Uncategorized

”DINNER WITH DINA CELEBRATING DINA”

By  | 
Tarehe 28 mwezi March 2013 nilishinda tuzo ya mwanamke wa mwaka kutoka Tanzania women of achivements.
Kwangu mie sio jambo dogo hata kidogo ni kitu kikubwa kutokea katika maisha yangu.Watu wengi walikuwa wakiniuliza tunashangiliaje?party wapi?mie sikutaka hayo yote nilisubiri muda ufike wa kufanya hilo na muda ndio huu.
Tarehe 14th june 2013 itakuwa ijumaa nitafanya “DINA WITH DINNER CELEBRATING DINA”
Ni dinner n dance maalum kusherehekea tuzo hiyo.Pia siku hiyo nitazindua project yangu mpya ambayo nimeidedicate kwa wanafunzi.Muda mwingi nadeal na wawanawake lakini kundi hili nimeliacha nina jambo kubwa sana juu yao.
Sasa basi hapa kwenye blog najua mpo wadau wangu wengi sana ambao ningependa kuwaalika.Lakini sitaweza kualika wote.Nitaalika wadau 10 tu.Na mualiko huo ili uupate unatakiwa kufanyaje?
Niambie blog hii toka uanze kuipitia imekusaidiaje?niambie kwa maelezo uliguswa na nini na kama limebadili maisha yako na mitazamo yako? 
Mimi binafsi kuna lolote nimefanya hapa ambalo limekugusa sana na kubadili kitu kwenye maisha yako?
Maelezo yenye mvuto ndio yatakupa nafasi hii sitachagua jinsia.
Tuma kwa email dina_marios@yahoo.com
Mwisho wa kupokea email ni tarehe 10 june,karibuni sana!!

14 Comments

 1. Anonymous

  May 28, 2013 at 2:18 pm

  jamani mumy leo umenigusa lazima nijitaidi tule wote iyo dinner. irene

 2. Anonymous

  May 28, 2013 at 7:55 pm

  mi imenibadilisha sana hasa jinsi ya kuishi na marafiki zangu chuoni hata nyumbani coz b4 walikuwa wananiumiza kichwa sana yan unaumizwa na marafiki kuliko mpenzi bt nw m focus on ma life hata waseme nn tena bila kugombana na mtu blog yako imenipa ujasiri katika maisha sana ukizingatia nimeshaanguka sana kitu kingine kikubwa ni kwenye kupungua nakumbuka mwanzoni nilikutumia mail kuwa nimeifata diet ilikuwa ni cku 3 tng nianze nilipungua kilo 3 sasa ni wiki ya nne nna kilo 72 kutoka kilo 88 na bado naendelea na diet nataka nifikie kilo 60 kwa sasa nimependeza sana nguo zinanikaa vizuri then najickia vizuri coz b4 moyo ulikuwa unanienda mbio sana,nachoka haraka cwezi kutembea mda mrefu na maumivu ya kifua ila sasa nna mabadiliko sana yan nilikuwa kama mzee wakati ni kijana wa 1990, niliangaika sana b4 sliming tea, mafuta ya ubuyu but nikaambulia kuongezeka kilo tu.Ila kinachoniumiza kichwa ni jinsi ya kumentain after diet

 3. dinamariesblog

  May 29, 2013 at 7:00 am

  Niandikie kwa email my dear dina_marios@yahoo.com

 4. Anonymous

  May 29, 2013 at 9:53 am

  DIET IPI WE ANONY WA MEI 28, 12:55 PM NASI TUIFUATE?

  • Anonymous

   May 29, 2013 at 3:44 pm

   DIET YENYEWE HII HAPA

   JUMATATU MPAKA JUMATANO ASUBUHI:supu ya mboga mboga isiyo na mafuta hata kidogo
   MCHANA:Juice ya matunda upendayo lita 2 hakikisha ni nzito ili iwe ndio kama mlo wako.
   Wakati wote unakunywa maji mengi angalau lita 2 kwa siku yasiwe ya baridi.Unaweza kuwa unatafuna matango na karoti kwa mchana kutwa.
   JIONI:Ikifika saa moja unaweza kunywa chai bila sukari ukatulia kidogo halafu ukanywaJuice yako nyingine nzitooo kama uji hivi.Kumbuka juice usiweke sukari.

   Huuu ni mpangilio ambao utaurudia kwa siku tatu kuanzia jumatatu mpaka jumatano.
   ALHAMISI
   ASUBUHI:SUPU YA SAMAKI
   MCHANA:Juice lita 2 na maji ya kutosha huku ukitafuna matango na karoti.
   JIONI:Samaki wa kuchemsha au kuchoma na salad nyingi.
   IJUMAAA
   ASUBUHI:Supu ya kuku na kiazi kimoja cha kuchemsha
   MCHANA:Juice lita 2,maji, na mboga mboga upendazo bila kusahau matango na karoti.
   JIONI:Kuku choma au wa kuchemsha na ndizi moja ya kuchoma au kuchemsha.Na salad.

   JUMAMOSI.
   ASUBUHI:Supu ya kuku na mkate wa brown
   MCHANA:Samaki wa kuchoma na mboga mboga
   JIONI:Kuku choma nusu,mboga mboga au salad ya kutosha .pia usisahau kunywa maji ya kutosha na matango ila hii sio siku ya juice.

   JUMAPILI.
   Kula chochote unachotaka ila zaingatia visiwe vya sukari wala mafuta mafuta.Maji ni muhimu sana sana kunywa maji mengi.

   Ikifika jumatatu unaanza utaratibu wa kila jumatatu mpaka jumapili kwa mwezi mzima.
   MAZOEZI.
   Kwa siku zote hizi usiache kufanya mazoezi maana yanasaidia unavyopungua mwili unakaa vizuri hauwi manyama yaliyolegea.Ruka kamba hata kidogo,situps kwa ajili ya tumbo.Mengine ntawaekea blog kama hauwezi kwenda gym unaweza kufanya mwenyewe nyumbani.

   PLS usicheat diet yako ntafurahi ukipata matokeo ili nami niwe nilikusaidia au kukutia moyo na wewe upungue.
   Kumbuka mlo wa jioni unaliwa mwisho saa moja pia fuatilia post zangu za nyuma nimekuwa nikitoa tip za kutengeneza juisi za aina mbali mbali.Ni diet ngumu mwanzo lakini ukizoea unapeta tu.
   KILA LA HERI!!

 5. emu-three

  May 29, 2013 at 1:07 pm

  Tupo pamoja mpendwa, hata kama sitafika hapo kwenye chakula cha usiku lakini nakuunga mkono na miguu, na kila kitu!

 6. Anonymous

  May 29, 2013 at 3:39 pm

  Kiu ukweli dada Dina mimi sio Blog yako tu naipenda hata wew mwenyewe nakupenda the way unavyofanya kazi zako, mipangilio ya kazi zako na hata urembo wako naupenda mama. Big-up for you LADY!

 7. Anonymous

  May 29, 2013 at 3:40 pm

  Kiu ukweli dada Dina mimi sio Blog yako tu naipenda hata wew mwenyewe nakupenda the way unavyofanya kazi zako, mipangilio ya kazi zako na hata urembo wako naupenda mama. Big-up for you LADY!

 8. Anonymous

  May 30, 2013 at 7:27 am

  Mboga Za majani lazima uweke mafuta kidogo ili digestion ifanyike kwa urahisi

 9. Anonymous

  May 30, 2013 at 11:29 am

  Maneno mangapi Dina jamani, Weka limit basi, nimefika page 6 sasa, natiririka tu maana DM blog ni balaa!

 10. Ruky

  May 30, 2013 at 11:08 pm

  DINA NIMEFAIDIKA NA MENGI…ILA USHAURI ZIDI KUANGALIA MBELE USIBWETE NIKAMA NISEME SIJUI NINI UNIELEWE..ALL THE BEST..

 11. Anonymous

  May 31, 2013 at 9:11 am

  Dina mimi tokea nianze kuangalia blog yako nimejifunza mambo mawili makubwa,ambayo binafsi nimeshayafanyia kazi:upangiliaji wa furniture za ndani na mapishi. Kwa upande wa furniture,nlivutiwa sana na sebule yako,especially black tv table yako na nakumbuka ulipotuambia kuwa umeinunua GAME mlimani city,na mimi nlienda nkanunua ya kwangu na mpaka leo ninayo. Mapishi nilivutiwa na mengi na mpaka sasa nimeshapika mawili,chicken salad(ile ya hoho za rangi na mahindi mabichi) na sausages za mayai…U are such an insiparation Dina,Be blessed!-Pam

 12. Anonymous

  May 31, 2013 at 10:43 am

  hi Dina hongera sana i think ulitakiwa kuiita Dinner with Dina celebrating Dina! and sio Dina with Dinner celebrating dina au sio! all the best

 13. Anonymous

  June 7, 2013 at 7:53 am

  Dina mi ki ukweli ni mpenzi wa blog yako na ninajifunza mambo mengi sijui niseme lipi,but niniakupongeza kama mwanamke mwenye heshima zako.
  1.we ni star lakini hujalewa u-star na naomba umshukuru alie kulea,maana na familia tunazotoka wakati mwingine zinachangia,coz huwezikutoka familia ya kishenzi ukawa muungwana.
  2.we ni mwanamka shujaaa unaejua kupangilia maisha yako na mambo yako,
  3.nakupongeza maana toka nimeanza kuwa mfuatiliaji wa blog hii sijawahi kuona umeigeuza kuwa uwanja wa kuwasema wengine.
  -kwa sababu hizo NAKUSIHI USIBADIRIKE ACHA WENGINE WAWE PHOTOCOPY BUT WE UWE ORIGINAL.

  blog hii imenifundisha mambo mengi,maana kila siku najifunza mapya,
  ubarikiwe sana DM.

Leave a Reply