Uncategorized

MAMA ALIYEKAA JUU YA PAA KUPINGA NYUMBA YAKE KUUZWA NA BANK!!

By  | 
Huyu mama alikaa juu ya paa kwa siku tatu tangu jumamosi kupinga nyumba yao kuchukuliwa na bank.Anasema mumewe alimdhamini mtu alipochukua mkopo bank miaka mingi iliyopita na kushindwa kulipa mkopo huo.
 Kwa mujibu wa maelezo yake kesi yao bado ipo mahakamani kwani tayari yule mdaiwa kuna mali zake zilizotaifishwa.
Mdaiwa alikopa ml 240 wameuza nyumba zake 2 na mabasi mawili.Wenyewe wanachodai katika hilo deni imebaki tsh ngapi na wao watoe?kama nyumba iuzwe watoe deni la bank na hela inayobaki wabaki nayo wao.
Nyumba ipo mbezi Tangi bovu na inaeneo kubwa sana mama anasema hata akiuza si chini ya ml 500 iweje atolewe kwa ml 240?wakati mdaiwa nyumba zake mbili zimeshachukuliwa na mabasi mawili yale makubwa ya safari za mikoani.Hiyo ml 240 haijatimia tu?na kama bado kiasi gani kimebaki?
Ndani ya nyumba vitu walishachukua hao watu wa auction mart  ndani kweupe.Na wakati haya yakiendelea hakukuwa na amri yoyote iliyotoka mahakamani wala hawakuwa na kibali cha mahakama.
Gea alimfata huko huko juu kumsikiliza na tumemsikia leo kwenye heka heka.Kesho pia itaendelea.
Hapa mabaunsa wakimfukuza
Wamemshika
Wamempa kanga nyingine 2 ajifunge maana hakuwa na nguo zaidi ya hiyo kanga moja.
Eneo la nje kulivyokuwa
 Nje ya geti la hiyo nyumba
Chumba cha habari cha clouds fm kimeenda kufatilia hapo bank ya Tanzania Investment bank(TIB)kujua kulikoni??
Maana wakati haya yakiendelea hiyo jana inasemekana hii nyumba imeshauzwa.Inauzwaje na shauri lipo mahakamani?Na jana mume wa huyu mama alikuwa mahakamani maana ilikuwa siku ya kesi kuendelea kusikilizwa.
Na mumewe alirudi na oda maalum kutoka mahakamani kuwa nyumba hiyo isiguswe na vitu vyao virudishwe.

42 Comments

 1. Anonymous

  June 13, 2013 at 11:27 am

  Majanga

  • Anonymous

   June 22, 2013 at 7:49 pm

   kuna maelezo yametolewa na gazeti jina sikumbuki wanasema huyu mama hakuonewa ila alipewa taarifa tofauti kutoka na mumewe, vyanzo vinadai yeye sio mke wa ndoa wa mwenye nyumba mke wa ndoa ambaye aliejenga hii nyumba wametengana na baba mwenye nyumba ndio akaingia huyu mama kwenye nyumba, huyu mama pamoja na kuishi miaka kadhaa na baba hana ndoa halali yenye cheti lakini ndio aliekua akiishi kwenye nyumba na baba kama mke na mume
   pili wanasema baba mwenye nyumba alimsaidia rafiki yake aishie Iringa kuchukua mkopo benki ambapo hii nyumba iliwekwa rehani vyanzo vinasema biashara haikwenda vizuri na rafiki akashindwa kurudisha mkopo wa benki ndipo benki ilipeleka shauri mahakamani, na waliitwa mara kadhaa ila walipuuzia kwenda kusikiliza shauri ndipo mahakama ikatoa amri nyumba ipigwe mnada kulipa deni alilokopa rafiki wa Iringa.
   kutokana na sakata hilo mke wa ndoa ambaye sio huyo mama alikwenda mahakama kudai nyumba ibadilishwe jina kwani sio ya mume peke yake na yaliyofikiwa huko hayakuandikwa na chanzo cha habari
   ukweli wa hii kesi wanaujua wenyewe na benki isitupiwe lawama tu kwani watanzania wengine ni wepesi kukimbilia kwenye vyombo vya habari na kulalamika wananyanyasika wakati wanaujua ukweli uko wapi, watanzania tuna katabia kakudharau amri ya mahakama na sheria za benki mambo ya rehani ni mabaya hasa unapoweka mali ya familia na rafiki naye sasa sijui anasemaje kuona mwenzako aliekudhamini anaadhirika na familia yake kwa upendo wake kwako mhh inatia huruma

  • Anonymous

   June 27, 2013 at 6:24 am

   Mimi sijapenda huyo mama kupanda kwenye paa, kwani haki ndo yapatikana huko juu? haki yapatikana kwa kwenda kwenye vyombo husika, hakuwa na sababu ya kukaa hapo juu siku zote hizo halafu mwanamke? na nimesoma hapa mwenyenyumba kaenda kuweka stop order ya kutokuuzwa na ndivyo inavyotakiwa. Hata wangekuwa na order ya kubomoa kukaa juu ya paa hakusaidii si watakushusha na greda lao.? Kwanza na mpaka benki ipige mnada nyumba ni kwamba mwenye mkopo hujatoa ushirikiano wa kutosha kwao, watu wanapewa grace period hata ya miaka miwili ili mradi unawaambia ukweli. Dina naomba ufatilie upande wa pili mi naona kuna zaidi ya hapo inavyoonekana. na

 2. fadhil linga

  June 13, 2013 at 11:46 am

  Huu ni utapeli wa wazi kabisa….afadhali mama kakomaa maana wakilemaa inauzwa kweli maana hizi fincial institution zote wizi wizi tu

  • Anonymous

   June 14, 2013 at 11:40 am

   KWANZA NI BENK GANI HIYOO MANAKE KWENYE MABENK NAKO NDIO USISEME MAJANGAAA

 3. emu-three

  June 13, 2013 at 12:11 pm

  Utu , Ubinadamu umeshatoweka,….

 4. Anonymous

  June 13, 2013 at 12:50 pm

  du mwanamke wa shoka ….ngangania chako Mama Dunia hii wamebaki Manyangau …Vya wenzao vitamuuuuuu , si wajenge za kwao ki vyao

  MUNGU ANAKUTETEA …UBARIKIWE

 5. Anonymous

  June 13, 2013 at 1:01 pm

  Jamani inauma sana kuona mtu ananyanyaswa kwaajili ya mtu mwenye pesa..Hapo itakua ni mtu mwenye pesa zake anaitaka hiyo nyumba na anatumia mabavu ya pesa kunyanyasa familia ya huyo mama..Jamani watu tunapoelekea ni kubaya sana kwakweli tunadhamini pesa kuliko utu wa mtu..Lakini malipo ni hapahapa duniani huyo anayemfanyia huyo mama hivyo ipo siku jua litamuwakia..Imeniuma sana kwakweli kuona watu wananyanyasika kwa kudai haki zao…Mungu atusaidie..

 6. Anonymous

  June 13, 2013 at 1:27 pm

  Jamani dada Dina ongela kwa kazi nzuri ila unaona Bank zetu zinavyotumiwa na watu wenye mimi najua kuna mtu atakuwa anaitaka hiyo sehemu watu wabaya. Nilimsikia huyo mama akisema waambiwe hilo deni lilobaki walilipe wao wanakataa kwa nini wanakataa wanasiri gani hiyo sehemu? bora watu tusikope Bank tuimalishe vikobe ndo watu wa Bank wakome
  mwanamama

 7. Anonymous

  June 13, 2013 at 2:24 pm

  Jamani Mungu awasaidie haki itendeke, anatia huruma kwa kweli!!

 8. Anonymous

  June 13, 2013 at 6:19 pm

  huy mu kaonga,mna kma mdaiwa kauiwa nyumba zake mbili na magari tayari pesa zao zimetosha sema nidhuruma tu watu hawatendewi haki Tz.pole mama

 9. Anonymous

  June 13, 2013 at 7:27 pm

  Big up kwa Gea….pole sana mama kwa yaliyowakuta naamini sheria itachukua mkondo wake.

 10. Ruky

  June 13, 2013 at 7:54 pm

  SEREKALI YA MTAA MUDA WOTE ILIKUWA WP JAMANI???INAUMA SANA..TUONE MWISHO WAKE..ALAFU DINA MBONA KILASIKU KSRIBIA NA MWISHO YA HEKA HEKA HUWA MNAONDOKA ON LINE MNAONYEZAGA NINI MAANA MKITOKA NYIE INAENDELEA..NIMETUMA COMENTS YAKWNZA IMERUKA SIJUI KM IMEFIKA

 11. Anonymous

  June 14, 2013 at 4:54 am

  Ni mbaya na wawatu????????utu umeenda wapi?????/ UFISADI MTUPU!!!!!!!! ULAFI!!!!!!!!!1 AM SO FUCKED UP WITH THIS COUNTRY. Wapi sheria????? what on earth is going on here….. MAMA NAKUJA HUKO HUKO JUU NIKUSAIDIE,NIPO NATAFUKA AK47 AKIJISOGEZA TU MTU TUNAMFULIA MBALI!!!!!! pumbavu sana mtu anajinyima raha zote za dunia ajengee familia yake nyumba halafu nyoko nyoko …… semeni ni shing ngapi imebaki basi! ala hapana chezea mali za watu!!!

 12. Anonymous

  June 14, 2013 at 7:36 am

  That is mistreatment to this poor woman! Human rights should play its part, How can someone be this unfair?
  Im loath to the auction Mart.

 13. Anonymous

  June 14, 2013 at 9:39 am

  nitafurahi kusikia huyu mama amesaidiwa

  • Anonymous

   June 14, 2013 at 10:29 am

   Duu huyu mama ni jembe bora alivyokomaa maana ufisadi umezidi

 14. linda

  June 14, 2013 at 10:33 am

  pole mama etu Mungu atakusaidia…
  Hakika dunia imejaa kila aina ya majaribu
  Eeee Mungu sikia kilio cha mama huyu..

 15. Anonymous

  June 14, 2013 at 10:48 am

  Mungu amtie nguvu huyu mama haki haipotei na aweze kusaidiwa jamani uonevu ni dhambi sn

 16. Anonymous

  June 14, 2013 at 11:43 am

  claus mko juu sana msaidieni huyo mama apate haki yake, ili muendelee kuwa supar braad

 17. Anonymous

  June 14, 2013 at 12:24 pm

  watanzania tunapenda san huruma za watu hata km makosa ya kwetu.DINA UKUBALANCE story,kuna pande tatu husika hapo kwenye ilo sakata,t.i.b, msama auction mart na huyo mama,lakini inaonekana mmefanya mahojiano na upande mmoja tu.mmepewa uongo mwingi sana na huyo mama,ambaye kwanza si muhusika wa hiyo nyumba.huyo mama alipanda juu ya paa siku ya jtatu asubuhi sio jmos km alivyowadanganya.aliyefungua kesi ni aliyekuwa mke wa mwenye nyumba na kesi imefunguliwa mahakama kuu kitengo cha ardhi ikipinga kubadilishwa kwa hati kwenda kwa mmiliki aliyeinunua na sio kupinga kutolewa ndani ya nyumba.walikwenda kuomba order mahakama kuu kitengo cha ardhi wakagonga mwamba ndipo wakakimbilia mahakama ya kinondoni kuomba stop order ya kutotolewa ndani,wakati washatolewa ndani.na kwa mujibu wa kisheria hiyo stop order ilikuwa batili kutolewa na mahakama ya kinondoni.leo walikuwa na kesi mahakama kuu kitengo cha ardhi,fuatilia mwenyewe upate ukweli.

  • dinamariesblog

   June 17, 2013 at 1:07 pm

   Msama alikataa kurekodiwa na alikuwa pale baada ya kuagizwa na bank kwa mujibu wa maelezo yake.Na bank tumeenda ofisini kwao wakasema shauri lipo mahakamani hawawezi kuongelea.Kama kuna mtu mwingine ni nani maana maelezo tuliyopewa na wahusika ni haya!!!Labda turudi tena kuhoji maelezo haya kwa huyo mama kama yana ukweli.

  • Anonymous

   June 17, 2013 at 11:22 pm

   Dina hata usiangaike kuwajibu watu kama hao ndio hao hao wenye roho zao mbaya wadhulumaji wakubwa alitaka story gani tena hapo zaidi ya iyo kama anajua ukweli sana si aende mahakamani uko akatoe ushahidi?? kuna watu yani kila kitu wanajua sana ndio nyie mnawajua watu kuliko wanavojijua si ajabu tu naye kasimuliwa basi povu linamtoka ova alikuwepo eneo la tukio

 18. Anonymous

  June 14, 2013 at 12:35 pm

  Pole sana mama, cjui hii TZ na watu wake tunaelekea wapi.
  Haaaa!!! Gea we kiboko mmempandia huko huko…kikikwii umeshingikana mama.

 19. Anonymous

  June 14, 2013 at 12:50 pm

  Kwa kweli nimesikitika sana. Kibaya ni kwamba mama anaeleza kua amewasiliana hadi na vyombo vya usalama lakini hajapata msaada wowote. JE NI WANGAPI AMBAO WANANYANYASIKA NA KUDHULUMIWA MALI ZAO NA HAO WENYE FEDHA BILA SERIKALI KUWASAIDIA?
  Nimependa moyo wa huyu mama haki huwa haiombwi hivyo watanzania inabidi tuamke serikali inadhulumu raia wake hivi hivi. Kwani pamoja na kuwa sijui sheria lakini hapo kuna uvunjifu wa haki za binadamu ulio wazi kabisa.

 20. Anonymous

  June 14, 2013 at 1:01 pm

  Hi Dina kwanza mimi nampongeza sana mama huyu ni jasiri kupita kiasi, halafu huyu mumewe mbona haonekani au inakuwaje siwezi kukubali mke wangu afanyiwe vitu vya namna hiyo. kwa kifupi dina nyie ndio peoples station tunaomba huyu mama asaidiwe mpaka mwisho hata mkipitisha mchango wa sh elfu kumi kumi tutachanga hiyo bank ilipwe mama arudishiwe nyumba yake.na tunaomba msiishie hapo tunataka kujua mwisho. na ni mwenye pesa gani huyo ambaye mpaka anakua na jeshi na polisi wake tumechoka na uonevu. lazima Jeshi la polisi litoe maelezo wao walikua wapi wakati familia inanyanyasika namna hii, haya mambo yakiachwa watu tusio na uwezo tutanyanyasika sana hii nchi imekua ya wanyenacho

 21. Anonymous

  June 14, 2013 at 1:13 pm

  jamani asaidiwe Dinna sauti yako naamini itasaidiwa wanyonge,sikuzote tunanyongewa umaskini taabu

 22. Anonymous

  June 14, 2013 at 6:30 pm

  Huyu mama kwa namna moja au nyingine ana haki zote kwa jinsi nilivyomsikiliza ktk hekaheka kuanzia juzi na ni matumaini yangu kwmba sheria itachukua mkondo wake na hatimaye huyu mama pamoja na familia yake wanatendewa haki,

 23. Anonymous

  June 15, 2013 at 8:40 am

  Hakuna wezi na mafisadi kama hawa watu wa Auction mart ni wezi tena sana wao kazi yao kukazania jinsi gani ya kupata pesa bila ya kufata sheria, kwanini wasihoji nyaraka za mahakama zinazoruhusu mtu huyo kuhamishwa na kuuziwa nyumba yake. WAKOMESHWE.

 24. Anonymous

  June 15, 2013 at 4:12 pm

  Yan kiukwel nimempenda xana huyu mdada…yan hv ndivyo wanawake 2navyotakiwa 2we wanawake 2cwe wanyonge Dunia hii ukizubaa 2 umeula wa chuya. pole xana mama angu Mungu atakuxaidia yataisha na haki yako utaipata…hv hao matapeli Mungu huwaon jaman! yan naumia xana nahc kama ni me, yan m2 ananyanyacka na jasho lake! Insh Mungu atakuxaidia mama angu

 25. Anonymous

  June 15, 2013 at 8:54 pm

  DINA…PLEASE FATILIA HUYU MAMA HASAIDIWE..NAHAPO KUTAKUWA NA MLAFI ANATAKA HIYO NYUMBA BILA AIBU..

 26. Anonymous

  June 16, 2013 at 9:07 am

  nimeumia sana kuona unyama aliyefanyiwa huyo mama na familia yake, kwani haikubalikik kisheria kabisa kwanini sheria zisifuatwe, hao pia watu wa auction mart ni wahuni tu na hawajui taratibu zozote za kisheria inauma sana, naomba serikali ilifuatilie hilo jambo na itoe majibu na mlolongo mzima wa kesi uwekwe hazarani na mwisho wafunguliwe mashtaka na kumlipa fidia huyo mama na familia yake. hiyo kampuni ya auction na mmiliki wake ni matapeli naomba serikALI iwachunguze maana sio jambo la kwanza hilo, wamefanya mengi kama hilo na mtu asipokuwa strong wanachukua mali kama ni viwanja au nyumba. natamani kuona sheria ikishika mkondo wake tuwatoe hawa wababaishaji hasa hao auction mart wananiuzi sana kujichukulia sheria mkononi bila utaratibu nadhani pia wanatatizo la elimu na utambuzi wa mambo. huku wanazulumu huku wanajifanya kusaidia yatima au kuandaa matamasha ya dini, hivi kama unauelewa unawezaje kumtukuza Mungu wa kweli alafu ukafanya unyama kama huo.

 27. Anonymous

  June 17, 2013 at 8:11 am

  Gea Habibu Shikamoo! Duuh! kila kazi ya changamoto zake mpaka juu ya PAA!!! SHIKAMOO TENA

 28. Anonymous

  June 17, 2013 at 8:16 am

  Dina tunaomba utupe updets za hii habari mpaka mwisho wake……mana nimeskia eti kumbe huyu mama wala sio mke wa huyu baba ni kimada….kama kweli chakujipandisha juu ya paa nawakati hakununua hata tofali la hii nyumba inahusu????????????

  • Anonymous

   June 17, 2013 at 11:32 pm

   Wale wale kasoro maandishi mpoje viumbe nyie?? kabla ujasema kitu ulichoambiwa uwe unatafakari kwanza kwa ufahamu wako mdogo ulionao ivi unadhani uyu mama ni chizi kiasi gani kutetea ivo iyo nyumba ? sawa uyo baba alikuwa na mkewe je uyu mama kaishi muda gani na uyo baba je uyu mama ajazaa na uyo baba ?? anachokifanya uyu mama ni sahihi kabisa anatetea haki ya watoto wake kisheria watoto wa uyu mama nao pia wanahaki yakupata sehemu ya iyo nyumba.. je unajua uyo baba aliachana vipi na mkewe ? Kabla ujashadadia kitu chochote tafakari kwanza angalia pande zote ndipo useme kitu tuache ushabiki usio kuwa na maana leo yeye kesho wewe

 29. Anonymous

  June 17, 2013 at 11:35 pm

  Dina uyu msama si mlokole mbona anatenda mambo ya ajabu hivi mbona bihashara za nyimbo za dini zinamlipa sana kwanini kaingia kwenye bihashara ya unyanganyi kweli pesa ulimsulubisha YESU msalabani

  • Anonymous

   June 20, 2013 at 1:50 pm

   Hapa kuna mambo yakujiuliza unapokopa kuna masharti hata kama wewe ni mdhamini naunaambiwa kabisa interest rate na bank sio wajinga wanakumbushia kwa barua usipolipa kwa wakati, hivyo utapewa deni lako kisha usipolipa hilo mkataba ulosaini wa interest unatumika maana hizo ni pesa ambazo wengine pia wanataka zikopa.Hivy kama umekopa 200 kuna muda unapewa wa kulipa na labda itakuwa 230 ukipita unapigiwa mahesabu ya deni lako na interest. Huu ndo utaratibu mikopo siyakutumia ovyo tujenge taratibu za kulipa haijalishi umedhamini, maana wote mwa saini karatasi moja. Hizi sio grant money

 30. Anonymous

  June 19, 2013 at 6:57 am

  Dina na Gea big up sana. NIMESOMA COMMENTS ZA WENZANGU HAPO JUU ILA NASHANGAA KILA ANAYEJARIBU KUULIZIA UPANDE WA PILI ANAAMBIWA MNAFIKI NA MANENO KADHA WA KADHA YA KEJELI. MIMI BINAFSI SIJUI A WALA B YA HUU MKASA NA PIA NINGEPENDA KUFAHAMU AU KUELIMISHWA MADAI YA PANDE ZOTE ZINAZOHUSIKA. BAHATI NZURI UMEELEZA MAELEZO YA UPANDE WA HUYU MAMA NIMEELEWA KATIKA HILO. KWA MSAMA NA KUNDI LAKE MIMI SIWEZI KUMLAUMU NA PIA NINGEOMBA WATU WAMWELEWE MSAMA KWAMBA HII NDIYO KAZI YAKE INAYOPELEKA WATOTO WAKE CHOONI. YEYE ANAELEKEZWA TU FANYA HIVI NA MARA NYINGI HUWA WANAFANYA HIVYO KWA MAELEKEZO YA BARUA SIYO KWA MDOMO. KWA HIYO KWA ALICHOKUWA ANAFANYA MSAMA MIMI NAWEZA KUMTETEA KUWA ALIKUWA ANAFANYA HIVYO KWA MUJIBU WA TARATIBU ZA KAZI ZAKE NA MAELEKEZE YA KISHERIA YA MAHAKAMA.

  ILA UPANDE WA WADAI HAPA MIMI NDIO NAONA TATIZO NA NDIPO NINAOMBA DINA NA TIMU YAKO MTULETEE TAARIFA KAMILI KUHUSU MADAI YA HAWA JAMAA. BAADHI YA MASWALI YALISHAULIZWA LAKINI HAYAJAPATIWA MAJIBU. MFANO NI KIASI GANI KINADAIWA HADI SASA NA NANI ANAYEDAI? NI UTARATIBU GANI ULITUMIKA KUONDOSHA SAMANI NA VYOMBO VINGINE VYA NDANI KATIKA HIYO NYUMBA.NYUMBA ULISHAPIGWA MNADA AU BADO? HUYU ALIYEFANYA HIVI KUHAMISHASHA SAMANI NI MMILIKI MPYA ALIYEINUNUA HIYO NYUMBA AU NI NANI NA KWA AMRI YA NANI? KUNA MAELEZO HAPO JUU KUWA BABA MWENYE NYUMBA HAWAKO KWENYE GOOD TERMS NA HUYU MAMA JE HAYA NI YA UKWELI? KAMA NI YA UKWELI HUONI KWAMBA PENGINE BABA ALIUZA NYUMBA BILA KUMSHIRIKISHA HUYU MAMA? MASWALI NI MENGI DINA UPANDE WA PILI KIUKWELI TYUNGEOMBA UFUATILIE MAJIBU ILI NA SIS TUWEZE KUTOA CONSTRUCTIVE COMMENTS BADALA YA KUEGEMEA UPANDE MMOJA TU

 31. Anonymous

  June 25, 2013 at 10:33 am

  Mimi ndio Maana nilikopa BARCLAYS na sijalipa na sitegemei lipa na nipo nje ya nchi na si rudi bongo kesho wala kesho kutwa,mdhamana wangu ulikuwa kazi na kazi sina so watachora chini, Mabenki yote ni wezi tu, Benki kuu wamewapa muongozo wa riba at 8 – 14% tu wao wanatupiga 21% yani hata Mungu mwenyewe anapewa 10% who is Mabenki mpk wapate 21%. Mama hongera sana kwa kukomaa.

 32. Anonymous

  June 25, 2013 at 2:13 pm

  GEA hongera mama unafanya kazi kubwa sana. Hongera sana.Ila nashangaa kila kukicha sifa anapewa Dina wakati anayeumia ni GEA. LEO TENA inasikilizwa kwa ajili ya hekaheka za Gea na wala siyo Dina. GEA atendewe haki jamani. Dina ina maana hujisikii hata aibu kidogo. Duu una roho ngumu!!

 33. james mark

  June 25, 2013 at 5:03 pm

  Mambo mengne yanakela sana tena sana

 34. Anonymous

  June 30, 2013 at 12:48 pm

  Nashangaa watu wanaotoa maneno makali sijui ufisadi,unyanyasaji, n.k. wakati hamjui stori kamili mnaegemea upande mmoja tu na kuhukumu. Dina, msipokuwa makini kwa kutokubali kutoa stori bila kubalance mtakuwa mnatumiwa bila wenyewe kujua, na mbaya zaidi mtakua mnashirikiana na wahusika kupotosha jamii kama hapo mlivyomsaidia huyo mama kupotosha jamii. Ukweli anaujua mwenywe kujitia ana uchungu na nyumba wakati hakuwepo hata inavyojengwa na kuwekwa rehani.

Leave a Reply