Uncategorized

MIHOGO YA MSIMU HUU MIZURI HATARI!

By  | 
Ndugu zangu mnaopika futari mtakubaliana na mimi safari hii mihogo mizuri jamani.Haina mizizi sio cherema na ina unga freshi kwa kupika ule muhogo wa nazi.Lakini sie wakristo ambao hatujafunga ndio tuitumie kwa chai asubuhi tupumzike chai mkate,vitumbua na maandazi.
Unaweza kuukaanga au kuuchemsha vizuri kama mie nilichemsha jumapili hii.Na sio jumapili hii mara nyingi tu sema kuna wakati mihogo inakuwa mibaya una bahatisha  ila safari hii mizuri.
Kachumbari(salad)
Hapo na chai ya rangi yenye viungo freshy kabisa,sikuishia hapo…
Nikaandaa mayai ya mboga mboga
Hiyo juu ni pilipili manga na chumvi
Motoni
Tayari kwa kuliwa,limekauka sana maana mie napenda yai likauke.Hapo nimekata vipande kama pizza tayari kila mmoja kuchukua kipande chake.
Chai ya rangi,muhogo wa kuchemsha,salad na mayai ya mboga mboga mlo wa asubuhi.
*Muhogo ni chanzo kikubwa cha carbohydrates lakini una protini ndogo sana sawa na hakuna.Una energy nyingi na hauna mafuta.Ukiula hakikisha unakuwa na chakula kingine chenye protini.
*una madini ya calcimu,phosphorus,potassium na magnesium kwa wingi.

12 Comments

 1. Mama 2 (Mrs M)

  July 16, 2013 at 4:22 am

  Ni kweli Dina, inabidi tupunguze kula mikate, maandazi au vitu vya ngano kwa ujumla. Mi naungana nawe sana tu.

 2. Anonymous

  July 16, 2013 at 5:56 am

  DU! Jamani Dina nimependa sana umenitamanisha sana ndugu yangu. Jumapili na mimi nitapika kwa ajili ya chai maana mikate imenichosha sana kwa kweli. Naamini mume wangu atafurahia sana. Asante sana kwa kutukumbusha asili!

 3. Anonymous

  July 16, 2013 at 5:57 am

  Dina ulikuwa na wageni? natumaini wageni wako walifurahi sana na walienjoy breakfast!

 4. Anonymous

  July 16, 2013 at 9:14 am

  dina kwa mtaji huu utapungua kweli?

  • Anonymous

   July 17, 2013 at 1:33 pm

   Hujaelewa au hujui nutritional facts za chakula hicho? Halafu unataka Dina apungue mara ngapi?

 5. frank sanga

  July 17, 2013 at 8:43 am

  nice mlo

 6. alex mwambela

  July 17, 2013 at 1:46 pm

  hinooooma dina sijui yamkoagani

 7. Anonymous

  July 18, 2013 at 9:15 am

  Wapenda Mapishi Shoste, huyo shemeji yetu atafaidi balaa

 8. Anonymous

  July 18, 2013 at 9:30 am

  DINA MIMI HUWAGA NAKUPENDAGA BURE TU ,NINGEKUWA MWANAUME NINGEWEZA KUJARIBU MOVE.NAOMBA KUULIZA SWALI LA KIZUSHI , DADA DINA WEWE UMEOLEWA? UNA MCHUMBA? MAANA KATIKA MISHEMISHE ZAKO ZOTE SIJABAHATIKA KUONA UKO BENNET NA MTU AU HATA KWENYE PICHA KAMA WANAVYOFANYAGA MASTAR WENGINE , NI MAMBO YA KINDANI LKN NAHISI KAMA HUWA NATAMANIGI KUMJUA UNAYEDATE NAYE AU MUME WAKO.
  ASENTI

 9. Anonymous

  July 19, 2013 at 5:46 pm

  du ndio mlo wetu huu, sikuizi kila weekend lazima tuandae kitu cha muhogo na kachumbali, but leo nimejifunza kitukipya cha mix na yai pembeni,

 10. Anonymous

  July 19, 2013 at 5:47 pm

  kama utumii mayai unaweza pia kuweka na samaki pembeni, looooooo atariiiiiiiii

 11. Anonymous

  July 23, 2013 at 9:14 am

  THANKS DINA KWA PISHI ZURI

Leave a Reply