Uncategorized

MSHINDI WA DINNER WITH DINA CELEBRATING DINA

By  | 
“DINNER   WITH  DINA  CELEBRATING  DINA”
Kwanza Mpendwa wangu nianze kwa kukupongeza kwa juhudi nyingi
unazofanya hadi kufikia mafanikio makubwa! Kiukweli nimekuwa shabiki wako au
rafiki yako wa muda mrefu bila wewe kujua na vilevile kunifahamu, lakini leo
nikasema hata kama sitapata bahati ya kusherehekea na wewe lakini acha nitumie
nafasi hii kukupongeza na kukueleza mawili matatu ambayo nina imani yatazidi
kukuletea mafanikio maana huu ni mwanzo na bado safari ni ndefu Mamy!.
Ni muda mrefu sasa nimekuwa nikipitia blog yako kila siku
iendayo kwa Mungu na wakati mwingine kuchukia na kusema jamani Dina mbona
anachelewa kuaupdate blog. Kwakweli nimepata habari nyingi ambazo nilikuwa sizifahamu
na kujifunza mengi kupitia blog yako Dina. Kwanza toka nianze kupitia blog hii nimekuwa
nikipata habari nyingi sana na kujifunza mengi sana ambayo nilikuwa siyafahamu
kwa mfano tu ni hii issue ya ‘Mwanamakuka’ kiukweli na kusoma kwangu kote
sikuwahi kusikia wala kufahamu lolote kuhusiana na Mwanamakuka! Lakini kupitia
blog yako nilifahamu hilo. Imenisaidia kufahamu mambo mabalimbali ya kijamii yanayotokea
ndani  na nje ya nchi.
Kiukweli Dina blogu yako imebadili maisha yangu na hata mitazamo
yangu. Kama mwanamke inanitia moyo sana blogu yako kuwa nisikate tama na kila kitu
kinawezekana na Mwanamke hatakiwii kukataa tama, kuna vitu vingi sana
nimejaribu kuvifanya na kufanikiwa lakini ni baada ya kuona au kusikia kupitia
blogu yako.
Nimejifunza mengi sana kwenye mahusiano na hata ndoa yangu
maana kupitia blogu yako  niliguswa sana
na ikabidi nami kuanza kuhudhuria ‘Kitchen Party Gala’ ambayo kwa asilimmia
kubwa imebadilisha ndoa yangu nakumbuka ile iliyofanyika Danken House, aunt
Sadaka alielezea vizuri sana kuwa wanaume wakoje kisaikolojia nikayafwata
yamenisaidia maana sishindani tena na mme wangu. Nimeweza kuwaelewa wanaume ni
watu wa namna gani,alinifurahisha kusema kuwa wanaume ni watu ambao wanapenda
kubembelezwa na kunyenyekewa!.
Nimekuwa mrembo kupitia blogu yako Dina, kwa wale
wanafunzi  wenzangu wa Tumaini Mass Com
Everning wataamini ninalosema maana nimechange sana kwa upande wa mavazi mpaka
make up za usoni, wananishangaa! maana naona unavyozungumziaga urembo na hata
picha unazoweka za matukio mbalimbali naona wanawake wanavyopendeza nami
nikaona nisibaki nyuma.
Amini usiamini Dina wewe ndio ulionifanya nipende movie na
kutumia kuangalia movie muda wangu wa ziada badala ya kwenda bar kunywa bia
mpaka ulivyoweka ile movie ya ‘The
Words’
nilienda kuitafuta na nikaipata lakini bahati mbaya nilipoenda kuiangalia
nikakuta haitoi sauti. Nisikuchoshe Mamy acha haya  yanatosha ingawa ni mengi sana dina nimeyapata
kupitia blog yako hata Mungu wangu ni shahidi kwa hayo niliyoyaandika.
Asante Sana!
Nakutakia kila la kheri.
Mimi naitwa Edith!
 Hello Edith
 hongera umepata nafasi ya kuwa miongoni mwa wale watakaoshiriki dinner with Dina.Pia nashukuru kwa email yako nzuri na imenipa nguvu na faraja kuwa kuna mtu sehemu ambae ni wewe nimeyagusa maisha yake.Tuombeane uzima na afya tele ili wote tuweze kutimiza ndoto na malengo yetu.Kuhusu filamu ya words pole kwa kupata yenye quality mbaya.Ntakuazima ya kwangu ukishaitazama utanirejeshea my dear nina namba yako tutawasilina.
Asante sana
Dina Marios! 

1 Comment

  1. MOJAONE

    June 1, 2013 at 9:08 am

    Na mimi??

Leave a Reply