toka kwake.

  Tafadhli nisaidie kwa swali langu. e mail yangu ni hatbah.mduma@yahoo.com.

  please dont publish my e-mail adress.

  • dinamariesblog

   May 22, 2013 at 1:20 pm

   oK JOLIE NA MUMEWE WANA WATOTO 6,Shiloh Jolie-Pitt
   Maddox Jolie-Pitt
   Zahara Jolie-Pitt
   Knox Leon Jolie-Pitt
   Pax Thien Jolie-Pitt
   Vivienne Marcheline Jolie-Pitt
   watoto wake wa kuwazaa ni watatu na watatu wengine aliwaasili kutoka nchi zingine.

 11. Anonymous

  May 20, 2013 at 5:49 am

  pole yake mungu yu pamoja nae. naomba kuuliza hao watoto ni wake wa kuwazaa au?

 12. Anonymous

  May 21, 2013 at 7:40 am

  Dina naomba uniulizie kwa walimwengu niko kwenye kipindi kigumu cha maisha ambacho sijawahi kuishi nina mume wa ndoa na watoto wawili. mtoto wa kwanza nilizaa na mwanaume mwingine maisha ya utoto nisema nilivyomaliza form six, baada ya hapo nilienda chuo nikaolewa na huyu kaka ambaye naye ana mtoto mmoja wa kike. kinachotokea ni kwamba kila mwanangu anachokifanya anasema eeh kachukua kwa baba yake miye nakaa kimya ana taka mtoto nimbadilishe jina nimwite jina la ukoo wangu miye, ninavyoondika huu ujumbe kanipiga kisa jina hilo hilo na isitoshe ni mume jina tu mambo ya kanisani nalea watoto wangu mwenyewe nawasomesha hana anachonipa ananitukana kila mara miye mchawi eti namroga hapati kazi ana kama mwaka sasa hana kazi hana shukrani hivi ndoa kama hii nikiondoka walimwengu watanisema vibaya kwasababu mtoto wangu wa kwanza ana baba mwingine nimechoka kupigwa kutukanwa kuonewa. akilewa anasifia wanawake zake wa zamani walikuwa wazuri baadaye anasema ni pombe kweli haya maisha jamani nipeni ushauri nimechoka jamani na hii ndoa bora nijikalie mwenyewe na kazi yangu awe mume wangu.

  • Anonymous

   May 22, 2013 at 12:47 pm

   dia unasubiri nini?..unasubiri akuue kabisa?..washirikishe wasimamizi wako wa ndo na mchungaji ikiwezekana..wakusaidie kutatua tatizo hili na ikishindkana..enda kaish maisha yako..mmaisha ni mafupi kwa nn unyanyasike ivo?

 13. Anonymous

  May 22, 2013 at 2:31 pm

  wataalamu wengine wanasema hakuna na kansa so kwanini atolewa…ilikuwa ni chance..je ni ushauri mzuri?…je ukiwa na hatari ya kansa ya mguu ukatwe mguu?..kuna article moja nimesoma ni kama wanawalaumu daktari wake kuwa angela alikuwa mzima wala hana kansa ila alikuwa na dalili tu…sasa solution ya kuyakata matiti ambayo ni healthy kabisa hayana matatizo ni kama doctors walikuwa waoga sana na wamemshauri kiuoga…anyways nimewakilisha tuu…ila ukiisoma hiyo imeandikwa kitaalamu utajua nini…nadhani hisia zaidi ya mama yake kufariki na kansa ya hivyo zilimpelekea ila yeye hana kansa kabisa na hakuwa nayo..hatari sana!!wao wanashauri sio mfano wa kuigwa alichukua

 14. Anonymous

  May 29, 2013 at 6:18 am

  nikitendo cha kijasiri……sana alichoamua kukifanya.

 15. Anonymous

  June 7, 2013 at 8:58 am

  Ni kitendo cha ujasiri sana inataka moyo Mwenyezi Mungu amsaidie awe na afya njema alee watoto wake..

Leave a Reply