Uncategorized

NAMNA MONIQUE ALIVYOPUNGUA UZITO!

By  | 
Kwa miaka mingi nimekuwa shabiki wa Monique, Monique Angela Hicks msanii wa filamu na comedy wa Marekani.Baadae nikaanza kumfatilia na talk show yake ya the Mo’Nique show ambayo sikuipenda hakunifurahisha kwa kweli.Nampenda kama muigizaji na comedian baasi.
Kwa miaka yote namfatilia kama mwanamke mnene kweli kweli ikawa kama identity yake.Toka kwenye vichekesho vya the parkers kwa wale mnaovikumbuka alikuwa kibonge.
 Amecheza movies kibao niipendayo zaidi hizi ya Phat girls,Welcome Home Roscoe Jenkins,Two Can Play That Game,Precious filamu iliyompa tuzo nyingi sana mwaka 2009 na zingine kibao.
 Monique akiwa na mumewe Sidney Hicks ambae wamefahamiana toka wadogo wakiwa na miaka 14.Kabla alikuwa ameolewa alipoachika ndio akaoana na Hicks.Ndoa ambayo wao wanaiita open marriage ‘hakuna siri’
Ikitokea umeona mtu mmetamaniana hakuna siri hata kama mmefaya tendo ukweli mezani maisha yanaendelea.Hakuna kuachana kisa mmoja ametembea na mtu nje ya ndoa duhhh!

Kwa muda sijamuona kwenye movies au popote hata talk show yake ilisimamishwa BET.Na mara ya mwisho kumuona alikuwa kapungua kiasi kutoka ule unene wake wa zamani.

Majuzi zimetoka picha zake akiwa kapungua sanaa hata ningeulizwa ni nani nisingemtambua.Sijui kwa nini nilikuwa nampenda alipopungua kidogo tu.Siri yake kubwa ni kula vizuri kwa afya na mazoezi ya nguvu.

11 Comments

 1. Anonymous

  May 22, 2013 at 1:10 pm

  Natamani ingekua rahisi hivyo kupungua dada Dina sisemi inashindikana lakini kwa mtu ambae hajawahi kuwa mnene kusema eti mazoezi na kula vizuri ndo kumemfanya monique apungue is an insult kwa mtu anae struggle kujaribu kupungua. #mtazamo wangu

 2. Anonymous

  May 22, 2013 at 3:41 pm

  Mi nashangaa watu wanaolalamikia unene ….kwani wakati unaanza kunenepa hujioni?!Mtu Anafika kilo 80 au 100 Ndio anaanza kushtuka utathani zile kilo alizipata siku moja ….si zungumzii wale ambao toka wako watoto ni wanene….Mimi binafsi toka niko A level nilikua muoga wa unene nilikua na kilo58 lakini nilishaanza kuogopa nikawa najianga jinsi ya ulaji wangu mpaka Leo Nina miaka 30 na watoto 2 na Nina kilo 55 najiangalia jinsi ninavyo kula na sikwamba Mimi sio Mtu wakunenepa nilishawahi kufika kilo60 nami ni Mtu mrefu na kimo cha 5 kwa 8….jamani watu jitazam eni mapema Mtu ukishajiona unakilo kuanzia 60 anza kua muangalifu majuto ni mjukuuu

 3. Anonymous

  May 22, 2013 at 4:41 pm

  Ehe wewe nawe sasa ulitaka uambiwe nini kimempunguza!!.mawazo yenu ya kijinga ya operation..'Kaza buti.piga tizi..acha zege kula vizuri uone..we bwege uliyecoment hapo juu

 4. emma kahere

  May 23, 2013 at 1:19 pm

  Yan huyu dada amenitia moyo sana,wacha namim nkazane mazoez majibu ntawapa hapahapa kwenye blog.,halafu dina mbona umeacha ku2wekea diet kama zamani?,pliz do it dear

 5. Anonymous

  May 24, 2013 at 12:51 am

  Kila kitu ukifanya kwa nia ya dhat kabisa inawezekana,ugumu kwetu ni kwamba majukumu huchukua muda mwingi sana,wenzetu kutokana na life style yao na anapoamua kustick kwenye jambo moja wanahakikisha mpaka wanalifanikisha,tatizo kwetu huku na unapokuwa mfanyakaz bas shida tu,asbh unajiandaa kwenda job saa 11 kuepuka msongamano wakat unarud unakutana tena na msongamano ukifika hm unakutana na majukumu mengine muda kwako huwa hafifu on weekend kuna harakat za kufua na kutembelea ndugu jamaa na marafik all in all kama unaamua kwa dhat kabisa na kuweka akil na nguvu zako kwenye mazoez hakika inawezekana kabisa

 6. Anonymous

  May 24, 2013 at 8:51 am

  Monique alikuwa na high blood pressure ndy chanzo cha yeye kupungua. Nakumbuka Mara nyingi kwenye show zake alikuwa anawasema Sana watu wembamba. Naona sasa unene kaona siyo issue.

 7. Anonymous

  May 25, 2013 at 1:31 am

  Hakuna any type hapo of insult nakubali kabisa. I used to weigh280lbs, nikaanza taratibu vitu vya sukari na wanga na kutembea jioni kidogo kidogo. Nikaanza kula vyakula either grilled, baked ama boiled na mazoezi nikajiandikisha gym kabisa. Maji kwa wingi na so far nimpe punguza 50 lbs. It wasn't easy and I fell of the wagon so many times ila ni kufanya maamuzi tu juu ya maisha yako. Mimi ni mama wa watoto wawili wadogo and to say the least I am doing this for them kwasababu I want to live long enough to see my grand kids. You are what you eat, change that and you see the difference. So inawezekana sana sio l lazima ufanyiwe upasuaji.

 8. Anonymous

  May 27, 2013 at 12:16 am

  hivi huyo mwenzako hapo juu kwa nini hakubali kula vizuri na mazoezi kunakufanya upungue??? mbona mimi nilikuwa bonge sana na nilipoanza tu mazoezi na kula kula vizuri na kuwatch potion ninazokula nilipungua sna tu

 9. Anonymous

  June 4, 2013 at 7:16 am

  jamani mimi sina ubonge wa kutisha ila tumbo, please msaada kwenye tuta, nimapata watoto wangu wawili kwa njia ya operation, huyu mdogo ana miezi saba, nimeongezeka kg kama tano ivi tangu nijifungue sasa nimefanikiwa kupunguza kg 3 kwa sasa nina kg 72,kinachonitesa ni tumbo nimeshafunga mikanda weeee sit ups nyingii naona limelegea mno na kujikata mara tatu..please kama kuna mtu anaweza kunisaidia kwa mawazo, ama chochote kile nitumie mail kwa adress hii,rwakye@yahoo.com AHSANTENI

 10. Anonymous

  June 6, 2013 at 7:30 pm

  mi pia ni mpenzi mkubwa wa Monique…ila kiukweli cjafurahishwa na alivyopungua… alipindeza san akiwa na umbo lake la unene….but kapendeza…Big Up to her

 11. Anonymous

  June 8, 2013 at 4:25 pm

  unene unatutesa ila bas tuu

Leave a Reply