Uncategorized

CHAKULA NA KEKI YA WATOTO KWENYE PARTY YA DADA DINA CARES

By  | 
 Chakula cha watoto kilipikwa pale pale Azura
 Janet Sosteness akisimamia watoto kunawa
 Kuna watoto walichukua chakula chao wenyewe
 Watoto wengine walipelekewa walipo wasanii Mwasiti,shilole na wasikilizaji wangu Blandina Mvungi,Halima Temu waliwasevia watoto chakula

 Niliweza kuongea na watoto
 Linapokuja suala la kujitolea kwa yatima na wasiojiweza watu wengi huwa wanaguswa.Nilienda Fying Chefs tambaza wale watengenezaji wa keki nikawaeleza juu ya mpango huu.Nilichowaomba ni wao kunitengenezea Keki ya watoto kwa siku hiyo hawakusita walishiriki na jana keki ikawa kama inavyoonekana.
 Nikakata keki,pembeni kuna mifuko mikubwa ya maandazi inaonekana.Maandazi hayo Fatma Almas Nyangasa wa itv aliwaletea watoto.Ilikuwa mifuko mitatu ambayo kila kituo ilibeba mmoja kwa ajili ya watoto kupata kitafunwa cha kunywea chai kesho yake.
 Niliwalisha watoto watatu waliowakilisha vituo vyao
 Watoto wengine waligaiwa kipande pamoja na wageni waliokuwepo.Keki ilikuwa kubwa sana tulikata mapande matatu na kuwapa kila kituo wakale wakirudi nyumbani.

 

Kama ambavyo niliona visions wakati nawaza kufanya hili jambo miezi kadhaa iliyopita na ndivyo ilivyotimia.Picha zato nilizokuwa nazo kichwani zilitimia jana pale Azura.Niliona kila kitu kabla na nikakifanyia kazi kukileta kwenye reality.Asante wote mlioshiriki kukamilisha picha hizi lakini zaidi ni Mungu maana naamini anatenda kazi yake kupitia mimi bila yeye mie si lolote.Nashukuru kwa wewe uloguswa na ukachangia kwa hali na mali na hata muda wako kuja kukaa na watoto toka zoezi linaanza.
Naamini kila mtu uwezo wa kujitolea kwa wengine anao ila ili awezekushiriki lazima awe na taarifa sahihi itakayomgusa kufanya hivyo.
Dada Dina Cares ni jina tu nililoamua kuipa hii campaign wala sio NGO ila watu wengi wanashauri iendelee kuwepo ili kusaidia jamii.
Next Project itakuwa kujenga wodi ya wazazi katika moja ya hospital.Mungu akipenda inaweza kuwa chini ya Dada Dina Cares or Leo tena ya clouds fm.
Ili kuendelea kuvipa suport vituo hivi na vingine kuna kitu nitakiintroduce kesho ukitembelea hapa utakiona.
Asanteni Wote na Mungu awabariki!

35 Comments

 1. mhinakisina

  August 12, 2013 at 7:42 pm

  Mungu akubariki kwa moyo wako

 2. Cymah Wandelt

  August 12, 2013 at 11:10 pm

  Ubarikiwe dadangu, nashindwa jinsi ya kushukuru ila nakuombea kwa Mola.

 3. Anonymous

  August 13, 2013 at 5:49 am

  hongera dina n jambo zuri ila umetoka km mjamzito vile

  • Anonymous

   August 21, 2013 at 6:35 am

   hata mimi nimeona kama mjamzito vile

 4. Anonymous

  August 13, 2013 at 9:56 am

  usichoke dina, na mungu atazidi kukuonyeshanjia na maarifa ya kuzidi kuwasaidia yatima.

 5. mrsAdoa(mama Grace)

  August 13, 2013 at 10:47 am

  Dina umeniliza Leo,Mungu akubariki na kukukinda.wewe ni mfano wa kuigwa,mengi najifunza kupitia wewe.nakuombea sn kwa Mungu akupe umri mrefu ili uzidi kuisaidia jamii.nakosa cha kuongea ila nimefurahi sana na najivunia uwepo wako japo sijawahi kukuona.nakupenda sn.Mungu awe nawe Kila atua unayopiga.

 6. stellah

  August 13, 2013 at 12:20 pm

  god bless u my dear

 7. Sarafina Migina

  August 13, 2013 at 2:38 pm

  Daaah! Mungu akupe aja ya moyo wako. love u

 8. Anonymous

  August 13, 2013 at 3:13 pm

  hongera sn sn sn kuhusu kujenga wodi ya wazazi jamani mungu akuwezeshe tulifanikishe ni wazo la mbolea sn dina BY THEW WAY HONGERA KWA MABADILIKO YA MWILI WELCOME TO THE CLUB luv u mingi

 9. Anonymous

  August 13, 2013 at 7:49 pm

  daa!yaan sioni kitu cha kukuambia ambacho kita fit apo ila all n all hongera saan yaan mno Mungu wa mbinguni akubariki na kukulinda,naamin uu ni mpango endelev ndo umeanza,pia nmependa wadada wenye upendo waliotoa support kwako mbarikiwe wote,wimbo wa i was here wa beyonce uwe maalum kwako dina,lv u m be blessed as always,yusta

 10. Anonymous

  August 13, 2013 at 9:07 pm

  Da cna cha kusema tungepata wanawake 10 kama ww tanzania machozi ya yatima wengi yangefutwa .nakuombea kwa Mungu na kwa mwanae Yesu kristu akupe kila unalitaman ktk hii dunia na baadae ktk ufalme wake

 11. Winnie Ngalaba

  August 14, 2013 at 9:18 am

  Mwenyezi Mungu akuzidishie kila lililo la kheri na akuongezee kila palipo pungua mama. Kweli ulistahili zawadi uliyoipata. Mungu akusimamie katika kila lako na kila ugusalo hata kama lilikuwa mawe basi ligeuke kuwa dhahabu. Ameeeen

 12. Anonymous

  August 14, 2013 at 9:25 am

  Mungu akubsriki mdada

 13. Majoy

  August 14, 2013 at 1:09 pm

  Hongera Dina

 14. Ruky

  August 14, 2013 at 6:35 pm

  DINA UMEFANYA KITU KIKUBWA SANA ENDELEA NA MOYO HUU HUU NA NINAKUOMBEA MAISHA MAREFU YENYE BARAKA TELE ONE DAY TUONANE JAPO NIKUSALIMIE KWA MKONO..

 15. Anonymous

  August 14, 2013 at 7:10 pm

  PLS SOMEN NA TUWASAIDIE
  DINA UBARIKIWE KWA FURAHA ZA HAO WATOTO .NCHI YETU SI MASIKINI WALA WATU WAKE SI MASIKIN .UMASIKINI TUNAULETA SIO KWA KUTOKUA NA UMOJA .HIVI KILA ALIYE NA LAKI 1 ANGETOA 5000 TU KUNUNUA VITU VYA WATOTO MASHULENI AU TUNGECHANGISHA SIDHANI KAMA TUNGEWEKWA KTKT KUNDI LA NCH MASIKINI .

  ANGALIA NCHI ZA SCANDINAVIA MF: SWEDEN HUNA KAZI WOTE MWENYE KAZI
  WANATOA KWA SEREKALI ASILIMIA 30 YA MSHAHARA WAO TAX. HIYO HELA NDO WANALIPWA WALOKUJA KAMA WAKIMBIZI, WASIO NA KAZI ,SHULE ZA WATOTO

  ""WATANZANIA NI MATAJIRI SANA TENA SANA
  .TUNAUTIA UMASIKINI KWA UCHOYO WETU
  MTU ANAJAZA MADHAHABU MWILINI NA SAAJABU HAKUNA ANAYEMWANGALIA KAMA ANAVYOFIRIA
  KITCHEN PART
  SINGO
  MWALI
  MDUMANGE
  MICHANGO YA SHEREHE IMEWEKWA MBELE KULIKO MAISHA YA WATOTO WASIO NA MAKOSA WAMELETWA DUNIANI KISHA WANATESEKA

  TUSIWATESE WATOTO HAWANA KOSA JAMANI TUJITOE
  USIMPE DINA HELA AU NGO YEYOTE TEMBELEA UWONE JE WANAHITAJI NINI KISHA WAPE
  MIE NAKITUO HUKO MIKOANI NAKISAIDIA JAPO SI MAPESA YA HIVYO LAKINI NAKISAIDI.NA NINAO 2 NAWALIPIA ADA
  KUNA MWAKA NILIKUJA NA CONTENA LA COMPJ NIKAGAWA
  NA SASA NAHANGAIKA NIPATE MAGODORO HATA YALOTUMIKA NISEND

  TAFADHALINI TUWAOKOWE WATOTO
  HATUJUI WETU WATALELEWA NA NANI
  DINA UBARIKIWE
  FRM SWED

 16. Asila bridal

  August 14, 2013 at 8:22 pm

  Mungu Akubariki kwa moyo mzuri dada dina,beautiful inside and out…

 17. Anonymous

  August 14, 2013 at 11:30 pm

  Habari Dada Dina,ni matumaini yangu kuwa haujambo kabisa, nafurahishwa sana na kazi unayoifanya kwa jamii,ukweli ni kwamba hao watoto wanahiyaji upendo, Mungu atakubariki kwa kila jambo. In Jesus name i pray. Nina swali moja kama inaweza kunisaidia, mtu akitaka kua adopt mtoto/ watoto katika hivyo vituo inawezekana? Mimi na mtoto mmoja ningependa ni adopt mtoto mmoja au wawili ili kuwasaidia academically na kumpa mapenzi kama mama na familia pia. Tafadhali nijibu kama utaweza., email yangu ni lizy76k@ yahoo.com.

 18. Anonymous

  August 15, 2013 at 12:27 am

  Safi sana Dina. Una moyo wa upendo sana.

 19. Anonymous

  August 15, 2013 at 9:45 am

  Ila mi nakupenda we dada ni mungu tu ndio anajua. nilikuonaga mara moja nikatamani kweli kukusalimia walau tupige na picha ila nkashindwa ningeanzaje maana nipo mtu wa kawaida sana.

 20. anonymous

  August 15, 2013 at 2:03 pm

  i lv u dina and u deserve ol d gud things that u wish 4…xoxo

 21. anonymous

  August 15, 2013 at 2:04 pm

  i lv u dina and u deserve ol d gud things that u wish 4…xoxo

 22. Anonymous

  August 15, 2013 at 8:43 pm

  Ubarikiwe sana

 23. Anonymous

  August 16, 2013 at 7:02 am

  Mdau ina maana Dina ni mjamzito? Maana nimeona hapo unampa hongera ya mabadiliko ya mwili. Kama kweli nami nampongeza sana Mungu zaidi kumtunza.

  • Anonymous

   August 20, 2013 at 11:56 am

   kuna chakushangaza kwani yeye ni mwanaume?? ni mjamzito ndio.

 24. Anonymous

  August 16, 2013 at 7:04 am

  Nampenda sana Janet Sosthenes Mwenda. I real like her, so cute!!

 25. lily Z

  August 16, 2013 at 7:58 am

  love you Dina very much may God keep my wish come true..hahaha im sure yu know it.

 26. RUKY

  August 22, 2013 at 3:07 pm

  DINA NAOMBA UNISAIDIE KUMWAMBIA GEA AFUNGUWE BC HATA FAN PAGE FACE BOOK AU AWE ANATOWA NO NASISI TUNAYE MSIKILIZA ON LINE TUPO NJE YA NCHI ANGALAU NASI TUWEZE KUOMBA TWAARAB JAMANI MBONA HAYUPO POPOTE? KWENYE SOCIAL NET/W YOYOTE KWANINI ANAKUWA MVIVU HIVYO..AU NDIYO KASHATIMIZA NDOTO ZAKE KWELI HUWA PKA NACHUKIA UTAMSIKIA ANAWARUSAHA MASHOST ZAKE TUUU KM VILE HAKUNA WENGINE TUNAOMSIKILIZA…NA WEWE VP KM UPO ISTAGRAM TUJULISHE BASI FAN WENU TUWAFAIDI HATA KWAMBALI? NIMESIKIA MY DINA UNAMIMBA KM KWELI NIMEKUFUARAHIAJE MY DEAR..ALL THE BEST BUT LEO NIMEAMKA NAMAHASIRA NIKAINGIA KUWASIKILIZA ON LINE MARA OOH MMEKATIKA WACHA ASIRA ZIZIDI..

 27. emma kahere

  August 28, 2013 at 4:50 am

  Ndio maana UNABARIKIWA dina,maana baraka unaombewa na watoto pia.mim pia nakuombea kwa Mungu akupe maisha marefu,ili uzidi kuwasaidia watoto hawa.mapenzi tele kwako

 28. emma kahere

  August 28, 2013 at 4:51 am

  Ndio maana UNABARIKIWA dina,maana baraka unaombewa na watoto pia.mim pia nakuombea kwa Mungu akupe maisha marefu,ili uzidi kuwasaidia watoto hawa.mapenzi tele kwako

 29. emma kahere

  August 28, 2013 at 4:51 am

  Ndio maana UNABARIKIWA dina,maana baraka unaombewa na watoto pia.mim pia nakuombea kwa Mungu akupe maisha marefu,ili uzidi kuwasaidia watoto hawa.mapenzi tele kwako

 30. Anonymous

  September 9, 2013 at 12:23 pm

  Hongera sana kwa kuconcive! Ki ukweli si jambo dogo Mungu akujalie ujifungue salama.

 31. Amor

  September 12, 2013 at 6:10 am

  Hongera sana na uendelee na moyo huo huo na Mungu atakubariki na utafanya mengi makubwa zaidi. Unakaribishwa pia kutembelea blog zangu:
  tzandusfashion.blogspot.com
  dailylifeandliving.blogspot.com

 32. Jd ChingaOne

  November 4, 2013 at 12:25 pm

  Wonderfully…. Mungu akubariki

 33. Anonymous

  November 11, 2013 at 10:30 am

  Safi sana Dina.

Leave a Reply