Uncategorized

EMAIL NILIYOWAHI KUANDIKIWA NA MDAU WANGU…SOMA UNIPE MAWAZO!

By  | 

Habari yako
Dina,

Mimi ni
msikilizaji wako mkubwa wa kipindi pendwa tanzania leo tena lakini pia ni
mfuatiliaji wa blog yako nimeingia kwenye blog yako muda mfupi uliopita,na nikaona
ile video uliyoweka ya mtoto anayeimba wimbo wa whitney kiukweli wewe umesema
machozi yalikutoka mimi nimelia sana,kwanza kwa furaha ya yule mtoto,lakini
pili nimelia kwa sababu yangu mwenyewe Dina ambayo kiukweli huwa siachi kuumia
nadhani mpaka nitaingia kaburini.

Nakumbuka niliweka video ya mtoto Aliyah Kolf 11yrs old wakati huo.Mshindi wa Holland got talent mwaka juzi.Jinsi alivyoimba kwa hisia na kwa kipaji chaa hali ya juu wimbo wa i have nothing wa marehemu Whitney Houston.


Dina mimi
kwa sasa nina miaka 32 kama utanikumbuka niliwahi kukuandikia mail ya kuomba
ushauri fulani,leo nimeguswa na yule mtoto nataka nikuambie
likichoniliza,ni kwamba Dina kila mtu amezaliwa ana kipaji japo kwa nchi zetu
ni ngumu sana kumtambua mtoto nadhani kutokana na malezi yetu na maisha
kiujumla,sasa bwana mimi kati ya vipaji nilivyojaaliwa ni pamoja na kuimba,na
kati ya wanamuziki waliokuwa wananifanya nijione kuwa maisha yangu nitaimba ni
whitney.
 
Baba yangu alikuwa ni mwalimu wa chuo cha ualimu kwa sasa amestaafu
lakini pia alipata stroke hivyo hajiwezi tena.Alikuwa anapiga vyombo vyote vya
muziki,alikuwa akipiga mimi naimba,pia nina kipaji cha kuchora ambacho
nacho nimekirithi kwa baba yangu ambaye alikuwa anaweza kukuweka hapo au picha
yako na kukuchora.Mbali na hivyo mimi pia nina kipaji cha uigizaji,naigiza kwa
kiwango cha juu na vingine vingi kama kudance japo kwa sasa ni mama nimekuwa
mzito kidogo lakini kipaji hakifi kwani hawezi mtu kucheza pale nikaiona style
nisiishike au nikiwa kwenye mkusanyiko wowote ule kama kuna mziki ni lazima
watu wote wakae pembeni na waanze niangalia mimi hizo nimeishaziona sana.Sasa
vyote hivyo ni vipaji Dina nilivyonavyo ambavyo naumia kuona vyooote vinakufa
bure,nilipomuona yule mtoto nililia sana kuona mimi nilivyopoteza karama zangu
ambazo Mungu alinipa hivihivi kwasababu tu ya kukosa njia ya watu kuviona
vipaji vyangu mpaka sasa nimekuwa ni mama na nina watoto.

Matokeo yake
nafanya kazi ambazo nazifanya tu ili niishi lakini si kwamba ndizo zilikuwa
kazi ambazo nazipenda kutoka moyoni,nachukia kuona nimeshindwa kuwaonyesha
watanzania kile Mungu alichonijaalia nimebaki kutazama wenzangu wakifanya na
naumia zaidi kuona wengi wao wanaharibu tuu hata sanaa haipo ndani yao,sina pa
kusemea Dina basi nabaki kuumia na kulia linapotokea kama niloona la yule mtoto
ambaye yeye amepata bahati ya kutambuliwa kuwa anakitu na hatimae kuuonyesha
ulimwengu,nimeumia sana,ila nadhani bado nina nafasi,as long as niko hai na
mume wangu ananisapoti na kujua nina vipaji,sijakata tamaa nitajitahidi
kuvipigania vipaji vyangu ili siku moja watanzania waone Mungu
alichonijaalia.Asante Dina,hii email nimekuandikia wewe tu ili kushusha kifua
changu kilichojaa machungu mengi,maana ukitoa kama hivi unapumzika,hivyo namimi
kiasi fulani kama nimepumzika hivi.

Nakutakia
kazi njema mamy,nakupenda sana.

 
*Nisamehe my dear kwa kushare email yako hapa ila nimeiweka kusudi.Email hii uliniandikia na tuliongea pia.Na ni toka mwaka jana niliipata leo nimepitia pitia emails nikaiona tena.
 
*Wadau je ni wangapi wenu mna vipaji lakini hamkuwahi kuvifanyia kazi badala yake mnafanya mambo mengine au kazi zingine?Je dada yetu hapa mnadhani bado ana chance ya kuonyesha kipaji chake tena,iwe kuimba,kuigiza,kucheza na kuchora?Mie naamini bado anaweza hajachelewa.

22 Comments

 1. esther nyalusi

  July 20, 2013 at 10:41 am

  Sio siri me naamini anayo chance anayo kinachotakiwa Ni kwamba ajitahidi sio siri watu wengi tunakufa na vpaji vyetu kwakuwa unashindwa jinsiyakukionyesha

 2. Gregory Sanga

  July 20, 2013 at 11:15 am

  Hi Dinna nimerejea kuuangalia huu wimbo aidi ya mara kumi kiukweli unagusa mioyo jinsi huyo mtoto anaimba hta siwezi kusema i wish hata nimuonae hapo juu awe ndiye mwanangu gladys. Asane mungu kwa kipaji chamtoto huyu mungu na umzidishie zaidi ya hii talanta ilipofika.asante mungu kwa yote sina la kuongeza . dina nitaku email

  • dinamarios

   July 22, 2013 at 1:12 pm

   hello,nimefurahi but mwanao Gladys anaweza kuwa na kipaji kingine tofauti na hiki.Ni wewe mzazi sasa kukigundua na kumsuport kiweze kuwa active kwa manufaa yake ya baadae.

 3. Davis Mazula

  July 21, 2013 at 10:06 am

  Bado anayo chance ya kutumia vipaji vyake.madhali amegundua kipaji chake na yuko hai basi hana budi havitumie.kama una uwezo da dina plz masaidie

 4. Davis Mazula

  July 21, 2013 at 10:06 am

  Bado anayo chance ya kutumia vipaji vyake.madhali amegundua kipaji chake na yuko hai basi hana budi havitumie.kama una uwezo da dina plz masaidie

 5. Davis Mazula

  July 21, 2013 at 10:06 am

  Bado anayo chance ya kutumia vipaji vyake.madhali amegundua kipaji chake na yuko hai basi hana budi havitumie.kama una uwezo da dina plz masaidie

 6. Anonymous

  July 21, 2013 at 10:58 am

  LLOOOH tupo wengi sana tunaacha maisha yatuendeshe yatakavyo.Unasoma kitu hukipendi kisa upate mkopo au upate ajira ya serikalini au kisa baba alifanya kazi hiyo.Mfano mimi i wanted to be mtangazaji/mwandishi olevel nilikuwa naandika sana hadithi na poem na wenzangu wanasubiria toleo kama vile la gazeti maarufu….gues what??????Mambo ya chuo na Target ya mkopo nikajikuta nasoma kitu tofauti kabisa. Sometimes Huwa nafikiria kuazisha kitu kama career inspiration ili ikiwezekana nielimishe watoto kuanzia primary ili wasome wakijua wanataka kuwaje baadae bila kupoteza muda na energy zao buree.Wake up Tanzania lets try to find out what talents our kids have and try to raise them jamani.Watu wanazaliwa na karama let doctors be doctors,let lawyers be lawyers,letmusicians be,Usitake mwanao aishi ndoto zako mzazi.Kisa we mwalimu/mkandarasi unataka na mtoto awe hvyo.HUYO DADA ANA NAFASI BADO YAKUONYESHA UWEZO WAKE MUNGU AMSAIDIE.AMEN

 7. Anonymous

  July 21, 2013 at 7:38 pm

  me Nampa pole na hongera mwanamke mwenzangu bado muda unao usikae kimya nenda kwa watu kama kina wema au johari na mwenzake ray uanze na kuwa acress hushindwi na kuimba integemea unaimba nini lakini nenda kwenye movie ni ajira tosha na kama unamtaji unweza ukatengeneza movie yako ukwashirikisha hao au nenda kwa kiongozi wa kaole anaweza kukupa ushauri lakini sio kwakukaa toka hangaika mungu atakusaidia

 8. Judith Mwanri

  July 22, 2013 at 6:30 am

  Dina bado nafasi anayo tena sana tu. Mi mwenyewe nina kipaji kikubwa tu na nacho fanya sio ninachopenda bt nafanyia njaa tu. Lakini bado sijakata tamaaa kabisa najua juhudi zangu hazitapotea bure ntafikia tu kufanya vile navyopenda.

 9. Tedddy Emmanuel

  July 22, 2013 at 8:32 am

  Dah, huyo dada amenigusa sana yani kama mimi navyoumia na vipaji vyangu, ee Mungu tusaidie na sisi

 10. dinnakaiza

  July 22, 2013 at 9:00 am

  mmmhh kiukweli tupo wengi ambao vipaji tunazeeka navyo mfano mimi najua kuchora,kutunga stories na kudesign home decors kama flame za picha kutumia shells za baharini na vitu mbalimbali ukiingia chumbani kwangu ni vitu ambavyo utakutana navyo kwanza ila ndo kipaji kinaishia chumbani na sebuleni kwangu na kwa baadhi ya nyumba za marafiki zangu. pia naimba ingawa kwa sasa naimba kwaya hapa chouni kwetu.natamani siku moja Tanzania na ulimwengu uone vipaji vilivo ndani yangu na bado sijakata tamaa nitajitaidi hata vipaji vichache nivitumie kuwainspire watu wengine. ila kiukweli mazingira ya familia tunazokulia hazitupi motisha ya kufanya what we have inside and what we feel to do out of love and disire.

 11. Anonymous

  July 22, 2013 at 12:02 pm

  mwee inauma,mi mwenyewe nimekuwa lawyer lakini napenda kuongea kipaji changu ni kuinspire watu nikimuonaga mahiga modesta kwenye capacity building au taji liundi akifacilitate event Napata vipele baridi!!!am just like them may be better niinue popote muda wowote kundi la aine yoyote I can make a statement that will make you happy or sad or inspired…depends on what u want. naumia jamani why cant I just do that and live!maskini mie nimekomaa na majitabu na ma masters degree ya sheria basi tu for salary,mdau umeniumiza roho

 12. RUKKY

  July 22, 2013 at 2:15 pm

  DAA TATIZOKUBWA NI MADHARAU YA WAZAZI WETU SIJUI NISEME NA HUKO MASHULENI.. MI PIA NINA VIPAJI VINGI TUU NA NIPO OVER 30 ILA SIJAKATA TAMAA SOON NTATOKA ISHAALAH TENA BILA KUENDELEA KUSUBIRI KUNYANYULIWA..MAANA NIMESUBIRI NIMEJITAHIDI VYAKUTOSHA NGOJA NIMALIZE SHULE.. WE MDAU UNAO MUDA TENA NA MUME ANAKUSAPORT SHUKURU MUNGU..

 13. Anonymous

  July 23, 2013 at 7:13 am

  Ushauri tu kwa wenye vipaji au karama walizojaliwa na mwenye enzi mungu kitendo cha kujua au kujitambua tu kama unauwezo wa kufanya kitu unatakiwa ukifanye mfano kama ni muimbaji mzuri nadhani chance nzuri ingekuwa kwenda kujiunga na kwaya kanisani na ukiweza inabidi kuangalia role model wako unaowa admire wametoka vipi,mfano kina Rose muhando na waimbaji wengi wameanzia kwenye kujumuika na waimbaji wengine na vipaji vyao nikachomoza ktkt ya kundi,unatakiwa kufanya umma utambue kama una kipaji na kati yao ndio utapata wa kukuendeleza, au kushauri na kukidhi dhana ya kipaji.Angalizo mara nyingi kipaji cha mtu ni lazima kitumike na nafsi haitulii mpaka kifanikishwe but kuna uwezekano wa kupenda kitu kama hobby na ukaweza kukifanya na kutamani kiwe kipaji na nafsi ikahalalisha hobby kuwa kipaji nawe ukaamini kuwa una kipaj, kama ndivyo hata usipofanikiwa kufanya upendacho ktk maisha yako utabaki kuumia tu pale unapoona tukio linalokukumbusha jinsi ulivyokuwa unauwezo wa kufanya jambo lakini sasa hufanyi.

 14. Anonymous

  July 23, 2013 at 9:17 am

  dah mi nilikua napenda sana sana kua DJ au mtangazaji haswa haswa DJ.. yan kazi inayonifanya niwe karibu na mziki coz napenda sana mziki, ila nt kuimba..my DJ RAY C (enzi hizo) na DJ FETTY ndo walokua waninspire nikaenda na maza ad kwa DJ fulani radio onea aliangaza watto wenye vipaj waende bt kufika kula magumash mengi , maza akaona sio kesi nikarud zangu xul nw nimeajiliwa wizara fulan tofaut na mambo ya muziki ndo kishadead tena..Limebaki jina tu DJ HINSY DJ HINSY..nahis ndo nilichoambulia

 15. Anonymous

  July 24, 2013 at 5:56 am

  jamani dina me naona hasa wanawake tusibweteke inabidi tujitahidi sie mwenyewe kwani tunaweza tukiamua sio mpaka tuwezeshe jamani. Aunt ata mie vipaji vya kutosha sana. Dina me naona wewe unakipaji cha uvumbuzi embu anzisha kagroup kama m2 anaweza kuimba bs wajoin. ama kufanya kazi yoyote mjoin ata watu 3 au 2 me nadhani mambo yataenda hapakama vp huyo dada kama yupo tayari anaweza kutaungana tukaimba ila mie napenda nyimbo za dini. na mambo mengine ya ubunifu na kuigiza it is our chance grab it………..

 16. gosbety

  July 25, 2013 at 8:44 am

  Daaa! dada Dina. Please, mimi najua upo exposed sana kwa watu wenye uwezo na nafasi mbalimbali. Mimi nakushauri, kama huyo dada yupo hapa Tz hebu jaribu kumuunganisha na watu wa bongo movie ili ajaribu kipaji chake au hata watu wa bendi na wachoraji vilevile. Mimi naamini bado ananafasi ya kuonyesha kile ambacho mungu amempatia. Unajua nini, km unanafasi ya kumsaidia, wewe msaidie isije ukaja ulizwa huko mbeleni kwanini hukumsaidia ili kuinua kile ambacho mimi niliweka ndani yake!. Muunganishe na kina ray, lucy komba, rose ndauka na wengineo na akaanza kama underground then ata take off!

 17. Anonymous

  July 25, 2013 at 2:29 pm

  dina yani watu tupo wengi ambao karama zetu tunazizika hivi hivi, dina mfano mimi pia kipindi nipo secondary, yani nilikuwa naandika hadithi watu shuleni wanafanya kuweka oda plz ukimaliza naanza mimi na wanandika majina ya booking kabisa, naandika vizuri kwenye daftari kana kwamba ni kitabu, natengeneza story dina mtu akisoma mpk analia, yani hata yale madaftari yangu sijui yalienda wapi. yani huwa wakati mwingine natizama movie zetu hizi zina niboa mbaya mana haina kichwa wala mguu, ni chache sana zinazoeleweka na zina story ndefu ya kudesrve hata kuwa na part one n two. lakini im sure wapo watu ambao wangeweza kutengenezea watu story na movie zetu zikawa nzuri na zisizojirudia na zenye mafunzo ya kutosha, ila ndo hivyo mamy, tunaishi maisha tofauti sana na vipaji ambavyo vingeweza kututoa kabisa.

 18. Anonymous

  July 25, 2013 at 6:45 pm

  dada Dina me naitwa Jabiri kuna kipindi nilikuaga England, nikaona hicho kipindi cha BRITAIN GOT TALENT, kuna mmama wa kama miaka 60 nakumbuka alikuja kushindana, yule mama alishangaza watu watu ki ukweli coz aikuwa na miaka isiyopungua sitini lakini alikuwa anaimba vibaya mno na hakuna aliyewahi kumuona yule mama kabla, so namshauri dada angu huyo asikate tamaa coz kiukweli kipaji hakifi so ipo siku kama ana nia kitaonekana tu ila asijifiche sasa ajaribu kuonana na watu wenye kazi zao, asante.

 19. Anonymous

  July 26, 2013 at 6:36 pm

  Nafasi bado anayo angali mzima tu Mamy wangu , stor imesisimu kiu
  kweli dah.

 20. Anonymous

  July 31, 2013 at 11:36 am

  duh tuko wengi wenye uchungu moyoni kwa kukosa kufuata talents zetu Mungu alizotupa, wazazi wa leo tujifunze watoto wetu wasifate makosa tuliyofanyiwa na wazazi wetu. dada ana uwezo wa kufanya analotaka kuonyesha karama zake na kama mumewe anamsapoti basi afanye
  asante dina

 21. Anonymous

  September 4, 2013 at 7:23 am

  Hi Dina naamini huyu dada ni wewe unayeweza kumsaidia kwa njia yoyote utayoiweza,jiulize kwa nini roho yake imeguswa kukuandikia wewe so please do something kumusaidia.Nchi yetu ina watu millions kwa nini akuchague wewe, usimuangushe tafadhali.

Leave a Reply