Uncategorized

MAPISHI:KIFUNGUA KINYWA CHA VIAZI VITAMU NA CHAPATI ZA MAJI.

By  | 
Kuna wakati katika leo tena tulikuwa tukipeana ideas namna ya kupangilia kifungua kinywa.Lengo lilikuwa kubadilishana mawazo ili kuondokana na mazoea ya kula kifungua kinywa hicho hicho kila siku.Tunaambiwa mlo wa subuhi ndio unatakiwa kuwa mlo mkubwa kuliko mwingine lakini nyumbani ni tofauti.Chai na mkate wa kwa mangi jioni sahani hiyoo ya ubwabwa na maharage.Kina mama walikuwa wakituma mpangilio wa vitafunywa au namna unavyoweza kuandaa kifungua kinywa kutokana na vyakula vinavyopatikana katika mazingira yetu ya kila siku.
Tuna viazi vitamu hapa
Viazi vitamu sokoni viko tele,mihogo na hata magimbi.
Nikavimenya,nikaviosha na kuvikata hivi kwa sababu mie nilikuwa navikaanga,unaweza pia kuchemsha.
Tayari kuliwa na unaweza kula na kachumbari pia lakini mie sikuweka kachumbari.Sikuishia hapo…Nikapika chapati za maji,huu ni mkorogo wa unga wa ngano na maji baridi niliweka,mayai manne,iliki na sukari.Niakavikoroga vizuri vyote kwa pamoja.Chapati za maji wapo wanaopenda za chumvi,wengine sukari.Mie napenda zote zote ila hizi zilikuwa za sukari.
Chapati za maji ni mlo rahisi sana kuandaa na fasta,najua kina dada na kina mama karibia wote mnaliweza.
Hapo chapati zipo tayari kuliwa.
Siku sahau matunda tikiti,sasa hivi matunda yapo kibao hasa ya msimu.Kuna mapapai,machungwa,embe,parachichi na matikiti.Tunda la msimu lisikose kwenye kifungua kinywa au tengeneza juisi.
Hapo kifungua kinywa kikawa tayari viazi vya kukaanga,chapati za maji,chai ya maziwa na matunda.
 
N.B Nipo kwenye maandalizi ya jarida la mapishi ya vyakula vilivyopo katika mazingira yetu ya kila siku.Jarida hili limehusisha wanawake na wadada waliopenda kushiriki kutoa ideas za mapishi yao wanayoyajua.Jarida hili la kwanza litagusa kifungua kinywa tu namna ya kupika na namna ya kupangilia huo mlo kwa kuzingatia mlo kamili wenye afya.Lengo hasa ni kumpa mama/dada mawazo kuwa kuna uwanja mpana wa vyakula asikariri.Hata dada wa kazi nyumbani linaweza kumsaidia pia.Mwisho wa mwaka ndio utalipata,tena bure…stay tuned!

14 Comments

 1. Anonymous

  July 29, 2013 at 8:48 am

  Litakuwa jambo zuri kwa kweli, maana watanzania wengi hatujui jinsi ya kupangilia milo yetu, tunakula tu pasipo kujua kama chakula tukilacho ni kamili hama la!

  Tupo pamoja

 2. Ruky

  July 29, 2013 at 12:52 pm

  Dina mayai umetia mengi…any whay kila mtu na mapishi yake mi huwa napika hivi km familiya ndogo yai moja km kubwa mayai mawili nayapiga piga kwanza yenyewe hii usaidia ukianza kychanganya kwa unga usipate harufu ya mayai alafu natia inategemea sikunyingine maji nilkuwa nafanya zamani wakujifundisha kupika ilasikuhizi natia maziwa,unga wangano nachanganya kuanzia kwa uzito iliusipate mabuda huku kidogo kidogo natia maziwa mpka saizi ya kuweza kuuchota na upawa nakorogea na sukari,iliki au vanila unakoroga vyakutosha..jikoni naweka kikaango kipate moto wakawaida nachota unga wangu namiminia kwenye kikaango alafu unazungushia juu kwa utaratibu ili isitowe vimacho macho na kupata round nzuri baada ya muda unacheki kwa chin km kuna brown imeeanza kuuiva unageuza hutii mafuata alafu unakuwa km unamasaji kwa wepesi coz hizi nilaini c km chapati alafu unazicheck utakuta rangi nzuri imetapakaa ndiyo unatia mafuta kidogo unaimasage kidogo tena alafu unaigeuza unaiacha kidogo unatowa tayari kwa kuliwa.. mwanamke kupika asikwambie mtu..DINA C KWAMBA NIMEKUKOSOWA NAMI NIMEKUONYESHA TU MAPISHI YANGU..COZ NAPENDA KUIKA KWELI..

 3. Mama 2 (Mrs M)

  July 30, 2013 at 11:26 am

  Mmh Dina bure! tutapata kweli wengine? Mi nalihitaji sana! kwa kweli litatusaidia kuandaa Breakfast.

 4. Anonymous

  July 30, 2013 at 11:32 am

  Pia wakati wa kupika tumia blue band na sio mafuta utazifurahia zaidi.

 5. Anonymous

  July 30, 2013 at 2:46 pm

  dina hivyo vyote unakula peke yako? au una familia kubwa? mayai umetia mengi kwa kweli…..nadhani moja linatosha.

 6. Anonymous

  July 30, 2013 at 2:55 pm

  Pia waweza ongezea kit.maji,carot na hoho unavikata kwa stail ndogondogo inaleta ladha nzuri

 7. Anonymous

  July 30, 2013 at 6:20 pm

  nami ningependa kupata hilo jarida!

 8. Anonymous

  July 31, 2013 at 4:56 am

  nimependa kweli hii mada i wish unishitikishe kwny jarida lako me napenda kwl upishi wa healthy food

 9. sarah

  July 31, 2013 at 8:28 am

  dina chapatti na viazi for me ni double starch/double wanga.Yafaa uweke protein pia, mfano hayo mayai manne badala ya chapati maji ungetengeneza mayai scrambled(ya kuvuruga) yenye mboga mboga ukala na viazi na matunda hapo balanced diet!au ungetengenez hizo chapatti maji kwa yai moja (kama uko peke yako au wachahe) au mawili kwa familia kubwa) halafu ukaanda kitu kam rojo la maini au nyama ya kusaga kidogo tu (nusu ya robo kilo) ambayo unaitengeneza pamoja na maboga mboga kama bilinganya,masukini hoho karots nk ulizokata size ndodo ndogo, na matunda yako pembeni ingekuwa mwake!

 10. Anonymous

  July 31, 2013 at 8:30 am

  ubahili wenu ndio maana mnaweka yai moja, lakini chapati za maji mayai matatu kwenda juu ndio utapata protein kwa wingi, sio yai moja unga ngano nusu au kilo, hapo hupati kitu zaidi ya kujaza tumbona chakula kisichokuwa na faida mwilini. hongera Dina kwa mapishi yako nimeyapenda.

 11. Anonymous

  July 31, 2013 at 4:09 pm

  we mdau hapo juu sio ubahili….ni katika kueleweshana tu……naona povu limekutoka mbona umepanic hivo.

 12. Anonymous

  August 1, 2013 at 6:13 am

  jitahidi na usafi eish izo tiles nazo!!

 13. Anonymous

  August 2, 2013 at 1:31 pm

  umetisher

 14. Anonymous

  August 5, 2013 at 7:35 am

  mh! Wadau jaman

Leave a Reply