Uncategorized

KAZI NI KAZI…MAMA MUUZA MBOGA ZA MAJANI.

By  | 
 
 Anaitwa mama Happy mkazi wa kawe.Shughuli yake kubwa ni kuuza mboga za majaniNilikutana nae njiani nikanunua mboga za nyumbani kwangu na nikamuuliza maswali ili kujua mazingira ya kazi yake.
Mama Happy huamka kila siku saa nane usiku kufata mboga Ilala.Mboga hizi huletwa hapo Ilala na wakulima na wao huenda kununua na kurejea nyumbani saa kumi usiku.Asubuhi anaingia mtaani na kapu lake kuuza mboga.
 Kapu la mama Happy kama unavyoliona mboga fungu Tsh 300 na 200 mpaka tenga liishe faida Tsh 5,000.Siku nzima pamoja na kutokulala usiku mama Happy huambulia Tsh 5,000 kama faida.
 Spinach
 Sukuma wiki
Mnafu
Chinese….siku zote nilikuwa najua hii mboga ndio spinach.Kumbe hii ni chinese nimekuwa najichanganya.
Baada ya kumuunga Mama Happy kwa kununua mboga tukaachana.Nikabaki natafakari maisha yetu kila mmoja na namna anavyojitafutia riziki.Kuna anaeingiza 5,000 kwa siku,mwingine 100,000,mwingine 1,000,000,na mwingine 10,000,000
Kwa kuongea na watu kama hivi najifunza kutokulalamika kila siku.Kumheshimu kila mtu unaekutana nae haijalishi anafanya kazi gani.Kuheshimu kazi za wengine kwani hujui ugumu anaokabilianan nao kila siku na nguvu aliyonayo kuikabili kazi husika.
 
Mama Happy anazunguka maeneo mengi kuuza mbona .Ni wale kina mama wanaopitaga mitaani kwetu wakiimba”mboga mbogaaaaa,matembeee,mchichaa,spinach”
Jua kali,joto,vumbi lakini bado anarudi nyumbani kuna watoto awapikie wale.Bado anawasomesha mwenyewe mume alisepa kitambo kodi ya nyumba inamsubiri.
 
KAZI NI KAZI.

20 Comments

 1. Anonymous

  September 27, 2013 at 6:20 am

  Kwa kweli Dina hii ni changamoto kubwa sana kwetu sisi wanawake. Mimi binafsi nawapongeza sana wanawake wenzangu wanaojituma japo kwa hicho kiasi kidogo wanachopata kuliko wale wanaopita kwenye maduka na kwenye nyumba za wahindi wakiomba msaada. Kama leo ijumaa wamejazana kariakoo wanaomba majumbani kwa wahindi hadi aibu, na ukiwaona ni wazima hawana kilema chochote na kiumrin bado wana nguvu sana, ni kujiendekeza tu pamoja na uvivu. Nampa hongera sana huyo mama kwakweli. Mwanamke wa hivyo akiwezeshwa atafika mbali sana maana ana bidii. Anaweza kubadili biashara akapika hata mama lishe.

 2. Anonymous

  September 27, 2013 at 9:32 am

  Am very happy leo. Dinna umerudi kwenye blog ?? jamani napita kila cku huku hata kama hujapost kitu kipya mie nimo, nimefurahi. Naendelea kuelimika na kuburudika. Japo hunijui ila nakupenda sana.

 3. Anonymous

  September 27, 2013 at 10:10 am

  Dina weka namba yake jaman kwanin hukuichukua watu hata wamchangie afanye na biashara nyingine jaman maisha nimagumu kwawkweli namim umenifundisha kitu khaaaa mtu unakuyta unalalamika huwez kwenda na fashion kumbe mwenzio hata hela ya chakulka nichangamoto mungu ambariki

 4. Anonymous

  September 27, 2013 at 11:09 am

  Umeona ehee Dina mi nikifika hapo tu nafyata Mdomo wangu kimyaaa na Kumshukuru Mungu kwa Yote !

 5. Anonymous

  September 27, 2013 at 12:47 pm

  We mbona siku hizi utuwekei pic zako… au ndio hiyo mimba… maana tumezipata toka mtaa wa pili . weka bwana

 6. Anonymous

  September 27, 2013 at 2:14 pm

  Dada Dina,

  Hii post imenigusa sana, Mwenyezi Mungu ametubariki kwa namna tofauti lakini pia tunajisahau sana kwamba kuna wengine hawapati tulichonacho.
  Ila ni changamoto pia kuona mama huyu alivyo mchapakazi na anajituma hata kwa faida hiyo ya sh 5000.

 7. Anonymous

  September 27, 2013 at 6:09 pm

  Dina mtafute utuwekee no ya cm jaman inaumiza kweli mwanamke mwenzetu jaman hatuna uwez kiivo lkn angalau kdg tu tumchangie.mie naumiaga kwel lkn cna uwezo huo wa kumtoa mtu.mungu aendelee kukupa roho hy ya upendo mama

 8. Anonymous

  September 28, 2013 at 8:27 am

  mwanamke ameumbiwa mateso kweli, lakini MUNGU huwa hamuachi, ebu angalia sijui mume amemkimbia, lakini yeye amebaki analea watoto wake kwa faida ya TShs. 5000/= kwa siku ambayo kuna kodi, umeme, shule na kila tu, EEEEh Mwenyezi wasititiri wanawake wote wanaopitia wakati mgumu kama huu.

 9. Anonymous

  September 28, 2013 at 10:58 am

  Dina kipindi chanyuma kdg ulisema utatoa gazeti la mapishi vipi: umefkia wapi?nimefurahi umeanza kupost,,utupostie na mapishi yko km zamani

 10. Davis Mazula

  September 28, 2013 at 2:09 pm

  mi mwenyewe da dina nilikua nachanganya spinach ndo nilikuwa nziita chinese kumbe v2 ni viceversa afu nilkuwa mbishi..kiukwer hayo ndo maisha na kila mtu MUNGU kampatia fungu lake.kuna wengne hata fungu lao ni 1000 kwahyo sote yatupasa kumshukuru.

 11. Davis Mazula

  September 28, 2013 at 2:13 pm

  Mi mwenyewe da dina nlkuwa naziita hizo mboga spinach badala ya chinese..kiukwer MUNGU amegawa riziki kwa mafungu kuna wengne kpato chao ni 1000 kwahyo yatupasa kushukuru kwa yote

 12. Anonymous

  September 28, 2013 at 4:50 pm

  Plse dina chbgamsha blog ilianza kuboa mnoo usipotee ivyoo twakumiss.ongera kwa kua mama kijacho

 13. Anonymous

  September 28, 2013 at 7:59 pm

  kama kuna janga lingine la kitaifa bac ni wanaume duh yani wanawake ndo wamekua vichwa, viwiliwili, misingi na miguu ya familia kha!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!11

 14. Anonymous

  September 29, 2013 at 11:37 am

  Ningependa huyo mama aendelee kufanya iyo biashara lakini aiboreshe. Badala ya kuuza tenga 1 basi auze hata kumi kwa siku. Pia aongeze variety za mboga. Tafadhali kama una contact zake tuwekee tumsaidie kwa ushauri na mtaji. Inawezekana.

  • dinamariesblog

   September 30, 2013 at 11:01 am

   Sina namba zake ila nikikutana nae tena nitazichukua.Hilo ni wazo zuri sana!

 15. Anonymous

  September 30, 2013 at 8:36 am

  maisha yake ni kama mama yangu mzazi, nawaheshimu sana wanawake hawa kwani najua mchango wao katika familia zao ni mkubwa sana, Mungu awape afya njema wamama wote wapiganaji, kama huyu.

 16. Anonymous

  October 1, 2013 at 7:03 am

  Dina plssss weka namba ya huyu mama tafadhali, tumtumie japo ka M-pesa apike na mama ntilie angalau kutoka kwenye faida ya 5,000 asongee mpaka 10,000 kwa siku. Kama huna namba mtafute tafadhali.

 17. Anonymous

  October 1, 2013 at 9:07 am

  Dada hapo hakuna mnafu kabisa

 18. Anonymous

  October 7, 2013 at 11:35 am

  mhhh jamani watu tupo tofauti 'Dina itafute number yake na mimi nitachanga kwa lolote iwe kufungua genge au mama ntilie'kwanini tupo tofauti?badala uchangie vitu vya maana unagombana kuwa hamna mnafu'sorry ni mawazo yako nisamehe kila mtu na mchango wake ktk mada .

 19. Anonymous

  October 8, 2013 at 7:50 am

  mungu akujalie afya njema na Baraka tele kwa moyo wa kusaidia jamii tunakuombea sana ubarikiwe kwa hili unalofanya. watu wengi wana shida sana na unatufanya tumshukuru mungu kwa hicho tunachokipata, nakupenda sana.

Leave a Reply