Uncategorized

MSHINDI WA DINNER WITH DINNER…BLOG HII YA DM IMEMSAIDIAJE?!

By  | 
Dina hongera kwa kubuni hii ‘tuzo’ ya Dinner with Dina kwa wadau wako wa
DM blog, kusheherekea tuzo yako ya mwanamke wa mwaka 2013. Blog yako
imenisaidia si tu moja kwa moja kutoka katika post zako, bali hata kwa
wachangiaji. Nami naomba niwashukuru wachangiaji kupitia kwako, ambaye ndiye
mwanzilishi wa DM blog. Hata kama sitabahatika kuwa katilka list ya watakaopata
chance hii, lakini ni sehemu maalumu pia ya kuonyesha appreciation, kwako wewe,
na kwa watoa comments. Mimi ni mama wa watoto wawili, naishi Dar, ni muajiriwa
.
           Dina mimi niliwahi kuingilia mada katika comments, sikumbuki ilikuwa ni
ya nini. Niliingilia kwa kuomba wana DM Blog wanisaidie nimpe nini/dawa gani
mwanangu hataki kula chakula vizuri. Pamoja na kwamba niliandika kama comment
out of topic lakini nilipata msaada mkubwa sana, mtoto wangu akaanza kula
vizuri. Kwa vile niliweka namba ya simu nilipigiwa simu na watu zaidi ya 10, na
kuandikiwa messages, hadi na akina baba wakinishauri. Nakumbuka mwingine
alitaka kabisa kumfanyia kama monitoring baada ya kumpa dawa. Lakini dawa
iliyonisaidia saana ni ya mchangiaji mmoja aliyenielekeza kwenda kununua pale
Nakiete, akanipa na jina na bei yake. Ilimsaidia sana mwanangu, akawa anakula
vizuri, afya ikarudi. Pamoja na hiyo dawa kuna mtu mwingine alinishauri jinsi
ya kubadilisha badilisha lishe ya mtoto ili kumwaongezea hamu ya kula, kwa
kuongeza, kwa mfano kwenye uji unaweka chungwa.Pia akanishauri si vyema
kumlisha mtoto vyakula vinavyofanana kila siku, kama ambavyo akina mama wa
Tanzania tulivyozowea UJI
          Dina haikuishia hapo, ikabidi nami niwe mtaalamu wa kushauri watu.
Nakumbuka wamama kama wa 3 hivi walinipigia baada ya miezi kadhaa, na hata
baada ya mwaka kuona kama nilipata msaada nami niwasaidie. Niliwasaidia, na
wakanipa feedback kwamba wamefanikiwa. Pia nimekuwa natoa comments pale ambapo
wamama wamekuwa wanahitaji msaada kama huo kwenye blog tofauti tofauti. Hii
imenisaidia kutokuwa mchoyo wa ku-share vitu nivijuavyo. Kwa mfano kwenye blog
ya Zeze kuna mtu aliwahi kuomba kujulisha jinsi ya kurudisha kitovu kikubwa cha
mtoto . Niliandika kwa comments maelekezo ya kufanya na nikaweka na number ya
simu. Nakwambia nilipigiwa simu! Niliwasaidia watu na walinipigia kunipa
feedback. 
          Naamini kuwa nimekuwa mama ushauri kwa upande wa kule watoto wadogo.
Siku hizi ndugu zangu wakishindwa kulea watoto, ati kisa hawataki kula huwa
nawaambia waniletee, baada ya kama 2 weeks kunakuwa na mabadiliko makubwa.Hivyo
najisikia furaha sana. Na naona Blog yako ndiyo imenipa ujasiri huo wa mimi kuweza kuelimisha wengine.
  Asante!
Hello my dear,nafurahi na moyo wangu umebarikiwa sana na kufarijika mnooo.Nilichogundua nina familia kubwa sana yenye mapenzi tele ya DM BLOG.Nakufahamisha kuwa na wewe umeibuka mshindi wa dinner with Dina.Tumeshawasiliana na tutazidi kuwasilina.
Asante!

30 Comments

 1. Anonymous

  June 4, 2013 at 12:11 pm

  Jamani huyo dada amenigusa sana, na mimi naomba anishauri kuhusu mtoto asiyependa kula, naomba anielekeze ni dawa gani aliyompa mwanae na mimi nikaitafute kwani mwanangu hapendi kula kabisa na nimeshahangaika sana bila mafanikio. namba yangu ni 0755 004499.

 2. Anonymous

  June 4, 2013 at 2:12 pm

  Jamani na mimi naomba anitumie jina la hiyo dawa,na haini julishe jinsi ya kurudisha kitovu kikubwa cha mtoto,mtoto wa dada anasumbuliwa sana na hayo matatizo.Namba yangu ni 0715196362.Asante.

 3. Anonymous

  June 4, 2013 at 7:41 pm

  Aisee dada yangu naomba na mimi nisaidie mwanangu chakula kimekuwa kama adui kwake 0754699223

 4. Masterbenny Tanzania

  June 4, 2013 at 9:02 pm

  Tuko wengi nami mwanangu umri ni mwaka na miezi nane anasumbua kula ningependa msaada wako dada dawa hiyo yaitwaje?nakiete naifahamu na labda utuandikie hata hapa ltk comments ka ushauri kidogo!0715 468392

 5. Anonymous

  June 4, 2013 at 11:37 pm

  Ongera kwanza kakupat tuzo,yani nakupendaje ss dada angu?jmn dada dina tupo wengi tunaokupenda sema tuko mbali sana,yn kma mimi sihachi kupitia blog yako kila cku na usipoweka huwa nakasilika kwel kuona haujapost kitu,ni vitu vingi nmejifunza kupitia kwako hasa ujasili na kujalibu pasipo kushindwa,yani ww ni role modo wangu ynnakupnda kuanzia mavazi na hasa ngozi yako yn napenda kuwa soft kma hivyo najarb kutumia kila kitu sema chunus zinanisumbua sana,na mengne nimeguswa na vile unavyowasaidia watto yatima namie nimesema ndani ya nafsi yangu mungu hakinijalia lazma nije kufanya ivyo,na kingne nimekuwa sana muoga wa kupenda au kupenda nikikumbua tukio la yule mama aliefanyiwa ukatili na mumewe wakuburuzwa na gari,nakuona bahadhi ya watu wakipata shida katika ndoa zao,najitaid kufanya kz kwa bidii kma ww ili nitiize ndoto zangu,kingne ulinifanya nijisikie mnyonge sana pale ulipotuma post kuhusu mama ako,yn nilimkumbuka mama angu nikatamn naye angekuwepo japo name niite mamaa,mna neno la mama mdomon kwangu limekuwa geni sikuhzi,nakupenda mna unamajungu wala huna makuu kma walivyo wadada wengne wamjin,nina mengi ila kwa haya ya leo yanatosha.nakutakia cku njema.

 6. Anonymous

  June 5, 2013 at 4:18 am

  Please mie pia jaman naomba nijue what ametumia maana mtoto wangu hataki kula kabisa nampa chakula tofauti kila siku but anagoma kabisa help please

 7. Anonymous

  June 5, 2013 at 6:37 am

  Nami nimeguswa sana na huu ujumbe na mwanangu pia hapendi kula kabisa inafika wakati akiona chakula chake anataka kulishwa huwa anatapika
  nilimpeleka hospital nikapewa dawa za kuongeza apetite ikiwemo PHAROVIT na nyingine ila ndio ilimfanya asile kabisa
  namba yangu ni 0762 902727 Asante

 8. Anonymous

  June 5, 2013 at 6:46 am

  0779748900 namiemwanangu narcolepsy

 9. Anonymous

  June 5, 2013 at 7:44 am

  jaman mdau hapo juu nina tatizo kama lako mwanangu ndio hataki kula kabisa ana miezi nane na kilo zake ni ndogo sana mpaka aibu kusema hakui haongezeki na mie naomba jina la dawa msaada wadau nimehangaika mpaka bac namba zangu ni 0757 792262

 10. Anonymous

  June 5, 2013 at 11:20 am

  Jaman mwanangu pia hapendi kula tunaomba hii iwe mada basi na wengine tuelimike nitashukuru nahangaika kweli sijui nimfanyeje apende kula

 11. Anonymous

  June 6, 2013 at 6:09 am

  dada mwenye ujuzi wa dawa ya kumfanya mtot ale pliz tuambie hata namba yako tukupigie

 12. Anonymous

  June 6, 2013 at 8:22 am

  Dada na mie naomba hiyo dawa ya mtoto kupenda kula jamani.mtoto hataki kula kabisa. Nitashukuru sana. namba zangu ni 0682 – 298702/0178-951383

 13. Anonymous

  June 6, 2013 at 8:42 am

  Hongera dina kwa tunzo yako, nami ni mdau mkubwa wa MD BLOG, nami mtoto wangu hapendi kula kabisa naomba dina huyo dada atuambie hiyo dawa maana ni tatizo kubwa kwa watoto. Ahsante

 14. Anonymous

  June 6, 2013 at 9:52 am

  Nimeanza ku-chat na baadhi, kwa kuwa ni wengi naomba na mama NANDI, kaka wa Tegeta please tusaidiane!

  • Anonymous

   June 9, 2013 at 4:05 pm

   Nashukuru nasubiri simu yako kwa hamu
   Be blessed
   Anon no 7

 15. Anonymous

  June 6, 2013 at 12:30 pm

  mimi sijui nsemeje maana ni kilio changu kila kukicha, mwanangu kagoma kula kabisaa hadi na mie nimepata stress maziwa yamekauka, naomba msaada plz ya hiyo dawa au diet a mtoto, mwanangu ana miezi 8, asante, no yangu ni 0762335081

 16. Anonymous

  June 6, 2013 at 12:54 pm

  Mdau kwanza napenda kukupongeza kwa ushindi uliopata HONGERA kwani ulistahili,, pili Binamu yangu ana mtoto ana kitovu kikubwa kipindi hiki cha mwezi wa 5 hadi wa 6 mwishoni ni anakohoa sana sana haswa majira ya usiku hadi asubuhi saa 2… inampelekea akatapika but sio mara nyingi. Tulimpeleka Hospital na Madokta wanasema tatizo ni kitovu kwani kinapitisha hewa… si madawa hayo aliyonayo utanzani tunataka kufungua Phamacy, na dalili ya kupona hakuna. Please mdau kama uliwai kutuma kwa 8020 Fashion sikuwai kuiona hii kitu, nitasaidie tafadhali dawa yake… ukirudia tena hapa utatusaidia wengi sana, Mungu akubariki. Kama utanisaidia kwa njia ya sms namba yangu ni hii 0656121353.

  • Anonymous

   June 10, 2013 at 10:04 am

   Hii tumemalizana na binamu yako tayari, umri wa kurudisha kitovu kwa uzoefu wa kitundu…ni kuanzia miezi mi3 hadi mwaka. Huyu kapitiliza, ana miaka mi2. Anatakiwa kusubiri miaka mi5 akatibiwe hospital

 17. Anonymous

  June 6, 2013 at 2:35 pm

  Jamani watoto wa siku hizi tatizo ni hili la kutokula yaani ni kasheshe mimi pia nahitaji msaada tafadhali clinic nikienda najisikia mnyonge sana ambavyo mtoto wangu haongezeki uzito vizuri naomba msaada namba yangu ni 0655296753

 18. Anonymous

  June 7, 2013 at 6:55 am

  heeee hivi dinna sikuhizi ni dakitari

  • Anonymous

   June 7, 2013 at 2:21 pm

   ni kupeana mawazo tu kupitia watu mbali mbali watoto wamekua wabishi kweli kula

 19. Anonymous

  June 7, 2013 at 8:55 am

  dada wa diet ya mtoto nisaidie mpenzi. namba yangu ni 0755411143

 20. Anonymous

  June 8, 2013 at 1:53 pm

  Itakuwa bora kama utatuwekea hii mada kwenye DM blog ili tusome wote hasa hii ya kuhusu lishe ya mtoto,kwani mataizo haya ya watoto kutokula yamekuwa sugu kwa jamii.Wasomaji na wapenzi wa DM blog tu wengi na tuna hayo maatizo,hivyo kueleza mmoja mmoja usumbufu utapata mwingi.Nami naomba ushauri namba yangu ni 075403528.KAHAMA Asante

 21. Anonymous

  June 10, 2013 at 7:15 am

  Habari zenu wapendwa,naona katika kutoa maoni yangu na kuomba ushauri nilikosa namba yangu ya simu,mimi ni mpenzi wa DM blog toka KAHAMA,namba yangu ni 0754035248.Naomba ushauri kuhusu lishe ya mtoto asiyetaka kula. BIG UP DM BLOG!

 22. Anonymous

  June 13, 2013 at 4:53 pm

  Jamani wamama wahanga wa watoto kutokula tupo wengi.. hawapendi kula tena ukiwepo ndio kabisaaa. tusaidie mdau hiyo dawa na aina ya vyakula tunavyohitajika kuwapa. namba yangu ni 0715624065 au tupe yako tutakupigia

 23. Anonymous

  October 14, 2013 at 7:57 am

  Hongera sana DINA mpendwa tunajifunza mengi sana kupitia hii blog.Jamani wapendwa kma kuna mtu ameshawasiliana na mtoa mada kuhusu tiba ya mtoto kula chakula anijulishe tafadhali tatizo ni kubwa kwangu mwanangu kula hadi tukabane yaani ni mateso kwakweli namba yangu ni 0766-212172 asanteni naamini mtanipa msaada.

 24. Anonymous

  June 26, 2014 at 8:54 pm

  Dada naomba nisaidie dawa uliyotumia mwanao akala chakula vizuri naomba sana 0757 205620

 25. Anonymous

  November 11, 2014 at 9:00 am

  Naomba msaada na mie watoto wote hawapendi kula. 0715 454874

 26. Anonymous

  December 30, 2014 at 9:45 am

  Naomba msaada na mm pia wanangu hawapendi kula kbs ..0766625762

 27. mary maika

  December 22, 2015 at 7:45 pm

  Wapenzi naombeni msaada pia na mimi mtoto hapendi kula kabisa plz dada angu tusaidie maana wazazi wengi tuna watoto wasiopenda kula na tunalea tu kupitia ushauri wa watu wengi
  Dada plz plz plz umetumia nini kwa mwanao
  Nisaidie
  Tusaidie
  0752 880107

Leave a Reply