Uncategorized

TAARIFA ZAIDI KUTOKA AFIKA KUSINI ZA KIFO CHA MSANII NGWEAR

By  | 
Nje ya mochwari ya Serikali Hillbrow
Johannesburg ulikohamishiwa mwili wa Ngwea.Picha za chini  ni Watanzania wakiongozwa na
Kinje Ngomale Mwiru wakitazama sample ya majeneza mbalimbali ili wajue
la kununua, hapa walikua na mfanyabiashara wa kampuni ambayo pia huwa
inashughulika na kusafirisha miili ambapo gharama yake ni zaidi ya
milioni nne na nusu
Wakikagua sample ya jeneza 
Watanzania waishio Afrika ya Kusini walipokutana juu ya msiba wa Albert Mangwea.Kifo cha Ngwear kimetokea juzi nchini humo baada ya kukutwa chumbani kwake akiwa tayari amefariki na msanii mwenzaki M to the P akiwa hajitambui.
 Millard Ayo akifanya interview na promota
Mtanzania ambae alikua tayari na kazi ya show tatu za ziada ya Ngwea
kabla hajafariki, zilipangwa kufanyika siku kadhaa zijazo.…
 Mwili wa marehemu Ngwair bado upo mochwari ya Serikali Hillbrow
Johannesburg
na leo ndio unafanyiwa uchunguzi ili kujua nini sababu za kifo chake.Pia taratibu za kuuleta mwili Tanzania ziweze kuendelea.

R.I.P Albert Mangwea
Habari na Millard Ayo akiwakilisha clouds fm Afrika ya Kusini ili kupata taarifa za kina juu ya msiba huu.

3 Comments

 1. Anonymous

  May 30, 2013 at 11:26 am

  hzo ndo habari za uhakika me adi milad aongee ndo naamini wengine wote maigizo, ila dina milad ni bonge la mtangazaji namuangalia baada miaka 5 mbele atakuwa mbali sana ata CNN au BBC

 2. Mama 2 (Mrs M)

  May 30, 2013 at 12:13 pm

  Asante Clouds Media kwa kutupa taarifa zenye ukweli, maana wa-bongo!!!! mmmmmh1 kwa kuandika habari za kutunga ndio wenyewe. Shukrani kwako Dina na Clouds Media kwa ujumla.

 3. Ally Rashidy Tunzay

  June 4, 2013 at 9:27 am

  Asante sana kwa update zako

Leave a Reply