Uncategorized

BAADA YA MLIPUKO WA BOMU JUZI,FBI WATUA ARUSHA!

By  | 
Makachero wa FBI kutoka Marekani wamewasili nchini
Tanzania kusaidia katika upelelezi wa shambulizi la bomu lililotekelezwa
katika kanisa katoliki mjini Arusha siku ya jumapili.


Mwandishi wa BBC Baruan Muhuza akiwa mjini
Arusha anasema makachero hao wa FBI wako Tanzania kusaidiana na Jeshi la
wananchi wa Tanzania na Polisi kutafuta undani wa tukio hili ambalo
limeishtua na kuiweka serikali ya Tanzania katika wakati mgumu.
Baruan Muhuza anaongezea hali inaonekana kuwa ngumu zaidi hasa
kutokana na aina ya matukio ambayo yamekuwa yakitokea katika siku za
hivi karibuni yakihusisha viongozi wa dini ambapo wengi ya wanaodhurika
huwa ni wa imani ya kikristo.


Wakati huo huo wakuu wa serikali wakishirikiana na viongozi wa kidini wameandaa mkutano utakaojumuisha viongozi wapatao 200.


Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Said Meck Sadiq
amewaambia wanahabari kuwa wamelazimika kuandaa mkutano huo wa siku
mbili kufuatia agizo la Rais Jakaya Kikwete.


Mkutano huo utajadili uhusiano bora baina ya wakrito na waislamu.
 Polisi nchini Tanzania inawashikilia watu wa nane kwa
madai ya kuhusika na mlipuko wa siku ya jumapili katika kanisa Katoliki
la Olasit viungani mwa mji wa Arusha.

Miongoni mwa washukiwa ambao wako mikononi mwa polisi ni raia wanne wa Saudi Arabia, na wengine wanne ni raia wa Tanzania.
Habari na bbc swahili.

8 Comments

 1. Mama 2 (Mrs M)

  May 7, 2013 at 1:21 pm

  Afadhali waje kutupa nguvu, maana hali hii inatisha Dinaa! watu tutaogopa hata kwenda makanisani. Sijui tunaelekea wapi!!!

 2. Anonymous

  May 7, 2013 at 3:04 pm

  Tanzania tumefikia mahali pabaya sana tena hali inatisha. watu wataogopa kwenda makanisani na watu wataogopa kwenda misikitini maana jino kwa jino!!! Hali Tanzania kwakweli inatetemesha nchi kabisaa. Rais wa Jamuhuri ya Muungano iwemacho kabisa maana Tanzania ile ya zamani yenye Amani, uhuru na umoja kwishne. eeeh Mungu baba yetu jionyeshe Tanzania.

 3. Anonymous

  May 7, 2013 at 6:39 pm

  Hao fbi wanazingua na serekal ia ki bongo wakat wa mabomu yamelipuka mbagala,meli zinazama,waislam wanapigwa mabomu na police morogoro,mwembechai,matukio kibao ya majanga mbona hawakuja kutoa ushirikiano au kwa kuwa hili lni la vatcan wao na serekali yao na ya kibongo kakvu tu,kama vp `waende wakasaidie syria hal baya pale zai ya watu milion 3 mpaka sasa wameshakufa sio na wengine hawana makazi

 4. Anonymous

  May 8, 2013 at 2:08 pm

  Sijui tumapoelekea ni wapi hali inazidi kuwa mbaya sana tanzania hakuna amani tena

 5. sunday komu

  May 9, 2013 at 4:39 pm

  bora waje kutoa support kuhusu unchunguz

 6. Anonymous

  May 10, 2013 at 8:13 am

  Mimi naona serikali iwe makini waache kufumbia macho mambo yanayotendeka hasa tabia ya Uislam kukashifu Ukristo. Baadhi ya misikiti utakuta CD imewekwa watu wamekusanyika wanasikiliza, Wakristo wanasikia, wamekuwa kimya, je,Wakristo nao wakiweka kukashifu Uislam?? Upele umekuwa kidonda hatimaye kidonda ndugu,sisemi Waislam wanahusika ila kipo kikundi chenye nia ya kuvuruga amani yetu. Baadae haohao watatupa bom Msikitini ili ionekane Wakristo wamejibu mashambulizi, kitakachofuata……………Mungu pisha mbali, ilinde Tanzania.

 7. Anonymous

  May 10, 2013 at 2:54 pm

  ANONYMOU MAY 7 TOFAUTISHA MABOMU YA MBAGALA NA HAYA YA MBAGALA NI MABOMU YALOHIFADHIWA YAMERIPUKA KUTOKANA NA MIGUSANO,JOTO AU UZEMBE HILO LA KANISA NI MTU KARUSHA
  MIE MWISLAMU SIPEND WATU WACHACHE WENYE HELA ZAO KUJA KUWARUBUNI WASOKUA NA MAWAZO YA KULINDA AMANI NA KUTUPIA BOMU KUHARIBU IBADA ZA WATU ,KUTIA UKILEMA ,AU KUUA ,
  WATANZANIA MNAANGALI NCHI ZA WENZETU ZENYE VITA YA KISIASA NA KIDINI?
  MWENYE AKILI TIMAMU HATO THUBUTU KUHARIBU AMANI AKIWA ANAJUA MATOKEO
  WAACHENI WATU WAABUDU WATAKACHO HUKUMU WATAIKUTA MBELE .
  KWANI HATA UAMUE UNATAKA WATU WAISHI VIPI JUA HAISAIDII KILA MTU ANKUFA NA KUZIKWA PEKE YAKE
  TUJIPANGE KUDUMUSHA AMANI

 8. Anonymous

  May 13, 2013 at 7:27 am

  Wandugu, lazima tuwe na uwelewa kidogo kati ya CIA, na FBI, sasa kwa uwelewa wangu FBI mipaka yao ya ku operate ni ndani ya Amerika.Na CIA ndio wana uwezo wa ku operate nje ya America. Kwahio basi makachero waliokuja Tz sio wa FBI, bali ni makachero wa CIA.Tusivutane mashati hapa na kupotoshana!

Leave a Reply