Uncategorized

DADA DINA CARES:ASANTE DUKA LAZ ZERO 2 TWELVE KWA NGUO ZA WATOTO!

By  | 
 Leo jioni nilichukua nguo za idd za watoto kutoka duka la Zero 2 Twelve.
 Niliongea na mmiliki wake kwa simu kumuomba ashiriki kwenye zoezi hili la kuchangia watoto.Nikamwambia najua si mara zote mzigo unaisha dukani aniangalizie kilichopo.Uzuri nilikuta dada moyo wake mweupeee akasema hamna taabu atanikusanyia atakazopata.Leo akaniita nikazichukua.
Mpaka chupi za watoto alinipatia
Duka la Zero 2 Twelve linauza nguo za watoto kuanzia siku moja mpaka miaka kumi na mbili.
 Nguo ni nzuri kweli kwa watoto wa kike na wa kiume
Msimu wa sikukuu nguo zipo nzuri kwa watoto.Zamani kulikuwa na neno la mama mpende mwanao kwa maana ya kwamba kina mama ndio wanunuzi wakuu wa nguo za watoto.Ila leo nimeambiwa siku hizi kinababa wananunua sana nguo za watoto wao.Wanunuzi wakuu dukani hapo ni wanaume kuliko kina mama.
Mafuta,lotion,sabuni za watoto
 Vitanda vya watoto
Wale wa kununua zawadi za baby shower hapa ndio penyewe sasa
Chupi za watoto wa kike na kiume kwa kila rika
Hii ni sehemu ya shukrani zangu kwa duka hili la zero 2 twelve.Hata mkoani wanakutumia mzigo ukitaka.
Mawasiliano yao ni 0716454580 kwa swali lako lolote.
Bado unakaribishwa kuchangia mradi wa Dada Dina Cares kwa lolote lile litakaloweza kusaidia watoto yatima wa kituo cha Sifa Bunju,Zaidia Sinza na Vetenari Temeke.
 

23 Comments

 1. Anonymous

  July 25, 2013 at 7:04 pm

  Hongera kwa kazi yako unayoifanya dada Dina. Tafadhali naomba unielekeze location ya ilo duka.

 2. Anonymous

  July 26, 2013 at 4:47 am

  Duka lipo wapi hilo naomba nielekeze dada dina

 3. Anonymous

  July 26, 2013 at 7:01 am

  hili duka ni zuri kwakweli liko sehemu gani?hongera mmiliki wa zero to twelve kwa msaada mlimuwezesha Dina,mko maeneo gani nimependa kulitembelea

  • dinamariesblog

   July 26, 2013 at 10:46 am

   nimeweka namba za simu sijui hujaziona?lipo Tranic plaza opp nyumbani lounge

 4. Anonymous

  July 26, 2013 at 8:09 am

  lipo wapi hili duka.

 5. Havintishi

  July 26, 2013 at 10:02 am

  Lipo wp hili duka dina

 6. Anonymous

  July 26, 2013 at 11:09 am

  woowh Mungu awabariki

 7. Mama Mia

  July 26, 2013 at 12:30 pm

  Hongera Sana Dina. Inshaallah M.Mungu akujaalie Kila lenye heri na wewe, uendelee kuwa na moyo wa kujitolea kwa hawa watoto, amen

 8. Mama Mia

  July 26, 2013 at 12:32 pm

  Lipo maeneo ya namanga jirani na best bite pale tranic plaza linatazamana na nyumbani lounge

 9. Anonymous

  July 27, 2013 at 9:11 am

  Jibu watu vizuri dina acha maringo na dharau ebo!

  • dinamarios

   July 28, 2013 at 5:35 am

   wewe wasema kuwa nimemjibu kwa maringo na dharau…ila nimemkumbusha kuwa nimeweka namba ya simu ili arudi kusoma kama hakuona kuna maswali atataka kuuliza hapo ndio atapata majibu zaidi.Na mwisho nikamwambia duka lilipo.Dharau iko wapi hapo?Anyway tupo tofauti kimtazamo!

 10. Anonymous

  July 28, 2013 at 1:07 am

  Dada mwenye duka ubarikiwe sana..nitakuja kufanya shopping ya nguo za mtoto wangu hapo

 11. Anonymous

  July 29, 2013 at 8:53 am

  mbona me sijaona jibu baya jamani kweli watu hatufanani.hongera mwaya Dinna kwa yotee'

 12. Anonymous

  July 30, 2013 at 9:00 am

  Duka lipo Tronic plaza pale nyumbani lounge kwa lady jay dee Morocco, wana vitu vizuri mno, yeah..Dina jibu vizuri acha maringo ya kihaya bwana, umeamua kuwatangaza basi watangaze vituri

  • dinamariesblog

   July 30, 2013 at 10:36 am

   Na kweli nimewatangaza maana mwenye duka kafurahi kweli jinsi simu zinamiminika na wanunuzi kibao.Mhhhhhh ila binadamu mna mambo maadamu nimeamua kudeal na jamii hadha zitokanazo na hayo ntazibeba.Asante sana!

 13. Anonymous

  July 30, 2013 at 4:59 pm

  kwani uongo umeshasikia wivu hapo mwenye duka anapata hela, tunakufahamu sana unajikosha tu.

  • Anonymous

   July 31, 2013 at 7:55 am

   wewe ndio una wivu na mwana wa mwenzio hata unachokisema huelewi.Hujielewi wala hujitambui ahera hutakiwi wala mbinguni hutakiwi!STUPIDY

 14. Anonymous

  July 31, 2013 at 7:02 am

  kabisa mama. Mungu kaumba hao nao viumbe wake. Mungu akutie nguvu, uvumilivu na akuwezeshe. wabarikiwe pia kwa mchango wao. Amina

 15. Anonymous

  July 31, 2013 at 7:50 am

  wakuache dada dina, wana yao hao! hata sioni maringo yako wapi ilimradi mtu apate cha kusema….pole mwaya ndio jamii yetu

 16. Anonymous

  August 3, 2013 at 9:41 pm

  Ndio mana hatuendelei watanzania,,badala ya kumsifu mtu kwa jambo zuri mnaanza umbea,,hapo dharau iko wap,,,nyie mmefanya lip kwa jamii kama dina,,,maza fanta

 17. Anonymous

  August 3, 2013 at 9:42 pm

  Ndio mana hatuendelei watanzania,,badala ya kumsifu mtu kwa jambo zuri mnaanza umbea,,hapo dharau iko wap,,,nyie mmefanya lip kwa jamii kama dina,,,maza fanta

 18. grace mpanduka

  August 7, 2013 at 6:32 am

  mh walimwengu mnamambo hiv nikuulize wewe unaesema dina anadharau kama anadharau hmu kwenye blog yake unafata nini au umbea unakuwasha uwo ni uswahili kuna njia nyngi nzuri za kumkosoa mtu lakin si hiyo unayotumia wewe haya tuambie kubwa lako lipi la kuzidi huyu mwenye zarau kushinda wewe? jiheshimu mwanamke huna lolote yote hiyo kwa sababu ya wivu wa kile dina anachofanya kuwa na adabu kwenye kazi za watu kelele nyingi we umeshanunua nguo ngapi hapo dukani? take care

 19. spice

  August 8, 2013 at 5:35 pm

  Jamani kweli nimeamini hata ukitenda wema hutakosa wa kukuchukia!sasa we bi dada unayemsema Dinna vibaya amekukosea nini au ndo wivu tu wa moyo kukuuma?kunywa tindikali basi!

Leave a Reply