Uncategorized

DADA DINA CARES :KITUO CHA KULELEA WATOTO YATIMA CHA SIFA

By  | 
Kituo hiki kiko Bunju mwisho kinachoangaliwa na Dada Sifa.Niliweza kukijua baada ya kupigiwa simu na mwanamuziki Stara Thomas maana niliongea nae juu ya azma yangu hii.Stara alinipigia simu na kuniunganisha na huyu dada ili niweze kufika huko.Na alinisisitiza kuwa kina uhitaji sana hata mimi nilivyofika nilijionea hali iliyokuwepo.
 Nilienda nikakuta watoto kama unavyowaona
Nikakaa na Sifa mwenyewe kunielezea kuhusu kituo.Ana watoto 20 wanao lala na wengine 30 wanaokuja na kuondoka.Hao 30 ni wale ambao wanakaa kwa mama au bibi,babu ila mazingira magumu hawaendi shule wala kupata mahitaji muhimu.Wanakuja kushinda hapo kuna walimu wanafundishwa,wanakula na kushinda na hao wengine jioni wanarudi makwao.Huyo pembeni ni mama mzazi wa Sifa.
Hapo watoto wanapokaa ni kwa mama yake na Sifa sio kituo rasmi ila Mungu akimjaalia atanunua kiwanja na kujenge nyumba ambayo watoto wanaweza kukaa vyema.Mama yake Sifa ndio anamsaidia kwa kiasi kikubwa kulea watoto wakati yeye akiwa kwenye pilika pilika zingine.
 Nikatembezwa kuangalia mazingira vizuri
Nikaambiwa kitanga kama hiki wanalala watoto wadogo wanne,juu wanne chini wanne jumla nane.
Hiki wana lala wanne kitanda kimoja wale watoto wadogo pia.
 STOO
 Mazingira ya jikoni
Msaada mkubwa Sifa anaouhitaji kwa watoto wake ni chakula,mavazi,viatu,vifaa vya shule,sabuni za kufua na kuoga,dawa za meno,mafuta ya kupikia na kujipaka.
Pia ikiwezekana apate ml 4 za kununua kiwanja atakachoweza kujenga hapo baadae eneo litakalokidhi mahitaji ya watoto kuishi na kucheza vizuri.
Muda wangu wa kuondoka ukafika kijana wangu hataki niondoke jamani ananivuta nirudi nyumbani.
Akajiangusha na chini kabisa kulia kuonyesha msisitizo
Akaliaaaa anataka kunifuata maana kuna mwendo kutoka kwenye kituo mpaka tulipopaki gari maana njia hairuhusu gari kufika huko.
Basi tukasindikizana wenyewe akaacha kulia
Basi akaridhika tukaagana,bibi anasema ni mtoto mpole na mkimya na huwa hashobokei mtu wanashangangaa kweli.Nikajisikia vizuri kweli japo siku fanya la maana zaidi ya kumpakata na kuongea nae tu nikamwambia ntampeleka kwangu maybe alijisikia kupendwa sijui.
 
Wadau kituo chetu kingine hiki hapa tutakachokichangia.
Sasa kwa wadau wa blog naomba mchango wenu uguse mambo mawili.Nguo za watoto nguo hizo zisiwe zimechakaa jamani ziwe zinaridhisha mtoto kuivaa pamoja na viatu.Cha pili vifaa vya shule madaftari,peni,penseli,rula n.k hivi tu basi.
Napenda mchango uwe katia uniform sio huyu amechangia sukari yule mafuta huyu sabauni hapana.Ndio maana nimegusia hivi viwili tu.Mchango huu uwasilishe clouds fm mikocheni.Kama utataka kuchangia na pesa niandikie kwenye email nikupe maelekezo namna itanifikia.
 
Kuna kampuni moja ya kutengeneza sabuni za kufua na kuoga,dawa za meno,mafuta itajitolea kipengele hiki.Ila nipo kwenye kuwashawishi wachangie kupeleka hivi vitu kila baada ya miezi mitatu kwa mwaka mzima katika hivi vituo.Nikifanikiwa hapa nitawafahamisha ni kampuni gani ila tupo pazuri.
kwa maoni,swali unaweza kuniambia kupitia dina_marios@yahoo.com
Zaidi endelea kutembelea hapa bado kituo kimoja sijakiweka na sikiliza leo tena ya clouds fm.

21 Comments

 1. Anonymous

  July 15, 2013 at 7:02 am

  Hongera sana Dina kwa hatua uliyofikia mungu akubarikia sana uweze kufanya hili na jingine,ila nimejishangaa ninalia baada ya kuziona hizo picha za huyo mtoto akikulilia hakika anahitaji mapenzi ya mama na hicho kitendo cha wewe kumpakata kimemfariji sana hadi akajisikia nae amepata mapenzi ya mama,yani natamani kama hali inakuruhusu umchukue huyo mtoto umlee,nahisi mungu ana mpango na wewe haiwezekani huyo mtoto akulilie wewe na ikiwa sio kawaida yake kushobokea watu. TAFAKARI CHUKUA HATUA.

  • dinamariesblog

   July 17, 2013 at 6:54 am

   asante sana na Nashukuru kwa ushauri ntajaribu kuufanyia kazi!

 2. Anonymous

  July 15, 2013 at 7:53 am

  Machozi yamenitoka pale mototo alipokulilia halafu akakusindikiza na mwisho akakuaga, machoz yanaendelea kunitoka.

 3. Anonymous

  July 15, 2013 at 10:13 am

  Mwenyezi Mungu ákupe umri mrefu Dina,mchango wako katika jamii ni mkubwa sana.una moyo wa imani sana,wachache wenye moyo wako na Jua ni mpango wa Mungu ili uweze kuisadia wenye uhitaji.nakosa la kusema ila ipo síku utalipwa méma yko.luv u Mingi mingi dina.

 4. The Lot

  July 15, 2013 at 12:48 pm

  Go Dina Mungu akutangulie.

 5. Anonymous

  July 15, 2013 at 5:01 pm

  Nitakuombea kwa Mwenyezi Mungu kila napopiga góti langu kuomba.damu ya Yesu íkapate kukufunika popote pale utakapokua.nakupenda dina,wewe ni mfano mzuri wa kuigwa.kila unachofanya jua kuna msululu wa watu upo nyuma yako.Mungu akutunze na kukulinda.

 6. Mrs adoa (mama Grace)

  July 15, 2013 at 5:15 pm

  Mungu akubariki na kukulinda.ákupe aja ya moyo wako,akuepushe na kila lililo baya.uzidi kufanikiwa zaidi na zaidi.go dina go.

 7. Mama 2 (Mrs M)

  July 16, 2013 at 4:29 am

  Hongera sana Dina! Mungu akubariki sana na akupe afya njema na uhai ili uweze kusaidia jamii.

 8. Anonymous

  July 17, 2013 at 6:38 am

  Hongera Dina. Nina mtoto wangu wa kike ana miaka 9. Anapenda sana kutoa misaada. Kila nikitembea naye barabarani tukikuta omba omba ananilazimisha niwasaidie. Ananiambia mama mpe hela huyo mtu mi namwambia sina hela. Basi anakasirika anaona km ninamnyima kwa makususi. Akiwa na hela yake ht km ni ndogo kiasi gani lazima awape ombaomba. Anapenda pia kutembelea vituo vya watoto yatima

  Kwa moyo alionao nineona nimpe sapoti. Mimi na yeye tutakuwa tunakusanya vijihela kidogo tununue mahitaji then tupeleke kwa wanaohitaji. Pia kuna nguo za zamani ambazo watu hawazitumii tutakusanya tupeleke

  Dada dina..nitakutafuta cku mwanangu akishakusanya vitu vyake ili ukiwa unaenda uende naye. Najua atafurahi.

 9. ayam yassin

  July 17, 2013 at 7:08 am

  Hawa watu wanaolea watoto wao wenyewe wanahitaji msaada kwa sababu hata mazingira ya maisha yao ni duni kwanini wanajibebesha mzingo si fikiri kama ni vema wewe mwenyewe uwe na shida kisha ujibebeshe mzingo na pia Mungu hapendi

  • Anonymous

   July 23, 2013 at 6:12 am

   sidhani kama upo sahihi…inamaana wewe huwezi msaidia mwenye shida zaidi yako kwavile wote mna shida?..sasa kama hakuna wa kuwasaidia wawaache wateseke au wafe kisa na wao wanashida…tafakari tena ayama!

   KAKA YENU!

 10. frank sanga

  July 17, 2013 at 8:47 am

  nawezaje changia?

 11. Anonymous

  July 17, 2013 at 9:48 am

  Hi Dina mambo, Mungu awabariki sana wote hapo mjengoni,kwa kazi za kusaidia jamii na hao watoto yatima ambao ni taifa letu la kesho jamani nimevutwa sana, mungu atawajazia hao wamama pale palipopungua,nafikiria jinsi gani nisaidie hata kidogo,niko mbali na home, hakuna mpesa na mtakoa number za huko home wapendwa.ila niatatafuta njia, na kila siku nasikiliza kipindi chenu cha hekaheka, Dina Love you all hapo mjengoni Hasa Team yenu ya hekaheka, have good day,

 12. Anonymous

  July 17, 2013 at 6:52 pm

  hi dina hongera sana kwa hekima uliyopewa na Mwenyezi Mungu aendelee kukulinda milele.

 13. Anonymous

  July 19, 2013 at 9:30 am

  Dada Dina Mungu akubariki mnoo nataman ningekua na uwezo namimi nchangie walau kidogo ila nmefulia kwa sasa my prayerz goes with u

 14. Judith Mwanri

  July 24, 2013 at 6:34 am

  napenda unachofanya na Mungu abariki kazi za mikono yako. am sure unagusa wengi kwani ni wengi kwani niwengi wanatamani wafanye lakini hawajui waanzie wapi kwa njia hii unayotumia utatimiza ndoto za wengi. Once again be blessed.

 15. Anonymous

  July 30, 2013 at 10:59 am

  Hap watoto wapo wangapi wanaosoma na kuhitaj uniform….yaan nataman kufanya kitu kwa ajili yao….

Leave a Reply