Uncategorized

KUTOKANA NAKUTOKUWA TAYARI KUWA MAMA,HUYU MTOTO BAADA YA KUZALIWA MAMA YAKE HAMTAKI

By  | 
 
 Ni katoto ka kike kenye afya teleee na ana siku tatu tu toka kuzaliwa.Bahati mbaya amezaliwa katika mazingira ambayo mama yake hayupo tayari kumlea na ilikuwa amtupe wasamaria wema wakaokoa jahazi.
 Mama wa mtoto ndio huyu pichani anadai hana wazazi walifariki.Akawa analelewa na dada yake huko Sinza na akapata ujauzito.Baada ya kupata ujauzito dada akamfukuza nyumbani na aliyempa ujauzito akamkataa.
 Kina mama pichani wakimwogesha mtoto baada ya kuzuia zoezi la mama kutupa mtoto
 Inavyosemekana mama wa mtoto alienda dispensary kuchoma sindano mimba itoke.Bahati nzuri mtoto siku zilikuwa zimetimia akamzaa.Alipozaliwa na kuwa hai mama mtoto akawa hamtaki anataka kumtupa.Mama wa mtoto hamtaki kabisaaaa mwanae.
Kina mama baada ya kuzima zoezi la mtoto kutupwa wakakaa na binti kuelewa nini kinamsibu.Wakamuogesha mtoto na mama yake pia akaogeshwa.Akapewa maneno ya kumsaidia kisaikolojia lakini haikusaidia mama msimamo wake ukawa ule ule.Mama aliyekuwa akimuogesha mtoto yupo radhi kumchukua mtoto na kumlea kama wa kwake maana mama yake hamtaki.
 
Niliwahi kuona movie zamani inafanania na hili binti mdogo alipata ujauzito lakini hakuwa tayari kuwa mama na akamtoa mwanae kwa mtu na mkewe waliokuwa wanamatatizo ya kupata mtoto.Alimtoa kwasababu yeye asingeweza kulea na kumpa mahitaji yote.Yule baba na mkewe ndio walikuwa wakihitaji mtoto zaidi yake.
 
Sikiliza kesho heka heka,story hii kanipa Gea Habib baada ya kuitwa kuishuhudia.

29 Comments

 1. Anonymous

  September 26, 2013 at 4:06 am

  ht mm hy movie nishw iona lool jmn alfu dd mzuri tu jmn

  • elibariki

   November 1, 2013 at 7:30 am

   naombeni hiyo movie please

 2. Mama 2 (Mrs M)

  September 26, 2013 at 4:18 am

  Mmh hiyo kali Dina! jamani kabinti kazuri, mtoto mzuri, hebu jamani huyo mama amsaidie. Na wajaribu kumpima akili huyo binti kama kweli yupo sawa. Jamani anamkataa mtoto mzuri hivyo. Duniani kuna mambo.

 3. Anonymous

  September 26, 2013 at 5:39 am

  Wewe uko tayari kumlea wako??

  • Anonymous

   September 29, 2013 at 8:24 am

   Mbona mnapenda kufuatilia mambo ya watu? Mtoto wake anakuhusu nini? Mungu akusamehe na akupe hekima ujue jambo la kusema na kutosema.

  • Anonymous

   September 30, 2013 at 1:25 am

   na wewe utakuwa na matatizo ya akili? sasa unamuuliza Dina ama nani kuwa yupo tayari kumlea wake? Ndo walewale wateja wa milemebe wako wengi mtaani ila hawajagundulika tu!

 4. Anonymous

  September 26, 2013 at 6:59 am

  Yani kitu kama Mungu kapanga ata ufanyaje u cant change it. wengine wanatamani wengine wanatupa. Amenikumbusha nilivyohangaika na kulea mimba mwanaume hakutaka bt nikakomaa sitatoa at the end nimejifungua tena kwa operation na mototo mwenyewe akawa bahati mbaya kafa, niliumia siwezi elezea… Huku wengine wanajifungua tena kiulaiiini wanatupa. jamani kweli hii ni dunia na walimwengu. Mungu amsaidie coz we knw nothing about her background am no body to judge her. WANAUMEE.. MH.!

  • Anonymous

   September 28, 2013 at 8:15 pm

   yani wanaume janga la kitaifa, ila jamani mabinti tulieni jamani uwiii nini huwa kinawakumba kuangaika na wanaume ungewajua tabia zao wanaume nyie mngekaa tu mtulie msubiri wakati ambao hata kama atakataa but utaweza kumtuza mwanao. duh katoto kacute jamani duh.

 5. Anonymous

  September 26, 2013 at 7:47 am

  jamani jamani yani watu tunahangaika huku na kule kila dawa unakula uongeze watoto watu wanapewa dhawadi hiyo wanayupa?ila uyo bint anahitaji dactari wa sakologia na kusaidiwa zaidi katika kulea mtoto ni kweli maisha magumu lakini ugumu wake haujafikia kutupa kiumbe hicho!isitoche mungu akikupa mtoto yy ndo hujua atakula nn wanadamu wengi huzani tunachokipata ni kwa nguvu zetu kumbe si nguvu zetu ni huruma yake mungu.binti anahitaji kumrudia mungu naamini ataweza kulea na mtoto wake.huyo mama amsaidie abaki na mtoto na huyo mama mtoto tumtafutie mwana sakologia na maombezi yafanyike juu yake ili akili ya huyo binti ipate hafueni.mtoto mzurii sana na kafanana na mama yake yani hadi nalia hapa sitaki amin nawezaje kuja waona jamani nami niweze kuwa namsaidia huyo binti katika malezi ya mtoto mpaka tuakikishe amekua huyo mtoto au mama ameweza kujitegemea..

 6. Anonymous

  September 26, 2013 at 8:08 am

  makubwa, mwenyezi mungu tusaidie, hii ni kutokana na binti kuwa bado na mawazo ya kitoto, ila angejua akina mama wanavyoangaika kupata watoto asingethubutu kufanya analolifanya sasa.

 7. Anonymous

  September 26, 2013 at 8:12 am

  Jamani Jamani kuna watu wanatafuta watoto kwa udi na uvumba hawawapati wewe haumtaki mtoto inamaana uchungu ulioupata umeshausahau? na kama haukutaka mtoto ulijiingiza kwenye mambo ya kikubwa ya nini? jinsi navyokuona wewe si mtoto sheria ichukue mkondo wake. mtoto mzuri jamani ningekuwepo hata mimi ningejichukulia.

 8. aalusinde

  September 26, 2013 at 9:10 am

  Mungu ampe moyo wa kusamehe yote na kusahau kila kitu na kukubali kumleaa mtoto wake maana hiyo ni zawadi aliyo pewa na Mungu

 9. Anonymous

  September 26, 2013 at 11:37 am

  Huyo binti apelekwe hospitalini apimwe akili, hata wanyama wanawapenda sana watoto wao wakishawazaa itakuaje binadamu lo !

 10. Anonymous

  September 26, 2013 at 5:18 pm

  kweli dunia duara, uyu ataki mototo, uku mwingine anatafuta usiku na mchana, aya maisha ndiyo yanayo changaya 2.

 11. Anonymous

  September 27, 2013 at 6:28 am

  Huyu binti angejua mimi ninavyotafuta mtoto jamani asingefanya hivyo. Kwa kweli nimehuzunika sana. Dina msaidieni huyu binti kumpata mwana saikolojia kama Chriss Mauki au dada Sadaka Gandi amsaidie kiushauri nasaha huyu binti ana shida si bure kabisa. Mtoto mrembo kama mama yake.

 12. Anonymous

  September 27, 2013 at 10:09 am

  MH jamani nimehuzunika sana jamani mi nna dada wa tumbo moja anaangaika kupata mtoto mwaka wa tatu huu sa huyu labda hajawahi ona watu kama hao mh jamani Mungu atusaidie sana

 13. Anonymous

  September 27, 2013 at 10:34 am

  Heee jamani mtoto mzuri mashaallah hata mm namtamani nimlee,bado ana akili za kitoto ipo siku lkn atakuja kujutia

 14. Anonymous

  September 27, 2013 at 12:13 pm

  kweli hii habari imeniuma sana. mimi nimeolewa nina miaka nane katika ndoa na sijabahatika kupata mtoto na hangaika usiku kucha kutafuta mtoto wengine wanatupa kweli huyu binti anadhambi kubwa sana kwa mungu, huyo mtoto ni malaika na mungu anasikia siku atakapokuja kutafuta mtoto kwa wakati wake ndo atajuta kuzaliwa. ni bora angewapa watu lakini si kumtupa.

  • Anonymous

   September 29, 2013 at 6:17 pm

   Huyu binti ana depression ya kuzaa. It happens to alot of women tatizo Afrika haijulikani au haiongelewi. Huku ulaya hiyo kitu iko mnooo na wamama wanapewa madawa na hormone pills to balance their health wanapona.
   Huyo binti si kichas na ugonjwa jamani anahitaji matibabu na Mungu mkubwa mtoto uko salama. Jina la Yesu lipewe sifa.

 15. Anonymous

  September 28, 2013 at 10:07 am

  Helo Kama unamawasiliano na Uyo mama Naomba anipe Uyo Mtoto taratibu Zote za kisheria ntafuta kumchukua…. I desparately wants a kid..

 16. Anonymous

  September 28, 2013 at 4:44 pm

  Dina binti huyu ana mapepo tena yanayoendana na ukoo wake maana hata yeye ukimuuliza maisha yake ni ya kukataliwakata liwa na hata huyu mtoto akikua ni hivyo hivyo labda aombewe tuuu maana hiyo ninlaananya familia yao labda kwa upande wa mama au baba.ni kweli ina huzunisha mnoo .pia huyo mama naye sema ata m hukua kulea what if yule mwanaume aka sema ana mtak mwaae itakuwa.na pia hili swala la kuadopt mtototanzania wameliwekea ugumu mnoooo mimi rafiki yangu alikua anatabi kila juma mosi ana enda kuwaona watoto yatima kwa ufupi an roho njema aka kutwa apacha wawili wameletwa siku hiyo aliwahudumi mika 3 wakahama nchi na mumewe akaamua wacha awachukie wale watoto lloh alisumbuliwa mwishowe akaacha ila mpaka leo aa wakumbuka ana nitim niwafuatilie russhwa ipo kubwa loh ila hili.lime uzunisha ila huyo dada nime mwelewa

 17. Anonymous

  September 28, 2013 at 4:45 pm

  Dina uwe una.update blog kama zamani una kaa.sana. Plse

 18. Grace

  September 29, 2013 at 12:54 pm

  we dada uliocomment 27, 2013 at 5:13 AM
  Jaribu kutomuhukumu huyo binti, huwezi kujua kichwa chake kimeharibika vipi. imagine, yeye ni mtoto yatima, dada aliyemtegemea kamfukuza, mwanaume aliyempa mimba kamkimbia, unafikiri kwa binti mdogo kama huyo anaweza himili yote hayo. anahitaji msaada kwa kweli.

  mimi pia nimesikitishwa na hii story, nna mwaka wa nne sasa natafuta mtoto sijafaniliwa. Sasa inabidi nizichange twende nje ya nchi tukajaribu IVF. kwa wale wadau kama mimi jaribuni kutafuta fertility specialists, kwenye nchi kama Turkey, south africa unaweza pata kwa bei nafuu. hapa bongo hatuna fertility specialists, kuna ma Gyno ambao kuna matatizo yapo nje ya uwezo wao.
  kwakweli mimi binafsi nimejaribu kusoma sana na kuelewa hali yangu kwanini nashindwa kupata mimba. Nasikitika hamna Gyno hapo Dar aliyeweza kunifanyia uchunguzi kwa karibu na kuielewa hali yangu. so nawashauri wale wadada anaotafuta mimba, jaribuni sana kusoma, unaweza kuta tatizo sio kubwa kivile.

 19. Anonymous

  September 30, 2013 at 3:00 pm

  breaking news!bint kakubali mtoto wake kumbe na ndugu zake wanauwezo tu wa kumlea na amesharudi kwa nduguze na mtoto anaendelea powa kumbe ni ukichaa wakee tuuu.

 20. Anonymous

  October 1, 2013 at 12:41 am

  lakini wawe mwangalifu na huyo binti asije fanya kitu chochote kibaya kwa huyo mtoto maana ameshaonesha hana mapenzi naye

 21. Anonymous

  October 1, 2013 at 1:37 pm

  Namshukur sana mama yangu kwa kunihudumia mpaka hapa nilipo .namwambia asantee sana sina cha kumlipaa.Mtu mwingine anaitwaFredrick Masanya nakushukuru sana love kwa kujitolea kumuhudumia mwanangu na kumsomesha na kumpatia malezi yote sina cha kukulipa zaidi ya kukushukuru kwa wema wako asantee sana munu akuongezee kila jema kwako.NAKUPENDA SANA

 22. Anonymous

  October 7, 2013 at 10:55 am

  hivi huyu mtoto akikuwa halafu aje aambiewe mama yako alikukataa, je yy angekataliwa angefika hapo alipo dunia imeisha jamani tumtumikieni mungu siku za mwisho zimekaribia

 23. Anonymous

  October 12, 2013 at 11:00 am

  Da jamani naombeni mnipe mimi huyo mtoto jamani awe wangu da watu wanatafuta watoto usiku na mchana du

 24. Anonymous

  October 17, 2013 at 9:18 am

  Jamani we binti kwanini unaiaibisha familia yenu? ni kweli huna baba wala mama lakini najua upendo wa wazazi wako! walikuwa watu wenye msaada sana kwa watu hasa baba yako. Hiyo ya kutupa mtoto umeitoa wapi? kama si wazimu wako. Nina uhakika waliokusaidai ukasoma huko Malaysia baada ya baba kufariki wangekusaidia kulea mtoto, na kazi unafanya kwa nini utupe mtoto?

Leave a Reply