Uncategorized

KUKU WA KIENYEJI KUTOKA SINGIDA,UNATAKA?

By  | 
 Mimi ni mpenzi mkubwa wa kuku wa kienyeji.Kwa miaka kadhaa sasa nyumbani kwangu hakupikwi kuku wa kisasa.Nimekuwa nikienda kununua mwenyewe wakati mwingine kuletewa ofisini.Nimejikuta nimewaambukiza na watu ofisini na wao wanapenda kuku wa kienyeji sasa.Kila alhamisi inatumwa oda ijumaa watu wanaletewa kuku wao wa kula weekend nyumbani.
Kama leo walikuja kuku ofisini ndio nikapiga picha hizi.
Kuku hawa wanaletwa kutoka Singida wanauzwa na kuisha kisha wanafuatwa wengine.Muuzaji anaweza kuwaletea mlipo iwapo mpo wengi mmeagiza au ni oda kubwa.Kama sisi  ofisini oda inakuwa kubwa ya kuku 7,10,mpaka 12 kila ijumaa.
BEI ZAKE
Kama hao pichani ni Tsh 15,000
Ila kuna wa 12,000 na 10,000 ambao sio wakubwa sana.
Kama ni oda ya mtu mmoja mpigie simu atakuandalia vizuri ukifika unalipa na kubeba.Yupo soko la manyanya ndio anauzia hapo kuku wake.Piga namba 0713200510.
Pia nilikuja kujifunza kuna kuku wa kienyeji original na kuna kuku chotara.Hawa kuku chotara ndio wanaliwa sana hapa mjini watu wakiamini wanakula kuku wa kienyeji.Sijui namna ya kumuelezea kuku chotara ila anafanania na kuku wa kienyeji kwa kiasi flani.

*SORRY
Namba ya simu ilikosewa hapo kabla ila nimesharekebisha.

20 Comments

 1. Anonymous

  September 28, 2013 at 6:04 am

  Dina Bwana Mi napenda sana Mambo yako na habari zako za huku , yaani unauendeshaji wa Blog wa kipekeyakopekeyako hivi , wish nitakutana na wewe siku moja

 2. Mbalu Mimi

  September 29, 2013 at 2:15 am

  Namba ya simu umekosea Dina.

 3. Anonymous

  September 30, 2013 at 6:08 am

  Dina umekosea no ya muuza kuku, nmepiga kapokea mtu mwingine, cheki vizuri.

 4. Anonymous

  September 30, 2013 at 7:19 am

  hiyo namba mbona tarakimu zimezidi, mi nataka mayai ya kienyeji anaweza nipatia au?

 5. Anonymous

  September 30, 2013 at 10:12 am

  Asante mpenzi kwa kutuhabarisha haya. Za masiku? maana ulitugaya hapa blogini. We love and miss you. Jitahidi hivyo hivyo hata kama zofulhali, jitahidi kutupia tupia.

  Naomba uicheki hiyo nambari basi maana naona kama imezidi digits. Maana wengine tunahitaji hao vyuku tulishaachana na kuku-sasa kitambo ila bei za hapo Mwenge utata mtupu.

  Asante, Kipapli

 6. dinamariesblog

  September 30, 2013 at 10:56 am

  sorry…nimeifanyia marekebishoo soma tena.

 7. dinamariesblog

  September 30, 2013 at 10:56 am

  asante sana,tutakutana tu my dear!

  • Mumul Eddie

   December 17, 2013 at 9:33 am

   love youuuu sana uko kipekee kiukweliii

  • Mumul Eddie

   December 17, 2013 at 9:34 am

   uko kipekeee kwa kweli wache wasemeee

 8. UNKNOWN

  September 30, 2013 at 11:33 am

  Hongera!

 9. Anonymous

  September 30, 2013 at 12:31 pm

  Dina naomba utuwekee na upishi wako wa kuku jamani. Mi napenda sana mapishi yako naomba utuweke mapishi ya kuku wa kienyeji na jinsi unavyopika nyumbani kwako tuwekee na picha kabisa ili tufurahi vizuri.

  • Anonymous

   October 4, 2013 at 11:42 am

   WELL SAID MDAU NYUMBANI KWA DINA MSAFII MWENYEWE.MAANA HAYO MAZINGIRA ALOWEKA KUKU KMA NI SINK LA JIKONI KWENU HAPO MJENGONI JMANI MLISUGUE MBONA PACHAFU HIVYOO ,MNISAMEHE JAMANI MINAPENDA SAANA MAHALI PASAFI HATA NIKITAKA KULA HOTELI NANGALIA MAZINGIRA,NAJUA DINA NIMSAFI SAAA NYUMBANI KWAKO HASWA JIKONI ,ILA HAPO ULIPOPIGA PICHA YAHAO KUKU PANATISHA MPENDWA MJITAHID KUSUGUA NAJUA WADADA HAPO MJENGONI MPO WAREMBO .JIKONI LA OFISINI HALIRIDHISHI. SORRY TO SAY THAT.MDAU SWEDEN.

 10. Anonymous

  October 1, 2013 at 6:36 am

  Uuuuuh am super happy for you, hongera Dina Mungu akulinde. Nakumbuka kuna mdada alikupa ushauri kwenye topic moja about your life. Let it be the source of your happiness and unconditional love. Kimya kimya hivyo hivyo, no showing up.

 11. Lily Z

  October 1, 2013 at 7:30 am

  asante dia nshaagiza mie wangu cant wait,yaani unavojua kuokoaga jahazi wewe mimi penda wewe saaana

 12. Anonymous

  October 2, 2013 at 2:37 pm

  Dina ,Hao Kuku Chotara Ni Hiv ,Wanachukua Vifaranga Vya Kuku Wa Kizungu Na Kuvifuga Km Vya Kienyeji ,Yaan Wanawap Vyakula Km Wanavyokula Kuku Wetu Wa Kienyeji Lkn Asili Yao Ni Kuku Wa Kizungu

  • Anonymous

   October 5, 2013 at 9:38 pm

   chotara wanapatikana kwa mtetea wa kienyeji kucrossed na jogoo la kisasa au chotara

 13. Anonymous

  October 3, 2013 at 8:14 am

  life yako naifagilia sana no mashauzi yaani unalewa kama vile umezaliwa miaka mingi kumbe ni mdogo sana tu napenda tabia yako kep it.

 14. Anonymous

  October 3, 2013 at 7:02 pm

  Dina nakupendajee mie?? Bless u mpz!! Ney ubungo!!!

Leave a Reply