Uncategorized

TUMSAIDIE KIMAWAZO JAMANI MUME KAWA MCHUNGU!!

By  | 
Dina naomba uniulizie kwa walimwengu niko kwenye kipindi kigumu cha
maisha ambacho sijawahi kuishi.Nina mume wa ndoa na watoto wawili. mtoto
wa kwanza nilizaa na mwanaume mwingine maisha ya utotoni 
nilivyomaliza form six,baada ya hapo nilienda chuo nikaolewa na huyu
kaka ambaye naye ana mtoto mmoja wa kike. 
Kinachotokea ni kwamba kila
mwanangu anachokifanya anasema eeh kachukua kwa baba yake miye nakaa
kimya ana taka mtoto nimbadilishe jina nimwite jina la ukoo wangu miye,
ninavyoondika huu ujumbe kanipiga kisa jina hilo hilo na isitoshe ni
mume jina tu mambo ya kanisani nalea watoto wangu mwenyewe nawasomesha
hana anachonipa ananitukana kila mara miye mchawi eti namroga hapati
kazi ana kama mwaka sasa hana kazi hana shukrani. 
 
Hivi ndoa kama hii
nikiondoka walimwengu siwatanisema vibaya? kwasababu mtoto wangu wa kwanza
ana baba mwingine nimechoka kupigwa kutukanwa kuonewa. akilewa anasifia
wanawake zake wa zamani walikuwa wazuri baadaye anasema ni pombe kweli
haya maisha jamani nipeni ushauri nimechoka jamani na hii ndoa bora
nijikalie mwenyewe na kazi yangu ndio iwe mume wangu.

76 Comments

 1. Anonymous

  May 22, 2013 at 1:25 pm

  Dina kama hana msaada wowote anamnyenyekea wa nini? Aondoke zake huyo Dada mwishowe ataja kufa hapo.

 2. Anonymous

  May 22, 2013 at 2:22 pm

  kama hakusaidii wa nn na una kazi yako mama,,,

  • Anonymous

   May 24, 2013 at 3:10 pm

   Ondoka achana nae

 3. Anonymous

  May 22, 2013 at 2:38 pm

  Aondoke kama hakuna msaada anaoupata kwa sbb anakazi yake bora akae mwenyewe

 4. Anonymous

  May 22, 2013 at 3:05 pm

  Me na mshauri aondoke tu akalee watoto wake huyo jamaa ataona umuhimu wake akiwa mbali nae kwann anakubali kunyanyasika wakati ana mlisha na kumuudumia..just leave

 5. X-Tina

  May 22, 2013 at 3:57 pm

  Ushauri tutakupa dada lakini haitasaidia kitu. Uulize moyo wako kama bado una mapenzi na huyo bwana vinginevyo tunaweza kukwambia uondoke lakini kama hujaamua mwenyewe itakuwa ni kazi bure. Kwa ushauri wangu mi naona uwahusishe wazazi, washenga/ wadhamini wa ndoa au viongozi wa dini asipowasikia basi dada ni vizuri uondoke ukajipnge upya uanze maisha yako na watoto wako kwani kuendelea kutumikia ndoa yenye mateso imepitwa na wakati. Fikiria kama angekufa ungekufa na ww? Maisha utayaweza tu tena mshukuru Mungu una kazi yako. Na isitoshe utakuta unatumia pesa yako nyingi kumtunza. Na usikimbilie kuwa na mwanaume mwingine kwani hawana tofauti. Mimi ni mjane wa miaka 8 sasa na nna watoto wawili lakini namshukuru Mungu nna kazi na watoto wangu nawalea na kuwasomesha mwenyewe sitaki hata kuolewa tena kutokana na wanaume walivyo hawana msaada zaidi ya kkrudisha nyuma. MUOMBE MUNGU ATAKUONYESHA PA KWENDA USILIE WALA USIKUBALI KUNYANYASWA. WANAWAKE TUKIAMUA TUNAWEZAAAAAAAAAAAAAAAAA………….

 6. Anonymous

  May 22, 2013 at 4:46 pm

  Eti walimwengu watasema vibaya! Mwee! Unataka kuwaridhisha walimwengu huku wewe unateketea, Mama weee jali maisha yako na wanao walimwengu kazi yetu kukucheka na kukushangaa hatunaga msaada wowote sisi wenyewe tuna-stress za kumwaga. Chukua wanao anza mbele nyakati za kunyanyaswa na wanaume zilishakwishaga mama.

 7. Davis Mazula

  May 22, 2013 at 5:41 pm

  kwanini ukae kumsujudia mwanaume asiekunufaisha na anakunyanyasa.ni wakati nawe utafute amani na umpe mwanao amani pia,hawezi kukua kwenye mazingira hayo.

 8. Anonymous

  May 22, 2013 at 8:42 pm

  kila siku kumbuka kujiweka wewe wa kwanza kabla ya mtu yoyote yule,usiogope kusemwa kwani wameaanza kusema kabla hujazaliwa na watasema mpaka mwisho wa dunia,huyo jamaa ni LOOSER,ondoka haraka kabla ajakupeleka kabulini

 9. Anonymous

  May 22, 2013 at 8:46 pm

  Ondoka kaanze maisha yko,huo ni unyanyasaji

 10. ELIUD SAMWEL

  May 22, 2013 at 10:41 pm

  Ushauri wangu kwa huyo dada ni vyema angemuacha na kuondoka na wanae ili kuepuka hayo mateso maana kuna siku atamuua kabisa kwani mtu kama huyo huenda ameanza kuchanganyikiwa! EPUKA MAHABA NIUE.

 11. Anonymous

  May 23, 2013 at 3:59 am

  Yaani mbona anachelewa kumpiga kibuti huyo mume suruali, angekua mstaarabu ingempasa huyo mume amuheshimu mkewe hasa kwa kuwa hatekelezi majukumu ya kumtunza mkewe. Mwanamke mwenzangu hebu jitambue, una kazi na mtoto na mungu yupo. Hebu zinduka acha nae asije kutia kilema cha maisha bureee, pole sana dear.

 12. Anonymous

  May 23, 2013 at 4:12 am

  Dada huyo anahitaji maombi sana piga goti mwombe mungu atakushindia hayo ni mapito

 13. Anonymous

  May 23, 2013 at 4:15 am

  Dada mungu atakusaidia hyuo anahitaji maombi tumwombee mungu ambadilishe huyo ni pepo

 14. Anonymous

  May 23, 2013 at 4:40 am

  Pole jaman, anza tu maisha ya peke yko kama unahs utaweza kuish bla huyo mwanaume au kama unampenda mumeo tafta njia ya kumbdlsha nahs kukosa kaz ndo kuna mfanya adate hvo!! Da dina nkfkriaga hvo vsa vya kwny ndoa hua ham na mawazo yakuolewa yanaisha kabsaaa!! pole dada

 15. Anonymous

  May 23, 2013 at 4:46 am

  pole jaman, kama bdo unampenda mumeo na unahs anaweza akabdlka hyo tabia muwekee hata vkao na wanafamilia, au kama unahs utaweza ukaish vzur bla msaada wake wala htaj lake tena ok ish mwenyewe

 16. Anonymous

  May 23, 2013 at 5:21 am

  Dina,

  Mwenye uamuzi ni yeye mwenyewe! unaweza kumshauri aondoke yeye akiwa bado anampenda, anaweza kuondoka baada ya muda mfupi anamrudia akisha bembelezwa akatumia hizo hisia za mapenzi badala ya akili anarudi. kama amechoka ki kweli afanye hivyo kabla mwana hajahalibikiwa zaidi kihisia. inamuumiza mtoto. baada ya kuondoka aende akamuone mtu kama dada Sadaka.

 17. Anonymous

  May 23, 2013 at 5:41 am

  sipendagi miwanaume inayopiga mke nakerwa na aina hii ya binadamu dada ondoka endelea na maisha yako utapata mwingine mwema ziadi ya huyo

 18. Anonymous

  May 23, 2013 at 6:18 am

  Dada yangu unaishi maisha mara moja tuu,haijirudii.kama mtu hakusaidii ni wanini,inamaana wewe ni mwanamke chapa kazi na unaejiamni,angalia furaha yako na ya watoto wako. asikutese mtu ISHITOSHE DADA UMESOMA, dot waste yout precious time na mtu asikudhamini, wengine watasema nakushauri vibaya ila mimi nakuambia ACHANA NAYE!!! bibi zetu ndio waliokuwa akionewa becouse hawakuweza kusoma,sio sisi!! mae hembu angalia furaha yako. life is too short to waste with fools. All the best sister.

 19. Anonymous

  May 23, 2013 at 6:58 am

  dada unapoteza muda wa nini.unakazi yako na mwamme akusaidii kwa lolote jiondokee mwaya

 20. Anonymous

  May 23, 2013 at 7:18 am

  Dada mimi naamini maisha mazuri ni kuwa na amani na furaha na usiangalie binadamu watakusemaje kama kweli moyoni mwako unaamini kuwa huyu mwanaume hakufai na umechoka achana naye na uendelee na maisha yako wala usiogope jiamini kama mwanamke na utaweza kwani ww kama mama usipokuwa na furaha hata watoto wako hawatakuwa na furaha, inshort listern to your heart lakini kuwa na uhakika na unalotaka kulifanya.

 21. Anonymous

  May 23, 2013 at 7:36 am

  ondoka haraka atakuua huyo, maswali ya nini kujiuliza wewe, shauri zako utjuta utakapoletewa ukimwi na kipigo unacho.

 22. Anonymous

  May 23, 2013 at 7:42 am

  inategemea yeye ni dini gani km ni mkristo please waone watumishi wa mungu watakusaidia huna haja ya kuondoka wala kulia mwanamke inabidi uwe jasiri kumshinda adui dina mpe contact za mama victor atamsaidia ndoa za siku hizi bila kuwa jasiri na mcha utashindwa..
  usife moyo dada yatapita..

 23. Anonymous

  May 23, 2013 at 7:56 am

  chapa lapa dada, ndoa sio kila kitu maishani hasa ukuzingatia huna furaha, you only live once baby, find u r way out and make your self happy and safe.

 24. Anonymous

  May 23, 2013 at 8:08 am

  Kama mtu hakuonyeshi upendo ya nini kumnyenyekea na kumng'ang'ania? kaka yako huyo?? pia kama Mungu ameshakujalia watoto wawili unataka nini tena kwake kwa mtu asiyekujali??? haijalishi eti kila mtoto ana baba yake…. wote ni watoto wako waliotoka tumbo moja… tena ukizidi kukaa nae huyo atasababisha watoto wako kubaguana na kuchukiana… Tatu; Mshukuru Mwenyezi Mungu una elimu, me nakushauri tengana nae (sio kuachana nae) kaanze maisha yako ukimtumainia Mungu na kumkabidhi maisha yako ayaongoze na kuwalea watoto wako kwa Amani na Upendo na katika njia impendezayo Mwenyezi Mungu….. POLE SANA… USIKATE TAMAA, HAYO NDIO MAISHA, shukuru kwa kila jambo kwani anaendelea kukukomaza kimaisha na kutanua akili yako zaidi!!!1 nakutakia kila la kheri na Mwenyezi Mungu akubariki na watoto wako….

  Brother from Arusha

 25. Anonymous

  May 23, 2013 at 8:10 am

  UVUMILIVU HAPA UMEFIKA KIKOMO ASIJE AKAKUUWA'ONDOKA DADA.

 26. Anonymous

  May 23, 2013 at 8:16 am

  Fanya maamuzi magumu, ondoka ukaanze maisha mapya na utakuwa na amani moyoni.
  Huyo mwaume anakunyonya isitoshe hana hata shukrani.

 27. Anonymous

  May 23, 2013 at 8:24 am

  Wanawake wengi wanakuwa waoga kutoka kwenye ndoa za manyanyaso wakiamini kwamba akiondoka huko aendako atapata shida au maisha bila mume hayaendi lakini sio kweli, hizo ni fikra zao tu hakuna kinachoshindikana, inachotakiwa ni kuwa na msimamo na kusimamia maamuzi yako.

  Sasa kama dada kazi unayo unahofia nini kuondoka? tena utakapokuwa mbali nae utajikuta una amani sana moyoni mwako na akili yako itaweza kufanya kazi vizuri sana na utajikuta ukipata maendeleo kwa haraka. Wala usiogope kwamba jamii itakufikiriaje hayo ni maisha yako.

 28. Anonymous

  May 23, 2013 at 8:27 am

  Najua utapata pingamizi kutoka kwa baadhi ya ndugu wakikutaka uvumilie, lakini unatakiwa kushika msimamo wako wa kuondoka na baadae watakapokuona una amani na maisha yako yanaendelea vizuri wataelewa ulichokuwa unamaanisha.

 29. Anonymous

  May 23, 2013 at 8:56 am

  Dina naomba tumpe ushari mzuri sababu tayari mwenzetu ana mtihani kama nimemuelewa anasema ameshazaa na mwanaume mwingine kabla ninachogundua hapa ni kuwa mwamama ana uoga wa kuendelea kuna mahusiano mengine au kuachwa sababu atahesabika vibaya kwa jamii eti anamaliza wanaume labda ila take my world mama mimi nimezaa na waume watatu tofauti na stori yako kidogo ifanane na yangu ila kwa ukweli nakushauri sikiliza moyo wako unataka nini?? unapofanya maamuzi usjali jamii au watu fulani sababu hayo ni maisha yako wewe binfsi uwe jasiri kwenye maamuzi usiwe muoga maana uoga wako ndiyo kifo chako kama mtu hakufai na hadi anakuambia wanawake zake wa nyuma hapo hakuna mapenziiiiiiiii huyo mwanaume yupo na wewe kwa sababu unamlisha na kumsaidia kimaisha sasa basi hapo ukiishiwa tu au ukiachishwa kazi imekula kwako la msingi piga moyo konde fanya maamuzi sahihi ambayo yatakupa amani ya maisha sikuambii muache sijui wewe binafsi moyo wako upo vipi kwa mumeo ila wazungu wanasema kila mtu yupo responsible for her/his happiness, kama unaona hakufai pleasee leave himi usitegemee kama atabadilika man never change my sweetie ila the way u sound unawezaaa songa mbele bila mwanaumee kata shauri sasa hivi.

 30. Anonymous

  May 23, 2013 at 9:36 am

  mvumilivu hula mbivu subiri ya kukute ya yule mama wa shinyanga aliyeburuzwa na gari na Dina alimtoa humu sote tuliona au we hukuona dada.pole hayo maisha yalishapitwa na wakati.kwani ulizaliwa nae uyo au mmekutana ukubwani?kama umezaliwa nae endelea kuvumilia,chapa lapa dada.

 31. Anonymous

  May 23, 2013 at 9:36 am

  pole dada kwa hayo yanayokukuta,nakupa ushauri huu kama mama ambae nimepitia the same situation, wanaume wengi wakiwa hawana kazi wanakuwa na maumivu ya wivu kwa wewe ambae ni mke wake na unafanya kazi hivyo hivyo yale maumivu yanamfanya aongee hovyo,akasirike,kupiga na mambo yote yanayokupata hayo ni maumivu yake ya ndani na huwa hawakubali au kuamini kuwa unafanya kwa upendo na heshina yale unayayafanya. ushauri ni bora uondoke kwa usalama wako na watoto wako, kwa afya ya mwili,kiakili na kiroho pia wanawake hatuolewi kuwa watumwa au ngoma ya kupiga, ili hali maisha ya familia unayasimamia wewe kwa upendo. Jipange tu uondoke ghafla maana ukimwambia atakufanyia fujo ila ukishaondoka toa taarifa kwa wazazi wote juu ya tabia yake. lea wanao kwa utulivu mungu atakujaalia.

 32. Anonymous

  May 23, 2013 at 9:38 am

  UH!MIMI NINA STORI INATAKA KUFANANA NA HII,MIMI ZAMANI NILIKUA MUISLAMU BAADA YA KUMALIZA KIDATO CHA SITA NIKAENDA JIJINI DAR ES SALAAM NA NIKAKUTANA NA KIJANA MMOJA AKANISHAWISHI TUKAPENDANA KWELI KWELI,KUMBE YULE JAMAA ALIKUA ANAMKE WA NDOA NA WANAMTOTO MMOJA,BAADA YA KULIGUNDUA HILO KUTOKANA NA IMANI YANGU NA NILIKUA NAMPENDA SANA NIKAAMUA LIWALONALIWE BORA NIOLEWE MKE WA PILI,NIKIWA MWAKA WA PILI NIKAPATA UJAUZITO BWANA AKAWA MKALI ANATAKA NITOE MIMBA NA MIMI KWA KUJUA ATHARI ZA UTOAJI MIMBA SIKUKUBALI NIKAAMUA KULEA MIMBA HIYO,DAH……SITAKI KUKUMBUKA ALININYANYASA SANA KIPINDI CHOTE NIKIWA MJAMZITO ALINITENGA ALISEMA NIMEFANYA MAKUSUDI NIMEMTIA AIBU NILILEA MIMBA KWA TAABU SANA NIKIWA NA MSONGO WA MAWAZO HATIMAYE NIKAJIFUNGUA MTOTO MWENYE AFYA DHAIFU SANA KWA KIFUPI NILITESEKA SANA HAPO NIKAWA SIWEZI TENA KUISHI HOSTEL NIKAWA NA HANGAIKA NAISHI SEHEMU ZA AJABU NA MWANANGU HUKU NAENDA CHUO,BAADAE MTOTO AKIWA NA MWAKA MMOJA MWANAUME ALIRUDI TENA NIKIWA NA HALI NGUMU SANA WAKATI HUO NIMESHAMALIZA CHUO SINA KAZI NAISHI MAGOMENI KWENYE CHUMBA NIMEPEWA HIFADHI AKANITAFUTIA NYUMBA UPANDE MZIMA NYUMBA NZURI SANA KUTOKANA NA SHIDA NLIZOKUA NAZO ILIBIDI NIKUBALI SABABU MWANANGU ALIKUA DHAIFU SANA. BAADA YA KUHAMIA KWENYE HIYO NYUMBA ALIYOTAFUTA AKANISHAWISHI TUFUNGE NDOA KUTOKANA NA MAISHA KUA MAGUMU,NA NILIKUA NAMPENDA KWA DHATI,SIKUTAKA KUENDELEA KUZAA WATOTO NA BABA TOFAUTI,PIA NILIKUA NAAMINI SANA KWENYE UISLAM KUWA NDOA ZAIDI YA MOJA ZIMERUHUSIWA NILIANUA KUKUBALI KUOLEWA BI MDOGO,AH…NDUGU ZANGU WALINIPINGA VIKALI ILA NILIKUA KAMA NIMEROGWA NILIKUA SISIKII LA MTU HATIMAYE MWAKA 2008 NOVEMBER NIKAOLEWA.LOH BAADA YA NDOA MAISHA YALIBADILIKA YAKAWA MAGUMU MWANAUME MALAYA HAFAI,WASICHANA WA KAZI WOTE NNAOLETA ANATEMBEA NAO,MAJIRANI WANALALAMIKA ANATONGOZA WATOTO ZAO NA WAKE ZAO IKAWA FEDHEHA MTAANI.NILIVUMILIA WAKATI HUO NATAFUTA KAZI KWA UDI NA UVUMBA SIPATI KILA HELA ANAYONIPA ANANISIMANGA NAYO,MARA ANANIAMBIA MIMI NA MWANANGU TULIKUA TUMEKONDEANA BAADA YA KUNIOA NINANENEPA HALAFU SINA SHUKURANI,KUNA SIKU ALINIPA LAKI MOJA NIKAFANYE SHOPPING YA NGUO ZANGU WEEE NAJUTA KILA KUKICHA NILIKUA NAAMBIWA HUNA AKILI NIMEKUPA LAKI MOJA NZIMA UKAFANYE SHOPING SINA SHUKURANI,MWANAUME AKAWA MCHONGANISHI HABARI ZA MKE WAKE MKUBWA NANILETEA MARA OH MAMA FULAN ANASEMA WEWE MALAYA,AKITOKA KWANGU ANAPELEKA HABARI ZANGU KWA MKE MKUBWA BASI KUKAWA NA VITA,MANENO YANI KWA KIFUPI NIKAWA SINA AMANI TENA NA NDOA ILE.HATIMAYE NIKACHOKA MWENYEWE NIKAAMUA KUONDOKA SIKU AMBAYO ALIMVULIA NGUO MDOGO WANGU MWENYE MIAKA 16 AKIMTAKA AMNYONYE UUME WAKE,NILIUMIA SANA ALINIDHALILISHA SANA MBELE YA FAMILIA UKIZINGATIA KUWA FAMILIA YANGU ILIKUA HAIMKUBALI NIKAONDOKA ALIJARIBU KUITA WAZEE WATUSULUHISHE ILA NILIAMUA KUFANYA MAAMUZI MAGUMU,NILIZIBA MASIKIO NIKSIMAMIA UAMUZI WANGU NIKAAMUA KUANZA MAISHA UPYA KWANI BAADA YA KUONA SINA DALILI ZA KURUDI KWAKWE ALININYANG'ANYA KILA KITU NGUO ZANGU NA ZA MWANANGU AKAZITUPA CHINI AKAENDA KWA MWENYENYUMBA AKARUDISHIWA KODI AMBAYO NILIKUA NIMEKOPA BRAC KWA JINA LANGU ILI TULIPE KODI NA TULIKUA TUMEKAA MIEZ MIWIL TU BAADA YA KODI HIYO KULIPWA BASI NIKAWA SINA UJANJA ZAIDI YA KUENDELEA KULIPA DENI LA WATU KWANI PESA ALIYORUDISHIWA HAKUNIPA.MUNGU NI MWEMA SANA BAADA YA KUTOKA KWAKWE MIEZI MIWILI BAADAYE NILIPATA KAZI NZURI SANA AMBAYO ILINITAKA NIENDE MKOANI.NAMSHUKURU SANA MUNGU BAADA YA KUHAMA DAR ES SALAAM NIKAPATA MCHUMBA AMBAYE ALITUPENDA MIMI NA MWANANGU MPAKA TUKAMSAHAU YULE JAMBAZI,NA SASA NIMEFUNGA NDOA KANISANI NILIAMUA KUBADILI DINI KWANI SINA IMANI KABISA NA DINI NILIYOTOKA ESPECIALLY SUALA LA NDOA ZAIDI YA MOJA,KWA SASA NAISHI MAISHA MAZURI NA MUME WANGU NA NILIJALIWA MTOTO MWINGINE KWAHIYO TUNAO WATOTO WAWILI!FANYA MAAMUZI YA BUSARA WEWE NDIE UNAYEJUA UGUMU WA NDOA YAKO.

 33. Anonymous

  May 23, 2013 at 9:39 am

  Pole dada kwa unayokutana nayo kwel hafanyi vizur bt pengne ni stress 2 za kukosa kazi ndo zinazompelekea yeye kufanya hvyo na daima m2 anapokuwa na hasira na akiona mambo yake hayakai sawa hasira huzmalizia kwa mnyonge wake embu iten wazaz na wadhamin pande zote 2 jarbun kukaa mtatue matatizo yenu kwanza na si kukimbia mume ana nafasi yake katika maisha wala kaz haiwez kuwa mumeo zaidi Mungu mshirikishe kwa kila kitu.barikiwa.

 34. mariam

  May 23, 2013 at 9:48 am

  HUNA HAJA YA KUENDELEA KUKAA KWENYE MATESO YA NAMNA HIYO NA KIBAYA ZAIDI KAMA ANASIFIA WANANAWAKE WA NJE MEANS SI MWAMINIFU, YA NINI AJE AKUUE BURE KWA MARADHI WAKATI SI MLEZI??? HAPATI KAZI KWA SABABU MUNGU ANAJUA, AKIMPA ATAKUNYANYASA ZAIDI YA HAPO, HAKUNA ATAKAYEKUCHEKA ETI KISA UMEAAMUA KUONDOKA ILA UNAVYOENDELEA KUBAKI NDO UNACHEKWA DADA, CHAPA LAPA

 35. Anonymous

  May 23, 2013 at 10:19 am

  kama kavumilia habadiri tabia bora aachane nae afate maisha yake,maana hawatafanya maendeleo kama hawaelewani

 36. Anonymous

  May 23, 2013 at 10:30 am

  we dada ondoka,achana nae mama!! wa nini huyo kumbe hata ndoa hamjafunga…,mwisho wa siku utaletewa magonjwa km akilewa hajitambui….anaomba msamaha eti pombe….Achana nae kwa nini unaishi bila amani raha huna….!!Muombe mungu akupe nguvu ondoka utamsahau ukaanze maisha mapya ulee wanao mama…kila la kheri

 37. Anonymous

  May 23, 2013 at 10:39 am

  Pole sana dd. Hata tukikushauri haitasaidia kitu kwani maamuzi hutoka moyoni mwako. Kwani wanawake wengine hushauriwa lakini kumbe ni mahaba niue. Hebu mshirikishe Mungu katka maamuzi yako atakuonyesha cha kufanya. pia mi binafsi sioni haja ya wewe kumn'gan'gania mtu ambaye anakutesa na bado ww ndio unaemuweka mjini. Kama ni maisha unayaweza tena Mshukuru sana MUNGU kwa kkupa kazi.

 38. Anonymous

  May 23, 2013 at 11:07 am

  ni bora aachane nae maana ndoa ni heshima na kuthaniniana na sio dharau na matusi. ni bora ajiweke pembeni asiogope walimwengu kwani kusema ni kazi yao. aanze maisha yake alee wanawe

 39. Anonymous

  May 23, 2013 at 11:50 am

  Mama maisha ya sasa ni mafupi sana, punguza mzigo wa moyo kwa kuondoka kwa huyo mumeo,ukajipange kuwalea watoto wako.achana na mitazamo ya jamii itakuelewaje, jaribu kuisikiliza nafsi yako inaamuaje

 40. Anonymous

  May 23, 2013 at 12:32 pm

  Pole sana nakulwa sana>
  mie pia nilipitia hayo mapito unayopitia sasa.
  Ulivyoelezea ni kama nasimulia mie vile.

  tena wangu alikuwa mlevi mbwa na alikaa mtaani kwa miaka miwili nazani umeelewa.Kikubwa ni kukazana kumtafutia kazi awe busy atajirudi na kuona mambo anayofanya sio sawa.
  Pole sana vumilia tu ila akipata kazi yatakwisha yote wanaume wengi huwa wanachanganyikiwa pindi wakosapo kazi au kokosa namna ya kuingiza kipato.

 41. Anonymous

  May 23, 2013 at 1:12 pm

  POLE DADA KWA YANAYOKUSIBU, ILA KAMA UNAONA HAMNA DALILI YA HUYO MWANAUME KUBADILIKA NI BORA UWASHIRIKISHE WAZAZI WA PANDE ZOTE, LAKINI PIA IKISHINDIKANA NI BORA TU UONDOKE MAANA HUYO MWANAUME INAONEKANA ANAMCHUKIA SANA MWANAO USISHANGAE SIKU UNAKUTA AMEFANYA MAMBO MABAYA SANA KWA MWANAO. SINCE YOU ARE FINANCIAL FREE ANGALIA USTAARABU MWINGINE WA MAISHA.

 42. Anonymous

  May 23, 2013 at 2:44 pm

  pole mwanamke mwenzangu
  MWANAUME HAKUPENDI DADA TAFUTA NJIA UKWAMUE MAISHA YAKO
  UKIPOKEA MATESO ATAKUTESA
  KABLA YAKE ULIKUA NA MWINGNE KWA HIYO TAFUTA NJIA
  USIKUBALI KUWA MTUMWA WA MAPENZI
  USIKUBALI KUNYANYASWA NA MWANAUME WAKATI MIGUU NA AKILI YA KUTAFUTA UNAYO
  USIMPE MWANYA MWANAUME AKUSIFIE YALOPITA KAMA NIPOMBE MBONA HAKUSIFII WEWE
  USIMWACHE MWANAUME AKUTUSIE MTOTO ULOMZAA KABLA

  USHAURI ACHIKA SIMAMA KWA MIGUU YAKO

  MWENYE THAMANI NA CHOZI LAKO HATO KUACHA UUMIE SASA KAMA ANAKUUMIZA NYANYUA KICHWA JUU ILI CHOZI LAKO LISIANGUKE CHINI UKASHUSHA THAMANI YA CHOZI LAKO KAMA HUYO ASIVYOKUTHAMINI
  TAFUTA ATAKAYE KUFUTA CHOZI SIO ATAKAE KULIZA,

 43. Anonymous

  May 23, 2013 at 2:53 pm

  Pole ila sikia yangu
  Mie upuuzi huo sina niko radhi nibadili wanaume .siko tayari mwanaume aninyanyase au akinyanyase changu huu ndo msimamo wangu.

  Naishi mara moja siruhusu shida za roho za kuletwa na mtu ntaruhusu shida zinazoletwa na Mola au maisha

  Nilikua na mwanaume mawifi walinitesa nikamuliza kanioa au wamenioa ? akajibu kanioa lakini wale ni dada zake sa ngne hana uamuzi
  nikamwambia aongoze mbele aoe mwanmke atayemilikiwa na familia mie nataka tumilikiana nikamwacha

  Heri uish upweke utapata jibu ¨
  Tatizo wanawake waoga
  ACHANA NAYE ATAKUFUJA AKUPOTEZEE MUDA

  ISHI MAISHA SIO MAISHA YAKUISHI WEWE

 44. Anonymous

  May 23, 2013 at 3:20 pm

  Ondoka haraka mama huyo hakufai dada

 45. Anonymous

  May 23, 2013 at 9:26 pm

  pole sana ndugu yangu kaa na familia yakw nayako umfahamishe hakusikia wewe si mtoto mdogo uwamuzi unao mwenyewe na huyu si mume wa kwanza inawezekana bado unampenda ukimchoka hutotaka ushauri la kuamua utalijua

 46. Anonymous

  May 24, 2013 at 7:09 am

  sasa mamy mume mwenyewe unasema hata hamjaoana kanisani mnaishi tu, kwa maan nyingine mnaendeleza uzinzi tu, mume hana msaada kwa lolote wa nini huyo??? ondoka zako endelea kuwatunza wanao kwa raha zako na amani, ukianza kuuliza walimwengu watakuchukulia vipi, hutafanya lolote, walimwengu watesema tuu, hata ufanye nini ndivyo walimwengu tulivyo, fanya yako yanayokupa amani na kumtukuza Muumba.

 47. Anonymous

  May 24, 2013 at 7:23 am

  Ndoa ndoano , tayari mmekuwa mwili mmoja , katika maisha ya ndoa ni uvumilivu , jambo ambalo wengi wanashindwa , Baraka zako zitaongezeka pindi ukishinda hayo majaribu …. hayo ni majaribu tuuuu…

 48. Anonymous

  May 24, 2013 at 7:29 am

  nawe unajitakia kunyanyasika, kama watoto unaweza kulea mwenyewe unamng'ang'ania nn huyo bwana? ACHANA NAE

 49. Anonymous

  May 24, 2013 at 7:30 am

  ACHANA NA HUYO BWANA ANZA MAISHA YAKO KIVYAKO. by mama nica, dsm

 50. Anonymous

  May 24, 2013 at 7:34 am

  we nawe inamaana hujui hapo ufanye nn? wanawake wengine wajinga ila we umezidi, ondoka na watoto wako uendelee na maisha kivyako

 51. Anonymous

  May 24, 2013 at 8:52 am

  Ondoka mwaya kabla hajakutia kilema cha maisha. wapo wanawake wengine huvumilia na hatma yake ni majuto zaidi kwani hata watoto hawapati malezi/mapenzi toka kwako na pia ni matokeo mabaya kwa kizazi cha hao watoto, yaani watoto watakuwa wakatili kwakutopata mapenzi ya baba wala mama. ni bora ulee watoto wako kwa upendo ukiwa nao kuliko kuendelea na masimango yasiyo na msingi.

 52. Anonymous

  May 24, 2013 at 8:54 am

  HUYO HANA HAYO MATESO ANAYOYASEMA MANAKE KAMA HALI ILIKUWA HIVI ANAVYODAI WALA ILIKUWA HAINA HAJA YA KUOMBA USHAURI ALITAKIWA AWE AMECHUKUA HATUA KARNE ILIYOPITA

 53. Anonymous

  May 24, 2013 at 9:16 am

  Aondoke ndoa ndoa Kwani yeye wa kwanza kuachika.

 54. Anonymous

  May 24, 2013 at 9:22 am

  dada kwanza jua walimwengu siku zote huongea mabaya hata ufanye mazuri alfu mia. kumbuka wewe ndo wakujionea huruma na si mwingine.you need to have a self confidence wherever you walk in this world,pia unahitaji a self decission before any body decide for you. same here ulipoamua kuolewa na huyu bwana i am sure hakuna aliyekushauri .thats apply here hata kuondoka hakuna atakaye kushauri.wote wanaotoka kwenye ndoa zao hawatolewi huondoka wenyewe bila kushawishiwa pale maji napofika shingoni.

  natamani ningeongea nawe uso kwa uso.hapo unatengeneza chuki between baba na huyo mtoto wa kambo.usitegemee huyu mtoto ataweza vumilia yote anayoyaona huyu baba anayokufanyia,pia unamuathiri mtoto ki saikolojia.pia hawa watotot wawili wanaweza wasipendane tokana na chuki za baba kwa mtoto wa kwanza. anataka umbadilishe jina la ukoo kwani wanatambika nae? muache mtoto atumie jina la babake mzazi kwani ndio haki yake ya halali hapa duniani. watoto tunaowazaa ndio mali zetu za halali katika dunia hii.

  usiogope, kama unalisha,unasomesha na kujilipia kodi mwenyewe ukiwa kwa mume kinachokushinda kufanya hivyo ukiwa peke yako ni nini? usitake kufa ukaacha watoto wako wadogo.lea wanao katika maisha yasio na fujo na kudhalilishwa kila kukicha. fanya maamuzi sahihi ndugu yangu.neno ndoa lina maana kubwa sana ,sasa kama hakuna haki inayotendeka hapo unangoja nini?huruma yako itazaa dhambi.ishi utakavyo usiishi watu watakavyo .

  wako walioachwa na kuacha waume zao na ikavuma dunia nzima ma elf ya watu wakajua sembuse wewe unayejulikana na watu 20 kijijini kwenu? mbona Winnie Mandela aliachwa na bado anaishi mpaka leo?hakujali waioteta na kusema au kufikiria vibaya,kama hana kazi wewe unakiwanda au kampuni ili umwajiri? wanaume wengi wa siku hizi wakibugi maisha tena kwa laana ya kutowasikiliza wake zao basi wanakimbilia kurogwa , hakuna lolote huyo ni mvivu na ameshaona anapata dezo …mjini hapa mtu akikupa kula x3 , kulala free na kuvaa dezo basi atakuona wewe fala,sasa ondoka uone kama hajakwenda kwa mchungaji akitaka asaidiwe urudi.

  tena huyo akipata hela atakuolewa mke wa pili tena wewe utakua bibi ambaye uzee wako hauwezi kuishia chalinze so ukifika dar huwezi itwa babie utaitwa bibi!!!

  kama uko tayari tafadhali tuwasiliane kwa hatbah.mduma@yahoo.com

  ILA FANYA MAAMUZI SAHIHI NA MAAMUZI YA MOYO WAKO

  • Anonymous

   May 29, 2013 at 7:35 am

   gud, umemshauri vizuri sana jamani, kwanini wanaume wako hivi ya huyu dada ndiyo ya kwangu ili nashukuru niliondoka na sasa naishi vizuri kwa furaha na amani.

 55. Anonymous

  May 24, 2013 at 10:02 am

  Dada vumilia tu na omba kwa jinsi ambayo hujawahi kumuomba mungu,tafuta waombaji uombe nao hakika mungu ni mwaminifu

 56. Anonymous

  May 24, 2013 at 11:32 am

  Hapo ni kuondoka tu ndugu yangu,japo tunashauriwa kuwa wavumilivu hapo si kushauri uendelee kuvumilia bora,nenda kajaribu maisha yako mungu hatakuacha kwani ndie mfariji.pole sana kwa yote.

 57. Anonymous

  May 24, 2013 at 1:41 pm

  wanaume ndkio walivyo walio wengi kuwanyanyasa wake zao wakati hata matumizi ya ndani anachangia mama kwa kiasi kikubwa,kama wamejijenga na wana mji wao walishilikiana kupata hizo mali asikubali kuomdoka na kumwachia hizo mali huyo mwanamume,na kama wamepanga tu na si ajabu hiyo kodi antoa huyo dada bora aondoke na kujitegea kuliko kupata pressure bure………………….huyo mwanamume hana utu

 58. Anonymous

  May 24, 2013 at 2:00 pm

  Mmh!huyo mwanaume sio mwema kwako hata mtoto akikua atambagua na belive me watoto wana good merory asikuambie mtu,huyo mtoto anaona hivyo anavyotukanwa na inastic kichwani kwake na hali hiyo ikiendelea huyo mtoto anajengewa mazingira ya kuwa mkaidi ushauri wangu mi naona anakutafutia sababu huyo ni hasidi hana sababu wewe tambaa zako,kaanze upya bwana na uzuri una kazi yako asije akakupiga akuue bure.

 59. Anonymous

  May 25, 2013 at 8:55 am

  mmh hizi ndio faida na hasara za kuzaa kabla ya ndoa tukiambiwa tunakuwa viburi,,

 60. Anonymous

  May 25, 2013 at 9:47 am

  unaogopa kuonekana umezaa na wanaume tofauti, ndio unavumilia manyanyaso? achana nayo, inawezekana wanaume wote uliokutana nao mpka huyo mwingine ukafunga ndoa si mpango wa mungu, jitokeee kawalee watoto wako

 61. Anonymous

  May 25, 2013 at 12:00 pm

  HUYO SI MME NI PEPO ACHANA NAYE LABDA ANACHOKINACHOMTIA UJEURI,,ANGALIA MBELE MDADA ILA POLE SANA KWA YOTE.

 62. misha

  May 25, 2013 at 6:49 pm

  pole sana dada,ndoa nikitu chakugeshimiwa sana,namitihani katika ndoa ipo mingi ila kikubwa nikumuomba mungu akuepushe nayo,nakushauri uwashirikishe ndugu zake nikimaanisha wazazi wake,ikishindikana waone wachungaji waliowafungisha ndoa ili awape mafunzo upya yandoa!!kuachana nae sio suluhisho lamatatizo,jiulize tuu dada yangu utaachana nawangapi??Kaa namumeo muongee napia umuombe mungu naamini nipepo tuu hilo.litashindwa katika jina la Yesu!!

 63. Anonymous

  May 25, 2013 at 8:31 pm

  Leave…. mana mwishowe utaishia na magonjwa na ukawaacha watoto wako yatima bure

 64. Anonymous

  May 25, 2013 at 11:20 pm

  Daah! Dada pole saana kwa yaliyokukuta japo kuwa wanasema ndoa ni kuvumiliana but huyo mwenzetu kazidi. Sasa mimi cha kuku shauri kabla ya kufanya maamuzi mengine yeyote jaribu kumwita na kumwambia maduduku yako. Then akiwa bado still anaendelea na huo ujinga wake jaribu kuomba ushauri kwa watu wazima either wazazi wenu ama wengine ambao una waamini. Na kama bado akiwa kidudu mtuuu! Sasa hapo dada sepa (ondoka) tena bila ya kusita wala kumuaga. Istoshe unakazi yako kwanini akunyanyase wakati unaweza ukapata ugali na kuishi bila ya maumivu ya kijinga.

 65. Anonymous

  May 26, 2013 at 8:21 pm

  dada kwanza nikuulize swali una mpenda mumeo ?kama bado una mpenda nenda kwenye maombi mungu ata mfungua mumeo ingawa haita kua rahisi maana yawezeka yeye ndiye mchawi au aliwahi kutembe na pepo ak dhani jini au tabia hiyo ina tokana na familia alikotoka .lakini pia mapenzi yenu yalikua ya aaina gani kweni mtoto kamua juziii pia unaweza wewe kuamua moyoni mwako nini wataka maamuzi kamili unayo wewe na mungu akusaidie

 66. Anonymous

  May 26, 2013 at 8:34 pm

  Dada wanaume ukiwaendekeza utachakaa kabla ya muda mpenzi yawezekana wampenda sana mumeo ila angalia unafuraha na aman ktk ndoa kama jibu ni hapana chukua hatua usiangalie walimwengu kila mtu anamaisha yake tafuta furaha yako na sio ya walimwengu. huyo mwanaume hana mapenzi na wewe eti unamroga sasa siaende kama kajua wewe wamroga ye ndo mshirikina kajuaje kama naye hajaenda kuroga.

 67. Anonymous

  May 27, 2013 at 4:58 am

  sasa dada hapa unaomba ushauri gani tena? kwamba umvumile ama? sababu kwa jinsi ulivyoeleza wala huitaji ushauri, ONDOKA ndugu yangu, mana hakupi msaada wowote zaidi ya kipigo na matusi, bado unasubiri ushauri? ina maana tukikwambia endelea tu kuvumilia utakaa?

 68. Anonymous

  May 27, 2013 at 5:52 am

  Dada mbona unanishangaza hivi kweli mwanamme hana msaada wowote kwako halafu anakupiga, anakutukana bado upo tu kisa ndoa ndoa mateso chapa lapa kaanze maisha yako dada.

 69. Anonymous

  May 27, 2013 at 9:50 am

  mwanume anapokuwa hana pesa, anapata taabu sana kuukubali ukweli huu, na hapo kila mwanaume ana-react kivyake. wengine ndo km hawa!! hiyo ni inferiority complex kwamba nimgandamize watu wasijue nalishwa na mwanamke(that I'm still a MAN enough). lakini kiukweli haifai kwa kuwa hakujali! mwisho wa mume km huyu atakudharau hata akipata pesa na kuna uwezekano asibadilike. lakini usikurupuke kuondoka jiandae na uwe na ratiba hata ya mwaka mzima. Ukitoka hapo uwe umesimama mwenyewe hasaa. Nakuhakikishie utaweza kuishi kwa amani na furaha bila ya mume.But anaweza kukuganda na kukufuata utakokwenda ndo maana ya kusema jiandae.kuwa na msimamo wa ukweli.km utarudiana nae pia weka msimamo kuwa akirudia anaondoka yeye. waache watu waseme; wewe angalia nafsi yako na watoto wako tu!! hayo ya watu waachie wamama zetu miaka hiyo ya 47. YOU LIVE ONCE. BEST WISHES

  • Anonymous

   May 28, 2013 at 9:57 am

   nakuunga mkono kwa ushauri uliyompa huyo dada.

 70. Anonymous

  May 31, 2013 at 6:44 am

  pole dada kwa maswahiba yaliyokupata huyu kijana anayekusumbua kukusababisha usilale usingizi,inawezekana tatizo hana salio/michongo haisomi sasa anajihami kuleta heshima ya ndoa kwa ngumi,mpe mda apate kwanza usimchukie mtoto kwa maji ya moto ya wiki 1,usikimbie nyumba yako tafuta wakubwa muweke sawa

 71. Anonymous

  May 31, 2013 at 10:30 am

  pole sana dada kwa yaliyokukuta maana wote ni wanawake na tunajua nini hasa maana ya mapenzi,mimi binafsi nimeguswa na matatizo yako ila inatakiwa wewe binafsi ujitambue,tuliza akili yako kwanza kabla hujafanya maamuzi maana kwa jinsi unavyosema naamini huyo mumeo ana stress ya maisha ndio inayompelekea kufanya hayo yote.ukishajitambua halafu utambue kama unampenda kweli huyo mwanaume,ukshayajua haya yote then utafanya maamuzi ya busara sana na wala usikurupuke my dear.Hakuna kitakachoponya ndoa yako bila kumshirikisha mungu hiyo nakwambia wazi utabadilisha wanaume hata mia katika hii dunia lakini kama huna mahusiano na mungu ni kazi bure.Ndo maana nimekwambia jitambue maana ndoa zetu shetani huzijaribu sana sasa shetani akikuta wewe wala mumeo mko mbali na mungu atawakoroga sawasawa,mpaka uyawaona wanume wabaya na ndoa utaiona chungu na ndilo linalokusumbua sasa,suala la wewe kumpiga tafu mumeo sio issue my dear haya ni maisha tu kesho wewe unaweza kudrop mumeo akakupiga tafu lakini cha msingi ni mapenzi ya kweli.maana hata sisi tukikwambia ondoka lkn nafsi yako inasemaje? Je unampenda mumeo?suala la kumtukana mtoto ni mbaya sana lkn sisi tunaichukulia kibinadamu lkn yupo mungu ambaye anaweza kumbadilisha mumeo in 1 second mpaka ukabaki unajiuliza ndio huyu kweli aliyekuwa ananitesa na kunitukana!!Kwa mungu hakuna kinachoshindikana mradi umuamini mungu na kujitambua, basi utasimama kwa ajili ya kumbadilisha mumeo na atabadilika kama huamini try,kama kweli unampenda basi simama kwa ajili yake maana hata leo ukiondoka utampata mwingine lakini mwisho wake utakua ni huu huu!! wanaume wamefanana na still wewe bado ni mdogo damu bado inachemmka,huwezi kuniambia mm utakaa miaka bila kuingia kwenye uhusiano mwingine je what is next ukiingia kwenye huo uhusiano mpya?utajikuta unabadilisha wanaume kila siku unless uniambie mm baada ya huyo utakuwa single mpaka kifo chako na hiyo haiwezekani itafika wkt utafall in love na mtu mwingine tu. So my dia mimi nimekushauri kutokana na experience yangu ya mapenzi you can take it or leave it. Lakini kumuacha sio solution tafuta solution.kama ni mkristo utanielewa nini namaanisha, sasa hivi uko kwenye vita na jitahidi uishinde na ukiishinda mungu atajivunia wewe.Hutaweza kuishinda bila kutumia jina la Yesu.mamlaka umepewa ya kumtumia Yesu mtumie atakubalishia maisha yako yote kwanza umsamehe mumeo kabisa,pili tubu kwa ajili yake halafu mpeleke msalabani mungu atamuokoa. Ndoa nyingi zinakua na mateso kwakua hutujui kutumia mamlaka tuliyopewa na mungu ndo maana shetani anasumbua ndoa zetu lkn ukisimama sawaswa utaniambia.Nakutakia kila la heri katika kipindi hiki kigumu ambacho unapitia mungu atakupa mlango wa kutokea hakuna jaribu lisilo na mlango.

 72. Anonymous

  June 3, 2013 at 8:11 am

  kula hamsini zako ili akili imkae vizuri maana sasa anakuchukulia poa na atambui umuhimu wako.so we sepa then uone atakavyokutafute kama pesa vile na wewe hapo ndo utakavyoringa mtoto wa kike.

  ni hayo tu dada yangu
  by juma yusuph nyakilebilo (facebook page)

 73. Anonymous

  June 6, 2013 at 8:52 am

  pole sana dada. ondoka na wanao kaanze maisha mapya.

Leave a Reply