Uncategorized

KITUO CHA WATOTO YATIMA NA WANAOISHI KATIKA MAZINGIRA MAGUMU CHA VETERAN TEMEKE!

By  | 
Katika ule mradi niliouelezea wa Dada Dina Cares nilipata nafasi ya kwenda temeke vetenary na kukutana na mwanamke huyu pichani.Mwanamke huyu ni mwalimu wa chekechea mlezi wa watoto yatima na wale wanaoishi katika mazingira magumu na hatarishi.Kihistoria ni mzaliwa wa mkoa wa Morogoro ambae alipata ulemavu akiwa mdogo baada ya kuugua ugonjwa wa polio anaitwa Honoratha Soud.Akiwa mdogo aliugua polio iliyopelekea kupata ulemavu mpaka leo.Hajaolewa na wala hana mtoto ila analea wadogo zake wawili na bibi yake baada ya wazazi wote kufariki.
Nilivyofika tu nikapata rafiki anaitwa Ad ni mcheshi kiutoto utoto tunasema mtundu nae analelewa na Honoratha.Honoratha alisukumwa kulea watoto kulingana na mazingira aliyokulia.Kuwa mlemavu katika familia maskini tena kijijini alikijuta akitengwa sana mpaka walipotokea wazungu wakamchukua kutoka kwa wazazi wake na kumuweka katika vituo kumlea na kumsomesha.Alinitajia kituo hicho nimekisahau ambacho wazungu hao walishaondoka ila walimuacha akiwa na elimu na uwezo wa kujisimamia.Elimu inayomsaidia mpaka leo kwani ni mwalimu wa chekechea na anashule yake mwenyewe.
Shule hiyo ndio anafundisha watoto wake yatima na wamazingira magumu na wale wenye wazazi.Wenye wazazi ndio wanalipa ada Tsh 10,000 kwa mwezi.Madarasa hayo usiku ndio wanatandika magodoro wanalala asubuhi wanakunja na kuwa shule.Aliweza kununua kiwanja na akajenga kwa msaada wa mdogo wake ambae ni fundi ujenzi.
Honoratha anaweza kuendesha maisha ya watoto kwa ada anayopata pia kilimo.Anasema zamani alinunua shamba mkoani mbeya anakojishughulisha na kilimo cha mpunga na maharage.Akivuna anauza pia kupata chakula cha wanawe.
Nilikuta watoto wanakula chakula cha mchana
Wadada wanaowasimamia watoto  kwa kuwapikia,kuwaogesha,kuwalisha n.k
jikoni kunakopikwa
Kwa nyuma huko ndio stoo na wanakoweka magodoro
Nilimkuta mdogo wa Honoratha akifanya ujenzi wa chumba ambacho wanatarajia ndio kiwe cha watoto kulala moja kwa moja.Sio kulala usiku asubuhi darasa.Challenge ndio vitanda,magodoro,mashuka,na vyandarua na madirisha kuyaweka nyavu ili watoto wasing’atwe na mbu.Amejitahidi mwenyewe kajenga vizuri kweli na mimi nikamuahidi tutamtimizia hayo.Mdogo wake huyu anamsaidia sana linapokuja swala la kujenga na ufundi wa vitu mbalimbali.
Hapo ana watoto ambao wanalelewa na bibi baada ya wazazi kufa na bibi hajiwezi kwa lolote.Analea watoto ambao wazazi wapo lakini hawana uwezo wa kufanya chochote kwa watoto wao hivyo kuishi katika mazingira magumu na hatarishi pamoja na wale yatima.
Nilichomuahidi ni vitanda,mashuka,magodoro,vyandarua,nyavu kwenye madirisha,sabuni za kufua na kuoga,dawa za meno,mafuta ya kujipaka,nguo na chakula.
Baada ya maongezi nikaondoka na mama akanisindikiza.Nashukuru baada ya kuongelea Dada Dina Cares respond imekuwa kubwa namshukuru Mungu kwa hilo naamini tutafanikisha.
Kila mmoja moyo wake unasukumwa kushiriki kujitolea kwa hali na mali.Pia nashukuru wale mlioniandikia kwa kunipa mawazo/ideas mbalimbali.
Nilimuacha my friend amelala hata sikumuaga.
Ntaenda tena next week!
 
Bado sijatoa utaratibu wa wadau wangu wa blog mtachangia nini,kwa sababu nafikiria kiwe kitu kimoja au viwili vya msingi.
Nakaribisha maoni pia kwa dina_marios@yahoo.com

15 Comments

 1. esther nyalusi

  July 6, 2013 at 3:06 pm

  Kwakweli tunaitaji kuwasaidia hawa watoto kwa pamoja sio siri wanaitaji msaada kwa pamoja tunaweza.tunasubiri utaratibu WA kuchangia

 2. Anonymous

  July 7, 2013 at 2:36 pm

  yaan hongera sana dina naomba npe maelekezo ya kufika mahali apo nna hitaji kufika apo kwan itakua rahisi kwangu. kwan nafanya kazi maeneo ya temeke na ninahitaj sanaa kufika kituon apo ikiwezekana. ata wik ii hapa asante.barikiwa sana na Mungu apajaze pale palipopungua

 3. Anonymous

  July 8, 2013 at 3:44 am

  count me in ukishasema mahtaj 2tajichanga changa 2 ucjal 2gether we can..

 4. Anonymous

  July 8, 2013 at 8:54 am

  Kituo kina itwaje,kama naweza kwenda,sijaelewa kuhusu ada ya sh elfu kumi ni nani ana lipa.

 5. ELIUD SAMWEL

  July 8, 2013 at 8:57 am

  Dada dina tuko pamoja sana katika kila ufanyalo pia endelea kufanya hivyo bila kuchoka kwa tunaamini mungu pekee ndo anauwezo wa kukulipa,sisi tunazidi kukuombea baraka na mafanikio tele

 6. nawinaspace

  July 8, 2013 at 10:07 am

  Hi Dina
  Unafanya kitu kizuri sana. Si kila mtu anaweza kuwapata wahitaji kama ambavyo umefanya. Isipokuwa ukiwapata kama hivi ni rahisi kuchangia hata kama una kitu kidogo tu. Keep up the good spirit. Tunasubiri utaratibu

 7. Anonymous

  July 9, 2013 at 6:51 am

  da imenigusa sana hata kama sn uwezo wa kusaidia but umewaza jambo jema sana na mwenyezimungu atakuzidishia duniani na kesho akhera, tuko pamoja

 8. Anonymous

  July 9, 2013 at 8:25 am

  Hongera Dina kwa kuonyesha moyo wa kuwasaidia watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu ili nao wapate mahitaji muhimu kama wanayoyapata watoto wengine.

  Mungu akuzidishie pale ulipopungukiwa kwa upendo mkuu.
  Janeth from Morogoro.

 9. Anonymous

  July 9, 2013 at 2:02 pm

  mpango mzuri tujuze utaratibu tupo nyuma yako

 10. Anonymous

  July 9, 2013 at 4:08 pm

  kwa kweli inatia huruma, naimagine na mimi kesho kama nimekufa mwanangu anaweza akaishije? God bless U Dina na wote mnaojitolea kwa ajili ya watu mwenye mazingira magumu, especially watoto ambao ni TAIFA LA KESHO.

 11. Anonymous

  July 10, 2013 at 8:38 am

  Kiukweli nimeguswa sana. huyo mama ni mfano wa kuigwa. na Watanzania wenzangu kutoa ni moto kama mama huyo mwenye ulemavu ameweza kujitoa kiasi hicho sisi tunasubilia nini???? tuwasaidie watoto hawa. Mtoto wa mwenzio ni wako. Dina Mungu awe nawe kwani kupitia wewe tutaweza kuwasaidia watoto wenye huhitaji,

 12. Anonymous

  July 10, 2013 at 2:45 pm

  Tuelekeze bac jinsi ya kuchangia

 13. Anonymous

  July 11, 2013 at 1:22 pm

  Dina weka namba ya mpesa tuchangie kwani wengine tuko mikoani hatuwezi kuja dar , tumeguswa na tutashiriki , endelea kuwa na moyo huohuo

 14. Anonymous

  July 12, 2013 at 7:30 am

  So touching God bless you..just praying for you to continue having that big heart of yours of helping others.

 15. Anonymous

  July 12, 2013 at 9:27 am

  huyu mama kuwa naye makini si mkweli hiyo ni biashara kama zingine si kwamba anasaidia watoto wanaoishi mazingira magumu.take it as advice ninamfahamu vizuri fanya uchunguzi utaniambia.email yangu kapuni plse

Leave a Reply