Uncategorized

HADITHI YA PUNDA NA MKULIMA!

By  | 
Siku
moja punda wa mkulima alianguka ndani ya kisima. Mnyama huyo alipiga
kelele kinyonge kwa masaa kadhaa wakati mkulima akijaribu kufikiri nini
cha kufanya.
Hatimaye,
aliamua kwakuwa punda wake alikuwa mzee, na pia kisima hicho kilihitaji
kufunikwa juu, Akaona hapakuwa na haja ya kumtoa

 Akaita
majirani zake wote waje kumsaidia. Wao wote wakachukua makoleo na
kuanza kuchota taka kwa koleo na kuzitupia ndani ya kisima.


 Mara
ya kwanza, punda aligundua nini kilikuwa kinatokea akapiga kelele kwa
nguvu. Basi, ikawashanganza wale watu punda aliponyamaza ghafla!
Baada
ya kutupa taka kadhaa kwenye hicho kisima. Huyo mkulima alishangazwa na
kile alichokiona. Kwamba kila koleo la taka lililorushwa juu ya mgongo
wa punda, punda alikuwa akifanya kitu cha kushangaza. Alikuwa
akijitikisa ili taka zimwagike chini huku akipiga hatua moja kuja juu.

Kadri
mkulima na majirani walivyoendelea kutupa uchafu kwa koleo juu ya punda
yule, alizidi kutikisa mgongo wake na kupiga hatua moja kuja juu. Muda
mfupi baadae, kila mtu alishangaa jinsi punda
alivyozidi kutokeza ndani ya kisima na kuja juu.

FUNZO:
Maisha
yatakutupia kila aina ya uchafu. Ili utoke nje ya kisima wahitaji
kujitikisa na kuchukua hatua moja juu. Kila tatizo ulilonalo, ni jiwe la
kukuwezesha kukanyaga na kupiga hatua kuja juu. Tunaweza kutoka nje ya
kisima kirefu kwa kuongeza bidii ya kupiga hatua moja kuja juu bila
kuacha na kutokata tamaa kamwe. Tikisa itikisa uchafu mbali na kuchukua
hatua kuja juu.

Kumbuka kanuni
5 rahisi ili uwe na furaha:

1. Weka huru moyo wako mbali na chuki – Samehe.

2. Weka huru akili yako mbali na wasiwasi – Wengi hushindwa kabisa kipengele hiki.

3.Tosheka / rizika na ulichonacho.

4. Toa zaidi.

5. Tarajia vichache kutoka kwa watu lakini zaidi kutoka kwako mwenyewe.

Asante Avit Kapinga kwa kututumia ujumbe huu.

9 Comments

 1. Anonymous

  August 2, 2013 at 1:34 pm

  kweli kabisa dada dina nimeipenda iyo na umenifundisha kitu

 2. #Anaconda

  August 2, 2013 at 5:02 pm

  Onyesha basi umeitoa kwa ladyjadee ,ndiyo maadili ya kiuandishi habari ukiitoa kwa mtu onyesha chanzo,unaogopa kibarua kitaota nyasi lakini unaikubali kimoyomoyo #anaconda.

  • dinamariesblog

   August 6, 2013 at 7:03 am

   Ungesoma mpaka mwisho ungeelewa lakini na wewe ni wale wale mnaokurupuka kuongea.Hizi ni zile email za kuforward zinazotembea na mimi ikatumwa kwangu na mdau anaitwa Avit Kapinga ukisoma mpaka mwisho utaona nimemtaja.Hayo mengine umeyasema wewe mie walaaa!

 3. Anonymous

  August 5, 2013 at 7:21 am

  Ujumbe mzuri sana nimeupenda,asante da Dina nimejifunza kitu ndan yake

 4. jackie malilo

  August 5, 2013 at 9:19 am

  Asante kwa ushauri mzuri tutayafanyia kazi inshallah

 5. Anonymous

  August 6, 2013 at 1:14 pm

  wadau acheni malumbano yasiyo na maana mbona Dina kaonyesha wapi ametoa habari hii inaonekana ww huwa unasoma heding tu na sio habari yote tupishe hapa siyo site yako

 6. Nilam Mohamed

  August 6, 2013 at 6:09 pm

  Nkupenda sana we dada na busara zako pia una moyo wa kipekee sana.Kila post unayoitoa alazima kuna kitu nitajifunza ndani yake.This time nikija mjengoni inshaallah nitakutafuta japo nikusalimie tu nitaridhika.Asante na mungu akupe maisha marefu zaidi.

 7. Amina K

  August 7, 2013 at 6:38 am

  mmmmmmmmmh, binadamu tuna roho mbaya. acheni jamni.ujumbe mzuri unafunza.

 8. Anonymous

  December 9, 2013 at 1:47 pm

  Dina thank you

Leave a Reply