Uncategorized

DADA DINA CARES:MANUNUZI YANAENDELEA

By  | 
 Hii ni kariakoo mtaa wa gerezani nilienda kununua vifaa vya shule
Niliweza kununua madaftari kuanzia chekechea mpaka sekondari,kalamu,penseli,vichongeo,vifutio,majaladio n.k
Tukalipa na kuendelea na michakato mingine
Nilienda home shopping centre kununua pazia na mashuka.Nikapata pazia lakin mashuka ya watoto yalikuwa yameisha maana saba saba waliyashusha bei nasikia yakanunuliwa yakaisha.Nikapita madukani kwengine sikupata mashuka yenye ubora ni lile shuka la kufua mwezi chaliii.Nikaenda mtumbani Ilala.
Nikanunua mashuka 20,kiukweli japo ni mtumba lakini ni zitoo cotton kabisa na bado yana hali nzuri.Siku weza kupata rangi moja lakini kwa uhitaji wa wale watoto yana wafaa na yatakaa muda mrefu.
Mpaka dakika hii nimeshakamilisha manunuzi kesho ndio naanza kusambaza vitu kwenye vituo.
RATIBA YA KUWASILISHA VITU VITUONI
Jumamosi ya tarehe 3 august kituo cha Vetenary Temeke
Jumapili ya tarehe 4 august kituo cha Sifa Bunju
Jumatatu ya tarehe 5 august kituo cha Zaidia Sinza

3 Comments

 1. Anonymous

  August 2, 2013 at 11:13 am

  mungu akubariki na akuzidishie

 2. mama gab

  August 2, 2013 at 3:10 pm

  Wau am so proud of u sister may God grant u many years to live and be succsefuly in everything u do luv u mwa mwa

 3. Anonymous

  August 12, 2013 at 9:03 am

  mmmh mngejua hizo ni hela za wafadhili na zinapigwa passu kwa pass hazifiki zote mnampa dinna bichwaaaa

Leave a Reply