Uncategorized

PICHA ZA MWISHO ZA KITCHEN PARTY GALA!

By  | 
Mama Victor yeye ni mwalimu wa mafunzo ya ndoa kidini zaidi na alitoa somo lake.Kwa nini mwanamke anaweza kupoteza kujiamini?pengine alikuwa akijiamini saana lakini akajeruhiwa njiani kama tyre ilopata pancha!Au hajawahi kujiamini kabisa toka amekuwa sababu ya malezi nyumbani.

 Getrude alitupa somo la me,myself, and i
Sababu mojawapo inayofanya wasichana na wanawake wengi kutojiamini ni pamoja na malezi.Akatupa story yake vile yeye alizaliwa baada ya mama yake kupata mimba shuleni.Akalelewa na bibi.Baba akaja kuoa mwanamke mwingine na mama akaja kuolewa kwingine na yeye kuendelea kulelewa na bibi.Akawa akiwatembelewa wazazi wake wote kwenye ndoa zao na yeye kubali kama stranger kwao mtoto wa nje ya ndoa.Akajihisi hana thamani akabaguliwa muda mwingi alikuwa akilia.Kwa bibi hakukua na maisha mazuri lakini wazazi wake walikuwa na maisha mazuri.Lakini alitumia mbinu zipi mpaka kufika kuwa hapo alipo?akashare nasi.

Nawashukuru wadada wamama wote waliokuja.
Kitchen party gala ipo maalum kukumbushana na kujuzana yale yanayotupa changamoto katika maisha yetu ya kila siku.Kwenye mahusiano,ndoa na sisi wenyewe ndani yetu kama wasichana na wanawake kwa ujumla.Ila mafunzo haya yanakuwa katika mfumo wa kiburudani ili yasichoshe.Ndio maana tunacheza,tunakuwa na wasanii na walimu kutoa somo.Tunajua hatuwezi kutatua matatizo yote lakini kupanua mawazo etu kwa ujumla.
Sisi theme yetu si yakutoa mafunzo ya ujasiriamali kama wengine ambavyo mnashauri kwenye maoni.Semina za ujasiriamali zipo watu wengi wanafanya na kufundisha na kina mama wanahudhuria huko.Hatuwezi wote kufanya hicho hicho tupeane mawazo kwenye hii tuongeze nini  na tupunguze nini kwa wale waliofika na ambao haujafika.Mapungufu yalikuwepo lakini siyamakusudi na hakuna wa kumlaumu.Tunafanya kila mbinu kutokomeza hilo.
(sura zilivyochoka kwa vurugu za siku hiyo ni noma)
Kwa niaba ya mkurugenzi wangu Vida Mndolwa tunawashukuru sana wadhamini wote,blogs zote zilizotupa ushirikiano na wote mliohudhuria kwa ujumla mtusamehe kwa mapungufu tutajitahidi kutokomeza japo hatuahidi kiwa sawa kwa kila jambo maana sisi ni binadamu.
Mpaka wakati mwingine kukiwa na jipya tutawafahamisha.

siku za usoni nitaweka videos hapa.

Leave a Reply