Uncategorized

NIMEKUWA BALOZI WA OXFAM TANZANIA WA KAMPENI YA “GROW”

By  | 
Ijumaaa ya tarehe 14 june mimi na wenzangu 6 tulisimikwa ubalozi wa Oxfam Tanzania wa kampeni ya GROW.
Kusimikwa huko kuliambatana na tuzo maalum ya kutambulika kwa mchango wetu katika kampeni hiyo.
Muigizaji maarufu Jackob Steven JB
Mbunifu wa mitindo Tanzania Khadija Mwanamboka
CARTOONIST,MTANGAZAJI na mtayarishaji wa vipindi vya tv Masoud Ally wa Kipanya
Blogger maaarufu Shamimu Mwasha
Mabalozi wengine ni mbunge wa jimbo la Kawe Mh. Halima Mdee na mbunge wa bunge la Afrika Mashariki Mh. Shyrose Bhanji ambao hawakuwepo kutokana na majukumu.
Mkurugenzi wa OXFAM  Tanzania Justin Morgan
TAKWIMU zinaonyesha, tuko watu Billion Saba ulimwenguni hadi sasa.
TAKWIMU hizo hizo zinaonyesha, kati ya hao, takribani watu Billion moja
hulala na njaa kila siku hiyo ikiwa ni tafsiri ya takribani mtu MMOJA
kati ya watu SABA.
USHAHIDI upo kwamba chakula kinachozalishwa kinatutosha kula hadi kusaza.
USHAHIDI upo masokoni na sehemu za kuuza chakula jinsi ambavyo chakula
hasa mboga mboga na matunda vinavyotupwa baada ya kuharibika.
USHAHIDI upo kwenye mashimo ya taka tunapotupa mabaki ya chakula.
USHAHIDI upo mashambani kwa wakulima wadogo wadogo wanaoacha mazao kuharibikia shambani kwa kukosa soko.USHAHIDI upo kwenye supermarkets chakula kinapotupwa kwa sababu kime-expire..
MAKADIRIO ni kuwa kufikia mwaka 2050 tutakuwa watu BIllion Tisa ulimwenguni.
USHIRIKIANO ni msingi sasa kuhakikisha tunawezesha mfumo wa chakula kuwa wa HAKI na USAWA. Hii ni kuanzia shambani hadi jikoni.
 Balozi mwenzetu mwanamuziki maarufu Afrika Angelique Kidjo
Mchngaji Desmond Tutu
Asilimia 70 ya wakulima na wauzaji wa mazao ni wanawake.
 GROW inataka tuoteshe na kuimarisha uzalishaji
na upatikanaji wa Chakula, uimarishaji wa haki na mustakabali wa
wanawake wazalishaji wa Chakula na pia kulinda mandhari ya uoto na
uhalisia wa sayari yetu.

GROW ni kampeni ya kimataifa inayoendeshwa na shirika la Oxfam. Kampeni
hii inataka tuoteshe na kuimarisha uzalishaji na upatikanaji wa chakula,
uimarishaji wa haki na mustakabali wa wanawake wazalishaji wa chakula
na pia kulinda mandhari ya uoto na uhalisia wa sayari yetu.
Dunia inazalisha chakula cha kutosha lakini watu wapatao milioni moja
wanalala bila kula kila siku. Mbaya zaidi, idadi kubwa ya hao ni
wanawake wazalishaji na watoto.
Ni wakati muafaka sasa, kuungana na kutokomeza mfumo huu dhalimu wa chakula.
Namna tutakavyokuwa tunafanya kazi zetu za kibalozi mtafahamu kupitia vyombo mbali mbali vya habari.
Na mie kama balozi ntawahabarisha hapa na katika leo tena.
Picha kwa hisani ya MP blog na 8020fashions.

37 Comments

 1. Adela Dally Kavishe

  June 17, 2013 at 1:27 pm

  Hongera sana you deserve my dear kila la heri tuko pamoja sana

 2. Anonymous

  June 17, 2013 at 2:39 pm

  hongera dada dina

 3. Anonymous

  June 17, 2013 at 3:30 pm

  Ni kazi ngumu na nzuri unahitaji kuifanyia kazi tunajivunia wewe na wenzio kwa oxfam kuwatambua. HONGERA SANA

 4. Anonymous

  June 17, 2013 at 4:02 pm

  hongeri sana, na muwe waadilifu katika kazi.

 5. Anonymous

  June 17, 2013 at 7:30 pm

  Congratulations c* Dinna u rily deserv it

 6. viva afrika

  June 18, 2013 at 1:13 am

  Hongera sana dina kwa kusimikwa huko kuwa balozi, imani yangu ni kuwa juhudi zako ndo zimekufanya uonekane na kupewa si tu heshima ya ubalozi bali na majukumu yanayokuja nayo, ni imani yetu sie tulio na imani juu yako kuwa utatenda iliyo sawa.HONGERA SANA

 7. Anonymous

  June 18, 2013 at 6:47 am

  Hongera sana Dina, Mungu akulinde na uifanye kazi yako kwa maarifa…Barikiwa

 8. Anonymous

  June 18, 2013 at 7:01 am

  Hongera dina.mungu akubariki na kukulinda ili ufanikiwe zaidi

 9. Anonymous

  June 18, 2013 at 8:48 am

  hongera sana Dina umefika stage ya juu, all the best afu umependeza make up imetulia.

 10. Ruky

  June 18, 2013 at 10:42 am

  HONGERA ZAKO DADA…POLE PLE NDIYO MWENDO…ALL THE BEST

 11. Anonymous

  June 18, 2013 at 11:48 am

  HONGERA SANA DADA DINA NAKUPENDAGA BURE YAANI NATAMANI SIKU MOJA TU TUONANE NIKUSALIMIE… MPE POLE GERALD HANDO KWA MKASA ULIOMPATA

 12. emu-three

  June 19, 2013 at 4:57 am

  Hongera sana mkuu tupo nyuma yako,

 13. Anonymous

  June 19, 2013 at 7:34 am

  Hongera ila nataka kujua kama mabalozi nini majukumu yenu katika kuhamasisha hilo?

 14. Mama 2 (Mrs M)

  June 19, 2013 at 8:23 am

  KAMA KAWAIDA! NDO KUMEKUCHA HIVYO, MILANGO YA NEEMA INAFUNGUKA. HONGERA SANA DINA! MUNGU NI MWEMA SIKU ZOTE.

 15. janetfashionsandstyles

  June 19, 2013 at 1:47 pm

  Hongereni naona wamama mnawakilisha
  safi sana

 16. Anonymous

  June 19, 2013 at 3:46 pm

  shamimu si ameolewa na mume mwingine, mbona bado anatumia Mwasha?

  • Anonymous

   June 25, 2013 at 12:36 pm

   Haikuhusu mbona mna maswali ya kijinga, unajuaje kama mwasha la mume wake je kama la ukoo au mpigie simu umuulize yeye

 17. Ashura Bendera

  June 19, 2013 at 7:46 pm

  Hongera sana Dina Kiukweli waliowateuwa hawajafanya makosa.UNASTAHILI

 18. Anonymous

  June 19, 2013 at 8:24 pm

  HONGERA SANA

  NAAMINI WALOKUANDIK VIBAYA NI WIVU ULIPOPEWA CHEO WAKAANDIKA HUKO ZEDDYLICIOUS,BLOD ET WEWE MWIZI HATA ZEDDY AKACOMMENT ET ULIMZULUM
  DINA MUNGU ATAKUBARIKI HAW WENYE MIDOMO MASIKINI WAACHE WASUKUTUE NA CHEO CHAKO
  UMEBARIKIWA LAZAIDI HAWANA WAKAMTAFUTE ALOKUPA CHEO SASA

  LOVE U

 19. Anonymous

  June 20, 2013 at 9:24 am

  Hongera sana dina, nw mwenyewe umependeza sana. Nimependa kucha zako naomba nisaidie ulipotengeneza.

 20. Anonymous

  June 20, 2013 at 10:18 am

  Hongera japo bado hujui kupangilia mavazi yako, viatu vilikutesa siku ile uongo kama ni uongo basi hata hao ulio kuwa nao hawajakushauri uvae nini? uko level ingine you have to chache may love.

 21. Anonymous

  June 20, 2013 at 1:46 pm

  weka post mpya tumechoka na hii. au ndo ubalozi huo.

 22. newton urban

  June 20, 2013 at 1:55 pm

  hongera

 23. newton urban

  June 20, 2013 at 1:56 pm

  hongera unaweza xana dada Mungu akujalie pia

 24. Anonymous

  June 20, 2013 at 8:04 pm

  Hongera dina

 25. Anonymous

  June 20, 2013 at 8:05 pm

  Hongera dina

 26. Anonymous

  June 21, 2013 at 9:39 am

  mafanikio yako ndio furaha yetu wadau wako, ONGERA KWETU SOTE.

 27. MMdau wako nikiwa nje ya nchi..huwa nakusikilza on line..nikitaja jina mama yangu hato penda maana kutwa anakusikiliza atajua ni mimi

  June 21, 2013 at 10:58 am

  Dina juma tatu plz juzi jana na leo..yangu..ni ya monica na brandy nyimbo ya the boys is mine inanikumbusha boy friend wangu wa kwanza alivyoondolewa gafla na baba yake shauri yangu nikaambiwa mimi ndiyo ninamfanya asisome sintokaa nikaisaha..coz mapenzi yalikuwa mototo na alipo fika nje ya nchi akanitumia wiving na cd ya the boyz is mine coz alikuwa najua mawapenda sana hawa wasanii na ndiyo ilikuwa imetoka..yapili ni fagilia ya mir nice..naye huyu mr.nice alipotoa wimbo huu ndiyo ukawa chanzo cha kuanza kunisaliti na marehemu diana..lakini nilikuwa nikimuuliza alikuwa ananikatalia mpaka nakutaka kunipiga mwisho nikaamua kuachia ngazi mwenyewe japo nilianzana nae kabla ya kuwa super star. Na ya 3. Ni wa mangwea mikasi. Nilikuwa nimekaa chaga bite na mdogo wake Mr.nice anaitwa moody alikuwa akijaribu kunipooza pooza mara wakatokea marehmu mangwea na wasanii kibao wamekuja kurecord nyimbo ya mikasi akaja kunisalimia tulikuwa twafaamiana akanyanyu hand bag yangu nilikuwa nimeweka chini nakuniambia sister mbaya bana kuweka pochi chini..tu kacheka masikini basi waendelea na shughuli yao ya kurecord mkasi.

 28. Anonymous

  June 21, 2013 at 6:46 pm

  Hongera sana u deserve to be balozi tupo pamoja

 29. Anonymous

  June 23, 2013 at 7:48 am

  Hongera mwaya my lovely sister,nakuombea kwa Mungu usonge mbele zaidi ya hapo ulipofikia,Much loveeee…..Farida Ismail from Iringa.

 30. Anonymous

  June 24, 2013 at 2:38 pm

  Hongera sana tena sana Dina. Nakutakia kila la heri naamini kupitia kwako na hao wenzako tutapiga hatua.

 31. mama roby

  June 25, 2013 at 6:09 am

  Hongera sana Dina juhudi zako na kujituma ndiko kuliko mkufanya ufike hapo endelea kujituma zaidi kwani mkuna mambo makuu mbele mungu aliyokuandalia ambayo huwezi kuamini yatakapo timia,hakika wewe ni mwanamke wa kuigwa,nakupenda sana sana sana na ninatamani siku moja nami niwe kama wewe.

 32. Anonymous

  June 25, 2013 at 6:25 am

  Hongera sana Dina mwendo mdundo. kila kheri katika kazi zako. Dina una upload blog yako mara ngapi kwa wiki au mara ngapi kwa mwezi? . inakatisha tamaa kila unapofungua unakuta habari ile ile.

 33. EMANUEL JEREMIA

  June 25, 2013 at 11:07 pm

  hongera sana dina

 34. EMANUEL JEREMIA

  June 25, 2013 at 11:08 pm

  hongera sana dina

 35. EMANUEL JEREMIA

  June 25, 2013 at 11:09 pm

  hongera sana dada dina

 36. EMANUEL JEREMIA

  June 25, 2013 at 11:10 pm

  hongera sana dina

Leave a Reply