Uncategorized

MTWARA SIO SALAMA

By  | 
Baada ya Waziri
wa Nishat ikusoma hotuba yake.Mwishoni
amesema bomba la gesi linajengwa kutoka Mtwara kwenda Dar hapo ndio vurugu zilipoanza.

Huko MIKINDANI ofisi zote za serikali zavamiwa na kuchomwa na mpaka daraja
la Mikindani nalo limevunjwa kwa maana hauwezi kutoka wala kuingia MTWARA 

 • Kuna madai kwamba silaha zimeibiwa (Haijathibitishwa) 
 • Maaskari wanafanya msako wa nyumba hadi nyumba maeneo ya Magomeni na Mangowela
 • Askari achomwa mshale. Haijulikani hali yake
 • Ni
  mapambano baina ya vijana na maaskari. Vijana hawaogopi tena risasi
  wala mabomu . Kundi limeelekea Shangani kwenye nyumba za vigogo.
 •  Nyumba ya kupumzikia wageni inayoitwa Shengena Lodge imechomwa moto kwa kile kinachoelezwa kwamba iliwapokea askari Polisi.
 • Ofisi ya CCM saba saba imechomwa moto, na baadhi ya waandishi wamezingirwa maeneo ya Sokoni, sasa ni milio ya risasi na mabomu.
 • Matairi 
  kila  kona  ya mji  yamechomwa  barabarani  polisi  na  zimamoto  
  wanafanya kazi ya kuzima na kufukuza wananchi. Kauli mbiu “Gesi haitoki hata kwa bomba la peni”
 • Kambi ya Upinzani yaukataa mpango wa serikali wa ujenzi wa bomba la gesi
 • Nyumba kadhaa  za watumishi  wa Serikali  zimechomwa  maeneo ya Shangani.(habari haijathibitishwa rasmi)
 • Ni magari ya FFU tu ndio yapo barabarani nayo hupata wakati mgumu
  kupita kwasababu ya mawe na magogo yaliyowekwa na vijana,baadhi ya watu
  kadhaa wamechukuliwa na askari eti kwakuwa walipita jirani na gari
  yao,askari wengi waliokuja si wa hapa Mtwara wengi wametoka Masasi na
  Lindi. Ving’ora vinalia ovyo ovyo.
 • watoto wamefungiwa mashuleni walimu wamekimbia
 •  Mabomu yanapigwa mfululizo maeneo ya Magomeni-Mtwara . Takriban mabomu 20 na ushee mpaka sasa. Na wanaendelea kupiga mabomu.
 • Sasa
  hali si shwari kila eneo, wakionekana watu watatu wanaongea maongezi
  maaskari wanapiga mabomu. Mabavu yamechukua mkondo wake. Wananchi
  wamejifungia majumbani mwao. Chuki dhidi ya Polisi yaimarika. Polisi
  wanapiga mabomu bila mwelekeo.
 • Magomeni na sokoni kimenuka, mabomu yanarushwa na wananchi wanakimbia ovyo.
 • Kituo 
  kimoja  cha habari  kinachorusha habari za bunge chazuia mawimbi yake
  kwa Mkoa wa Mtwara hivyo hakisikiki(Redio na TV). Na kimewanyima haki
  wananchi wa Mtwara ya kupata taarifa.(Hatimaye wamerejesha matangazo
  yao)
 • Maduka
  yote yamefungwa, baa zimefungwa, hakuna huduma za usafiri, ofisi za
  serikali zimepwaya kimsingi hakuna lolote linalofanyika
 • Boda boda zinazoonekana maeneo ya Nkanaledi na abiria zinapigwa mawe.
 • Makachero nao wanajifanya madereva wa boda boda na Bajaji, Tax wengine wanatembea na magari ya Serikali.
 • Maeneo yote yametawaliwa na ukimya.
Habari kwa hisani ya www.mtwarakumekucha.blogspot.com

8 Comments

 1. ELIUD SAMWEL

  May 22, 2013 at 10:37 pm

  Mi naona kuna umuhimu wa serikali kuwashilikisha wananchi kabla ya kufanya maamuzi hasa kwenye mambo kama haya.nazani ndo njia pekee na salama.

 2. Anonymous

  May 23, 2013 at 8:08 am

  Ndugu zangu, watanzania wenzangu, huu si uungwana.. mbona wote tu wamoja..kuna mambo ya msing sana kupigania.. sio gesi kuja Dar..

 3. Anonymous

  May 24, 2013 at 8:25 am

  NDIO SERIKALI YENU YA CCM IYO,KILA MTU KWAO NI MCHUNGU,UKIHOJI NA KUULIZA UNAITWA MCHOCHEZI,UKIPITA KITAA UNAKAMATWA NA UNAZUSHIWA KESI ZA KISHENZI,UKIITISHA MKUTANO WEE GAIDI,UKIKOMENTI KTK INTERNET UNAFATILIWA ULIPO KUHOJIWA,UKIWAKOSOA WATAWALA WA CCM UNANG'OLEWA KUCHA NA MENO BILA GANZI,WANAINCHI TUNA AKILI NA TUNAONA KILA UOVU NA UFISADI WA HII SERIKALI DHALIMU NA IPO SIKU ATA KAMA MIAKA 20 MEBLE WATATOKA TU HAWA NA TUTAWAFILISI…NA WANAMTWARA WAPOE KWANZA ILA HII CHUKI HAITAFUTIKA MILELE POLISI NI CCM NAONA NA JESHI NALO LINAINGIA KTK SIASA NGOJA TUONE

 4. Anonymous

  May 24, 2013 at 1:17 pm

  Hii nimeikuta kwenye mtandao wa Jamii Forums, inakuhusu wewe Dina na Shamim Mwasha. HUPASWI KUKAA KIMYA KWA SABABU INAKUCHAFUA SANA , NA SISI MASHABIKI NA WANAWAKE WENZAKO TUMEKUTETEA SANA TUMNESHINDWA…. POLE SANA KWA HILO COZ LIMEANZA KUTAPAKAA MITANDAONI.

  Dina marios na shamim mwasha wanasagana?

  Tetesi kutoka kwa vyanzo vya kuaminika zinasema, wanadada Shamim Mwashi wa 8020 FASHIONS BLOG na Dina Marios wa Clouds Fm wana uhusiano wa mapenzi ya jinsia moja. Tetesi hizi zimekuwa za muda mrefu sana. Kama ni kweli basi maadili ya wanawake wa kitanzania yatakuwa yameshuka sana. NITAFURAHI SANA KAMA TETESI HIZI ZITAKUWA SIO ZA UKWELI

  CHANZO : https://www.jamiiforums.com/celebrities-forum/454672-dina-mariois-na-shamim-mwasha-wana-uhusiano-gani-3.html

  • dinamariesblog

   May 27, 2013 at 12:45 pm

   hahahahahah duuuuh,anyways siwezi kushangaa binadamu wanamengi sana ya kutunga ya uongo na uzushi ili kumshusha mtu fulani.Sijihusishi na mapenzi ya jinsia moja my dear.Sikuhizi kashfa wameona ni kumuita mtu msagaji au gay!!!??.Sifanyi mambo hayo.Sitashangaa kesho wakiniita mchawi lol

 5. Anonymous

  May 25, 2013 at 10:41 am

  Mambo Dina,jamani nimeona jamii forum kuna topic ya kwamba wewe na shamimu mwasha mnasagana,yani watu wamewashambulia sana sasa sisi mashabiki wako tunabaki njia panda kujua ukweli wa jambo hili embu tujuze jamani,naskia ndo sababu iliyopelekea shamini kuachika.

  • dinamariesblog

   May 27, 2013 at 12:46 pm

   hahahahahah duuuuh,anyways siwezi kushangaa binadamu wanamengi sana ya kutunga ya uongo na uzushi ili kumshusha mtu fulani.Sijihusishi na mapenzi ya jinsia moja my dear.Sikuhizi kashfa wameona ni kumuita mtu msagaji au gay!!!??.Sifanyi mambo hayo.Sitashangaa kesho wakiniita mchawi lol

 6. RUKY

  May 27, 2013 at 1:49 pm

  JAMANIIII HIVI WATU WANAFIKIRIAGA NINI KUWAZUSHIA WENZAO VITU VYA AJABU. HIVYO…..MH USIJALI DINA HUU NDIYO GARAMA YA UMAARU AS LONG FANS WAKO TUNA KUKUBALI KWA UTULIVU WAKO DONT WORRY..LOVE U….

Leave a Reply