Uncategorized

SIKU YA BABA DUNIANI

By  | 
Weekend ijayo tutakuwa tunasherehekea siku ya baba duniani.Siku ya baba duniani ipo ili kutambua nafasi ya baba kwa mtoto,influence ya baba kwa mtoto na jamii.
Siku ya baba duniani ilianzishwa na  Sonora Smart Dodd wa nchini Marekani mwaka 1910.
Sonora aliipigania siku hii baada ya tayari kuwapo kwa siku ya mama duniani ambayo ni kubwa na ina nguvu sana.Sonora aliangalia nafasi ya baba yake aliyewalea yeye na ndugu zake sita baada ya mama yao kufariki.Sonora ni jina la mwanamke sio mwanaume aliona nafasi ya baba ni kubwa sana katika familia hasa akiangalia familia yake ambayo ililelewa na baba pekee.
Ishu hiyo ilienda ikirushwa rushwa bila kupitishwa.Ilipofika mwaka 1972 ndio ikapitishwa rasmi ma Rais Richard Nixon ambayo husherehekewa jumapili ya tatu katika mwezi june.
Katika leo tena toka mwaka jana tumekuwa tukihamasisha sana kina baba kutambua nafasi yao katika malezi ya mtoto.Na mwaka huu kuelekea siku hii ya baba duniani tunafanya hivyo tena.Na tutaangalia makundi haya yafuatayo:
1.Nafasi ya baba kijana aliyepata mtoto akiwa teenager
2.Nafasi ya baba aliyepata mtoto katika miaka ya ishirini na akiwa hajaoa na pengine aliyempa mimba sio anaemfikiria kumuoa.
3.Nafasi ya baba aliyendani ya ndoa na amejaaliwa watoto.
4.Nafasi ya baba aliyefiwa na mke na kubaki na jukumu la kulea watoto.(single father)
5.Nafasi ya baba aliyedivorce yupo yeye na watoto au watoto anao mama.
7.Nafasi ya baba aliyeachana na mkewe au mkewe kafariki na ameoa mke mwingine.
Makundi yapo mengi sana lakini wote kwa pamoja wanawajibika kwa watoto wao.
Ukitaka kushiriki kwenye hili  katika leo tena unakaribishwa sana kwa namna yoyote kwa kadri unavyoguswa na siku hii.Niandikie kwa email yangu dina_marios@yahoo.com

6 Comments

 1. Anonymous

  June 4, 2013 at 10:10 am

  Hi Dinna. Mimi niliandika "thesis"yangu kuhusu binti (teenager) anayepata ujauzito, na kwa mbali nilitaja kuhusu kijana anayekuwa baba katika kipindi hiki cha teenage.
  Jamii nyingi zimekuwa zikimuangalia zaidi binti na kuona ndiye anakuwa vulnerable, lakini yapasa tufahamu kuwa hata kwa mvulana msongo uko palepale. Hebu tufikiri ile siku anapopewa taarifa kuwa anatarajia kuwa baba wa mtoto ilhali yeye bado ni mwanafunzi, hebu fikiri habari hii inapomkuta ilhali ndio kwanza labda ameanza kibarua ama biashara (wale wasioendelea na masomo). Piga picha anapowaza ni kwa namna gani ataweza kumtunza binti aliyempa mimba na ni kwa namna gani atampokea mtoto na kuendelea kumlea. Kweli ni changamoto inayohitaji wanazuoni na jamii kuifanyia kazi na kutambua kuwa kundi hili nalo linahitaji support na si kulaumiwa ama kuchukuliwa sheria kali.
  Niwape heko wababa wote waliopata watoto wakiwa teenagers na wakakubali kuwa pamoja na wenzi wao hata wakamudu kupata mtoto/watoto wao na kumlea vema. HAPPY COMING FATHER'S DAY

 2. RUKY

  June 4, 2013 at 10:47 am

  KWANZA NAPENDA KUMUOMBEA BABA YANGU KILA KUKICHA APUMZIKE HUKO ALIPO NA MOLA AMUONDOLEE ADHABU YA KABURI.. HUWA NAKUMBUKA MENGI SANA KUHUSU BABA YANGU ALIKUWA NI BABA RAFIKI YANI ULIKUWA UKITUKUTA NAE HUWEZI AMINI KM NI BABA YETU NA ALIKUWA HACHOKI KUTUONYA KILA ANAPOTUONA TUNA ENDA NJIA MBAYA MAANA KWETU TUMEZALIWA SABA NA MPAKA ANAFARIKI TULIKUWA WOTE NA MAMA YETU MPENDWA KTK MAISHA BORA NA YENYE MISINGI MIZURI YA MALEZI BORA. HUWA NAMKUMBUKA KILA NINAPOFANYA IBADA MAANA ALIKUWA ANAPENDA KUNIAMBIA KAMA HUSWALI NIKIFA UATANIOMBEAJE? NAPIA HUWA NAOMBA SANA MUNGU ANIPE MUME BORA KM ALIVYOKUWA MAREHEMU BABA YANGU KWA MAMA YETU YANI BABA NA MAMA WALIKUWA KM NDUGU YANI MTU NA DADA YAKE, MTU NA RAFIKI YAKE JAPO MIKWARUZO HUTOKEA LAKINI C YA KUTOISHA CK HIYO HIYO..NA WEZA KUJIVUNIA MPAKA SASA SIJAONA MFANO WA BABA KM BABA YANGU KWEKWELI.. UKIPATA BABA ANAYEHAKIKISHA ANAKUJENGEA MSINGI MZURI WA MAISHA SHUKURU SANA NA C WAKUKUPA SIJUI HELA HAPANA NI MALEZI YAKUKUWEZESHA KUISHI MAISHA YOYOTE UTAKAYOKUTANA NAYO KTK MAISHA YANI ANAKUWAANDAA KTK MAISHA YAKO YA BAADAE.

 3. Anonymous

  June 4, 2013 at 3:57 pm

  Uko sasa Dada Dinah Morious

 4. Anonymous

  June 6, 2013 at 7:36 am

  Hello Dina…..pole na kazi. Kuelekea siku ya baba duniani napenda kumwambia baba yangu nampenda sana na nakumbuka alipokuwa akinibeba mgongoni nikiwa mdogo na kuniogosha na kunilisha maana Mama yangu alikuwa mjamzito na hakuweza kufanya yote. Nmpenda baba yangu na namtakia maisha mema na afya tele

 5. Anonymous

  June 11, 2013 at 7:59 pm

  Shkamoo dada Dina,
  Baba yng ni baba aliyenipata akiwa na umr kat ya miaka 20, kutokana na tofaut ya dini hakuweza kumuoa mama yng,
  Lkn hyo haikumfanya acwe baba bora, Baba yng ananipenda sana
  Amensomesha mpaka muda huu, alioa mke lkn hakupunguza upendo kwang……
  Haach kunianbia "AM PROUD OF YOU DAUGHTER"
  Baba anacklza mawazo yng nakunipa moyo kwa meng……
  Japo yupo mbal na Tanzania lkn mawacliano ye2 ni kama 2po karibu ,
  Cjawah kuish na baba nyumba 1 lkn anafanya la ziada ili kunifanya niwe sawa na wanaoishi na baba zao pamoja….
  Baba yuko radh kufanya lolote kwa ajil yng,
  Nakupenda sana baba yang ABDI BUNGARA
  Mungu akujalie neema na baraka tele.

  Cna zaid kwa siku yang hii ya kuzaliwa 12/6/ zaid ya Mungu kumjaza furaha
  I LOVE YOU DADIE
  By your daughter QUEENRUKIA

 6. Anonymous

  June 13, 2013 at 1:45 pm

  Alikuwa baba bora,alitulea vyema na kutupa kila tulichohitaji. Kwa mipango yake Mungu alimchukua nikiwa na miaka 9 tu na sasa nina miaka 26. Hakuna siku inapita bila kumfikiria baba yangu. Natamani angekuwepo leo ninaamini angejisifu kwa kuwa na mabinti watatu wanaojituma. Japo hayupo lakini bado ninampenda.

Leave a Reply