Uncategorized

DADA DINA CARES:MANUNUZI YAMEANZA YA MAHITAJI YA WATOTO

By  | 
Leo ndio nimefanya manunuzi ya awali kabisa ya vyakula vitakavyoenda kwenye vile vituo vitatu vya watoto yatima.
Nimenunua mchele kg 300,unga kg 300,sukari kg 300 na maharage kg 300.
Kila kituo kitaondoka na mchele kg 100,unga kg 100,mchele kg 100 na maharage kg 100.
Tayari kwa safari,vipo viroba vingine ofisini vilivyoletwa na wadau mbali mbali wa clouds fm
 Pia nimenunua maboksi 9 ya sabuni za kufulia za miche hapa muuzaji alikuwa akinipangia.Box moja linakaa miche 10.Kesho nitaongezea sabuni zingine za kufulia na ndoo za mafuta ya kupikia maana haikuwa kazi ndogo hasa manunuzi ya vyakula mpaka kichwa kinauma.
 
*Kuna jambo moja halijakaa sawa ishu ya nguo,bado nguo haziji kivile.Inaonekana muda wa kukaa kuchambua haupo.Ila nimepata option moja nasikia bela 1 la mtumba ni Tsh 250,000 nimewaza kwa nini nisinunue mabela mawili nguo za kiKe na nguo za kiume.Niwaite hawa kina mama wa vituo kama mtumbani vile yafunguliwe wakae wasagulee wawachagulie watoto wao.
Hii bajeti haikuwepo nani yupo tayari kuwezesha hili?? haba na haba hujaza kibaba naamini halishindikani
MPESA 0759 789863 na TIGO PESA 0657
795654.
Tuendelee kuchangia wapendwa.
 
RATIBA YA KUWASILISHA VITU VITUONI
Jumamosi ya tarehe 3 august kituo cha Vetenary Temeke
Jumapili ya tarehe 4 august kituo cha Sifa Bunju
Jumatatu ya tarehe 5 august kituo cha Zaidia Sinza

17 Comments

 1. Anonymous

  July 30, 2013 at 4:35 pm

  Hakika kwa hili da dina Mungu atakuzdishia kwa kila hali n wengne wote waliojitolea…your number 1 fan.

 2. Anonymous

  July 31, 2013 at 7:18 am

  hali si mbaya. be blessed for that.!

 3. Swahiba Rajab

  July 31, 2013 at 9:23 am

  Ubarikiwe sana da Dina…

 4. Anonymous

  July 31, 2013 at 11:05 am

  Mungu akutangulie ktk hili all the best mpendwa

 5. Mama 2 (Mrs M)

  July 31, 2013 at 12:19 pm

  Mungu atakuzidishia Dina, hujui tu ni kwa kiasi gani hao watoto watapeleka Dua zao njema kwa Mwenyezi Mungu, Mungu na akubariki sana!!!

 6. Anonymous

  July 31, 2013 at 1:08 pm

  mungu akuzidishie dina akupe haja ya moyo wako ubarikiwe sana kwa ulichokifanya katika kuwakumbuka watoto yatima

 7. Anonymous

  July 31, 2013 at 4:43 pm

  Hakika dadayangu wewe ni mfano wa kuigwa inshaallah mwenyezi mungu atakulipa

 8. Anonymous

  July 31, 2013 at 6:24 pm

  Helo dina hongera saana kwa kazi nzuri hiki kituo cha sinza kipo maeneo gani nimewiwa pia nami kwenda Mungu akiniwezesha

 9. Anonymous

  August 1, 2013 at 6:23 am

  inshaallah kheri mwenyezi mungu atakulipa kwa kila ulifanyalo na atakuzidishia na kukufanyia wepesi inshaallah.

 10. Anonymous

  August 1, 2013 at 8:04 am

  Hello Dinna, tunazo nguo za watoto wadogo tumekusanya pamoja. Tunao mpango wa kuzileta kwako wiki ijayo jumatatu. Naona ratiba inaanza kesho, je tutakuwa tumechelewa sana?

 11. Anonymous

  August 1, 2013 at 9:37 am

  kila la kheri mpendwa,jee inawezekana kupata contact za hivyo vituo? maana kuna wadau wengine hatuwezi kujumuika pamoja na da dina.lakini tunaweza kujipanga kwenda kuwatembelea siku yeyote.naomba kupata contact zao kama number ya simu au email zao.m.mungu atakulipa kwa hili na atakufungulia kila unalolitaka lifanikiwe

 12. Anonymous

  August 1, 2013 at 7:15 pm

  Mungu awabariki wote waliohusika kwa namna moja au nyingine. Pia sikushauri kununua Balo la nguo bihashara hiyo nilishaifanya kununua Balo ni kubahatisha nguo zilizomo unaweza ukapata nguo nzuri chache sana watu huwa wanaenda kwa watu wanaofungua Mabalo kama Ilala wanachagua watakazo na balo kama baya inakuwa inakula kwa yule mfunguaji japo wale ni wataalam wanajua mzigo mzuri.

 13. Anonymous

  August 2, 2013 at 7:01 am

  mungu akujalie,akuzidishie, na akubariki kwa kila unalofanya mana umeonesha moyo wa kujitolea na kupiga kampeni za kuwachangia watoto hao katika vituo na mungu awajalie na wale wote waliotoa kwa moyo ili kuwasaidia

 14. Anonymous

  August 2, 2013 at 1:38 pm

  ubarikiwe sana dada dina

 15. Anonymous

  August 2, 2013 at 1:57 pm

  Mungu akulinde sana da Dina kwani we ni mfano wa kuigwa.

 16. Anonymous

  August 2, 2013 at 6:54 pm

  Jamani Dina mungu akubariki sana maana vitabu vya mungu vinasema "ana kheri yule awasaidiaye wenye shida mbalimbali", unaweza ukaona umefanya kidogo lkn ni kitu kikubwa sana, Yaani sijui niseme nn mmh!

 17. Anonymous

  August 4, 2013 at 7:35 am

  kweli mungu akupe haja yamoyo wako dada dina

Leave a Reply