Uncategorized

MRADI WA DADA DINA CARES

By  | 
Wadau napenda kuwatambulisha kitu changu kinaitwa Dada Dina Cares au Dada Dina Anajali.Hizi ni zile shughuli za kusaidia jamii nitakazokuwa nazifanya mimi binafsi.
Mnakumbuka niliahidi baada ya kushinda ile tuzo yangu ya mwanamke wa mwaka nilipanga tufanye Dinner with Dina celebrating Dina.
Baada ya kuwaza nikasema hapana acha nifanye jambo litakalogusa maisha ya mtu mwingine.Ndio nikaja na hii Dada Dina Cares.Wale washindi wangu wa email tayari nimeshawasiliana nao kuwaeleza wazo hili na wamelipokea vyema.Mie nimejikuta naitwa dada Dina na wasikilizaji wangu iwe kwa kutuma msg,email au hata tukikutana ndio nikaona acha niendeleze hii dada Dina.
Wote tunaelewa role ya dada katika maisha ya kila siku.
Nilichoamua ni kuchangisha pesa,chakula,nguo na vitu mbali mbali ili kuvisaidia vituo vitatu vya watoto yatima.
Nimeshatembelea vituo mbali mbali vya kulea watoto yatima na wale wanaoishi katika mazingira magumu ili nione changamoto walizonazo na ni vipi tunaweza kuwasaidia.Nimekutana na walezi pamoja na watoto wazuri wazurii ambao maskini waliachwa na wazazi,wazazi hawajiwezi au wanalelewa na bibi na babu ambao hawawezi kuwapa mahitaji yao.
Dada Dina Cares itashirikiana na wewe mdau,wasikilizaji wa clouds fm,wanasiasa,makampuni,mastar wa bongo na taasisi mbalimbali kufanikisha hili.
Mahitaji niliyoyakuta huko ni pamoja na ukosefu wa vitanda,mashuka,magodoro,vyandarua,nyavu za madirisha,nguo,chakula,sabuni,mafuta.
Vituo vingine vinadaiwa kodi za nyumba yaani changamoto ni nyingi.
Walezi wa vituo hivi wengi ni wanawake na unakuta wamekimbiwa na waume sababu ikiwa ni kujitolea kwao kwa hawa watoto.Kila unaemuuliza ana kwambia hajui kwa nini ila anajikuta anasukumwa kulea watoto.
Changamoto yao kubwa pia ni kwenye elimu serikali inawasaidiaje watoto hawa yatima kusoma bila usumbufu.Wao wamewapa makazi na malazi lakini inapokuja ishu ya kuwasomesha inakuwa kazi sana kwani hawana pato la kuwatosheleza.
Zoezi hili nitalifanya katika mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani.Activity za kuwawekea vitu kwenye vituo zitafanyika wakati huo pia.Na siku ya Idd pili nitawakutanisha watoto hawa kwa chakula cha mchana na michezo mbali mbali.Watakula na kucheza na watoto wa wasikilizaji wangu,wadau wangu wa blog,mashirika na makampuni yatakayopenda kushiriki,wanasiasa na macelebrity.Nataka watoto siku hiyo wafurahi sana.
Nitawapa maelezo vizuri ya namna ya kushiriki kuchangia na kuhudhuria ile shughuli ya chakula na michezo ya watoto.
Hivi ndivyo nimeamua kusherehekea tuzo yangu ya mwanamke wa mwaka.Tayari ofisi yangu imeshajitolea milioni 2 kwa ajili ya Dada Dina Cares.Kampuni ya Maxmalipo ml 1,UWF ml 1…..naamini wengi watajitokeza kadri siku zinavyoongezeka.
Kesho nitaanza kuwawekea picha za kituo kimoja wapo katika hivyo vitatu.Kwa maoni niandikie dina_marios@yahoo.com

16 Comments

 1. Anonymous

  July 1, 2013 at 5:49 pm

  Wazo hilo ni zuri sana hata mimi nimelipenda sana tena sana kwani ungesherehekea hiyo tuzo yako kwa ule mtindo wa awali ingetunyima sisi wengine nafasi ila kwa wazo hilo nimelipenda nasi tutashiriki kwani mi niko mbeya na nilitamani sana nami nishiriki kwenye hiyo dina with dinner celebrating lkn ilinivunja moyo sana kwani hata kam ningekuandika hiyo email na ukanichagua nami nihudhurie ingekuwa ngumu sana kwangu kuja dar lkn kwa mtindo huo tuko pamoja.

 2. HabbieH

  July 1, 2013 at 10:04 pm

  I wish niparticipate, hata kama mimi sina basi atleast I'll try to inform others.

  May God lead this service.
  Bless!!!

 3. Anonymous

  July 1, 2013 at 10:33 pm

  nakupenda dd dina, umefanya vizuri. ila naomba msaada wa kupunguza unene!

 4. Anonymous

  July 2, 2013 at 5:11 am

  Hongera dna tutashrikiana na ww mtoto mzr ,

 5. emu-three

  July 2, 2013 at 6:33 am

  Hongera mpendwa, hapo umegusa penyewe, wajalini sana hawa wasiojiweza kuliko sherehe za kifahari, ….gharama nyingi kwenye sherehe hizo ambazo zingelisaidia watu kama hawa!

 6. Anonymous

  July 2, 2013 at 10:05 am

  Mungu akubarikina kukulinda día.mawazo mazuri.katika huku utabarikiwa sana dada dina,tuko pamoja

 7. Anonymous

  July 2, 2013 at 10:08 am

  kip it up dinna huwa napenda unafikiria kabla ya kutenda God be with u mamy pamoja sana

 8. Ruky

  July 2, 2013 at 12:13 pm

  Daaa umenigusa..ishaalah tuombeane uzima tupo pamoja..

 9. Anonymous

  July 2, 2013 at 1:06 pm

  Dina mimk nawazo ukilipenda nijulihe mwanangu amekua.na amechanguo nyingi na viatu sikuona haja ya kuwapa watoto wa.ndugu.zangu maana wana.wazazi.na uwe so nilikua na mwambia kua tupeleke kituo cha watoto yatima so kama uta zioe da nikuleteee mana sijjuni nguo mpya unatka au hata za zamani maana bado ni nzuri sna .ongera kwa jambo jema lakimungu kutoa ni bora kuliko kupokea mungu akubariki.utakua mama bora siku ukiwa na wanao

 10. Ald

  July 3, 2013 at 6:00 am

  Hongera sana, unaendelea kufanya mambo mazuri mno mno. Kuna jambo moja tu hujanifurahisha mie binafsi(japo ni kwa mapenzi ya Mungu). Ninakuombea akujalie kwa hilo, nawe uwe na moyo wa ujasiri wa kuamua.

 11. Mama 2 (Mrs M)

  July 3, 2013 at 8:15 am

  Hongera sana Dina! hilo ni jambo jema sanaa!

 12. Anonymous

  July 3, 2013 at 9:28 am

  Wow, ni wazo zuri mnooooo, Mungu akuzidishie moyo wa huruma…

 13. Anonymous

  July 3, 2013 at 12:24 pm

  MBONA HUJATUWEKEA PICHA ZA HARUSI YA ASMA MAKAU? ACHA WIVU BI DADA SIJUI SAFARI HII UTAKUJA NA UTETEZI GANI KAMA KAWAIDA YAKO UTASIKIA MARA KAMERA YANGU ILIKUWA MBOVU KAMA ULIVYOFANYA KWA DA HU. HATUJASAHAU DADA. BADILIKA!!

 14. Gee

  July 5, 2013 at 6:14 am

  Aiseee! Dinna hongera sana mamy kwa kweli umenigisa nami, japokuwa sina uwezo mkubwaaaaaa ila nitatoa kile kidogo nilichobarikiwa tupo pamoja, nitakuandikia kwenye email yako nijua details zaidi, Ubarikiwe mamy ……

 15. Femmy

  July 6, 2013 at 3:42 pm

  U r so great Dina,me love u mungu mingi, wish u all the best may Allah light up ur way.

 16. perry senya

  July 11, 2013 at 8:39 am

  Mungu akuzidishie apanue mipaka yako na ubarikiwe sana wewe umewekwa na mungu kua msaada kwa wengine

Leave a Reply