Uncategorized

NAMNA YA KUCHANGIA MPANGO WA DADA DINA CARES!

By  | 
Dada Dina Cares inaendelea vizuri kabisa na Mungu akipenda malengo yatafikiwa.Mwezi huu mtukufu wa Ramadhan nachangisha pesa,mavazi,chakula,mahitaji ya mafuta,sabuni,vifaa vya shule n.k
Vitu hivi ni maalum kwa vituo vitatu vya watoto yatima cha vetenari kipo Temeke,Sifa kipo Bunju,Zaidia kipo Sinza.
Pesa ni maalum kwa kununua chakula,vitanda,mashuka,vyandarua,magodoro.
 
Namna unaweza kuchangia pesa maana wanasema haba na haba hujaza kibaba kwa kadri utakavyojaaliwa kwa MPESA 0759 789863 na TIGO PESA 0657 795654.
Napokea pia nguo,viatu kina mama kagueni nguo za watoto wenu mnazoona zinafaa lakini watoto zimewaruka labda nifikishie hapa clouds fm mikocheni.
Nawashukuru sana Clouds fm,Uwf,Mwamvita Makamba,wasanii Shilole na Godziler.Wadau wa blog ambao mmechangia mpaka dakika hii.Kuna wadau wa blog,kampuni siwezi kuwataja wamechangia tayari kutokana na wao kutokutaka kutajwa napenda mjue nawashukuru sana.
 
Napenda mjue hiki ninachofanya ni sehemu ya shukrani zangu kwa Mungu kwa mengi aliyonijaalia ikiwemo tuzo yangu ile ya mwanamke wa mwaka.Kama nilivyosema mie sio tajiri kipesa ila kipaji alichonipa Mungu kinafanya sauti yangu isikike mwa mamilioni ya watanzania.Na uwezo huu utanifanya niwaunganishe watanzania kusaidia kulea hawa watoto yatima.Na walio katika mazingira magumu.Tuwasaidie hawa walio na mioyo ya kukaa nao kuwalea na kuwapa mahali pa wao kupaita nyumbani.Kama mzazi Mungu amekuweka umeweza kulea watoto hadi leo kumbuka wapo wazazi hawajaweza kufanya hivyo na watoto wao kuitwa watoto yatima na kuishia kulelewa kwenye hivi vituo.Tusaidie kadri tulivyojaaliwa.
Sio lazima kupitia dada dina Cares.Unaweza kuangalia mwenyewe pato lako ukaenda katika kituo ukaamua kuwa unamuwezesha mtoto mmoja au wawili kusoma na kupata mahitaji yake muhimu.Unakuwa unampelekea nguo,mafuta na sabuni,uniform na vifaa vya shule na ada.Tena kama bado yupo elimu ya msingi gharama ni ndogo.Mara moja moja unamkutanisha na watoto wako anashinda nao au kulala na kucheza atajisikia kupendwa.Hawa watoto wanajua kabisa kuwa ni yatima ila uwepo wako unamfanya aone kuna mtu mwingine anaeweza kumjali na kumpenda.

11 Comments

 1. frank sanga

  July 21, 2013 at 6:30 pm

  #tutachangia mwaya

 2. Anonymous

  July 21, 2013 at 7:42 pm

  Dina me ndugu nilie nje ya nchi aishi huku lakini natamani sana kusaidia maskini nikija nikija nitakutafuta usijali hongrera mungu akusaidie ila me baada ya kuonana nitakusaidia mengi

 3. Anonymous

  July 24, 2013 at 7:46 am

  hicho kituo cha bunju kiko sehemu ipi miye naishi huko niweze kuwatembelea hawa watoto

 4. Anonymous

  July 24, 2013 at 4:46 pm

  Hongera sana Dina kwa kazi nzuri, Mungu akubariki! Naomba kuuliza je kwenye hivyo vituo kuna watoto wadogo
  , kuanzia mwezi mmoja na kuendelea? Mi ninazo nyingi sana, ningependa nichangie.

 5. joyce kiria Wanawakelive

  July 25, 2013 at 3:37 pm

  Hongera sana sana Madam Dina. Tupo pamoja unafanya kazi nzuri mno. Mw/ Mungu akutie nguvu na abariki kila unachogusa na kila hatua unayopiga.

 6. joyce kiria Wanawakelive

  July 25, 2013 at 3:41 pm

  Mchango wangu unakuja Madam Dina. Wewe ni Mwanamke wa mfano, na kwa hakika hata mimi nakuona wewe ni Role model wangu. Songa mbele madam tupo nyuma yako.

  • dinamarios

   July 25, 2013 at 7:41 pm

   NASHUKURU SANA NA KARIBU SANA DADA.

 7. Anonymous

  July 26, 2013 at 9:10 am

  Be blessed madam dina,am behind u with prayers.

Leave a Reply