Uncategorized

MAISHA BILA MAMA!

By  | 
Jana ilikuwa siku ya mama duniani kote.Wapo waliosherehekea wakiwa na mama zao wapo waliosherehekea wakiwa na memories za mama zao ambao walishatangulia mbele ya haki kama mimi.Hivi unajua maisha bila mama mzazi yakoje hasa anapofariki ukiwa mdogo sana?
Mama
mzazi ni muhimu sana katika makuzi na malezi ya mtoto,Mama ni mungu wa pili
duniani.Inafahamika kiasi gani connection ya mama na mtoto ilivyo toka
tumboni,kuzaliwa na pindi mama anapomnyonyesha mtoto.Hata katika uchanga mtoto
hujua kabisa nani ni mama yake na nani sio mama yake.

Mtoto
anapokuwa mama ndio mwalimu wa kwanza kwake kumwelekeza lililo baya na
zuri.Ndio maana mtoto akishika kiwembe mama atamwambia usishike
utajikata.Akisogelea moto mama atamuondoa haraka na kumuweka mahali salama hii
ina maanisha kuwa mama ni mlinzi pia wa mtoto.Maisha bila mama mzazi yanakuwaje
hasa kwa mtoto wa kike?

Mimi
mama mzazi alifariki na kuniacha katika umri mdogo miaka 3 mwaka 1988.Mama yangu alifariki akiwa na miaka 27. Katika umri wa miaka mitatu nilikuwa
na uhitaji mkubwa wa uangalizi wa mama.Alituacha mimi na kaka yangu mkubwa
ambae namfatia.Nilikuwa mdogo kiasi kwamba hata wakati wa msiba nilikuwa naona
watu wengi tu wamejaa kwa babu yangu. Muda ulipofika wa kuaga mwili nilienda
nikaaga nikamshika lakini uelewa wangu hakuwa mkubwa kujua nini kilikuwa
kinaendelea.Baada ya hapo katika kukua unasikia tu ndugu wakisema mama yao
alishafariki sasa kwa sababu nina picha 
kichwani za msiba ule ndio nikaanza kujumlisha na kupata majibu kuwa
sina mama tena.

Wakati
mama anafariki hawakuwa na maelewano mazuri na baba hivyo tukawa tunalelewa na
bibi mzaa mama.Na nikasikia kuwa wakati anafariki mama yetu alikataa
tusichukuliwe na baba  ila tulelewe na
babu.Babu yetu ambae pia ni marehemu alikuwa muelewa sana akasema lazima
tuchukuliwe na baba yetu maana sie ni wanae 
hawezi kutung’ang’ania.Muda ulipofika baba yetu akaja kutuchukua na kuja
kuishi na baba hapa Dar akiwa ameoa mke mwingine ambae tulitambulishwa kwake ni
mama yetu.Kuanzia hapo nikaanza kujifunza mambo mengi sana kwa changamoto
nilizopitia.
Nilipita safari yenye milima mabonde ambazo sitamaliza kuzielezea.Sikupata kujisikia kupendwa wala kujihisi ni wathamani lakini  ndani yangu nilikuwa nina kitu kilichokuwa kinaniongoza.Nilishasikiliza sana ule wimbo wa dokta Remmy Ongala mama uko wapi?Kwa miaka mingi nimekuwa naona kuna kitu kimekosekana kwenye maisha yangu.Upendo wa mama unaozungumzwa,ulinzi wake.Natamani angekuwepo ili nifeel uwepo wa mama katika maisha yangu.Sina memory yake yoyote toka aliponiacha nikiwa na miaka mitatu.Nakumbuka vitu vidogo vidogo sana.

Kuna wakati niliamua kublock kichwani kutaka kujua kuhusu mama yangu.Sijawahi kuongea hata na baba yangu kuhusu mama Ila mwaka jana nilipoenda kumsalimia bibi ndio nikamuuliza kuhusu mama yangu.Alifariki lini,alikuwa mtu wa aina gani?alifariki akiwa na umri gani?na mengineyo.
 Kuna athari nyingi sana nazipata kama mtoto wa kike kwa kukosa kulelewa na mama toka mdogo.Kuogopa ndoa na kuanzisha familia nipo kwenye tiba ya hii hofu kwa sasa.
Ukipitia
maisha yangu utagundua lazima uanze kujitegemea mapema.Hakuna
kudeka,kujiendekeza,ni kupambana mwanzo mwisho.Kila alie karibu yangu huwa
wananiona kama mama sababu ya kujitegemea kwangu kimawazo na hata mfumo mzima
wa maisha yangu.Huwa nasikia wakisema aah Dina ni wife material kabisa  anafaa kuolewa alee familia.Hayo ni mawazo
yao lakini mie najiona nipo sawa kwa vile hivi ndivyo nilivyo.Kila siku
natamani mama yangu angekuwepo aone ni jinsi gani nimekuwa mkubwa na
ninajitegemea sasa. NaombaMungu anisamehe kama namkufuru  kwani ndio mapenzi yake.Kuna wakati naelemewa na mambo ya dunia natamani angekuwepo nimshirikishe anishauri.Na utu uzima hu zipo siku ambazo nalia kwa kukosa uwepo wa mama.
Namshukuru baba yangu kwa kutulea kwa kadri alivyoweza yeye.
Mwisho
nasema mama uliyepewa pumzi na mwenyezi mungu ya kulea watoto wako.Wape
upendo,wapiganie,wathamini,walinde,wafundishe,waongoze maana  yupo mama aliyetamani kufanya hivyo kwa wanae
lakini mungu alimwita mapema na kuwaacha wakiwa wadogo.Na kwa wewe mtoto mpende na kumuheshimu mama yako ili upate baraka nyingi na heri hapa duniani.

Ulale
pema peponi mama yangu

Rehema
Shaaban.

178 Comments

 1. Anonymous

  May 13, 2013 at 2:06 pm

  Nimeguswa saana!! polee dinna,

  • Anonymous

   May 16, 2013 at 7:28 am

   Mimi pia mdau, nimeguswa sana. Mungu akupe nguvu na pia akubariki uishi uje kuwa mama bora wa familia. wewe ni role model wangu kabisa.

 2. Anonymous

  May 13, 2013 at 2:13 pm

  A touching story Dina, pole sana for your mum, may her soul R.I.P.

 3. Anonymous

  May 13, 2013 at 2:14 pm

  ooooooh jamani kisa hiki kimenigusa sanaaaa dina pole sanaaaa

 4. Anonymous

  May 13, 2013 at 2:14 pm

  pole Dina maisha yako yanataka kufanana na mapito yangu, ila tofauti ni kwamba my mama yeye alifariki nikiwa form six na alifariki kwenye mikono yangu so hii picha haijawahi toka kichwani mwangu, na naumia zaidi kwa sababu nina mengi ya ku kumbuka kuhusu yeye, kwenye msiba wake one of my shangazi aliniambia bado hujalia mwanangu hapa unapiga kelele tu ipo siku utakayo lia vzuri. Dina kwa kweli we acha tu it has become an endless cry for me kila nnapokumbuka kimoja ktk vingi alivyofanya huwa na lia, sasa ni mke wa mtu na watoto wa wili lkn bado naliona gap, jamani watoto make the most of ur mothers they are irreplaceable. mama wa shebby na fatihia.

 5. Anonymous

  May 13, 2013 at 2:18 pm

  Pole sana Dina..mimi pia nimepitia na ninapitia maisha kama yako.Mama alifariki nikiwa mdogo nikalelewa na mama wa kambo…mama yangu huyu wa kambo alikuwa mkali sana kwangu ninashukuru alinifundisha kazi nyingi nikiwa mdogo maana nilikuwa hata sipati muda wa kucheza na wenzangu..niliyoyapitia ni mengi sana kwa kweli ila kwa kifupi mapito hayo yamenisababishia majeraha makubwa sana KIAFYA..ni makubwa sana Mungu peke yake ndio anajua huu msalaba mzito wa afya mbovu nilionao na ugonjwa wangu huu kwa mujibu wa dokta (Specialist) tena sio daktari mmoja ni kuwa ugonjwa umetokana na STRESS…tangu 1986 hadi 2006 nilipoanza kujitegemea 20yrs of stress oh My God..yaani nahitaji kumuona mtaalamu wa saikologia maana hii hali haitoki nimejitahidi ku take it easy inashindikana..Sina boyfriend,sina shosti hata nikiwa kwenye kundi sinaga story maskini ya Mungu.am 32yrs now.

  • Anonymous

   May 14, 2013 at 12:33 pm

   so sorry my dia.muweke mungu mbele omba imani matumaini na upendo kila ufanyapo ibada ya aina yoyote ile.

  • Anonymous

   May 14, 2013 at 1:17 pm

   Tunafanans me nilihisi niko peke yangu me sina rafiki sina maongezi natamani niwe na marafiki lakini sina na cja kuzungumza sini me pis nilinyanyaswa sana na sangazi yangu nasikia uchungu sana

  • dinamariesblog

   May 15, 2013 at 1:10 pm

   Duuuh poleni sana wapenzi mie nipo tofauti sana na nyie kwani nina marafiki wengi wakubwa kwa wadogo,wakiuke na wakike,kinababa na kina mama.Lazima tufungue mioyo.

  • dinamariesblog

   May 15, 2013 at 1:11 pm

   Niandikie email nipate mawasiliano yako tuone utasaidiwa vipi.Pole dear!

  • joyce Anselimu+

   January 29, 2014 at 8:52 am

   Dada Dina, historia yako imenigusa sn dada yang, my mumy alifariki ndio nimemaliza la 7, ni meangaika kimaisha mpaka bc, kiukwel historia yk imeniumiza cz nimeona unaniongelea mm, jaman wenyewe bahat yakuwa na mama zao mpaka ss watoe hata shukuran kwa Mungu cz akiwa hayupo ndio utaona umuhimu wake, dada Dina hongera pia kwa kupata mwenza wa maisha anayekupenda kwa dhat Mungu afunike uhusiano wenu na malengo mliyopanga yatimie. nakupenda dada yangu my imail ni janselimu@gmail.com naomba ukaribu wako cz nimekuwa mtu wa mawazo hata afya inakuwa shida cz nahisi kuna kitu nimekikosa kwenye maisha yang. asante na mapumziko mema love u much.

  • joyce Anselimu+

   January 29, 2014 at 9:01 am

   Dada Dina, historia yako imenigusa sn dada yang, my mumy alifariki ndio nimemaliza la 7, ni meangaika kimaisha mpaka bc, kiukwel historia yk imeniumiza cz nimeona unaniongelea mm, jaman wenyewe bahat yakuwa na mama zao mpaka ss watoe hata shukuran kwa Mungu cz akiwa hayupo ndio utaona umuhimu wake, dada Dina hongera pia kwa kupata mwenza wa maisha anayekupenda kwa dhat Mungu afunike uhusiano wenu na malengo mliyopanga yatimie. nakupenda dada yangu my imail ni janselimu@gmail.com naomba ukaribu wako cz nimekuwa mtu wa mawazo hata afya inakuwa shida cz nahisi kuna kitu nimekikosa kwenye maisha yang. asante na mapumziko mema love u much.

  • Anonymous

   February 7, 2014 at 11:37 am

   NIMEUMIA NIMEGUSWA SANA NA HII YAKO, MIMI MAMA YANGU YUPO HAI, ILA NIMEPITIA MAGUMU SANA, KWA KIFUPI NILIPOPATA AKILI YA UELEWA NIKIWA DARASA LA PILI NDIPO NILIGUNDUA MAMA YANGU MZAZI HANA UPENDO, TULISHIA MAISHA MAZURI KAMA FAMILIA ILA TRUE LOVE HAIPO, MAMA YANGU NI MTU WA VISASI, MANENO YAKE NI YA LAANA SANA, HAJUI KUSEMA ASANTE, HAJUI KUBARIKI MTOTO, ANADHAMINI MTOTO MWENYE HELA , ANACONTROL SANA MAISHA YA MTOTO HANA HESHIMA KWA WAUME ZETU, NAKUMBUKUKA TUKIWA WADOGO MAREHEMU BABA ALIKUWA ANASEMA SANA SIKU NIKIFA MTAPATA SHIDA SANA , HATUKUWA TUNAELEWA TULIJUA NI KUTOKANA NA HIGH STANDARD YA MAISHA TULIYOKUWA NAYO SASA LABDA AKIFA MAISHA YATABADILIKA NA MAMA HATAWEZA, KUMBE HAKUNA NA NIA HIYO ALIMJUA MKEWE SANA YAANI MAMA, HATA BABA ALIPOKUWA ANAUMWA MAMA HAKUMTUNZA KAMA MAMA HALISI NI UKALI UKALI NA LUGHA ZISIZO NA UPOLE, ALIPOFARIKI MAMA ALITAPANYA MALI ZA BABA IKAWA KAMA NI LAANA HAKUNA ALILOVUNA KWANI HAKUNA KILICHOBAKI, TUMEOLEWA ILA NI KUKALIWA HANA HESHIMA KWA WAKWE WALA WAUME ZETU, HAKUNA JEMA KWAKE, YAAANI NIMEANDIKA HAYA MANA NINAUMIA SANA SANA NIKIONA MTU ANAMKUMBUKA MAMA YAKE KWA WEMA MKUU HIVI……..MIMI KWANGU NASEMA HAKUNA KAMA BABA……………..NINAMWOMBA SANA MUNGU WANANGU WAPATE JOTO LANGU………….NIMELIA SANA BAADA YA KUSOMA HAYA DINA MARIOS …….WENGINE TUNAJITAHIDI KUJENGA BOND YA MAMA ZETU ILA ANAKAA MBALI YEYE PESA MBELE……..NIMEUMIA NINAUMIA SANA JUU YA HILI. NAJUA WENGI HAMTANIELEWA ILA NDIO UKWELI…….

  • Anonymous

   February 27, 2014 at 10:46 am

   Pole sana Da Dinna ila mshukuru mungu kwa yote uliyopitia na unayoendelea kuyapitia, Mungu yu mwema sana kwako mpaka hapo ulipofikia na mafanikio yako japokuwa hauna malezi ya mama lakini uko tofauti sana na wale malezi yote yaani baba na mama , kwa upande wangu me niko tofauti kidogo sina Baba aliniacha katika mazingira magumu sana Da Dina yaani ndo nimemaliza matihani wa darasa la saba naingia form one hivyo nimesoma kwa shida kwani mama angu hakuwa na kazi ya kuweza kulipia ada za shule kiukweli nilikua na akili japo sio sana kivile ila nasikitika sana kwani niliweza kuishia kidato cha nne tu niliapata divission 4 ya 29 kutoka na hali ya kiuchumi kwetu sikuweza hata kusonga mbele niliishia hapo tu na nikaanza kufanya biashara ya genge nikaweza kujisomesha Computere japo ya mitaani sio chuo kabisa kwa sasa ninafanya kazi stationari ya mtu binafsi ila natamani sana ningeendelea na masomo hatimaye na mimi maisha yangu yawe mazuri kiukweli toka moyoni mwangu napenda sana kusoma kutoka na hali ya familia yetu angalau na mimi siku moja nije kuwa ukombozi wa familia yetu ila ndo hivyo tena kwani mpaka sasa nilianza kujitegemea siku nyingi sana kabla hata ya miaka 18 kwa kila kitu. ila da Dina nina historia ndefu ya maisha na nahitaji sana ushauri wako na msaada kwangu nitafarijika sana kama tutawasilia email- yangu ni medanyemo@yahoo.com please nahitaji msaada wako DA dinna

 6. Anonymous

  May 13, 2013 at 2:21 pm

  dina pole sana. i passed the same life ya kuishi na mama wa kambo ikabidi nianze kujitegemea tangu nimemaliza 4m six, chuo nimesoma kwa hela ya Board ya mkopo, from ada hadi matumizi. it was so hard unaona m2 chuo anapewa hela kwao had raha. nashukuru mungu nilimaliza shule na kupata kazi nzuri. mungu ni mkubwa ila tunajifunza maisha mapema sanaa.

 7. Anonymous

  May 13, 2013 at 2:55 pm

  Jamani Dina, dont do this again please, nimelia mwanzo naanza kusoma hii post yako hadi mwisho, hadi mume wangu amenishangaa, very sorry Dina, we love you, take us as your mumy please, kiss kiss.

 8. Grace Munuo

  May 13, 2013 at 2:57 pm

  Alale pema peponi. Kwakweli una ujasiri, kuishi bila mama na umeweza kusimama na kufika hapo hongera sana na kuombea kwa Mungu akupe ujasiri zaidi,nguvu,kuendelea na mafanikio. Na akujalie familia yenye furaha na ikiwa ni mapenzi yake akupe miaka ming uwaone wajukuu wa wajukuu zako. Nimejifunza pia inabidi nimuheshimu sana mama yangu na nimpende isiwepo sababu ya kumfanya aone simpendi simueshimu. Na zaidi kumuombea. *Nakupenda sana da Dina*

 9. Anonymous

  May 13, 2013 at 2:58 pm

  pole sana Dina..hayo yote ni mapenzi ya Mungu. Na pia hatunabudi kumshukuru Mungu kwa kila jambo!

 10. Anonymous

  May 13, 2013 at 3:16 pm

  duu tuko wengi Dina ila mimi kumbukumbu za mama ninazo aliniacha nikiwa na miaka 18 inaniuma mpaka leo kumkosa uwepo wake MUNGU AMLAZE pema ila nashukuru MUNGU kwa kutupa nguvu sisi na baba yetu ambae kiukweli anajitahidi sana kadiri ya uwezo wake kutimiza wajibu wake NIKITAFAKARI maisha bila mzazi mmoja huwa naomba SANA Mungu ampe babangu maisha mamareeefu

 11. Anonymous

  May 13, 2013 at 3:20 pm

  Dina pole mwaya ila mshukuru mungu kw kila jambo.hapo limetokea hilo ili uwe hapo ulipo ssa,labda mama angekuepo bas usingekua dina huyu leo.kaz y mungu haina makosa.
  ubarikiwe

 12. Anonymous

  May 13, 2013 at 3:27 pm

  pole dada dina,tupo wengi sana ambao tumepoteza wazazi wetu hasa mama,mie pia uwa nalia kila siku nikikumbuka ua kuona u pic yake mna mambo mengi yadunia yananelemea nataman angekuwepo ila sina jinc yote namuhachia mungu,nawatamania sana walio na mama.ila yote kheri wacha tumuhachia mungu,RAHA YA MILELE UWAPE EE BWANA NA MWANGA WA MILELE UWAHANGAZIE WAPUMZKE KWA AMANI..NAKUMIC SANA MAMA ANGU NA NAKUPENDA SANA.

 13. Anonymous

  May 13, 2013 at 3:34 pm

  Be blessed Dina. Mungu ni mwema hope ur mama is still taking care of u ndio maana uko hapo ulipo. Mshukuru Mungu kwa kila alichokupa leo. Muombe akupe hekima zaidi.

 14. Anonymous

  May 13, 2013 at 3:46 pm

  Nimelianimefikirimengi sana mimi ni mama wa watoto watutu mama yangu yuko hai lakini umri kuanzia 13 nimeishi na watu bila mama wala baba ule utofauti wa kutokua na wazazi muda wote naufaham nawazaga je wale waliofiwa inakuaje nimeadhirika sana watoto wangu hata likizo kwa mtu sitaki naona hofu nimeathirika mno mwenyezimungi awape nguvu wote waliopoteza wazazi wao.

 15. Anonymous

  May 13, 2013 at 3:57 pm

  jmn pole sn mum…nimipango ya Mungu

 16. marc

  May 13, 2013 at 4:06 pm

  pole dina kwa kuondokewa na mama yako yaani nimepata feeling za uchungu sana kwani mama ni kitu cha pekee hapa dunia upendo wa mama ni watofauti sana kulinganisha na upendo wa mtu mwingine kuna mtu unaweza ishi naye ukiwa mdogo akakupenda lakini hawezi kumfikia mama ,
  mimi ni mama naona kwa wanangu ni wakubwa wa miaka 14 na 12 lakini wakisema leo hatusikii njaa tumeshiba yaani najisikia vibaya nafanya kuwabembeleza wale ata kidogo ndio walale hapo napata faraja wakiwa wamerudi shule hawana furaha na mimi automatic nakosa amani mpaka nauliza nini kimetokea kama mmoja wapo kuna mtu kampiga au kamuonea namfariji namkumbatia mpaka anakuwa happy yaani kuna direct feeling kwa mama anapata kutoka kwa mwanae nakumbuka nikirudi kazini nimewekewa chakula nataka kula wanangu wakitaka kula na mimi ata kama walisha kula yaani najisikia niwaachie wao wale mimi ata nisile nakuwa happy tu bora wao yaani kuna mengi sana ndio maana nimekuonea huruma sana dina mpenzi kuukosa upendo wa mama lakini Mungu ni mwema amekutia nguvu hadi leo upo very strong Mungu ata kusaidia utakuja pata mume bora na watoto wazuri utawapa upendo ulioukosa wewe na furaa ya ajabu ndani ya maisha yako kwani watotot ndio watakuwa mama na baba yako .

 17. Anonymous

  May 13, 2013 at 4:25 pm

  Pole Dina nimependa ulivyotupa story ya mama nikweli amekuacha mdogo alafu ukawa mkubwa hukawa humuoni kweli inauma sana. Lakini inabidi tukubali nakumwombe kwa mungu. Mm naamin kiroho huko naye dina. Mm ninarafiki yangu mama yake alikufa kwenye ile meli ya MV naalimwacha mdogo sana yani mpaka leo akikumbuka hana mama analia sana. So dina endelea kumwezi nakumwombe sala. TUMSIFU YESU KRISTO.

 18. Anonymous

  May 13, 2013 at 4:47 pm

  dah umechoma moyo wangu,pole Dina

 19. Anonymous

  May 13, 2013 at 4:57 pm

  Pole Dina, story yako imenisikitisha, inataka kufanana kidogo yangu ila mimi mama yangu hakufa nikiwa mdogo, lakini huwezi amini sikupata malezi yake, aliachana na baba yangu nikiwa na miaka minne na mdogo wangu ana miaka miwili, akakataliwa kutuchukua tukalelewa na mama wa kambo, hatukuwa tukipewa nafasi ya kwenda kumuona mama, tulienda kwa kujiiba, kutoroka shule na vitu kama hivyo, nimepitia milima na mabonde kwa mama wa kambo,

 20. rosie

  May 13, 2013 at 4:57 pm

  Da Dina hii post imeniliza mpk kichwa kinaniuma!mm mama yng yupo na nimeishi nae kwa kpnd tng niko mdg mpk nimemaliza primary nimekuja Dar kusoma Secondary na kujiendeleza kdg,ila nlfkia kwa baba yng mdg kutokana na tabia za baba yng mzazi,ni muda ss mama yng kahamia Dar na anaishi na wdg zng lkn naweza kukaa ht mwezi bila kwenda kumuona japo cyo mbali!kila nikienda kumuona najikuta nalia na hasa nikiwaona wadogo zng na kfkria mm ndie nilie mkubwa najckia vibaya sn…natamani sn ningempata mtu wa kunifanyia canceling au mtu km ww Da'Dina japo nikuelezee tu unickilize labda utkw na chcht cha kunishauri!naogopa kuwaelezea marfk zng kwa sbb wanawafahamu wazazi wng watawadharau….nataka nimuelezee mtu wa mbali kbs

  • dinamariesblog

   May 15, 2013 at 1:17 pm

   Polee my dear,niandikie email ili tuwasilianae nione nakusaidiaje.

 21. Anonymous

  May 13, 2013 at 4:59 pm

  Basi mwaka 2008 nikaolewa hapo ndio nikapata muda wa kuwa na mama yangu nilipojifungua Septemba 2009, nikamchukua mama yangu nikae nae angalau nienjoy mapenzi ya mama kwa mara ya kwanza, huwezi amini Desemba alifariki kwa kuumwa kichwa tu. inaniuma sana dada hadi leo namtizama mama yangu wa kambo simmalizi, acha tu

 22. Anonymous

  May 13, 2013 at 5:31 pm

  Mweh kwakweli its soo touching, ila ni mapenzi ya Mungu hakuna cha kufanya.Kwakweli mama ni mtu muhimu sana kwa maisha ya wanae,na kila inapoitwa leo namuomba Mungu anipe maisha marefu nipate kulea wanangu na kuona wanakuwa watu wazima,mimi ni mkubwa kuliko wewe Dina but i rely on my mum soo much in many ways. Niko nae mbali lkn nikizidiwa huwa narudi kuwa mtoto kwa mama. I oveher so much,she'smy first best friend. we talk a lt,we encourage one another. y dad passes 5 years ago. Ilikuwa ngumu sana kwangu lkn kuna rafiki yangu mmoja akaniambia shukuru unae mama.

 23. Anonymous

  May 13, 2013 at 5:46 pm

  pole sana dada dina,nimekumbuka mbali sana.hata mm inafanana na wewe ila mimi mama yangu alifariki nikiwa darasa la 3,nimelelewa na kaka na ndiye alienisomesha mpaka chuo kikuu.kwangu mm kaka yangu ndio kama mama na baba yangu.mungu ambaliki kaka yangu.ni mm salum slim

 24. Anonymous

  May 13, 2013 at 5:53 pm

  Dah…very very sad to be honest sister Dina ujumbe wako umenitoa machozi japo mimi wazazi wangu wote wawili wapo hai japo babangu ckubahatika kuishi nae yeye ana familia yake nyingine pole sana sister wangu just a party of life…Love you so much Sister Dina I wish to meet with you me nipo Iringa.

 25. Anonymous

  May 13, 2013 at 5:54 pm

  Dina dada yng, pole kwa yte ni stori ya kuumiza sana me pia natamani kulia kwa hayo uliyo pitia pia yatupasa kumshukuru Mungu kwa kila jambo. Me nakutakia mafanikio mema na yenye heri ni kuzidi kumuombea mama huko aliko lala alale kwa amani na pia asante kwa ushauri au ujumbe wko kwetu ni mzuri sna na unamaana kubwasna binafsi nitafanya kama ulivyo tuagiza. Mungu azidi kukupa nguvu na mafanikio mema.

 26. Anonymous

  May 13, 2013 at 6:28 pm

  jaman umefanana sana na mama dinaaa. POLE maeee

 27. Anonymous

  May 13, 2013 at 6:29 pm

  mungu akusaidie dina.nimeumia sana juu yako

 28. Anonymous

  May 13, 2013 at 6:38 pm

  oohh Dina toka nimeanza kuangalia hii blog yako sija wahi hata siku 1 kujaribu comment ila leo umenitoa machozi; pole sana kwa yote yalio kufika, tumshukuru mungu tu, hata mimi mama yangu ameniacha nikiwa na miaka 20; kwa sasa na 36; ila ninatamani angeona wajukuu zake; kuna kipindi huwa pia nakufuru Mungu kwa kumchukuwa mapena mama yangu kipenzi;ila amini nikwambiavyo siku ukipata mtoto huo upweke ulio nao kuhusu mama yako utapungua kwa 80%; mimi nimebahatika kupata watoto 2 wa kiume 5jr na wakike 1,5 jr; my dear Dina pata mtoto hata kama sio wa ndoa, maana kama ndoa haiji ujuwi mungu amekupangia nini maishani mwako; watoto watakupa faraja ilioje ambayo hujawahi kuipata; mama yangu alinilea kwa mapenzi mazito sana tupo 5; ila alikuwa na maisha mangumu sana baba yetu alimtelekeza akamwacha na watoto,alikuwa hajuwi,kulima lakini alianza kulima miogo basi akawa anachemsha ana uza shule mungu mkubwa baada ya 3 to 5 jr amini mama yetu alikuwa ni mama maharufu pale kwetu ubungu kila mtu alikuwa ana mjuwa kutokana na biashara zake zilivyokuwa kubwa akajenga nyumba yake na kununua magari yake; alituonyesha utajiri sio lazima uwe na mamilion au upewe na mwanaume; pia tumejifunza kujitegemea wenyewe:
  amefariki bado hakuna hta mtoto wake 1 ambaye amepata mtoto yaani hakuona wajukuu;
  kwa sasa hivi mimi nipo holland , dadangu yupo london kakangu yupo brussel; na wengine 2 wato bongo; namaanisha hajala matunda ya wanae alio kuwa ana uza nao miogo ya kuchemsha na vikaranga;
  NAKUOMBA usiogope kuwa na family
  tena ukiendelea kukaa ndio utajuta baadae huu muda unao upoteza
  wako katika blog mama karim na Khadija

  • dinamariesblog

   May 15, 2013 at 1:23 pm

   Asante mama Karim nimeuelewa ujumbe wako na nitaufanyia kazi.Mungu akubariki sana wewe na familia yako.

 29. Anonymous

  May 13, 2013 at 6:42 pm

  pole sana dina historia yako inkaribiana na yangu maisha bila mama ni magumu mno una face changamoto nyingi sana kulelewa na mama tofauti machozi yananitoka nikimkumbuka mm she left me once i was too young bado napita katika changamoto kubwa mno ila naamini Mungu atnivusha.Mungu umrehemu huko aliko

 30. Anonymous

  May 13, 2013 at 6:48 pm

  dina umenifanya nilie mpenzi, nakupenda sana dia.

 31. Anonymous

  May 13, 2013 at 7:05 pm

  ulichoandika nakielewa sana kwani nimepitia most of it,na nimekuwa na fear kama yako,ctaman ndoa kwani nina watu wengi wanaoniangalia kwa msaada kwan mm ni kama mama wa familia sasa,i hope i heal too

 32. Anonymous

  May 13, 2013 at 7:17 pm

  Dina mama, we acha tu……..Nami pia sina mama ila mie nilipoteza mama nilipofika umri wa miaka 30! Uchungu nilionao mpaka leo siwezi kuueleza katika lugha yoyote! Maana mimi nime experience upendo na utamu wa mama haswaaaa. Uchungu wangu ni kwamnba Mama aliondoka wakati mwanae ndio nimeanza kupata ka uwezo kidogo……Ni wakati ambapo Mama angeanza kula matunda yake kutoka kwangu. Ndio hivyo kazi ya mungu haina makosa…..!!???
  Natoa pongezi kwa kila Mama Duniani!

  ELMMY

 33. Anonymous

  May 13, 2013 at 9:16 pm

  maneno yako yamenitoa machozi, mimi pia namekosa malezi ya mama naumia sana rafiki zangu wakiongelea juu ya mama zao. Nimeolewa kwa sasa ila kuna kipindi natamani mama angekuwepo japo nimueleze yanayonisibu. Kulelewa na mama wa kambo kunahitaji moyo sana, lakini ukimgeukia mungu manyanyaso yote huwa na mwisho wake, na unaweza ukaja kuwa msaada mkubwa kwa huyo mama aliekulea na akaona thamani yako. Nawashauri watoto wanaolelewa na mama wa kufikia wawaheshimu tu hao kinamama kwani itafika siku na wao watakuwa na maisha yao. Na wala wasiwalipizie kisasi ila wawasaidie kama mama zao wazazi. NAUMIA SANA KUMPOTEZA MAMA YANGU MZAZI, japo angekuwepo afaidi matunda ya mwanae. NANI KAMA MAMA? HAKUNA NA HATATOKEA

 34. Anonymous

  May 13, 2013 at 9:22 pm

  Pole sana my dear! Asikwambie mtu upendo wa mama hakuna katika dunia hii! Me nikikaa nikifikiria hivi mama yangu leo hii akiiacha dunia hutokwa na machozi na ndio nimeishakuwa na familia yangu! Ila umuhim,ushauri wake bado navihitaji san! Mungu amlaze pema peponi bi Rehema Shabani! Wa jina lala mama yangu ameeeen. Asiha Ilala

 35. Anonymous

  May 14, 2013 at 1:32 am

  niko nje ya nchi kwa sasa lakini huwa napenda sana hii blog dada dina kila siku lazima nipitie yaani nimesoma hii habari ya dina kuhusu mamayake yaani imenitouch vibaya sana sijui hata nielezaje nilivyojisikia yaani natamaini nirudi nikakaae na wanangu niliwaacha sikunyingi kwasababu ya kuwatafutia maisha mimi ni mwanamke hii habari imenihuzunisha sana pole dada dina jipe moyo Mungu ni mwema nanimkubwa sana mshukuru kwakila jambo hizo changamoto ulizo pitia ndiyo zimekujenga na kuwa imara na kuwa na akili ya kuweza kuishi vizuri na watu wewe ni mfano mzuri sana wa kuigwa hakika dada dina usihuzunike sana wala usikate tamaa yuko mama na baba wa yatima ambaye ndiye Muumba wetu aliye juu ya yote yeye atakufuta machozi utakapoli na kukufariji unapokata tamaa usijali hauko peke yako mwenye hali hiyo wako wengi pole sana huyu Mungu aliyewkufikisha hapa ndiye atakuongoza na kukuonyesha njia iliyo sahihi utapata wako wakukujali na kukupenda kwa dhati nakuziba hilo pengo la mama ambae atakuwa mume wako ubarikiwe dada kumbe ulikuwa na siri kubwa sana moyoni

 36. Anonymous

  May 14, 2013 at 3:50 am

  Pole saana dina najua vp unajickia ila kazi ya mungu haina makosa ndugu yangu, 7bu mimi ni mama pia namshukuru mungu mama yangu yupo hai na nampenda saana mama yangu na yeye anatupenda sote mwenyezi mungu ampe umri mrefu. Amiin ….. CNA CHA KUKULIPA MAMA MALIPO YAKO KWA MUNGU MAMA . NAKUPENDA SAANA MAMA. FATMA ALLY.

 37. Anonymous

  May 14, 2013 at 4:18 am

  what a sad story pole sana dada yaani nakuelewa na umenipa changamoto ya kuzidi kupenda wanangu na kuwafanyia kila niwezalo. mungu amekupa kipaji kikubwa sana Dina keep it up utafanikiwa zaidi, by the way anzisha kipindi cha mama ni wazo tu natoa. mungu akubariki in everything u do.

 38. Anonymous

  May 14, 2013 at 4:50 am

  So touching Dina..pole mdg wangu

 39. Anonymous

  May 14, 2013 at 4:57 am

  too touching Dina may God keep on guiding your ways……

 40. Anonymous

  May 14, 2013 at 5:01 am

  Pole sana Dina Mungu akutie nguvu na wala usikate tamaa katika jambo lolote lile maana Mungu anamakusudi kukufikisha hapo ulipo mamy, workhard ma dia tafuta kwabidii utafanikiwa.
  usiogope kuface familia japo kunachangamoto lakini Mungu ndie kila kitu hakuna aliwahi kumuomba na akashindwa kumfanikisha hata siku moja mm japo sikufahamu lakini huwa nakuombea baraka na mafanikio kila iitwapo leo. Marufuku kukata tamaa!!! its me Janeth!!

 41. Anonymous

  May 14, 2013 at 5:06 am

  This is so touching my dear am sorry ndo mipango ya mungu

 42. Mama 2 (Mrs M)

  May 14, 2013 at 5:06 am

  Pole sana Dina!! Yote ni mapenzi yake Mola!! Mshukuru kwa yote!!Na zaidi ni kumshukuru kwa hapo ulipofikia.

 43. Anonymous

  May 14, 2013 at 5:14 am

  Dina kwakweli nimelia ukizingatia nami mama yangu ametangulia mbele za haki,ujumbe unasikitisha mpaka wenzangu wananishangaa hapa ofisini.Pamoja na yote Mungu ni mkubwa na nina furaha kukuona uko ngangari na maisha yanaenda vizuri!

 44. Anonymous

  May 14, 2013 at 5:32 am

  pole sana dina,mshukuru mungu kwakila jambo.mungu amekulinda hadi umekuwa mkubwa wa kujitambua mwenyewe,kama ulipitia magumu yote yasahau,nina imani umeanza upya na mungu akutie nguvu,pambana katika maishampaka kieleweke na wala usiogope kuanzisha familia kwani zinatofautiana sana,na muombe sana mungu katika hili.ubarikiwe!

 45. Sophia

  May 14, 2013 at 5:43 am

  Pole sana Dina, ila na mie pia sina mama tena bora wewe ulibahatika kulelewa na baba mpaka umejitegemea, mie nilianza kufiwa na baba nikiwa na umri wa miaka 16 namshukuru mungu mama alihangaika nasisi wanawe mpaka alipomchukua mama nikiwa na umri wa miaka 31 tena nikiwa na mwaka 1 ndani ya ndoa, angalau nimepata mengi tuu. Ila kikubwa ni kumshukuru mungu na kuwaombea wazazi wetu waliotangulia na kwa wale walio hapa Duniani basi na waheshimiwe kama ulivyosema kwakuwa wao ndio mungu wa Dunia.

 46. Deborah

  May 14, 2013 at 5:43 am

  Yote ni ya Mungu na ana makusudi yake! Pole sana ila wewe ni mwanamke jasiri sana hilo lazima uelewe. Mungu azidi kukuongoza katika yaliyo mema.

  Mimi Deborah wa Mbeya

 47. Anonymous

  May 14, 2013 at 5:48 am

  Pole Dina maneno yako yamenigusa sana kiasi kwamba kila sentens niliyokuwa nikiipitia machoz yalinitoka, mimi pia sikulelewa na mama!pengo lake naliona mpaka leo.

 48. Anonymous

  May 14, 2013 at 5:56 am

  very touching, hadi machozi yamenitoka.

 49. Anonymous

  May 14, 2013 at 6:14 am

  Yaani Dina pole kwa yote Maisha yanaendele nimesoma hii msg yako nimetokwa na machozi, nami sina mama toka 1999 kaniacha nikiwa na miaka 14 napitia maisha magumu natamani my mum angekuwepo nimshirikishe km mama ila hayupo Mama anauma sana ila shukuru kwa yote maana me ht Baba sina! Tujipe moyo tutashinda mpendwa

 50. Anonymous

  May 14, 2013 at 6:24 am

  Pole sana Dina yaani nimelia kwa ajili yako kwani inaumiza sana kwa jinsi ulivyoelezea kuhusu kukosa mapenzi ya mama mzazi ila kumbuka tu kila likufikalo lina sababu na mungu ndiye ajuaye sababu nafikiri ndio maana umekuwa msaada mkubwa sana kwa jamii inayokuzunguka na kukupelekea kupata tuzo ya mwanamke bora wa mwaka naweza sema hiyo ndiyo sababu mojawapo. Nakupenda sana Dina

 51. Anonymous

  May 14, 2013 at 6:45 am

  Very Sorry Dina, Mipango ya Mungu ni wengi wenye machungu kama yako..Na Kila nafsi itaonja Mauti..Umenifanya Nilie Dina Kwa memory ya Baba yangu aliyeaga Dunia Bila kujua Mapenzi yake..Tuwaombee wapumzike kwa Amani.

 52. Hilda Lyatuu

  May 14, 2013 at 6:48 am

  Pole Sana Dina, nimeguswa sana na ujumbe wako. Mungu aendelee kukutia moyo. mimi pia nimempoteza mama yangu kipenzi mwaka jana mwishoni na najiona nimepungukiwa sana na mimi ni mtu mzima nimeolewa na nina watoto wawili.Sasa wewe uliempoteza tangu una miaka 3 kweli inauma sana. Lakini yote ni mipango ya Mungu na yeye anayajua machungu yako. Endelea kumtegemea atakunyanyua zaidi na zaidi.
  Kazi njema

 53. amallu

  May 14, 2013 at 6:49 am

  Nakuonea huruma sana Dina maana mimi sasa nina Miaka 28 na mama tangu amefariki ni wiki ya tatu sasa, nimeolewa na maisha yangu yamekuwa ya mateso tangu apo lakini machungu yangu yalikuwa yakiishia kwa mama maana ndiye mtu niliyekuwa nakimbilia na kulia kwake huku akinifariji na kunipa ushauri na ujasiri maana mimi nimekulia upande wa mama tu na mama ndiye aliye kuwa Rafiki yangu wa kweli baba yangu yeye anaishi zake Mombasa wala hajali sana kuhusu mimi, na mimi ndiye dada mkubwa nikiachwa na wadogo zangu amabao mama yao ni mimi sasa, naona nashindwa kabisa kuikabili hali hii nikizingatia yeye ndiye aliyekuwa Rafiki yangu wa kweli na akinijua katika hali zote sasa mimi ni mtu wa presha tu na machozi nikiwa najua huu ni mwanzo tu kuna mengi yanakuja, MUNGU AZIWEKE ROHO ZA MAMA ZETU PEPONI DAIMA

  • Anonymous

   May 14, 2013 at 11:13 am

   Trust in God,usiwe wa presusure na machozi,wadogo zako wanakuangalia wewe,kwahiyo jikaze,muombe mungu akutie nguvu. I wish you well in all your life. May your mom's soul rest in peace. always wear that pretty smile on your face.

  • amallu

   May 15, 2013 at 6:42 am

   thank your Dina, AMINA

 54. ROSE

  May 14, 2013 at 6:49 am

  yaani dina nimesoma maneno yako nimesikitika sana kweli najua ni jinsi gani unavyoumia kumkosa mama,.pole sana mpenzi wangu,!amini mungu anakila sababu ya kufanya hivyo cha muhimu mshukuru mungu na uzidi kumuomba sana mungu akusaidie na kukupa mwongozo mzuri na wenye baraka katika maisha yako,!.wewe ni mwanamke ambae na kuheshimu sana na ninakuona utakuja kufika mbali sana kwenye maisha yako…amini hilo my dina.mungu aileze roho ya mama dina mahali pema peponi na azidi kukupa baraka na amani tele moyoni mwako

 55. Anonymous

  May 14, 2013 at 6:52 am

  Pole dina umenisikitisha sn na huu ujumbe wako mpnz wng, mpk nmehic machoz kunitoka kwa sababu na mie npo on the same way hakuna ki2 kigumu kama kumpoteza mama jamani maisha bila mama ni ya kubahatisha sn na uchungu wake anaujua aliefiwa na mama, MUNGU azid kukulinda ktk maisha yako na mwisho wa cku utaolewa 2 kwa sababu ww ni mwanamke dina cha muhimu muombe MUNGU akujaalie kupata mume mwema, ubarikiwe sn. RIP wamama wote walliotangulia mbele ya haki.

 56. Anonymous

  May 14, 2013 at 6:52 am

  I do understand what ur going through..mimi mama yangu alifariki nikiwa form 4 mwaka 2005, ndo lilikua tegemeo letu kubwa sana mimi pamoja na dada yangu na mdogo wangu kutokea pale maisha yalibadilika kabisa sababu tulikulia katika mikono yake peke yake..lakini tunamshukuru mungu tumevuka magumu yote na leo hii maisha yanaendelea ingawa kunaupweke mkubwa sana..kama unavyosema sometimes unawaza kama mama leo hii angekuwepo ingekuwaje lakin yote ni mapenzi yake yeye aliyetuumba.pole sana

 57. Anonymous

  May 14, 2013 at 6:53 am

  Pole sana Dina yaani waraka wako umenisisimua sana kiasi machozi yamenilenga wallah,inshaallah mwenyezi mungu wetu anatupenda ndio maana upo hadi leo na unaendelea kukua,kila kitu ni mipango yake YATUPASA TUMSHUKURU KWA HILO,INNA LILLAH WAINA ILLAH RAJIUN.

 58. Anonymous

  May 14, 2013 at 7:11 am

  Dina leo umenitoa machozi kwa message yako, mwenyezi mungu akupe uvumilivu, yaani umenikumbusha mbali sana, na me nina historia kama yako lkn miaka tofauti, baba angu alikufa nikiwa na miezi 4, na mama yangu alikufa nikiwa form 1, 2001, alimuacha mdogo wangu ana miaka 4, uwezi amini ulikuwa mtihani amna mfano, namshukuru bibi yangu mzaa mama ndo alinilea mimi na mdogo wangu, nlimaliza shule adi chuo, kama unavyosema ukiwa na matatizo kama hayo uwazi kuolewa wala kuzaa, nina miaka 28 cjaolewa wala cna mtoto, mdogo wangu ndo kila kitu namuita mwanangu sasa yupo form 3, mbezi beach secondary, uwezi amini nilivyomaliza tu chuo nikapata kazi tena stationery nilisomea secretary, 2007, nikaanza kazi na majukumu ya kumlea mdogo wangu jamani inauma sana, uwa naliaga peke yangu na kumshukuru mungu, lkn sasa najitegemea bahati nikapata kazi katika kampuni fulani ndo npo adi sasa namshukuru mungu sana, maisha nayaweza kuyamudu mimi, mdogo wangu na bibi. mama ndo kila kitu katika dunia, ukimkosa mama utaona mapungufu yake. Apumzike kwa amani mama yangu kipenzi. Mimi IRENE wa Magomeni.

 59. Anonymous

  May 14, 2013 at 7:12 am

  maskini Dina pole mmefanana maskini

 60. Ald

  May 14, 2013 at 7:24 am

  Dah!!
  Pole mpendwa. Mungu aendelee kukutangulia kwa kila utakachokifanya. Amina

 61. Habiba

  May 14, 2013 at 7:32 am

  Yaani Dina leo umenifanya nilie mpaka basi,umeongea maneno ya kutia huzuni sana pole sana mpenzi ila kaza moyo kwani haya ni ya kila mmoja wetu,its true mama ndo kila kitu kwa mtoto na unapomkosa katika maisha yako huwa ni mateso sana,maana yeye ndie mwalimu wa kwanza duniani

  • Anonymous

   May 14, 2013 at 8:41 am

   Dina mungu akutangulie.Ila nakushukuru kwa kutumia siku ya mothers day kumkumbuka mama ako.Ubarikiwe

 62. Anonymous

  May 14, 2013 at 7:36 am

  pole Dina kwa kukosa upendo wa mama, hata mimi niliyakosa tena nikiwa na miezi hata mwaka sijatuimiza baada ya mama yangu kuniacha kwa bibi mzaa mama na kwenda kutafuta maisha Nairobi so nikalelewa na bibi mpaka nikafika darasala nne baada ya hapo mjomba wangu akanichukua kuja naye dar amenilea mpaka leo hii na mimi naitwa mama wa watoto wawili namshukuru Mungu, Dina kusema kweli mapenzi ya mama ni muhimu sana sasa hivi ndio naona jinsi nilivyoyamiss hayo mapenzi kutoka kwa mama yangu kupitia kwa wanangu kwa jinsi wavyodeka na mimi nalipiza mapenzi niliyoyakosa nawapatia wanangu so dina dawa ya kuondoa upweke uliokuwa nao ni kuanzisha familia yako nakuhakikishia utayasahau yote. Asante.

 63. Anonymous

  May 14, 2013 at 7:41 am

  pole sana Dina story yako imenigusa sana mpaka machozi yamenitoka,nami pia mama yangu alishatangulia mbele ya haki hivyo ninajua upweke wa kumkosa mama jinsi unavyouma,Hakika HAKUNA KAMA MAMA.

 64. puli

  May 14, 2013 at 7:41 am

  Very touching story. Mungu akujalie watoto wako na akupe maisha marefu ili uweze kuwapatia watoto wako upendo wa mama ulioukosa wewe.

 65. Anonymous

  May 14, 2013 at 7:42 am

  Pole dada dina, yote ni maisha. Endelea kupambana na maisha japokua ni kweli kuna kitu unakikosa hasa hasa ule upendo wa mama lakini ni mipango ya mungu najua ww ni strong woman mpaka hapo ulipofikia na najua unaweza zaidi ya hapo. Stori yako imenisisimua kwa kweli.

  Nakutakia kazi njema.

  Vero

 66. Cymah Wandelt

  May 14, 2013 at 7:44 am

  Pole Dina habari inauma sana, hata Mimi niliondokewa Na mama ila nilikuwa na miaka 10, kidogo nijirushe kaburini hasa nilipowaona wadogo Zangu Na wamwisho alikuwa Na miaka kama yako, inauma sana, ila namshukuru Mungu hivi sasa ni mama Na nitajitahidi kadiri ya uwezo Wangu kuwalea vizuri. Mungu awarehemu Mama zetu amen.

 67. Anonymous

  May 14, 2013 at 7:57 am

  Pole sana Dina. Ujumbe wako nilipousoma nimejikuta natoa machoz.
  Mungu azid kukupigania na kukuonyesha yanayofaa kufanya.

 68. sakina

  May 14, 2013 at 8:04 am

  Its so touching! jamani nimesoma na kuishia kulia tu,pole sana Dina muombee sana mama kila baada ya sla muombee Allah amrehem.

 69. Anonymous

  May 14, 2013 at 8:28 am

  ooooh pole sanaa dada inaumiza sanaa hii story, mungu azidi kukupa nguvu kwa kila jambo, inahuzunisha sanaaa

 70. Anonymous

  May 14, 2013 at 8:42 am

  Pole sana

 71. Anonymous

  May 14, 2013 at 8:43 am

  duh pole sana dina umeniliza, jipe nguvu kwani kazi ya mungu haina makosa zidi kumuombea uko alipo baraka zake zitakufikia,

 72. Anonymous

  May 14, 2013 at 8:58 am

  ooh jamani DINA pole sana mamii,,hadi machozi yamenitoka yani,,m/mungu amuweke mahala pema peponi mama yetu,,amina

 73. Anonymous

  May 14, 2013 at 9:00 am

  Siku zote nawashauri sana Wale wote wa namna kama yako Dina Kwa kuwaambia Kweli anaweza kuwepo upate mapenzi mazuri kama unavyofikiria na pia mambo yanaweza kua tofauti kabisa na unavyotegemea.
  Mimi nimekua kwa kulelewa na bibi mzaa Mama, Mama yangu yupo mpaka leo lakini sijawahi kuhisi upendo wake kwangu na hajawahi kunisaidia kwa lolote na sijawahi hata kutamani kukaanae kama mamangu.
  Kanifanya nichukie kuwa mama, kaharibu maisha yangu ya Leo na Sijui ni kwanini imekua ivi!!

 74. Anonymous

  May 14, 2013 at 9:05 am

  Pole dada yangu, pole sana. Umesafiri hadi hapa endelea kusimama kidete hivyohivyo. Mungu aendelee kukufariji siku zote.

 75. nyakorema rioba

  May 14, 2013 at 9:15 am

  this lady is an iron!! sitaki ku imagine nife sasa huku mwanangu tumaini akiwa ana miaka 4.lakini inawezekana tu hasa kwa nchi hizi za kiafrika amabzo riski ya kifo ni kubwa saana hasa kwa ajali. DINA you are ana inspirer!

 76. nyakorema rioba

  May 14, 2013 at 9:16 am

  this lady is an iron!! sitaki ku imagine nife sasa huku mwanangu tumaini akiwa ana miaka 4.lakini inawezekana tu hasa kwa nchi hizi za kiafrika amabzo riski ya kifo ni kubwa saana hasa kwa ajali. DINA you are ana inspirer!

 77. Anonymous

  May 14, 2013 at 9:20 am

  yaaani kiukweli hiii sms na niliisikiliza wakati nikiwa kwenye daladala nilijikuta nalia kwani nikama msumari wamoto umepita kwenye kidonda kibichi. sababu mimi nilifiwa na na mama yangu nikiwa darasa la 4 1993 tukiwa watoto wanne wote wa kike dada yetu mkubwa akabeba jukumu la kutulea nikiwa nimemaliza darasa la saba dada mkubwa nae akafariki mbaya sana hapo ndipo maisha yangu yalipo badilika kwa kukosa uelekeo nilibaki naishi na dada yangu pili ni stori ndefuu sana . mpaka hapa nilipo kiukweli ni MUNGU TUUU NDIO ALIE NIWEZESHA kwani nimepita milima na mabonde mengi sana yenye maumivu na machungu mengi huwa kunawakati nalia sana na kufika wakati na kufuru MUNGU . lakini mwisho najifariji kwa nyimbo na sala. maisha yanakwenda. Kiukweli siku ya mama duniani huwa siiifuatiliagi kabisaaaa. Kiukweli HITAJI LA MAMA LIPO KILA SIKU PENGO LAKE HALIZIBIKI NA KILIO CHA MAMA HAKIISHI HADI UTAKAPO INGIA KABURINI. nakupenda mama yangu kipenzi LIDYA KIMWERI huko uliko mbele za haki PUMZIKA KWA AMANI MAMA.

 78. Anonymous

  May 14, 2013 at 9:22 am

  POLE SANA DINA NAKOSA CHA KUSEMA KWAKO ILA DINA MUNGU AMEKUJALIA WATU KIBAAAAAAAAAAAAAAAAAO TUNAOKUPENDA MSHUKURU KWA HILO DADANGU…….

 79. Anonymous

  May 14, 2013 at 9:26 am

  Dina umenigusa sana, yani maisha uliyopitia ni kama yangu kabisa.. tumetofautiana kidogo tu mimi nimelelewa na dada… kwakweli ata mimi huwanasikitika sana mtu anapomjibisha mama yake.. natamani sana nami angekuwepo walau niite mama… neno MAMA ni geni mdomoni mwangu. hivyo ulivyo ndo mimi nilivyo dina.. Siwezi kukueleza sura ya mama yangu.. zaidi ya picha. kweli mama mi mhimu sana katika maisha yetu. bola wewe unapata tiba. ILA mungu anamakusudi yake. Tushukuru kwa yote. MUNGU WALAZE MAMA ZETU MAHALI PEMA PEPONI..

 80. Anonymous

  May 14, 2013 at 9:37 am

  dina umeniliza sana sana my dia, its so touching, yan nimejikuta nalia tu . pole sana my dia ila pia mshukuru mungu kwa kila jambo kwani yeye ni muweza wa yote. endelea kumuombea mama kila upatapo nafasi.

 81. Anonymous

  May 14, 2013 at 9:41 am

  daaah! jamani… cna hata cha kusema mana nmejkuta machoz yakinilengalenga vle npo ofcn nmejzuia kulia ila ningeisoma hii stori nkiwa hom nadhan ningelia mpaka basi….

  kweli mama ndo kila kitu, binafsi nimekua na wazazi wangu wote na ninamshukuru Mwenyez Mungu bado wapo hai had leo hii nasema Asante baba Mungu. kwa sababu wkt nakua sikuwah kujua umuhimu wa mama wala baba lkn baada ya kumzaa mwanangu wa kwanza kiukweli nilijua ni nini mana ya mama…. make kuna maneno niliyasema wkt natoka leba manesi ilibidi wacheke lkn kweli mama ni mama na hakuna kama wala zaid ya mama.

  Pole sana Dina ninakuombea Mungu aendelee kukupa ujasiri, usiogope wala usikatae kuolewa mana utakua unaenda kinyume na mapenzi ya Mungu alootuumba, kubali ipo sk utampata mwenza na utajaliwa watoto wako na utawalea kwa mapenzi kadiri Mungu atakavyo kujalia, usiogope da Dina. Mamayangu mm alipitia maisha kama yakwako kabisa ila alipoolewa ametuzaa sisi tupo wanne na unaona Mungu amemjalia uhai bado yupo had leo na bdo analea wajukuu ambao ni watoto wetu, kwahiyo usiwaze labda nawe utajawaacha watoto wako wateseke hapana, Mungu wetu ni mwema sana na ana sababu kwa kila jambo.

  Jipe moyo my Dina, kila kitu kinawezekana ukimtegemea Mungu. Polesana na Kila la Kheri ktk maisha yako. Asante kwa kutushirikisha hii story ya maisha yako.

  • Anonymous

   May 24, 2013 at 9:00 am

   AMEN TO THIS…hata mie Jehovah ata sasa ametupigania kwa huruma zake tu kwani nna wazazi wote warili na wanatupenda ajabu ata sina lugha ya kueleza.kweli wazazi ni miungu wa pili duniani na hakuna kama mama aseee.
   ingawa walitengana na ilikua tabu kweli ila wazazi wetu walijitaidi sana ku-balance malezi yetu na sasa Jehovah ametubariki kila mtoto ana maisha yake mazuri tu na watoto wetu (wajukuu).Yani apa imebidi nimtumie sms my mama just to greet her uwiiiii adi machozi yananitoka ajabu…eeh Mungu turehemu pale tulipoonyesha kupotoka/ukaidi kwetu juu ya wazazi wetu kuna watu wanalilia hii nfasi adimu

   Mungu awatie nguvu wote waliopoteza wazazi au mama Yeye ni mfariji wa ajabu msife moyo

 82. Anonymous

  May 14, 2013 at 9:49 am

  KWA WAKATI HUO KWELI MAMA YAKO ALIKUA MREMBO DINAH. MUNGU AMPUMZISHE KWA AMANI

 83. Anonymous

  May 14, 2013 at 11:18 am

  Dina pole sana mdogo wangu, imagine mi ni mama mtu mzima na watoto pia lakini mama yangu kafaliki huu mwaka wa pli kila nikipata mawazo naliaaaaa halafu namuwaza pole sana

 84. Anonymous

  May 14, 2013 at 11:48 am

  DINAH…WEWE NI MPIGANAJI..MZURI NA MWENYE HOFU YA MUNGU..ww ni role model wa wengi..may God be with you

 85. Anonymous

  May 14, 2013 at 12:56 pm

  OOH, POLE SANA MDADA, NINA AMINI PENGINE MUNGU ALIAMUA KUKUCHAGULIA NJIA HIYO YA MAISHA, ILI UJE KURUDISHA TUMAINI JIPYA KWA WENGI AMBAO WAMEPITIA NJIA KAMA YA KWAKO. BE BLESSED NA UZIDI KUWA IMARA

 86. Anonymous

  May 14, 2013 at 1:06 pm

  its too hurt story dina.tuombe mungu awape wazazi afya njema wawalee watoto wao angalao waweze kujitambua

 87. Anonymous

  May 14, 2013 at 1:11 pm

  You are a strong women Dinah and God has a purpose for everything we go through, take heart that your Mother is in a good place. so touching, after reading your message i called my mom and told her how much i love her.

 88. Anonymous

  May 14, 2013 at 1:21 pm

  pole sana Dina nimehuzunika juu yako ila Mungu anajua pengine leo hii usingekuwa hivyo ulivyo yaache maisha yaendelee Mungu mwema ataendelea kukupigania tupo wengi tunakupenda sanaa keep it up…

 89. Anonymous

  May 14, 2013 at 1:40 pm

  Dina usiogope ndoa dadangu am sure you will be the best mum ever lav you xoxoxoxoxoxoooxo

 90. Anonymous

  May 14, 2013 at 2:55 pm

  Mama is Everything,BIG LOST TO LOOSE A MAM Especially like u at that Age.I dont knw m ningekuwaje kama ningepitia hiyo hali.Coz i can see dat lov from my mum and how it help me through for sure..Pole Sana Dinar! na Hongera pia kwa Moyo imara uliokuvusha mpaka hapa ulipo,its also because of her blessings for GOd seak…LOVE U MAM,ALWAYS!

 91. emma kahere

  May 14, 2013 at 3:10 pm

  Story yako imenifanya nizid kukupenda nakukuona kama dada yangu wa hiyari.,POLE SANA DINA ila chakumshukuru Mungu nikwamba amekucmamia na mpaka leo umekuwa mfano mzur sana kwa jamii hasa kwangu pia.,najua ni kiac gan unaumia lakin ndio mapenz ya Mungu.,nazid kukuombea ili kwenye ndoa yako uish kwa aman nawatoto wako wajivunie kuwa namama mwenye maadili.

 92. Anonymous

  May 14, 2013 at 3:18 pm

  lakini yote ni mipango ya mungu huwezi jua mama yako angekuwepo si ajabu usingefika hapo maybe ungepata ujauzito mapema ukiwa shuleni ukakatisha ndoto zangu, kwahiyo mshukuru mungu kwa kila jambo maana yeye ndiye anayeijua kesho, pia mwombe mungu akupe mume mwema usiogope aliyopitia mama yk, vunja laana isije ikakufuatilia katika mahusiano yk.

 93. Anonymous

  May 14, 2013 at 3:52 pm

  Pole sana mdogo wangu mimi mwenyewe nimesoma nimejisikia vibaya sana japo mimi mama yangu yupo lakini tuko pamoja nakumbuka ule msemo wa mama Salma Kikwete mtoto wa mwenzako ni wako tushukuru kwa kila jambo tunazidi kukufariji zidi kumuombea mama alale mahali pema peponi mungu ni mfariji wa kila kitu shukuru hapo ulipofikia mdogo wangu

  maria wa Dar

 94. Anonymous

  May 14, 2013 at 4:09 pm

  Pole sana mdogo wa D. nilisikiliza historia yako kwenye leo tena na kusoma kwenye hii blog nimeshindwa kujizuia kwani nimelia sana ukizingatia kila mara wanangu wanaponikosea huwa nawaambia siku mkinikosa mtalia sana, sasa hayo maneno yamerudia na kuniumiza.Usijali Mungu yupo nawe atakupigania.Pamoja na kuwa mama yako ametwaliwa ukiwa mdogo, lakini Mshukuru Mungu kwa kila jambo. Sisi fans wako tunakupenda sana, hivyo basi usijione uko peke yako. Pia usikate tamaa kwani Mungu wetu ni mwema na mwaminifu ana kupenda na kukuthamini ndio maana anazidi kukuinua mpaka umekuwa mtu wa watu. Hivyo basi usikatae kuolewa kwani tunakuombea kwa Mungu akupe mwenzi mwema atakae kupenda na kukusahaulisha yote. MUNGU AIWEKE ROHO YAKO DINA MAHALI PEMA PEPONI amen.

 95. Anonymous

  May 14, 2013 at 4:15 pm

  Pole sana sisy dina.you have realy touched my heart nimemaliza chuo nafanya kazi and both my parents wapo my father is not kind of a loving and caring husband but mama yangu amekuwa imara kuvumilia yote kwa ajili ya watoto wake.Huwa anasema mimi ndio nimechagua mume kwa hiyo nimewachagulia baba nitamvumilia kwa kila hali kwa ajili yenu.sisi tupo 6 kwenye familia yetu.Yani baba angu anawatoto nje ambao hata mdogo wangu wa mwisho mkubwa na mama anajua.Hakuna kama mama jamani mama anaweza fanya lolote ili motto awe na furaha.Pole sana sana dina.

 96. Anonymous

  May 14, 2013 at 4:18 pm

  you real are a fighter dina and sure you will achieve more and more by his grace.love you sisy I send you lots lots of kisses n huggs

 97. Anonymous

  May 14, 2013 at 4:27 pm

  duuuu!!! ama kweli nikupe pole na hongera kwa uvumilivu kwa mapito hayo. Ni ngumu kuikubali hali hiyo lakini ni mapenzi ya mungu. Jamani sote tunapaswa kumshukuru mungu kwa kila jambo hasa unapokuwa na nguvu na punzi ya uhai ya kufanya hivyo. Mimi nina miaka 40 plus lakini wazazi wangu wote wawili wapo hai najivunia hilo na namshukuru mungu wangu kwa hilo.Siyo mimi nilipanga hivyo ila mipango ya mungu. Ila najaribu kufikiria wewe ambaye hukubahatika kumjua mojawapo ya mzazi wako tangu ukiwa mtoto mdogo sipati picha inakuwaje ila kwa kweli ni maumivu makali sana

 98. RUKY

  May 14, 2013 at 4:51 pm

  DINA NIMESOMA ZAIDI YA MARA NNE SINA LAKUSEMA ZAIDI YA POLE SANA SANA FAHAMU TUPO PAMOJA….NA MUNGU YUPO PAMOJA NA WEWE….ILA USIJE JARIBU KUSEMA UNAOLEWA KWA KUFURAISHA WATU SABABU YA MANENO KWANZA WE BADO MDOGO NA UNAMUDA PLZZ TAKE YR TIME..MIE NIMESHA PITIA HATA MAISHA YA NDOA KWA SASA SITAKI HATA KUSIKIA WALA SIONI KM NIMUHIMU KIVILE KUTOKANA NA MASWAHIBA YAIYONIKUTA HALII HII MIE NINA MAMA JE NINGEKUW SINA KM WEWE NAHISI NINGEKUWA KM KICHAAAA……

 99. Anonymous

  May 14, 2013 at 7:24 pm

  Pole sana Dina,naona ni heri mama akuache mtoto hujui kinachoendelea,mama yangu alikfarki mwka jana june 14 nikiwa na miaka 26,inaniuma sana kumpoteza kwani ndiyo alikuwa shoga yangu na kla kitu kwangu,alinisomesha kwa shida mpka nkamaliza chuo mzumbe 2007 cha kusikitisha alifark miezi miwili tu baada ya kuanza kazi so hakufaidi chochote kutoka kwangu,baada ya kifo chake najihisi cna sababu ya kupenda tena naona kama ameondoka na mapenzi yote sitamani mwanaume wala sifikirii kuolewa kabsaaa,muda mwngi nautumia kumuwaza yeye tu!mungu amrehemu mama yangu Mariam Mbega……its neema issa

 100. Martha

  May 14, 2013 at 10:26 pm

  Pole DINA, Mungu akupe nguvu

 101. Anonymous

  May 15, 2013 at 5:22 am

  pole dina my dear,yaani machozi yamenitoka kwa hii story.hata mimi nilipitia hayo ya kuonokewa na mama ila tofauti mama yangu aliniachanikiwa mkubwa kidogo kuliko wewe ulivyoachwa .Mimi ni mamawa watoto watatu na miaka nane katika ndoa ila kuna wakati huwa nalia sana tena sana ninapopata changamoto katika ndoa yangu ,nahisi kama kuna kitu nilikikosa kutoka kwa mama yangu ambacho kinafanya changamoto hizo zitokee ktk maisha yangu ya ndoa.Mungu atakupa faraja katika hilo na nakuombea utoe hofu ya ndoa ili uje kuwa mke na mama mwema

 102. Anonymous

  May 15, 2013 at 5:51 am

  jamani dinna wewe! yaani mwenzio nikiwa na wenzangu utasikia nimemtumia mama hela basi natamani sana mama angu namie angekuepo nimnunulie hata kitenge cha bei rahisi. inauma asikuambie mtu!

  • Anonymous

   May 20, 2013 at 7:12 am

   inauma sana hasa akifa ukiwa mdogo na wakati wakutembelewa shule wenzio wazazi wao wanakuja wewe huna mtu wa kuja

  • Anonymous

   May 24, 2013 at 9:05 am

   jamani poleni wapenzi Mungu aliye mfariji wetu na awape faraja,nguvu na amani na mapenzi tele muishi bila stress mana mmekosa mama.Fanya Mungu Jehovah awe mama na rafiki yako hutajuta.

   Tupo pamoja nanyi wapenzi

 103. Anonymous

  May 15, 2013 at 6:22 am

  Pole sana mpendwa wetu Dinna. Hayo yote ni mipango ya Mwenyezi Mungu. Huwezi kujua Mungu ana makusudi gani juu yako. Pole sana. Pia usiogope ndoa. Ile experience mbaya iliyokuwepo kati ya marehemu mama yako na baba si kwamba na wewe itakupata. Yamkini, ukiolewa mme wako anaweza kuwa mfariji wako namba moja. Uwe na amani na nakushauri tu uingie kwenye maisha ya ndoa. Utaona raha zake. Japo changamoto haziwezi kukosekana lakini ukiwa kwenye ndoa utaisha vema zaidi kuliko sasa hivi. Kama utaendelea kuwa peke yako kama ulivyo sasa hivi mwisho wake itakuwaje? Kumbuka pia kwamba kuolewa pia kuna umri wake. Si kwamba wakati wowote unaweza kuolewa. Lakini pia kuna suala la kupata mtoto. Ukiolewa utapata mtot ambaye pia itakuwa faraja zaidi kwako. Yamkini akizaliwa mtot wa kike unaweza kuwmita kwa jina la mama yako. Kila utakapokuwa unamwita mtoto yule basi utasahau yote na utakuwa kama vile umemwona mama yako. Tuako pamoja katika kukuombea na hakika utafanikiwa. Maana kila aombaye hupata. Hata siku moja huwezi kumwomba Mungu mkate akakupa jiwe au ukaomba samaki akakupa nyoka.

 104. Anonymous

  May 15, 2013 at 8:08 am

  sina neno Dina, pole sana. Me nakupenda sana na ninatamani kusikia sikumoja unaolewa na kutengeneza familia mpya moyoni mwako na katika maisha yako kwani naamini yote ayo yatakwisha.

 105. Anonymous

  May 15, 2013 at 9:31 am

  Hi Dina,

  pole kwauliyopitia,unajua kila Mungu analopanga lina sababu.usiendelee kuhuzunika,jua Mungu yupo na endelea na maisha,yeye hufanya njia pasipokua na njia.

 106. Anonymous

  May 15, 2013 at 1:08 pm

  polee ndugu una kila sababu ya kuonewa huruma na kupewa pole ila mshukuru mungu japo ulipelekwa shule wengine wanafiwa na mama zao hata shule inakuwa tabu,,utakapo kuwa na mtoto utafarijika na utapunguza machungu uoni mwenzio zamaradi angalau mwanae anamfariji

  • Anonymous

   May 17, 2013 at 9:54 am

   pole sana, hii story imenigusa sana, mimi pia mama yangu alifariki nikiwa darasa la kwanza,kila mara huwa namkumbuka sana, nikiwaona watu na mama zao natamani ningekuwa mimi, cha muhimu kuwaombea wapumzike kwa amani,Mungu amewapenda zaidi.

 107. Anonymous

  May 15, 2013 at 1:47 pm

  Hi Dinah
  pole sana dina, nimesoma historia yako nimelia sana, nimejiona kama mkosaji vile kwa mama yangu nampenda sana lkn naona km haitoshi kwa jinsi alivyopigania maisha yetu peke yake mpk dk hii,kweli maisha bila mama mzazi its nothing maana hata ndg wa kuzaliwa nae atakusimanga lkn mama hawezi,

  pole sana dinah hilo pengo litazibika kwa asilimia kidogo angalau utakapokuwa na mtoto/watoto wako hiyo ndiyo itakuwa faraja ya pekee sana kwako, usiogope kuolewa au kutengeneza familia fanya maamuzi sahii utapata faraja. irene

 108. Anonymous

  May 15, 2013 at 2:35 pm

  Mama yako alikuwa mrembo sana enzi hizo, Mwenyezi Mungu ampumzishe kwa Amani, tunakupenda sana Dina.

 109. Anonymous

  May 15, 2013 at 6:46 pm

  Jamani kila mtu anasema pole, sijui nakuhurumia!! yaani wote hamjui mapenzi ya Mungu.Mimi nakupa hongera sana kwa hatua ya maisha uliofikia kwani hayo ya kufiwa hayakwepeki muhimu ni kujua unachoweza kufanya katika maisha yako kama unavyofanya sasa na hayo ndio muhimu ya kumshukuru Mungu.Inawezekana mama yako angekuwepo ungeharibikiwa na ungedeka sana na usingefika hapo ulipo.Mambo mengine lazima muwe mnageuza shilingi upande wa pili siyo kuangalia upande mmoja tu.Mimi wazazi wangu wote walitangulia na sasa Mungu kanibariki na namshukuru Mungu kwamba ameniwezesha kujifunza kujuauhimili wangu mimi kama mimi pasipo kuangalia nani yuko pembeni kunipiga jeki.Alichotushirikisha Dina hapa siyo kuwalilia wamama waliotangulia bali kujililia wenyewe kwa maisha yetu tulionao na kuthamini wazazi tulio nao na sisi wenyewe tulioanza kuwa na familia kujijua umuhimu wetu kama wazazi.Asante Dina na hongera kwa hatua nzuri ya maisha yako na kujikubali.

 110. Anonymous

  May 16, 2013 at 6:18 am

  Dina hii ni stori yako au ya Rehema aliyeandika jina baada ya stori? hebu waelekeze wadau maana pole zinakujia wewe. Next time vema uweke utangulizi kuwa hiyo story inatoka kwa nani.

 111. Anonymous

  May 16, 2013 at 6:49 am

  Duh msg inaumiza sana, ni nzito sana, iko deep sana,na inachoma sana kwa kweli, hasa ukijaribu kujiweka mahali pako Dinna,pengine huwezi kupata picha vizuri kama mama yako ni mzima na kila kitu kinaenda sawa. Pole sana Dinna, poleni sana wote mliopoteza wazazi wenu hasa wale waliopoteza WAZAZI wakiwa bado watoto wadogo kama Dinna Marios.

 112. Anonymous

  May 16, 2013 at 1:18 pm

  Pole sana jamani…..Allah amuepushe na adhabu zote za kaburI na tuzidi kuwaombea dua marehemu wetu

 113. Anonymous

  May 16, 2013 at 3:32 pm

  What a sad story..pole sn mum.mungu azidi kukuweka imara dina.love u

 114. Anonymous

  May 17, 2013 at 8:54 am

  pole sana dada, we share same story tho yangu ni worse ila namshukuru mungu kwa hapa nlipofika ingawa sio mbali sana but at least i can take are of myself…

 115. Anonymous

  May 17, 2013 at 9:02 am

  Ahh! Pole sana tena sana Dina!! So touching jamani. Mungu akupe faraja for your mom.

 116. Anonymous

  May 17, 2013 at 10:20 am

  Pole sana Dina, Ata me nilimpoteza mama yangu nikiwa na miaka 2 na nusu ila nashukuru baba yetu alitulea kwa upendo sana, alikaa 14 yrs bila kuoa kwa ajili ya me na kaka yangu, mana mama alituacha 2 me na kaka yangu, so alikuja kuoa tukiwa kidato cha 4 mama yetu ya kambo alitupelekesha sana lakini me na kaka yangu tulikuwa na umoja sana hatukuyumbiswha ingawa kwa kiasi fulani ilitutingisha kidogo,na bahati mbya tukampoteza baba yetu 2003 ndo nikiwa nimemaliza chuo, namshukuru Mungu maisha yanaenda na ni mama wa watoto 2 sasa, wananifariji sana na nawapenda sana.

  • Anonymous

   May 24, 2013 at 9:08 am

   umenobariki sana mpendwa,sijui kwanini wanawake hao wachache ndio wanakua waleta majuto kwa watoto wa kambo…kwanini lakini??sipatagi jibu

 117. Anonymous

  May 17, 2013 at 10:33 am

  Dina, sijafungua ukurasa wako muda mrefu. Nipo ofisini nikasema wacha nimsomeDina ana swaga gani. Hii story imenifanya nilie mpaka staff wenzangu wanashangaa. Najaribu kuimagine, nimwache mwanangu? Nina mtoto ana miaka 2 tu, kila ikifika majira ya saa 12 jionikama sijafika nyumbani yeye anataka mlango usifungwe na anakaa nje kizingitini anaimba mamamamaaaa ataimba mpaka msichana wangu wa kazi ananipigia nakuniuliza kama nitachelewa maana dogo kagoma kuingia ndani. Pole sana Dina. Mama anauma sanaaaa. Mama yangu anaishi morogoro lakini jinsi anavyonijali mpaka najiona siwezi kumridhisha kabisa kama anataka kitu na nikishindwa kukitimiza.Pole sana, tena sana. Mungu yupona anasababu zake. Inshallah utapata mtu atakayekusahaulisha. I WILL ALWAYS LOVE MY DAUGHTER AND GIVE SWEET LOVE WHILE AM ALIVE!!!!!!!!!

  • Anonymous

   May 24, 2013 at 9:09 am

   do that as much as u've got all the time now…love n protect her na mama alot…nimempenda mwanao uyo

 118. Anonymous

  May 17, 2013 at 11:55 am

  Hi, mim huwa c mtu wa kucomment sana ila huwa nasoma sana hii blog, ila hii hadith imenigusa sana.Mim mama yangu alikufa nikiwa na umri wa miaka 14, nikaishi na baba na mama wa kambo, huyu mama hajawahi kuwa mtu mzuri kwangu na ni mama aliyekua na mambo ya kishirikina sana, watu wengi wanasema mambo hayo hamna ila omba mungu usiishi na mtu mwenye mambo hayo, ni mama ambaye amekua akinipiga vita kimaisha sana, yeye hataki kuniona nikiwa na furaha, amenigombanisha na ndugu za baba, yani nimepitia maisha mazito sana. Mwaka 2007 niliolewa na nna watoto mapacha ila ndoa haikudumu tulitengana, ila namshukuru mungu wanangu ndio ndugu zangu na marafiki zangu. Ila naamin hata ningepitia mambo magumu ningekuwa na mama yasingekua magumu kama yalivyokipindi hiki, kila ninalofanya watu wapo kuniangalia ili wanione naangua au nafanya mabaya kwa ubaya nilioenezewa kipindi ambacho nilikua nakua, huwezi amin baba yangu yupo hapa dar ila naweza nikakaa hata miezi mitatu hata simu sijampigia, huwa sijivunii kwenda nyumbani kwake kwani yule mama bado yupo na bado ananipiga vita, dah nna mambo mengi ila angalau nimeshare haya kidogo, kwani maisha bila mama kwa sisi watoto wa kike ni magumu sana.

  • Anonymous

   May 24, 2013 at 9:16 am

   pole sana mpenzi na zidi kujiweka wewe na uzao wako huo mikononi mwa Mungu,hakuna nguvu za kichawi wala uganga utaokushinda soma agano la kale kama wewe ni mkristo,dumu katika sala na maombezi utaishi kwa ushindi sana haijalishi watu wanaokuzunguka wanataka uanguke ww songa mbele (Bahatai bukuku song)..na usishindane nao hasilani ww fanya bidii kwa maendeleo yako na wanao.

   nakuelewa sana ata mie tulipitia umo uyo mama wa kambo ana ushirikina hatari adi ilifikia wakati tulipokua boarding na chuo tulikua hatuoni umaana na kurudi likizo kwa baba kwani uyu mama alikua soooo,sie tulikua ni kwa mama tu ila tulijipa moyo na Yesu wetu alikua upande wetu baba yetu tunampenda sana sana so tulikua tunaenda kwa roho ngumu tu KWA SABABU YA BABA TU mana alitulea vizuri sana na kutulinda dhidi ya uyo mkewe nyie acheni tu….ila now tushakua watu wazima na nyumba zetu na uyo mama wa kambo anatukodolea macho tu na hatujamchukia na uwa namsaidia matumizi mawili matatu na kudrop kumpa hi tukirudi dar

 119. Anonymous

  May 17, 2013 at 4:51 pm

  Dina yote hayo ni ya Mungu yeye ndo mpangaji, naamini iko siku utapata faraja tu na atakufanyia wepesi ktk maisha na maamuzi yako. Funga roho ukipata mume olewa mdogo wangu pata watoto ili uje uwape upendo wa dhati ili nawe uwe mama mkamilifu. ktk dunia kuna mashak mengi hata ukiondokewa na mzazi ktk umri mkubwa , mimi yamenikuta baba mam wamekufa nikiwa na miaka 35 lakin dada mkubwa anachotufanyia mpka leo hii ni kitendawili ni stori ndefu ntajaribu kushea na wewe kwa email ili uone na ujuwe mtandao wa mikasa na maisha kwani si mama wa kambo tu wanaonyanyasa hata ndugu tena mlitoka tumbe moja

 120. Anonymous

  May 18, 2013 at 4:19 am

  Mh habari yako Dina,katika blogs hata mi huwa nasoma na napita ila kwa hii nimeguswa na si mbaya japo nikatoa neno kidogo,washauri ni wengi ila endelea tu kujitunza na Mungu akujalie upate family yako ..si ungani na ushauri mmoja ulioupokea hapo juu kwamba UZAE TU BILA NDOA,mama utalia na kuongeza msiba mwingine kuwa you wish mama yako angekuwepo ndo utamkumbuka zaidi ..maana kulea peke yako si mchezo,furaha ya mtoto inakamilika pale anapokuwa na wazazi wake wawili ndo hata atakufuta machozi yakumkumbuka mama yako maana atakuwa kama rafiki yako wa karibu,wewe ni binti mzuri unayeopendwa hopeful yupo jamaa Mungu kakuandalia ili muwe family…nakushauri tena USITHUBUTU KUZAA tu utalia hata kama umejikamilisha kimaisha kuna areas bado zitakuletea ugumu zaidi,mi nina mtoto mmoja na mume wangu life inakuwa more easier mkiwa wawili,pole kwa kumpoteza mama ila Mungu alijua why! nakutakia maisha mema na ya baraka na Mungu azidi kukupa faraja itokayo kwake, Amen!

 121. Anonymous

  May 18, 2013 at 4:23 am

  mungu akutie faraja kuu

 122. Anonymous

  May 18, 2013 at 8:06 am

  Mungu akutie nguvu dada yangu na pia akuondolee hofu hiyo uliyonayo sasa ya kuanzisha familia. Endelea kumuomba Mungu sana na kama ulivyosema kwamba upo kwenye matibabu ya hofu hiyo basi naamini Mungu atafanya njia.
  I believe and hope few years from now, we'll hear wedding bells.
  Stay blessed.

 123. Anonymous

  May 18, 2013 at 8:29 pm

  pole sana ndg yangu.kiumri tumelingana ila napenda kukuchukulia kama dada angu mana unamambo mengi mazuri nnayoyapenda.Mungu ni mwema atakupa familia mpya itakayo kupa faraja ya ajabu katka maisha yako.Mume mwema na mtoto mzuri atakaye kutii na kukup faraja ktka maisha yako.Ubarikiwe dada angu,Love u

 124. Anonymous

  May 19, 2013 at 1:31 pm

  Hi Dina,pole sana nimesoma story yako nimesikitika sana nilikuwa bado nipo ofisini napitia blogs mbalimbali nakamkumbuka mtoto wangu nikaamua kuzima kompyuta na kurudi nyumbani kucheza na mwanangu ili angalau apate nafasi ya kuwa na mimi mama yange na kupata mapenzi yangu ningali mungu bado amnanipa nafasi ya kuishi hapa duniani.

 125. Anonymous

  May 19, 2013 at 7:32 pm

  mimgumu lakini leo dinah umeniliza,hadi nimekumbuka sometime ninavyo mjibu mama yangu ovyo,sitorudia tena nitamheshimu

 126. Anonymous

  May 20, 2013 at 5:46 am

  pole my dear. Kila kitu hapa dunia kina sababu yake. kumuombea tu apumnzike kwa amani

 127. Anonymous

  May 20, 2013 at 7:09 am

  ni kweli dear, mama ni mtu muhimu sana. namiss na muhitaji sana ila Mungu aliamua kumchukua japo nilikuwa darasa la saba ila niliumia na sijui nani ataondoa hayo maumivu yake. Mungu akutie moyo tuliendeleze gurudumu la maisha

 128. Anonymous

  May 20, 2013 at 10:26 am

  pole sana dina

 129. Anonymous

  May 20, 2013 at 11:09 am

  So touching my dear. Pole sana na mungu akupe nguvu.

 130. Anonymous

  May 20, 2013 at 12:07 pm

  Dina pole saana na mungu wa mbiguni aliye baba yetu akupe ujasiri.kwani na mimi mama yangu ametwaliwa siku ya jumapili ya pasaka tarehe 31 mwezi wa nne mwaka huu kwa ajali ya moto lakini namshukuru mungu kwa kuendelea kunipigania kila iitwapo leo bwana ametoa na bwana ametwaa jina la bwana libarikiwe,pumzika kwa amani mama yangu mzazi laurencia shillinde.

 131. Anonymous

  May 21, 2013 at 6:49 am

  Pole sana ndugu yangu Dina, leo nimelia machozi yani niko ofisini mara nikaingia kwenye blog yako ila hii story imenifanya nitoe machozi hata sipati maneno ya kukuambia ila mungu ni mwingi wa huruma mtumaini yeye tu na utapata haja ya moyo wako.

 132. Anonymous

  May 21, 2013 at 11:31 am

  pole sana Dinna. machozi yamenitoka jamani, asante kwa ku share story yako na sisi, kweli nitakuwa mama mzuri kwa watoto wangu, naomba Mungu atujalie wamama wote tuwalee watoto wetu kwa mapenzi yote.God bless you always

 133. Anonymous

  May 21, 2013 at 1:31 pm

  DINA my sweet dada ukipitia comment zote hizi utatambua jinsi gani watu wanakupenda sana mshukuru MUNGU kwa kila jambo,alikuwa na sababu zake maalum story nzuri na wote wamekutia moyo, my dear MUNGU ni mwema atabariki kila ufanyalo na utapata mume mzuriiii na utazaa motto wako na utamlea vizuri kama mama, mbona saizi unaishivizuri na unamama ambao wanakuangalia kama mama yako
  so much love usifikirie kwanini ilikuwa kwako
  nakupenda sasa dada dina
  mkami-katoro

 134. Anonymous

  May 21, 2013 at 1:44 pm

  Your mummy was beautiful, be proud of her pole sana nimeumia nimelia sana kazi ya mungu haina makosa, Mimi mama yangu amefariki miaka 3 iliyopita na ametuacha wakubwa tu mdogo wangu wa mwisho anafanya kazi tayari lakini nakuambia tukikutana tunalia siku zote kwa kumkumbuka hamna zaidi ya mama Naimagine nyie mlikuwa wadogo pole sana tena sana.

 135. Evelyn Msuya

  May 22, 2013 at 5:19 am

  Dina pole sana. mwenyezi mungu azidi kukutia nguvu. ujue Dina mama humuoni machoni lakini mama yuko nawe siku zote, ndio maana unapambana na maisha na uko kama hivyo ulivyo Dina!. La muhimu mkumbuke mama kwa kumuombea kila siku Dina , mama ni ngao yako na ujue yupo tuu karibu yako japo humuoni.NAKUPEDA DINA,

 136. jenifa

  May 22, 2013 at 9:43 am

  Very Touching. Hili limenifanya niandike kitu. Mungu akutangulie, najua atakufikisha.

 137. Anonymous

  May 23, 2013 at 9:01 am

  Dada Dina MUNGU akutie nguvu. Duniani hakuna raha wala utukufu, mwenye hili ana lile. Nimeisoma hii story yako nimejisikia vibaya sana. Imenifanya nikumbuke maisha ambayo tulilelewa sisi na mama yetu. 90% ya maisha yangu nimelelewa na mama sio kwamba baba yangu hakuwepo, sio kwamba baba yangu hakuwa na uwezo. Alikuwa ni mtu mwenye kipato cha kutosha lakini alitutelekeza kwa ajili ya kujifurahisha yeye na wanawake wa nje. Lakini MAMA yetu alipigania maisha yetu, alihahakikisha tunakula, tunaenda shule na mahitaji mengine tunapata kulingana na uwezo aliokuwa nao. Tulifunga ice cream, tulitengeneza visheti, tuliuza mbogamboga ili kupata nauli ya kwenda shule + matumizi mengine, ila yote hayo tuliyafanya tukisimamiwa na MAMA. Yaani wakati mwingine unawaza asingekuwepo mama, au angekata tamaa na kutuacha sijui leo tungekuwa wapi. Namshukuru MUNGU hatukuwa na tamaa ya kutamani maisha ya hali ya juu, tuliikubali hali ile na tuliweza kusoma mpaka leo kila mmoja anajitegemea. Baba yetu aliendelea kubadilisha wanawake hatimaye mungu alimchukua mwaka 2012 kwa ugonjwa wa HIV. MAMA ni muhimu sana kwenye maisha yetu ya kila siku, whether U like it or not.

 138. rena

  May 23, 2013 at 11:55 am

  me pia ni mmja wapo kiukwel cna kumbukumbu ya mama yangu alikufa nikiwa mdogo sana yaan ckumbuki chochote me nimelelewa na mama mwingine yuko fresh ingawa huwez kudeka au kufeel kama uko na mama yako huwa nataman mama yangu atokee hata mara moja nimuone,baba hakuwah kunanbia kuhusu mama mpka leo nina miaka 25,niliambiwa na majiran juu juu nikaenda kumuuliza shangaz akanambia stor yote ila nae hakunipa picha nimuone.rest in peace my mum emelensiana

 139. Anonymous

  May 23, 2013 at 12:10 pm

  pole dinna,hata me mama yangu alifalik nikiwa mdogo hata cmkumbuk wala picha yake cna me nimejikuta nalelewa na uncle huwez amin nilidhan ndo baba yangu na aunt niladhan ndo mama yangu walikua poa baadae baba angu akaja kunichukua alikua ameoa mke mwingine nae alikua poa ila ndo huwez kukidekeza au kufeel kama mama ndo mama yako nina miaka 25 wala baba hajawah kuniambia chochote na me naogopa kumuuliza.ila ikitokea naulizwa na wish kitu gan nitataman nimuone walau saa moja mama yangu. huwa namkumbuka sana though cna picha yake nina imagine tu ingawa picha zipo.rest in peace my sweet mum emelensiana

 140. Anonymous

  May 27, 2013 at 10:41 am

  pole, Sana Mwanangu Dina, maisha hayo wengi tumepitia, mama yangu aliriki miaka 31 iliyopita,tuliachwa watoto 5, miaka yangu ilikuwa 14 tu hakika kile kipindi sipendi kimkute yoyote duniani yalikuwa maisha mabaya sana kwangu kwani mimi ndiye nilikuwa mama wa wezangu imeniuma sana.japokuwa ni mimi ni mama wa kutosha lakini bado kuna gap kubwa juu ya mama natamani angekuwepo aone hata wajukuu zake, nimweleze hata makovu ya moyoni niliyopitia ee mungu wasaidie hatima wote. naona machozi yananitoka

 141. Anonymous

  May 31, 2013 at 1:43 pm

  Ooh, nalia kila iitwapo leo, the same story, nina miaka 34,sina baba,mama, kaka,dada,niliachwa mwaka 1, now home ni makaburi ya kinondoni,daily lazima nipite, nammiss mama yangu, nashindwa hata kuamini, sina mume wala mtoto, acha tu mdogo wangu maumivu yake anayejua ni Mungu tu,pole sana, umenifanya nianze kulia upya

 142. Anonymous

  May 31, 2013 at 2:06 pm

  oooh pole sana dina imenigusa umenifanya nilie nakupenda sana

 143. Anonymous

  June 4, 2013 at 7:02 am

  Yani kwa kweli Mungu na azidi kukutia nguvu mpenzi, mimi nilipoteza baba nikiwa darasa la saba,maisha yalikuwa magumu mno kwa sababu baba ndo alikuwa provider, Ila HATUKUWAHI kupungukiwa na UPENDO na furaha mana mama alikuwepo, tulilala na njaa sana ila mama yetu alitengeneza mazingira ya kutufanya tucheke na wala tusifikirie machungu yanayotuzunguka, kwa kweli i cant imagin yale maisha bila mama.
  Nazidi kukutia moyo, endelea na ujasiri huo,nakuombea upate mume mwenye upendo atakayekupa furaha kwa kadri anavyoweza,pia pata familia yako upendo utakaopata kwa watoto wako utajaza ile sehemu unayoona iko wazi.Barikiwa sana mamy

 144. Brenda

  June 5, 2013 at 12:35 pm

  I am touched by your life story! Mwenyezi akulinde na ukupe faraja na kila ushikacho kigeuke kuwa dhahabu (ufanikiwe) ….Amen!

 145. Anonymous

  January 29, 2014 at 12:59 pm

  poleni

 146. Anonymous

  January 29, 2014 at 1:07 pm

  so sad stories, jamani mpaka nimefil like crying. poleni sana waathirika wa kukosa mama, i thank God mama yangu yupo i love her so much na mimi ni lastborn kwetu married with 2 boys, ila uchungu wa mzazi naujua sbb nilifiwa pia na baba yangu 2002 mwaka nilioolewa pia, niliumia sana but unakubali tu kuwa sasa tutalelewa na mzazi mmoja. MAY GOD REST THEIR SOULS IN INTERNAL PEACE, AMEN

 147. Anonymous

  January 31, 2014 at 11:53 am

  Dear Dina nimesoma comment nyingi saaana za watu kwa uelewa wangu nimegundua wengi ni wanawake lakini nimeamua kukuandikia tu. Mimi ni mwanaume lakini kunakitu umekiandika kimenigusa saaana wanaume wengi tunamatatizo saaana haswa ya kisaikolojia na tunapambana nayo wenyewe kwa uwezo wako wa kuandika kwamba upo kwenye matibabu ya hofu ya ndoa umenigusa saaana KWASASA MIMI NATAMAN SAANA KUOA LAKINI NAOGOPA UKINIULIZA NINACHOKIOGOPA HATA SIJUIIIII lakini umenisaidia kuangalia effect ya familia ktk maisha yangu…… nimelelewa katika familia isiyokuwa na mapenzi sikuwahi kabisa kuamini kama kunawatu wanapendana kwa moyo wa kweli nimelibeba hilo saaana lakini nikiwaaambia ndugu zangu pale wanaponiuliza kwanini uoi nilikua nawaaambia siamini kama tunaweza kuishi na huyu binti milele so kimekua kikinisumbua saaana lakini i hope unaweza kuniunganisha na mwana saikolojia nikaaanza maisha mapya manake maisha yangu hayaendi yameshikiliwa na hofu

 148. Anonymous

  February 3, 2014 at 8:03 am

  my dear mie ndio nasoma leo story yako, kwa kweli imenigusa sana na mie pia nimepita huko maisha bila mama ni magumu hata kama alikua ni masikini bado ni mama na yupo hai. pole sana mamy. hii story imenikumbusha mbali sana.
  Mungu ni mwema sana (zaburi 32:8) ….amen!

 149. Anonymous

  February 4, 2014 at 8:56 am

  Maisha ya mama wa kambo ni mabaya yanakuwekea maumivu ambayo hayafutiki kwa kweli mimi nimeolewa na watoto 2 lakini bado huwa nalia naumia mnoo namuomba mungu kila siku anijalie umri mama yangu yu hai lakini bibi mzaa mama na baba walikuwa wameshafariki so step bibi mzaa mama alikataa mama kurudi home na sisi.. wakati mwingine natamani bibi zangu wangekuwa hai labda tungelelewa nao. ila nashukuru mungu kila likizo tulisafiri kwa mama na alikuwa akituambia VUMILIENI WANANGU MTAKUWA YATAKWISHA. Naandika hapa machozi yanatoka … aaah maisha bila mapenzi ya mamaa

  • Anonymous

   February 23, 2014 at 9:15 am

   Hi Dina hongera kwa mtoto ndio atakuwa chanzo cha furaha yako na kusahau yote. May God make ur man love u most .Amen

 150. Lydious

  February 14, 2014 at 2:07 pm

  Pole sana my dia dada, ckuwahi soma story hii. Mtumaini bwana kwa moyo wako wote wala usizitegemee akili zako mwenyewe… Katika shida, changamoto na maaribu yote upitiayo Mkiri yy naye atayanyoosha mapito yako… Farijika daima na maneno haya

 151. Anonymous

  February 20, 2014 at 9:41 am

  pole sana Dina mungu ni mwema kwako hawezi kukuacha kamwe

 152. Anonymous

  February 22, 2014 at 8:26 am

  pole sana jamani mimi bado Mama yangu yupo na nina watoto 4 kwakweli sitaki kuimagine their life without me, I love you so much mom, Mungu akupe uhai mrefu umtunze Zion mpaka uone wajukuu wake

 153. Anonymous

  February 26, 2014 at 1:38 pm

  Dina pole sana, ingawa nimechelewa ila ujumbe wako umenigusa sana, yani hapa nasoma natetemeka nami nimempoteza mama miaka miwili sasa kwa kweli kila kukicha nintamanki sana angekuwepo kwa sababu familia yetu upande wa baba hakuna maelewano na walikuwa hawampndi mama kwa hiyo na sisi tuliwachukia kwa hiyo ndugu yeyote wa baba akikwambia kitu hata kama ni kizuri unamuona adui yako na anataka kukuangamiza kwa kweli mm kila siku naumia na nimebahatika kuingia kwenye ndoa kwa sasa ni mjamzito sina mama wala mama mkwe na ujauzito ulivyo na changamoto nyingi cjui hata nanki wa kunisaidia ushauri wakati mwingine mpaka nasema yawezekana na mm nikawa mmoja wanaokufa wakijifungua. ila wakati mwingine nasema ni mawazo ya kishetani na ninayakataa. Hapa nilipo naamini kwa uwezo wa Mungu safari nitaimaliza salama ingawa mpaka sasa natgema ushauri wa dokta wangu tu maana sina hata ndugu wa kunishauri kwetu mimi ndo mkubwa na simuamin ndugu yeyote wa baba. Kwa kweli mama ni kitu muhimu sana duniani.

 154. Anonymous

  March 21, 2014 at 1:00 pm

  dada dina kiukweli umeniliza nilikuwa sijasoma wala sijawahi kuingia katika blog yako ingawa nakupenda sana, kwanza hongera kwa kupata mtoto, pia hongera kupat familia ya mchumba wako imeonyesha kukupenda sana, pole kwa kukosa mama, mimi niko kama wewe, nilizaliwa mwaka 1989 siku niliyozaliwa na mama alifariki dakika chache hivyo mpaka leo simfahamu na hakuna hata ndugu mmoja ninayemfahamu licha ya kufutilia sana na kuzunguka karibia Uganda nzima kutafuta ndugu ikawa ngumu, kwa kifupi tuu ni msichana niliyelelewa kituo cha watoto yatima msimbazi na baadae baba alinichukuwa nikapelekwa kwa mama wa kambo kule kulikuwa na ndugu zangu wengine wa 4, kwa kweli maisha yale sitaki kuyakumbuka na wala sitapenda mtu yeyote ayapitie, dada Dina nimeteseka mimi na kwa kuwa baba yangu alikuwa mtu mkubwa sana Katika serikali hii lakini mama hakumruhusu kunipa hata hela ya shule na hata kunipeleka shule baba naye alikubali, nikawa nyumbani nilivyokuwa na miaka 16 utadhania nina miaka 50 nilivyozeeka, sikuwa na hela hata ya kufanya chochote, kiukweli ikanibidi kujiingiza kwenye mapenzi nikiwa mdogo ili nipate hela hata ya kujikimu, bahati nzuri Mungu akanisaidia nilipata Mume wa mtu najua ni dhambi lakini sikuwa na jinsi, mke wake hakuwa mtu mwenye kauli nzuri, nilivyojua hvy mimi nilinyenyekea kwake sana na alikuwa nafanya kazi BOT aliniuliza ninahitaji nini nilimwambia kusoma nashukuru alinisomesha kuanzia kidato cha kwanza hadi cha sita kwa kurushwa rusha na nilisomea Uganda maeneo ya Nsangi, wakati nakaribia kumaliza mitihani ya form six yule baba alifariki kwa ajali, ila Mungu ni mwema nikapata nafasi ya kuingia chuo lakini sikuwa na hela. Nikarudi huku nikakuta nimetayarishiwa mchumba mkurya anioe kwakweli sikupenda ila nililazimishwa sana taratibu zinaendelea na sikuwa na pa kukatalia, ila yule kaka alinitesa sana kwa jinsi alivyokuwa anafanya na hata nikisema naambiwa nivumilie atapoa tuu, nilimlilia Mungu sana na Mungu alisikia maombi yangu ilibaki week mbili tufunge ndoa yule kaka alinivunja mguuhapo nikapata la kujitetea, ndoa ikavunjikia hapo, nilivyopona mguu nilifukuzwa nyumbani kwakuwa niliwatia aibu kwa kukataa kuolewa, nilihangaika sana sana na hii dunia, kuna siku nilipata kijipesa tuu nikasema leo na mimi niende kutembea sea cliff hotel kwa kweli ile naingia tuu pale getini nilikutana na mkaka ni raia wa Nowray alinipokea utadhania mimi ni mgeni wake, kwa kweli kwa muda mfupi nilitoa kilio pale hotelini haijawahi kutokea nilijaliwa na watu nilieleza matatizo yangu na kila kitu na mguu haukuwa umeunga vizuri, pale pale yule kaka alinitamkia nitakuoa na utaishi kwa raha, nikijiangalia sina shepu ya kuolewa na mzungu maana mimi ni mnene nikafunga mdomo, ni story ndefu sana ngoja niiishie hapana. kuna siku karibia na christmass ya mwaka jana nilikuja hapo cloud kuonana na Dr. Maro kuomba anifanyie kipindi maana ninamaisha ya kufundisha wadada wenzangu ingawa sasa mimi ni mama ila Dr. Maro alikuwa anasafiri na sikurudi tena. lakini manyanyaso ya mama wa kambo yamenipeleka kunifanya niwe mke wa mzungu na nina ishi maisha mazuri sana tena sana na sasa nina watoto pacha wakike nina kama week mbili toka nimejifungua na nikipata nguvu nitarudi kusoma. ila niliwasamehe wale wote walionifikisha hapa. Dina mimi nakutakia Maisha mema na uwe mama bora. nakupenda Dina

 155. Anonymous

  May 8, 2014 at 8:37 pm

  Pole dada yangu kwa kufiwa na mama yako tangu ukiwa mchanga, Mapenzi ya Mungu yatimizwe. Sikuwahi dada yangu kufikiri kwa uchangamfu na upendo ulio nao kwa watoto yatima kama wewe unaishi bila mama! Uchungu umenifanya nilie lakini nina imani kuwa Mungu amekupigania na ataendelea kukupigania mpaka mwisho! Nakuombea maisha mema na yenye mafanikio Mungu akubariki na kukupa nguvu na uvumilivu katika kukabili changamoto unazopata kwa kukukosa malezi ya Mama mtu wa muhimu sana! Tuko pamoja dada yangu!

 156. Pingback: WAPENZI WANGU HAPPY NEW YEAR 2014. – Dina Marios Blog

Leave a Reply