Uncategorized

JUMAPILI HII YA TAREHE 11 DADA DINA CARES KULA NA KUCHEZA NA WATOTO YATIMA.

By  | 
Katika kukamilisha ule mpango ulioanza wa kuchangia vituo vya watoto yatima jumapili hii watoto watakutana kwa chakula na michezo.Watoto hao ni kutoka kituo cha sifa bunju,zaidia sinza na vetenari temeke.
 
Jumapili kuanzia saa tano asubuhi watakutana Azura Beach Kawe.Basi maalum lililoandaliwa kutoka clouds fm litapita vituo vyote kuchukua watoto.Mchana watakula chakula maalum kilichoandaliwa.Watacheza michezo mbalimbali,face painting tuliyoandaliwa na Kids Event shukrani za kipekee ziwafikie.MC atakaewaburudisha watoto atakuwa Mpoki kutoka Original Komedi.Tutakata keki kubwaa tuliyoandaliwa na watengeneza keki waliobobea hapa Tanzania flying chefs wale wa tambaza.
Wasanii kama Peter Msechu na Barnaba wamejitolea kuja na gitaa kuwaimbia watoto.Wasanii wengine watakuwa wakiwahudumia na kuwaangalia watoto.
 
Viburudisho kwa ajili ya watoto sijui pipi,juice,biscuit,cake,chocolate vitakuwepo vya kutosha.Tutakuwa na mashine ya kutengeneza popcon za watoto itakayowekwa na Kids Event.
 
Kwa unaetaka kumleta mwanao kushiriki
piga namba hizi 0759 789863 na 0657 795654 na utapewa maelekezo.
Si kwa mtoto tu hata wewe mzazi utakutana na wazazi wa watoto wengine kwa kufahamiana na kubadilishana mawazo.
 
Kwa sababu hii ni event ya charity sio onesho mzazi usije mikono mitupu beba chochote.

2 Comments

 1. Anonymous

  August 9, 2013 at 10:42 am

  Dina hongera kwa hili unalofanya Mungu akuongoze ma ubarikiwe Milele…

  Naomba kama utaweza Jumatatu tukijaaliwa kuamka vema naomba unichezee huu wimbo please ni wa Dada wa South , Utaupenda midundo yake ningependa kushare na wasikilizaji wako unaitwa

  Zahara – Incwad'Encane

  Nakutakia Sikukuu njema

  withlove

  Da Rhoder

 2. mama luqman

  August 12, 2013 at 2:25 pm

  hongera dina mungu akubariki akuongezee hapo palipopungua nimeguswa na uliyoyafanya naomba nikupongeze mama hongera sana uendelee na moyo huo huo vile watoto wanavyoshukuru dua zao zinapokelewa moja kwa moja na mwenyenzi mungu,

Leave a Reply