Uncategorized

BABA BORA NA WA MFANO

By  | 

Kuelekea siku ya baba duniani…………

Hizi ni baadhi ya Sifa za baba bora:
* Mwenye upendo kwa watoto
*Mwenye kujali watoto wake
*Baba mcheshi anaeweza kucheza na watoto wake japo hii inategemea maana kuna wababa uso wa mbuzi hao.
*Baba mwenye mawasiliano mazuri na watoto wake
*Baba mwenye subira na mvumilivu
*Baba muelewa
*Baba rafiki wa watoto
*Baba mwenye muda na nafasi ya kukaa na watoto wake kuwasikiliza sio baba busy milele hakuna siku haupo busy kwani hizo mali unamtafutia nani?
*Baba mtafutaji na naetunza familia yake kwa kuwapa watoto wake mahitaji yao
*Baba mwaminifu
*Baba mlinzi na mhimili mkuu wa familia na watoto wake.
*Baba anaewajibika kutatua matatizo ya familia kwa hekima na busara.
*Baba anaempenda na kumuheshimu mama wa watoto wake(mkewe).
Hizi ni baadhi tu kama kuna zingine waweza kuchangia.Ntakuletea pia baba asiye wa mfano.

12 Comments

 1. Anonymous

  June 4, 2013 at 1:30 pm

  mmh jamani sasa hawa wababa wa kibongo wanazaa na wanawake kibao sijui atampenda nani kati yao!!!!!! Majanga

 2. Anonymous

  June 4, 2013 at 1:36 pm

  Mi ningemchagua Frank Mgoyo aisee anapenda sana watoto wake

 3. Anonymous

  June 5, 2013 at 6:03 am

  wee nawe! kwani kuna uchaguzi hapa?

 4. RODER

  June 5, 2013 at 9:34 am

  BABA YANGU MCHESHI SANA ANATUPENDA,,YANI NI KAMA RAFIKI SIO BABA,,COZ NIPO FREE FULL UTAN AISEEE,GOD BLES MY PARENTS,,MR AND MRS E.MBUYA,,

 5. Anonymous

  June 5, 2013 at 9:36 am

  da Dinah sijawahi changia lakini leo ngoje nichangie kwa kweli mme wangu Mungu amsaidie na ampe maisha marefu ili aendelee kuona mwanae anayemkuza akikua jamani, Yaani huyu baba hata aniambie nimzalie watoto ishirini nitazaa jamani. alinisaidia sana tangu nilipopta mimba ikiwa na mwezi mmoja mpaka nikajifungua. na siku ya kujifungua alikuwa labor Dinah ananipa massage ingawa nilikuwa saa nyingine namchukia but he was still there for me. sasa ngoje nikuambie kwa nini ni baba mzuri Tangu nimejifungua dear sijui kumlisha mtoto usiku au mchana ni mara chache sana wakati akiwa hayuko nyumbani au kama yuko kazini. anaamka usiku kumlisha mwanae na kumbadilisha. akitoka kazini mtoto akitaka kula ananiambia mamii pumzika mimi nitamlisha miezi tisa ulifanya kazi ya kutosha kumbeba huyu mtoto tumboni. anamuogesha mwanae yaani he does a lot of staff which Iam just admiring him. Mungu ambariki mme wangu jamani. yaani hapa sijui hata nimtafutie zawadi gani ya fathers day ili ajisikie kama he is a good daddy. thanks. mama Cherish

  • Anonymous

   June 7, 2013 at 9:32 pm

   Usiache kumshukuru Mungu kwa kupata mume wa aina hiyo, muombee baraka na afya mana watoto wenu watakuwa wema pia kwenye maisha yao.

 6. Eliud samwel

  June 6, 2013 at 7:30 am

  dada dina mi kuna baadhi ya wababa huwa siwaelewi kabisa ,utakuta mama anapomuadhibu mtoto kwa kukosea jambo lolote yeye kama Baba kwa kuwa anampenda mtoto huyo nae Anampiga mkewa tena mbele ya watoto,sasa sijui hayo nayo ni mapenzi? Ni mimi Eliud samwel

 7. emu-three

  June 6, 2013 at 8:39 am

  Duuh, siku ya baba duniani, kumbe ipo, basi baba bora niyule anayejua kuwa yeye ni baba, na aantimiza ubaba wake na sio ubabe wake, au sio?

 8. ELIUD SAMWEL

  June 6, 2013 at 8:54 am

  hakika baba yangu ni baba bora pia

 9. MOJAONE

  June 6, 2013 at 9:18 am

  Mie ni baba wa watoto 3 wa kike na mmoja wa kiume nawapenda sana watoto wangu wote kwa usawa, pia nashindwa kuelewa eti kuna wazazi hupenda baadhi ya wtt zaidi ya wengine … how come.
  Mie hutimiza wajibu wangu ninaopaswa nifanye.

 10. Anonymous

  June 6, 2013 at 11:38 am

  baba yangu alikua baba mwema sana.masikini mungu amrehemu uko aliko.alikua zaidi ya rafiki.anaupendo sana .

 11. Anonymous

  June 7, 2013 at 9:29 pm

  Dina Mimi Baba Yangu alikufa nikiwa form one, tulikuwa tukiishi kijitonyama, hizo sifa ulizotaja hapo juu i swear God is my witness alikuwa nazo, ingawa alikuwa mkali sana ukikosea lazima kipondo chake utahisi dunia inakumeza, ila akishamaliza kukupa kipondo atakuacha ulieeee alafu ukishatulia lazima aongee nawe, hii ilimpa sifa hata kwa Watu tuliokuwa tunaishi nao hapo kijitonyama yani ali influence hata vijana kujaribu kufanya alivyokuwa akitufanyia.

  Maajabu nami Mungu amenibariki nimepata Mume wa mwenye hulka hizohizo, yani Mimba ikiingia tunaibeba wote mpaka mtoto azaliwe, mi kazi yangu kubwa inakuwa kunyonyesha, kabla hajaenda kwenye shuhuli zake anahakikisha asubuhi anamlisha mtoto, anamuogesha anamvalisha anamlaza ndo anaondoka, wakati huo anani encourage mimi nipumzike ili akiwa hayupo anajua nitakuwa niko busy, yeye huwa haesabu ya kuwa housegirl ndo wa kulea mtoto wake,majukumu tu ndo yanamlazimu aruhusu msichana awe na muda na mtoto.Ki ukweli am very Lucky na ninamshukuru Mungu mno kwa kunipa Mume Mwema kama huyu.
  Wakati mwingine watu hufikia kusema ni mume bwege, but yeye hajali, anasema watoto wake na mkewe ndio ndugu zake, mali yake na utajiri wake hivyo anahitaji kuitunza tunu hiyo.
  Sisemi kama hana mapungufu anayo tena mamkubwa ila kwa jinsi anavyotutendea mimi na watoto kiukweli sioni shida kuwa naye,nazidi kumpenda kila kukicha NAMUOMBEA MAISHA MAREEEEFU NA YENYE AFYA NA FURAHA MUME WANGU, BABA WA WATOTO WANGU.NAKUSHUKURU MUNGU KWA KUNIPA ZAWADI ADIMU KAMA HII.
  WAKATI MWINGINE NAHISI KAMA MUNGU AMENIREJESHEA BABA ALIYETUACHA TUKIWA BADO TUNAMUHITAJI.PENGO LAKE HALIJAZIBIKA LAKINI MUNGU AMENIPA FARAJA NYINGINE.
  HAPPY FATHERS DAY TO ALL GOOD MEN OUT THERE.

Leave a Reply