Uncategorized

HABARI ZENU MABINTI?SOMA HAPA.

By  | 

Kuanzia sasa katika blog hii nitakuwa nawasaport wasichana/mabinti katika kazi zao mbali mbali.Nafanya bure bila malipo.Najua na kuelewa ugumu wa maisha ulivyo na harakati za msichana katika kujikwamua kiuchumi.Na zaidi ni wale wanaotumia ubunifu hasa kazi za mikono yao katika kujiendeleza.Nitakuwa nawaweka hapa ili wadau muweze kuwaunga mkono katika kazi au biashara zao.Kwa kununua na ushauri pia.
Kilichonisukuma kufanya hivi ni namna ambavyo wasichana wamekuwa wakinifata au kuniandikia email,meseji na hata kupiga simu ili kuomba ushauri katika maeneo wanayoyafanyia kazi.Wengi huniomba mawazo au kudevelop idea aliyokuwa nayo.Japo wengi huwa nawarudisha kwani nataka kusikia mawazo mapya au ubunifu na sikudandia idea za watu wengine.
Sio kwamba najua kila kitu labda ni namna wao wanavyokuwa na hisia za kuona naweza kuwapa mwanga.
Napenda nione msichana anaumiza kichwa kubuni jambo fulani.Apiganie ndoto yake,aondoe ile akili ya kufanyiwa mambo au kupewa,awe na njaa na ari ya kufanikisha atakalo bila kukata tamaa.
Kwa hiyo kama una kazi yako,mradi wako fulani na unahitaji sapoti yangu karibu sana.Nitawafikishia wadau kwa maoni au kukuunga mkono.Hii itakuwa hatua ya kwanza,hatua ya pili bado nawaza nikipata ntawafahamisha.Nitumie picha na maelezo na picha ziwe na quality.
Kumbuka nimesema wasichana.Sijui usichana unaishia miaka mingapi?ngoja niwaze.
email yangu ni dina_marios@yahoo.com

26 Comments

 1. Anonymous

  June 7, 2013 at 11:32 am

  that's good idea Dina Mungu akubariki sana plan yako ibarikiwe Mungu azidi kukunyanyua na kukupa maarifa na upeo wa kuweza kuona mbali zaidi uzidi kusaidia na wengine God bless you

 2. Ruky

  June 7, 2013 at 4:13 pm

  safi sana…

 3. Anonymous

  June 7, 2013 at 7:59 pm

  gud dada dina,keep it up!

 4. emma kahere

  June 8, 2013 at 2:50 pm

  Yea gud idea kiukweli DINA,ila me nina ushaur kidogo juu yahili.,weka ambao ndo wanachipukia ucwaweke wale ambao tayar biashara zao zinajulikana

  • dinamariesblog

   June 11, 2013 at 12:43 pm

   nataka wanaochipukia wazito tutakaa mezani kibiashara zaidi heheheh

 5. Anonymous

  June 8, 2013 at 8:22 pm

  Hongera sana kwa juhudi mbalimbali unazozifanya my dia. Mungu akubariki sana.

 6. Anonymous

  June 9, 2013 at 10:36 am

  Mungu Akubariki Dina kwa kuwa na moyo mkubwa kama wako na kufikiria wengine,ni kweli ukiwa mwanamke au msichana kuna matatizo ya hapa na pale,Asante Mungu kwa kutujalia mtu kama Dina anaetumia muda wake mwingi kuwaza atatusaidiaje sisi wasichana,love u Dina

  • dinamariesblog

   June 11, 2013 at 12:44 pm

   asante basi mkiwaona huko washaurini wafate utaratibu huu!!

 7. Anonymous

  June 10, 2013 at 8:07 am

  una kila sababu ya kushinda ile tuzo

 8. Anonymous

  June 10, 2013 at 8:16 am

  Big up dina.love u mingi mingi

 9. Anonymous

  June 10, 2013 at 6:58 pm

  Tumekushtukia mburula. Unajidai eti huwa nawarudisha wakaumize vichwa kumbe unataka kuyatumia mawazo yao ili ufanyie project zako. Mweeee!
  Na umejua wasichana ndio wengi wenye mawazo mtaji(capital thoughts) duuuu. Kwahiyo hapo wewe ni kama unadesa ideas zao./propsal zao. Haya bibi

  • dinamariesblog

   June 11, 2013 at 12:42 pm

   heheheeheheheheheh kipenzi nina ideas mpaka naumwa kichwa.Hujui unachokinena niache kama nilivyo fanya yako usipoteze muda na yangu utakesha!!

  • Anonymous

   June 12, 2013 at 4:50 am

   Nimeipenda hiyo quote, inafaa kuwekwa kwenye khanga "Fanya yako usipoteze muda na yangu utakesha!! …DM.

 10. Anonymous

  June 11, 2013 at 8:46 am

  hakika mungu kakujalia kipaji,hongera sana kwa kuwa mbunifu Dina,love u saaaaaaaanaaaaaaaaaaaaa.
  Mungu azidi kukubariki kwa kila utakalo lifanya na katika kutimiza lengo lako hili la kuwasaidia mabinti.

 11. R

  June 11, 2013 at 1:05 pm

  gud idea dada dina,,wenye chuki binafsi tupa kapuni,,songa mbele na maisha yako

 12. Anonymous

  June 12, 2013 at 5:25 am

  da dina hngera kwa hili mungu akuongoze ktk hilo ufankiwe zaidi!! hao wanaoponda achana nao inaonekana jamaa hapo juu anataka awe kama ww apate angalau na yy watu wakamuombe ushaur ila kashndwa na hata weza coz hana busara!! haters wapo kla semehem ktk jamii yetu wazoee wackuumize kchwa!! all da best

 13. Anonymous

  June 12, 2013 at 9:50 am

  Hongera mummy na usikate tamaa japo kuna watu wanataka kukurudisha nyuma huyo ni ibilisi hataki uzifikie baraka Mungu alizokuandalia.

 14. Anonymous

  June 12, 2013 at 4:18 pm

  Uwiii ungekua na ideas kibao ungekua clouds kwa vilaza !!!my fooot

 15. Anonymous

  June 14, 2013 at 9:03 am

  Ukomo wa umri tafadhali.Hongera kwa idea

 16. Anonymous

  July 1, 2013 at 1:44 pm

  hongera dina wakatishaji watu tamaa hawakosekanagi kwani wewe hapo juu umelazimishwa kuweka idea yako humu hahaha maneno ya mkosaji, dina songa mblele na mungu yu pamoja nawe

 17. fatuma Hans

  July 2, 2013 at 8:41 am

  ahsante dada Dinah kwa mchango wako hasa kwa sisi wasichana Mungu akubaliki!

Leave a Reply