Uncategorized

DADA DINA CARES:KITUO CHA WATOTO CHA ZAIDIA CHA SINZA

By  | 
 Kituo cha watoto cha Zaidia cha Sinza pia nilikitembelea na kipo kwenye mpango wa Dada Dina Cares

 Watoto wakiwa tuition jioni na mwalimu akifundisha.

 Vyumbani kwa watoto
Stoo wanapohifadhi vitu
Bibi Zaidia akituonyesha mazingira!
Bibi Zadia akiwa na mwanae mkubwa wa kike huyo wa katikati na nduguye mwingine.
Napenda niendelee kushukuru wadau mbali mbali mnaoendelea kuchangia mpango huu.Yaani mambo yanaenda vizuri mpaka basi.
1.Duka la zero 2 twelve wamenipa nguo mpya kwa ajili ya sikukuu ya idd.Nguo hizi sio nyingi kutosheleza vituo vyote nimeamua nitazipeleka kituo cha Zaidia maana watoto wake ni waislam na wamefunga.
2.Kuna msikilizaji  wangu wa leo tena ambae hajapenda jina lake kutajwa ametoa magodoro 10.Ijumaa nina meeting na Magodoro Dodoma pia nao watanipa magodoro sijajua idadi..
3.Kampuni ya dawa ya meno ya Familydent watatoa box 6 za dawa za meno kila  box linakaa dawa 76.
4.imeshalipia vitanda vitano vya double decka vinachongwa jumla ni vitanda kumi vya kuweza kulala watoto 20.Vitanda hivi ni vile vya kituo cha Vetenary Temeke.Bado mashuka,vyandarua,nyavu na mapazia.

Muda unavyokwenda ntazidi kuwaupdate yanayojiri.
Mpaka sasa nina uwezo wa kununua mchele kilo 100,maharage kilo 100,unga kilo 100 na sukari kilo 100 kwa kila kituo.Pia Pesa ikiongezeka naweza kununua chakula zaidi na mahitaji mengine kama mafuta ya kupikia na kujipaka,sabuni za kuoga na kufulia n.k
 Bado unaweza kuchangia pesa kama bado MPESA 0759 789863 na TIGO PESA 0657 795654.

18 Comments

 1. Anonymous

  July 25, 2013 at 11:40 am

  This is good news Dinah.Mungu akubariki

 2. Anonymous

  July 25, 2013 at 12:35 pm

  ubarikiwe dinna kwa moyo wako

 3. Anonymous

  July 25, 2013 at 3:45 pm

  Mashallah dina

 4. Anonymous

  July 25, 2013 at 3:56 pm

  maashallah, mola awazidishie walitoa na wenye nia ya kuwa saidia watoto yatima, pamoja na wewe DINA.

 5. Anonymous

  July 25, 2013 at 4:57 pm

  INSHAALLAH MWENYEZI MUNGU ATAKULIPA KWA HILI ULILOBUNI.
  Wachache huwa na moyo wa kutoa pasipo kuangalia IMANI, Dada we ni miongoni mwao sio kama nakusifia kwa kuktaka kukukweza, Hata Mtume Muhammad(SAW)amewasifia watu wenye moyo wa kutoa pasipo kusubiri sifa au malipo na kuwatabiria pepo duniani hata ahera.
  Hata yule Rais wa UAE amezindua kampeni kubwa kwa wananchi wake kutoa kwa watu wengine n kuiita kampeni hiyo KUVALISHA NGUO WATOTO 1,000,000 Duniani kote kule ambako wanamatatizo na hadi kufikia tarehe 23/07/13 walikuwa wameweza kuvalisha watoto zaidi ya 890,000 na wanatarajia hadi mwisho wa kampeni yake yaani tarehe 26/07/13 watakuwa wamevuka lengo walilojiwekea.(Source:Gulf News)
  Mungu akupe wepesi katika maisha yako.Ameen

 6. Brighton Joseph

  July 26, 2013 at 6:33 pm

  Good news DINA

 7. Brighton Joseph

  July 26, 2013 at 6:35 pm

  Good news DINA

 8. Anonymous

  July 27, 2013 at 11:33 am

  STAY BLESSED, NI WACHACHE WANAYOFANYA UFANYAYO, NINGESHAURI HOME DECO NAO WACHANGIE RANGI, NAONA SEHEMU KAMA STOO NA PENGINE VYOONI KUNAHITAJI RANGI, LAKINI NITAFWATILIA NINGEPENDA NICHANGIE RANGI

  • dinamariesblog

   July 28, 2013 at 6:20 am

   sawa ntajaribu kuongea nae kama atakugwa na wewe pia asante kwa hilo.

 9. Anonymous

  July 27, 2013 at 11:34 am

  RANGI NA MAFUNDI WAKE

 10. Anonymous

  July 28, 2013 at 12:21 pm

  Unafanya kitu kizuri sana Dina, Mungu akubariki na akuzidishie kwa kila jambo, na pia wale wanaochangia Mungu awabariki na kupajaza pale palipopungua!!

 11. Anonymous

  July 29, 2013 at 11:41 am

  God will take u far my dia for ur good heart of helping others,keep going gal.

 12. Anonymous

  July 29, 2013 at 1:56 pm

  halow dada dina 4 me sina pesa za kuchangia lakin nina viatu na nguo zilizonibana je naweza pia kuchangia?ni nguo kwa ajil ya watoto wa kike na viatu pia,je naweza kuviandaa pia nikuleteee uvijumuishe hapo?

 13. Anonymous

  August 1, 2013 at 10:15 am

  dada dina habari, mungu akaubariki kwa kile ukifanyacho, mimi binafsi nimeguswa sana na nafrahi sana kuona kuna watu wenye moyo kama wewe katika huu ulimwengu.! natamani kuchangia hata kwa kujitolea kuwa nawafundisha hao watoto tuisheni angalau mara tatu kwa wiki kila nitokapo kibaruani kwangu! kama inawezekana kuchangia kwa njia hiyo.

Leave a Reply