Uncategorized

JANA NILIKUTANA NA ALIYEWAHI KUWA HEADMASTER WANGU O LEVEL MR.STEVEN MUSHI.

By  | 
Nilipata simu kutoka kwa mwanae akaniambia mjomba yupo hapa Dar ana hamu ya kukuona na anaondoka kesho kurudi kwake Rombo ambayo ni leo.Nikamwambia basi ntajitahidi kuja kumsalimia hata kama niusiku msisite kunifungulia mlango.Kweli  usiku saa nne niliporudi tu nyumbani nikawasiliana na mwanae akanipa maelekezo ya kufika huko sio mbali na kwangu kumbe nikaenda kumsalimia.
Miaka 11 imepita toka nilipopaliza o level Shauritanga secondary school(shasesco).2002
Mzee Steven Mushi alikuwa ndio headmaster pale kwa miaka mingi baadae tulipomaliza sisi miaka kadhaa mbele nikasikia amestaafu.
Ni headmaster ambae kwa wale waliosoma Shauritanga hawatamsahau.Alikuwa akisifika kwa kucheka na smile hata kama mmemkasirisha.Yaani kwa sababu ya kusmile kwake hutaamini kama fimbo zinakuja.
Nikamkumbusha tukio moja tuligoma kufanya testi ya Maths tukaitwa wote tuliogoma.Tulikuwa wengi lakini alituchapa fimbo 4 kila mmoja.Na baada ya hapo tukaambiwa tuombe msamaha walimu na wanafunzi wote kwa utovu wa nidhamu.Tena sio wote kwa kikundi bali mmoja mmoja unasimama mbele ujieleze.Nimemkumbusha hayo yote wala hakumbuki kabisa anakumbuka matukio mengine.
Alipitia matukio mengi kama mnakumbuka ya shule kuungua na wanafunzi wengi walifariki mwaka 92 na kuzikwa kaburi moja pale pale shule kaburi lipo.Pia mwaka 2002 shule ikaungua tena lakini alikuwa jasiri na mvumilivu katika hiyo mitihani.
Kabla sijaondoka akanikumbusha maneno ya ajabu aliyokuwa akituambia ni muhimu kuyazingatia katika maisha “POLE,SAMAHANI NA ASANTE”
Tarehe 8 june wanafunzi wake wanashirikiana kumuandalia sherehe ya siku yake ya kuzaliwa atakuwa akitimiza miaka kadhaa ya kuzaliwa.

45 Comments

 1. Anonymous

  May 7, 2013 at 11:21 am

  good nadhani alikuwa ni zaidi ya Mwalimu Mungu akupe maisha marefu headmaster wetu Mr.Steve!!

  • dinamariesblog

   May 7, 2013 at 12:47 pm

   Aminaaaaaa!

  • Anonymous

   May 16, 2013 at 8:57 am

   Nimefurahije Dinna yaani umenikumbusha mbali sana kumwona mwalimu STEVE MUSHI yaani alikuwa ni baba kwa kweli kwa jinsi alivyokuwa na upendo kwa wanafunzi wake mimi nimemaliza muda mrefu Shauritanga miaka 23 iliyopita nipo Dar Mnakutana lini na wapi katika kikao hicho cha siku ya kuzaliwa MR.MUSHI nami ningependa kuhudhuria ishu hiyo muhimu sana.jibu mapema mwanangu maana naona siku zilizobaki ni chache.

 2. Anonymous

  May 7, 2013 at 11:37 am

  Umesoma shauritanga ndio maana unaona Mange kimambi mashuhuri.ungesoma kifungilo ungemtoa
  Mange Kwenye hiyo list .Nimekushangaa mnooo

  • dinamariesblog

   May 7, 2013 at 12:47 pm

   Soma maelezo mpaka mwisho usinitolee maneno sio mimi niliowataja hao watu wote ni comments.Kama hukucomment wewe basiii kuna waliocoment na link nimeweka kipi kisichoeleweka hata ningesoma chini ya mwembe am proud of that ni sehemu ya njia nilizopita siwezi kujikana ndio wazazi wangu waliona kwa uwezo wao pananifaa mie kusoma hapo.Na ni sehemu ya Who iam now.Una tatizo na Mange kuwa hapo washambulie waliomtaja coz wote unaowaona hapo walitajwa!

   Pamoja na kuwa kwako unaniona sina maana kisa sijasoma kifungilo kubwa ni kwamba umeingia kwenye blog ya aliyewahi kuwa mwanafunzi wa shauritanga.Asante na karibu tena!

  • Anonymous

   May 7, 2013 at 1:16 pm

   wacha madharau mdau, mimi nimesoma shauritanga na nimemaliza 1996..hapa nilipo ni mama wa familia, ni msomi na ninafanya kazi umoja wa mataifa…im so happy kumuona mwl MUSHI bado ana afya nzuri, nimekumbuka mbali Dina we acha tuu, nimesugua tarazo na kufanya usafi kwny lile kaburi la pamoja la wanafunzi sana..
   kuna mwl wa kiume tulikuwa tunamuita mchafuzi, ulimkutaga Dina?
   looh! kweli mmenikumbusha mbali sana..
   greetings to all my fellow student form 4 ya 1996..
   .

  • dinamariesblog

   May 7, 2013 at 1:46 pm

   hahahahah shikamoo dada hapana sikumkuta ndio lile kaburi lilikuwa ni lazima liwe safi kila wakati dahhh memories!

  • Anonymous

   May 8, 2013 at 5:35 am

   Dear, kama wewe humpendi Mange, kuna watu wanaompenda, kwahiyo usimkashifu Dina kisa chuki zako binafsi na Mange. Dina kashajieleza kuwa ni mapendekezo ya watu, we bado unatoa kashfa zako. Kwani Shauritanga sio shule? Me nimesoma Kifungilo lakini nampenda sana sana Mange, na nina wish sikumoja kukutana nae. Acha kudharau watu kwa wivu wako wa kijinga. Hutaendelea kamwe.

  • Anonymous

   May 11, 2013 at 7:01 am

   Nimesom kifungilo lakn whats the point ya kusoma kifungl au shauritang? Huyo anonymous ni bure kabisa who cares where u studied? Point ni unaleta mchango gani kweny jamii. Km mtu hampendi mange au dina muwe na grounds za kutompenda sio kusikia na kufuata mkumbo. Na yes dina waingie kweny blog hii wakijua umesoma shauritanga. Acheni majigambo i

 3. Anonymous

  May 7, 2013 at 11:38 am

  Shauritanga hiyo Shule nayo

  • Anonymous

   May 7, 2013 at 6:06 pm

   Vidole havilingani! Tafuta kwanza ufalme wa mbinguni. Mengine ndio yatafuata.

  • Anonymous

   May 7, 2013 at 6:15 pm

   Dharau nyingine wala hazifai,kama shauritanga sio shule ni nn sasa ladba kwa mfamo?hv watu hamuwezi kuwa na Hekima ata zaa kujilazimisha/mkoje??????chefuuuuuu

  • Anonymous

   May 24, 2013 at 9:31 am

   kwani tulisoma shule za vodafasta tunakula kwako?hatuvuti pumzi hii unaovuta?hatuna pesa hatuna maisha?taratibu mdau,watu wakisema waaze kuonyesha jinsi wanaoishi na tulinganishe na wewe sijui wa wapi??!!utakimbizwajeeeee utaumbuka hatari hahahahaha tucheke sie

 4. Anonymous

  May 7, 2013 at 1:14 pm

  NYIE WANYAMA MNAOMSHAMBULIA DINA MKOME TENA ACHENI UJINGA HII BLOG NI YAKWAKWE HUPENDI USINGIE HUMU KULETA UBISHANI WAKIUGOMVI YEYE ALISEMA WATU WATAJE WAKAMTAJA MANGE KAMA UNAMCHUKIA AU UNAWIVU NAE HIYO WEWE UJUE KUNA WANAOMPENDA MANGE TENA SAANA NA DINA TUNAKUPENDA SAANA MAANA HUNA UBAGUZI MTU ASOME ASISOME WOTE NIBINADAMU.HAYA WEWE MDAU NAHIYO ELIMU YAKO MBONA HUNA MBELE WALA NYUMA MPYUUUU MIJITU MINGINE BWANA INAPENDA KUWAHARIBIA WATU SIKU NA MUDI,SONGA DINA ACHANA NAO WASIKUMIZE VICHWA KWA WIVU WAO NA CHUKI,

 5. Anonymous

  May 7, 2013 at 3:09 pm

  Nyie mnaosema shauritanga sio shule kumbe ni nini?acheni madharau asiposifia shule yake mnataka asifie shule zenu,mbulula nyie mnakwaza

 6. Anonymous

  May 7, 2013 at 3:59 pm

  mijitu mingine hopeless kweli kama una stress za kuachwa na bwana usiingie kucomment pumbavu who is mange? c limbukeni tu ana nini mpk afananishwe na watu? kuna watu wana maisha mazuri wako kimya. na huyo mjinga mwingine eti shauritanga nayo shule we uliyosoma iko wapi? stop hating u don't like the blog usiingie kutuchafulia hewa pelekeni stress zenu kwingine idiots

 7. Ruky

  May 7, 2013 at 5:53 pm

  Mmh kuna watu wanaroho mbaya mpaka hazijifichi…we mdsu hapo juu karibu tena humu kwa dina japo kimya kimya..

 8. Anonymous

  May 7, 2013 at 8:14 pm

  hapo sasa teacher na nwanafunzi

 9. Cymah Wandelt

  May 7, 2013 at 8:21 pm

  Hongera Dina kukutana na mwalimu wako wa kitambo, ila mpenzi ume ongeza kg tena au macho yangu mama? make na mimi siku za nyuma nimeanza diet ghafla nikapanda lol!

 10. Anonymous

  May 7, 2013 at 10:44 pm

  Kwani kama hamna comment si mnyamaze we unaesema shauritanga nayo shule?we hiyo shule yako ndio shule?au Kifungilo tu ndio shule?acheni dharau na mashauzi hata usome wapi angalia pua yako inatazama wapi hiyo ndio itakua shule yako ya milele washamba na malimbukeni nyie wazazi wenu walisoma wapi?Dinna big up jivunie na ulichonacho inawahuuuu!!!!anae ingia kwa blog yako na kutoa kashfa ana wivu huyo achana nao!!!?

 11. Anonymous

  May 8, 2013 at 4:43 am

  ongera dina usijibu wajinga hao wanavyo endelea kumchukia mange ndio ana zidi kupendwa mwana dam ni mwana dam tuuu lakini wacha mungu aitwe mungu. kwannza umefanya heshima kwenda kumwona na tabia njema good

 12. Anonymous

  May 8, 2013 at 5:09 am

  Jamani mambo ya kukashfiana sio mazuri, Mungu hapendi wapendwa. Duniani hapa sote tunapita kumsemea Dina vibaya kwa sababu ameweka watu ambao hamuwapendi sio vizuri, Dina kakosea nini hapo sasa?
  Mimi binafsi natamani sana kukutana Wema sepetu na wewe Dina sijui nitawaonea wapi. Hata tufahamiane tu kwa salam. Mwee

 13. Anonymous

  May 8, 2013 at 5:40 am

  nakupenda dina acha na watu wanaokusema vibaya hao maisha yamewashinda sie mashabiki wako tupo nyuma yako. luv uuuuuuuuu always

 14. Anonymous

  May 8, 2013 at 6:45 am

  Dina umenikumbusha mbali, mim nilimaliza 2000 yan mzee katutoa mbali maana hamna kumwita mwl mnamutia mzee,, nakumbuka tunakusanywa asembli usiku fimbo nne, nne kila nahuwezi dogde maana anawafahamu wote.. pia j2 manapewa pipi au biscut shule nzima.. ole wako ukutwe napipi sasa.. mim nakumbuka nilishameza pipi nzima kisa nilimwona anakuja,,baadae akacheka tu akaniambia kimbia.. nipo mkoani ila ntachanga maana nilipata sms yamchango..

 15. Anonymous

  May 8, 2013 at 7:05 am

  Wewe unaedharau shauritanga huna maana watu kibao wamesoma pale wanamaisha mazuri na kazi nzuri, pia wengi biashara zao zimesisisma kwasababu ya nidhamu ya kazi.. mr. Steve mungu ampe maisha marefu

 16. Anonymous

  May 8, 2013 at 9:33 am

  mwe hata mimi natamani kukutana na wema sepetu dina na huyo mange nawapenda sana. acheni ujinga shule ni shule wazazi wako walikupeleka kifungilo sawa wengine walienda shaulitanga poa tu yote maisha mwisho wa siku wote tuna vyeti mtu mzima ovyooooooooooooo

 17. Anonymous

  May 8, 2013 at 9:33 am

  NAWAPENDA MANGE WEMA NA DINA MKO JUUUUUU

 18. Anonymous

  May 8, 2013 at 11:00 am

  Big up Dinna,Nami pia Nilisoma Shauritanga nilimaliza Form iv mwaka 1998 na sasa ni mama mwenye familia yangu,Ninafanya kazi UNICEF nawashukuru sana wazazi wangu kwa kuona kuwa shule ile itakuwa ni moja kati ya njia zangu za mafanikio,NAWAPENDA NA MUNGU AWABARIKI SANA WANAFUNZI WENZANGU TULIOSOMA NA WALIO BADO PALE SHULENI SHAURI TANGA<WILAYANI ROMBO MKOANI KLM

  • Anonymous

   May 8, 2013 at 1:14 pm

   pamojaa!!

  • Anonymous

   May 10, 2013 at 1:30 pm

   Kwanza nikushukuru Dina Kwa Posting yako kuhusu kukutana kwetu after 11 years.
   I was very Happy na Namshukuru Mungu sana.
   Nimesoma comments za wadau wa blog yako zimenifurahisha sana.
   Kila mtu amepwewa talenta zake na mwenyezi Mungu. Kuna waliopewa 5, wengine 2 na wengine moja. Tunapaswa kuziheshimu zote.Wenye busara ndio talenta yao waliopewa na mwenyezi Mungu. Hata waropokaji nao tuwaheshimu kwa kuwa ndicho walichopewa. Kwenye blog lazima tuvumiliane na tusameheane. The way you see things sio lazima na mwenzio aone hivyo. The end of the day madhumuni ya blog ni kutufanya tuwe well informed na kutufanya tuwe happy. Nawatakieni jioni njeme.

 19. emma kahere

  May 8, 2013 at 6:10 pm

  Yan katika wanawake ninaowapenda nakuwaona kioo cha maisha yangu ni DINA MARIOS na LADYJAYDE,dina all da best mamiiii wanaosema shauritanga mbaya wao hzo shule nzur walizosoma mbona hawana cha maana walichofanya.

  • Anonymous

   May 24, 2013 at 9:34 am

   namkubali saaaaaaaaaaaaaana LADYJAD sijui kwanini…ingawa sio mdau wa muzki wake ila she is something else of a woman walahi.

   pili,naaza kumkubali uyu dada Dina Marios nitakuja kwenye zile Women Gala zenu siku moja nikusalimu pia na tujuzane maisha kwakweli unaonekana uko na busara saaaaana shosti,pamoja Dina

 20. Anonymous

  May 9, 2013 at 6:22 pm

  Da Dina hongera kukutana na mwalimu wako mwaya kitu kama hicho kizuri sana then huwa kinakumbusha mbali,Pia umependeza blauzi yako nimeipenda sana,naitwa Farida wa Iringa….

 21. Anonymous

  May 9, 2013 at 9:23 pm

  me pia natakakuchangia

 22. Anonymous

  May 10, 2013 at 10:46 am

  Sasa Dina, mbona uneanza tena kunenepa my dear,Azura Vipi Tena?

 23. Anonymous

  May 14, 2013 at 8:37 am

  Wasamahe hawajui wlitendalo, mradi waandike tu na wao.

  • Anonymous

   May 16, 2013 at 1:10 pm

   Kwa kweli anaihitaji kusamehewa watu wengine bwana ili mradi tu na wao wamechangia bila kufikiri wanachangia nini,aliyesema ukisoma shule hizo anazozijua ndo utafanikiwa comment yake haina logic kabisa.potezea Dina

 24. Anonymous

  May 16, 2013 at 8:11 am

  Dina mi pia dada yako nimesoma Shauritanga nimemaliza 1988, nimefurahi kumwona Mwalimu Steve Mushi yaani bado anadai azeeki. Sisi tulikuwa tunamwita HOMA YA JIJI naye akawa anasema MVUA ZA MASIKA ZITAWANYESHEA akimaanisha kuchapa viboko natamani hiyo pati yake ya kuzaliwa nami niwepo katika maandalizi hayo. email yangu ni sophia.ninje@gmail.com

 25. Anonymous

  May 16, 2013 at 4:16 pm

  Hata mimi nimefurahi sana ulipokutana na mwalimu wako ni jambo jemA SANA nami napenda japo cku moja nikutane na mwalimu wangu mkuu nilisoma huko huko Moshi shule inaitwa KIBOHEHE SEC SCHOOL mwalimu wetu mkuu alikuwa anatokea GHANA nilimaliza 1989 alikuwa mcheshi sana yaani kwa ujumla alikuwa na roho ya kitajili,hongera sana dada DINA

 26. Anonymous

  May 17, 2013 at 9:47 pm

  Hivi km shauritaqnga ni shule mbaya? ingetoa mwanamke wa mwaka kiujumla?

 27. Anonymous

  May 21, 2013 at 2:07 pm

  watu tumesoma shule za kata na tuna maendeleo ya ukweli. Wewe uliesoma English medium sijui fm academy tuonyeshe yako tuone..mijitu mengine ovyoooo kakojoe ulale

  • Anonymous

   May 24, 2013 at 9:52 am

   Dina mbona kimya tuandikie basi michango inawasilishwa wapi na kiasi gani ninatamani nami kuhudhuria hiyo sherehe ya siku ya kuzaliwa MR. STEVE MUSHI kwani mi pia nimesoma Shauritanga natamani nionane na waliosoma huko nipo Dar.

  • Anonymous

   May 24, 2013 at 9:56 am

   Huyo alietuma email yake mfahamishe basi kwani naye ana hamu ya kuwa pamoja na nyie wenzake mliosoma huko Shauritanga katika pati ya mwalimu mkuu. Mpe ratiba kupitia email yake ili mkutane anaonekana ana nia ndio maana akaandika email yake.

 28. Anonymous

  May 26, 2013 at 2:24 pm

  miafrika ndo tulivyo dharau nyingii, Dina usife moyo we piga kazi achana na madungayembe ambayo kila kitu mpaka yakosoe, hauna cha kucomment si ukae kimya tu. Mange anaingiaje hapa wakati post inajieleza jamani nina mashaka na upeo wa kufikiri wa baadhi ya wanaocomment humu.

 29. Nas Mwanaharakati

  February 10, 2016 at 8:51 pm

  Hakuna shule niliyofurahi kusoma na kuwa na amnai kama Shauritanga….Naipenda sana…
  Mwalimu Steve tulienda kumuona kwake akiwa tayari kastaafu ila yupo fiti kweli

Leave a Reply