Uncategorized

WALE WAPENZI WA MOVIES ANGALIA NA HIZI KAMA HUJAZIONA!

By  | 

Hii movie ni nzuri sana sitaki kusimulia wewe nenda kainunue uangalie mwenyewe.Ni movies wameigiza Bradley Cooper na Zoe Saldana mwanadada aliyetamba kwenye Avatar na Colombiana.
The place beyond pines.Wameigiza Ryan Gosling,Bladley Cooper na Eva Mendes.Katafute ziangalie hii ni mpya kabisa ya mwaka huu.
Zote zinaburudisha na kufundisha kitu kuhusu maisha haya tunayoishi kila siku.Ningependa kina baba muangalie hii zaidi kuliko hata wanawake.Athari za baba kutokuwa karibu na mtoto wa kiume katika kumlea.
Athari zinakuja kujitokeza akiwa mkubwa.Unadhani watoto wa kiume ni strong kihisia?sio kweli.Wenyewe hawalii lakini sauti zao za kulia huonekana katika matendo yao.Mtoto anaweza kuwa mwizi,mvuta bangi,kuvuta madawa ya kulevya hata kuwa jambazi,mtukutu hasikii kisa hakupata enough atention kutoka kwa baba.
Baba hakuwepo wala hakuwa good role model kwa kijana wake si kwa tajiri wala maskini.Baba unaweza kumpa mwanao kila kitu hasa wenzetu matajiri lakini kama haupo pale kihisia upo busy kusaka mahela ni kazi bure.

11 Comments

 1. Mama 2 (Mrs M)

  May 15, 2013 at 1:59 pm

  Kweli kabisa Dina! Hawa wanaume wanajifanya wako busy, halafu mwisho wa siku wanawake ndo tunaonekana kama tunawaharabu watoto kumbe, watoto walikosa attention kutoka kwa baba!! Nitaitafuta niiangalie. Thanx!

 2. Anonymous

  May 16, 2013 at 7:30 am

  tuelekeze hizo movie unanunua duka gani au unaazima shilingi ngapi? na ni wapi ili tukachukue na sisi tuangalie ili tufaudu uhondo

 3. Kivugo

  May 16, 2013 at 8:44 am

  Dada Dina asante kwa updates.
  Ni kweli kabisa, malezi ya watoto akina baba huwa wapo busy na kujisahau kwamba uwepo wake kwenye malezi ndio zaidi unahitajika na sio pesa pekee, wapo wengine hulea kwa kutoa maagizo kwa simu akiona hapo hakuna shida ilimradi hela ipo mtoto atapelekwa kokote anapotaka kwenda ila sio na yeye baba bali na mtu mwingine.
  Akina baba tuwe makini na hilo.

 4. Anonymous

  May 16, 2013 at 10:38 am

  thanx Dina nitaitafuta

 5. Anonymous

  May 16, 2013 at 11:21 am

  ntaitafuta mdada. na nikweli kabisa mtoto anahitaji ule ukaribu wa pande zote baba na mama

 6. emu-three

  May 16, 2013 at 12:35 pm

  Mpendwa umemaliza , kazi ni kuacha kununua vitafunio, na kwenda kuutafuta huo mkanda: Kweli, `Athari za baba kutokuwa karibu na mtoto wa kiume katika kumlea, …na je kwa mtoto wa kike kwa mama je? oh, kisa kitafuta kwenye blog!

 7. viva afrika

  May 16, 2013 at 9:27 pm

  only uwepo wa EVE MENDEZ m totally going for it!!

 8. Anonymous

  May 17, 2013 at 7:47 am

  DINA JANA NILIKUSIKIA KWENYE KIPINDI CHAKO UKIMUWEKEA MAZINGIRA YA USHINDI JACK WOLPER ILI ASHINDE, HIYO HAIKUWA SAHIHI, KAMA UNAAMUA KUMSIFIA MMOJA BASI INGEBIDI WASIFIWE WOTE, NA SIO MMOJA TU ILI WATU WAMCHAGUE. THAT WAS TOTALLY WRONG. WEWE NI MWENDESHA KIPINDI UNATAKIWA USIEGEMEE UPANDE MMOJA, KUMBUKA NASI TUNAOSIKILIZA TUNA AKILI PIA. NI MAWAZO YANGO TU.

  NADHANI UMEONA KUWA WEMA ATASHINDA KWA HIYO UKAWA UNAJARIBU KUMPUNGUZIA SPEED. TAFADHALI USIRUDIE SIKU NYINGINE, WATU WANAKUPIMA KWA VINGI – INCLUDING KATIKA HIVYO VIPINDI VYAKO.

 9. Anonymous

  May 17, 2013 at 9:45 am

  Hapo ndio nakupendaga Dina, mi mpenzi sana wa Movie. Keep it up dling

 10. Anonymous

  May 20, 2013 at 12:37 pm

  Dina hiyo THE WORDS nimeiona nzuri sana lol

 11. Anonymous

  May 30, 2013 at 11:37 am

  the words ni nzuri hakika, niliiona kwenye ndege ya EMIRATES, kwanza inafundisha kutokata tamaa, pia jinsi ambavyo mwanadada alivyokuwa anamsaport mtu wake katika ku make sure kitabu chake kinafanaikiwa. tamu sana jamani. the must watch kwa wapenzi wa movies.

Leave a Reply