Uncategorized

MAMA JUDITH APATIWA MSAADA

By  | 
Ijumaa kuna mama alikuja ofisini na watoto wake watatu mdogo kabisa akiwa ni mchanga wa wiki moja.Mama huyo alikuwa amepoteza uelekeo wa maisha baada ya mume kkumkimbia na mwenye nyumba kumfukuza baada ya kushindwa kulipa kodi.Mume aliingia mitini toka mimba ina miezi miwili.
Basi Gea akamsikiliza na habari yake tukairusha kwenye heka heka ili aweze kuchangiwa hela ya kodi ths 100,000 na apate mtaji wa vitumbua tsh 50,000 angalau laki mbili hapo hapo apate pesa ya kujikimu.
Tukajiuliza huyo mwenye nyumba wa kumfukuza huyu mama na mtoto wa wiki kwa nini lakini?
Bahati nzuri walikuja wadada wawili wakatoa laki moja na ikabaki laki moja.Wafanyakazi wa clouds tumekuwa na kawaida wakija watu wenye shida tunachangishana mwenye buku,elfu 2,mia tano mpaka hela inapatikana muhusika anapewa.Hata kwa huyu mama tulichangishana hivyo hivyo hiyo laki nyingine ikapatikana.
Pichani Gea ndio alikuwa akiendesha harambee hiyo
 
Ofisi ikatoa gari dereva akakabidhiwa pesa akafika kule akamuona mama mwenye nyumba akalipwa kodi yake Tsh 100,000.Mama mwenye nyumba akasema alimfukuza kwa sababu alimvumilia mda mrefu na yeye mjane na anashida sana huku akitegemea nyumba hiyo hiyo.Mungu ni mwema Mama Judith akapata hela ya mtaji pamoja na ya matumizi juu.
 
*Tumshukuru mungu na tujifunze kuhesabu baraka zetu.Wakati ukilalamika ona kuna mtu anahangaika kwa kukosa laki moja tu pengine wewe una mengi mazuri umejaaliwa ila hushukuru kutwa kulalama.

1 Comment

  1. Anonymous

    July 16, 2013 at 8:41 pm

    Dinna mtoto wa kike wa kiume, nina nguo nyingi za mtoto wa kike ningezituma ila kuzitoa huko itakuwa ni hela ama.

Leave a Reply