Uncategorized

DADA DINA CARES TEMEKE KWENYE KITUO CHA WATOTO YATIMA VETENARI KUWASILISHA MAHITAJI YAO!

By  | 
 Hii ilikuwa juzi jumapili….baada ya kuwasili mizigo ikashushwa
 Kitabu cha wageni kilihusu
 Bi Honoratha akiangalia vitu tulivyompelekea
 Mzee Masoud kutoka clouds alinisaidia sana hata kukijua hiki kituo alikuja pia kushiriki
 Nikicheza na mtoto wa binti anayelelewa hapo
 Nikakabidhi nilichopeleka magodoro,vifaa vya shule,vyakula,mafuta ya kula,mafuta ya kujipaka,sabuni za kufulia,mapazia,mashuka,nyavu n.k
 Picha na wadau nilioongozana nao
 Akifanya yake mwenyewe
 Blandina Mvungi akishow love na mtoto
 Vitanda fundi alikuwa hajamaliza nikavibeba kama vilivyo nikamwambia akae hapo atengeneze mpaka viishe masihara sipendi.
 Mafundi wakichakarika maana hela zilizobaki nilimpa mama nikamwambia wakimaliza ndio awalipe.Wakadai niwape siku 2 nikawaambia sawa lakini kambi iwe hapo mpaka viishe na kuvifunga.
Kazi ya hapa ilikamilika salama tunamshukuru Mungu.Lengo lilitimia ila ntarudi tena kuona chumba kimekuwaje baada ya madirisha kuwekwa nyavu tuliacha tumefunga mapazia.Vitanda na magodoro kuwekwa pia.
 
KUMBUKA
Jumapili ya tarehe 11 nitawakutanisha watoto wa vituo hivi kwa chakula na michezo.Unataka kushiriki kwa kuja na mwanao piga namba hii kwa maelekezo zaidi 
 0759 789863 na  0657
795654.
Tukio hili kufanyika Azura beach

20 Comments

 1. moffat donald

  August 6, 2013 at 5:08 pm

  MUNGU AWAZIDISHIE MNOJITOLEA KUWASAIDIA WASOKUWA NACHO

 2. Anonymous

  August 6, 2013 at 6:42 pm

  hongera sana dina, mungu akuzidishie roho ya imani na akuongozee uhai na akufungulie rizki kwa mapenzi ulonayo kwa watoto yatima, na mwezi huu wa ramadhani insha allah.

  • Anonymous

   August 12, 2013 at 8:52 am

   mnafikiri hizo hela zinatoka mfukoni mwake ni tajiri kiasigani afanye yote hayo mwenzenu kajitengenezea ulaji hapo hela zinatoka kwa wafadhili alio jitengenezea kula akili kichwani kila mtu anaweza kuyafanya haya endapo tuu utabuni chochote kuhusu watoto yatima.

  • lily Z

   August 16, 2013 at 7:48 am

   weeeeee kaaa!!mbona una roho mbaya hivooo looh kwani we ulishindwa nini kama unaona ni rahisi tu kupata hizo hela na ukafanya the sem!!sasa angalia kama baraka atakayopata yeye na wewe unaesema hajatumia hela yake uka kaa doro bila kusaidia hata tu kwa mawazo katika jitihada za kutoa misaadaa,ni sawa.hebuu kalalee usituharibie mudi

 3. Anonymous

  August 6, 2013 at 6:44 pm

  HIVI DINA KWA NINI HUMCHUKUI HUYO MTOTO WA KIARABU UMLEE? YAANI UTAFIKIRI NI MWANAO UKIMBEBA. NAUMEPENDEZA SANA MAVAZI YAKO KWA KWELI.

 4. Anonymous

  August 6, 2013 at 6:46 pm

  wallah dada dina badilisha dini uwe muislam,nimekupenda sana kuanzia mavazi naimani yako kwa watoto yatima.

  • Anonymous

   August 8, 2013 at 4:48 pm

   hayo uliyoyapenda ni matunda ya kuwa mkristo, shika dini yako Dina Mungu atakuzidishia.

 5. Anonymous

  August 6, 2013 at 8:38 pm

  DINA UMENIVUTIA SANA NA KAZI YAKO. AM A TANZANIAN LAKINI SIISHI TZ,NIKIJA TZ NITAKUTAFUTA LAZIMA, PROMISE KUCHANGIA KIDOGO. MUNGU AKUBARIKI NA AKUPE NGUVU.

 6. Anonymous

  August 7, 2013 at 5:29 am

  mungu akuzdshie sana

 7. Amina K

  August 7, 2013 at 6:48 am

  Mwenyezi mungu akuongoze dina pia akupe moyo huo na afya tele pamoja na wote waliojitolea kuchangia.Mimi nilipenda nami niwe mmoja wao ila sijajaliwa bado ila inshaallah namuomba mungu nikipata kidogo nami nitoe mchango wangu.

 8. Anonymous

  August 7, 2013 at 11:06 am

  Hivi we anon wa August 6, 2013 11:46 a. m. unayesema Dina awe mwislam unamaanisha nini? Kwani kwa dini aliyo nayo amepungukiwa nini? Badili mawazo na mtazamo wako.

 9. Cymah Wandelt

  August 7, 2013 at 12:09 pm

  ubarikiwe Da Dina kwa kweli najivunia kukuchagua, manake matendo yako ndo kama niliyokuwa nayaota, ubarikiwe sana dadangu mpendwa. ubarikiwe dada.

 10. Anonymous

  August 7, 2013 at 12:20 pm

  sijakupenda hata kidogo wewe uliyesema Dina abadilishe Dini awe muislam….. Ipo siku utamuambia asaidie waislam tuuu….. Kwani si ni katika imani aliyonayo ndiko alikofundishwa awalee yatima???? Biblia inatuambia dini safi ni ile inayokumbuka yatima na wajane… uwe muislam au mkristo kama hukumbuki yatima na wajane huna ulifanyalo kiimani….. ACHA MAWAZO POTOFU NA YENYE UDINI…. DINA KEEP THAT SPIRIT HAI….. EPUKA COMMENTS ZA KICHOCHEZI MUMIE… WATANZANIA NI NDUGU….

 11. Anonymous

  August 7, 2013 at 2:54 pm

  nimekapenda ako katoto kanacheza kenyewe alafu kazuri kweli,hongera mamii kwa kujitolea mungu akuzidishie

 12. Anonymous

  August 7, 2013 at 6:46 pm

  Umependeza Dinna , ila GIM nauna umetupia kuleeeeeeee umenenepa tena

 13. Mrs. Mwanga

  August 8, 2013 at 7:31 pm

  Dina only God knows cha kukulipa, kwa yote uliyofanya kwa ajili ya hao watoto, na amini haikua rahisi km tunavyoona sisi, behind the scene lazima kulikuwa na vikwazo na kukatishwa tamaa, but u stand for it and u made it. Dina for me ur the IRON lady. congrats expecting more from u, i beliave this is just the beggining.

 14. Mrs. Mwanga

  August 8, 2013 at 7:35 pm

  dina hongera sana, can i call u THE IRON LADY? please reply

 15. LILY

  August 12, 2013 at 3:45 pm

  HONGERA MY DEAR DINA KWA YOTE MAZURI UNAYOYATENDA NA MUNGU AZIDI KUKUBARIKI JAPO NIMESHAIONA BARAKA KUBWA ZAIDI YAAJAA MBELENII!!!hoNGERA PIA KWA KUWA MAMA KIJACHO.

Leave a Reply