Uncategorized

NI TENDO GANI LA UPENDO,WEMA AMBALO UMEWAHI KUTENDEWA NA MTU NA HUTAMSAHAU.

By  | 
Nimewaza tu kwamba kwenye haya maisha kuna watu wametugusa kwa namna ya kipekee kabisa.Iwe ni ndugu,jamaa,rafiki au hukuwa unamjua alitokea na kutenda jambo la upendo na wema kwako na hautamsahau kamwe.
Ilikuwaje?na alifanya nini?anaitwa nani?

22 Comments

 1. Anonymous

  September 30, 2013 at 2:48 pm

  Mie siwezi kusahau wakati nikiwa shuleni sekondari,shule ya bweni nilipata changamoto ya kuugua mara kwa mara. Kwa kuwa familia yangu ilikuwa na uwezo wa kawaida tu na hivyo hata pesa ya matumizi haikuwa ya kutosheleza. Nilikuwa na rafiki yangu mpenzi anaitwa Jane, alitoka kwenye familia iliyojiweza zaidi yangu, japo sio sana. Jane alikuwa ananohudumia kama ndugu yake, kunifulia, kuhakikisha nina maji ya kuoga na ya kunywa, lkn pia alikuwa ananinunulia maziwa nyumbani kwa mwalimu mmoja. Aliweka bill akawa anaenda kuyachukua kila siku kwa gharama zake mwenyewe!kwa muda karibu mwaka mzima mpaka nilipopona. Wakati mwingine alikuwa anaenda kantini ya shule kuninunulia chakula kizuri angalau mara moja moja. Kwangu mimi siwezi kusahau kwani alimifanya nione inawezekana kusoma hata ktk hali ile na kwa kweli nilikuja kifaulu.Ni miaka kumi imepita sasa.

  • Anonymous

   October 1, 2013 at 8:02 am

   wow! natumai bado mnawasiliana. she was such a swt girl.

 2. Anonymous

  September 30, 2013 at 4:27 pm

  Mmmmh..ukiacha mama…kuna a friend alinisaidia kwenye mtihani wa chuo Udom wa critical thinking ulikua so tight…siwez sahau alniandikia majibu kwenye kitambaa…na namna ya kuangalia majibu Ilibidi nizuge nafuta jasho usoni nilipata tabu…IlA nlifaulu sikupata SAP….Maana nilikua naogopa mno siwez msahauni emeran….Ney from sinza.

  • Anonymous

   October 1, 2013 at 11:48 am

   hahaaa mdau umenifurahisha sana na umenikumbusha mbaliii!! hata mm nilisaidiwa na rafiki yangu mtihani huo huo nikaepuka suo… lol!

 3. Anonymous

  October 1, 2013 at 7:17 am

  Mimi ukiacha mama yangu, sitamsahau mdogo wangu anaitwa Aneth, Mungu ambariki sana, niliachwa na mume wangu akaenda marekani nikawa sina mawasilano nae kabisa,maana wakatia anaondoka aliacha ofisi yetu ilifungwa, nikawa sina pesa sina cha kufanya nilipita pagumu sana, mdogo wangu alinihurumia pamoja na mshahara wake mdogo akaniambia dada yangu inabidi usome, akanilipia chuo, nauli kila siku kwenda na kurudi na hela ya chakula shuleni wakati mwingine alihelemewa lakini aliniambia usiwe na wasiwasi, sina cha kumlipa nasema Mungu aliye hai akutene na haja zake na ambariki sana, kupitia yeye nimeweza kusoma chuo, kufanikiwa na nikapata kazi ingine ambayo naendelea nayo, yeye alijinyima ili mimi nifanikiwe hakutaka nikate tamaa katika kipindi kigumu nilichopitia.

 4. Anonymous

  October 1, 2013 at 7:22 am

  Zaidi ya mama yangu mi nina mmoja ambaye alinisaidia kipindi nilipoachwa na mwanaume nilimpenda na aliniacha katika kipindi kigumu sn. aliniacha narudi toka nyumbani kujifungua mototo amefariki, narudi nakuta vitu vya chumbani kwangu vimeuzwa na niliemwachia chumba changu. sitosahau maisha yangu yote; kwani nililia sikuile adi nikatamani ardhi ipasuke muda ule ule niingie ili nisisikie maumivu niliokua nayo kwa mda ule, bt asante Mungu hakuniacha niaibike sana kuna mdada nilikua nimemwachia ofisi yangu nilivyorudi pale ofisini ata kuongea skuweza time ya kwenda home imefika ila sikua ata nataka kuondoka, ikabidi tu nimwambie nyumba nilivyoiona siwezi kuishi pale. Akanikubalia niishi kwake adi nipate chumba sehemu nyingine, thanx to God nikafanikiwa mwezi uliofata nikahamia sehemu poa ambapo naishi adi leo. Namshukuru sana Happy kwani alinisadia kwa kipindi ambacho nilikua na machungu mengi ya kujifungua kwa operation na mototo kufa tar. 7/10/2011 baba yangu kufariki mwaka huo huo tar. 16/10. mwanaume mwenyewe kaniacha ata hataki kujua na hali gani. ulikua mwaka mgumu sana kwangu. Thanx to her and thanx to God am gud to day.

 5. Anonymous

  October 1, 2013 at 8:45 am

  NAKUMBUKA BOYFRIEND WANGU MMOJA ALINILIPIA CHUO KWA PESA ZAKE KAMA MILIONI TATU NA LEO NINAKAZI NZURI INGAWA SIKO NAYE , ALIMUOA MDADA ALIYEZAA NAYE BAADAYE BASI NASHUKURU SIKUACHWA MTUPU NIMEACHWA NA ELIMU , NAMSHUKURU SANA SANA SANA DAVID POPOTE PALE ULIPO

 6. Anonymous

  October 1, 2013 at 8:47 am

  Ni mke wa binamu wa mume wangu, anaitwa Lucia alinifulia nguo yangu niliyotumia wakati najifungua mtoto wangu wa kwanza, ki ukweli ni zaidi ya ndugu kwa wamama waliozaa wanafahamu hilo. Ninamheshimu sana na kumthamini sana na sintasahau wema wake huo.

  Wa pili anaitwa Mariam, nilikuwa napitia wakati mgumu sana katika maisha yangu, alinishauri nimtegemee Mungu na alifunga siku kadhaa kwa ajili ya tatizo langu. Abarikiwe sana.

  Mama D, Dar es Salaam.

 7. Anonymous

  October 1, 2013 at 10:27 am

  Dina Duniani kuna watu bwana, Mungu ameumba. Ninamshukuru Mungu kwa kunikutanisha nao. kwanza kabisa nimshukuru dada yangu Beresha Msangi kwanza ndiye Msimamizi wangu na kiongozi wangu amenilea na kunielekeza sana jinsi ya kuenenda katika maisha na hata sasa anachoniambia yy ndicho ninachokielewa kuwa ndio sahihi kufanya. Pili kuna kipindi niliugua sana nilikuwa na matatizo ya mgongo nikafanyiwa operation dada yangu huyo kwa kushirikiana na marafiki zangu wapendwa Eva, Esther, na Farida waliniangalia na kunisaidia katika safari yangu ya kurecover mpaka sasa ninaendelea vyema sana na Mungu ameniponya.

  Lakini pia kuna kubwa kuliko yote mwaka jana 2012 mwezi 10 tarehe 26 nilifiwa na mume wangu mpenzi kwa ajali mbaya ya gari lakini Mungu pia akaniinulia watu wa kunifariji sana katika shida yangu akiwemo mama mkwe wangu SUZAN MCHAO, Mama yangu MARY AMANI, dada zangu wote na Wifi zangu ambao ni kama dada zangu Cellina, Happy na wengine wengi. Lakini pia bila kuwasahau rafiki zangu wapendwa Farida, Eva na wengine wengi

  Bt kuna mmoja anaitwa Hindu Lubuma (Mama Nasra)kwani ndio nilikuwa nimekutana nae kwa kipindi kifupi sana kwenye hili ndio nilielewa kweli huyu ni rafiki wa kweli na mpendwa kwangu kwani alinishika na kusimama na mimi katika kila hatua mpaka hivi leo ninavyoandika comment hii ninamshangaa Mungu kwa ajili yake kwani hata niliporudi kwenye maisha ya kila siku ya kawaida alihakikisha ninakua comfortable na amani ninakula na kushiba ninalala kwa amani na faraja ya hali ya juu alafu c kwa cku moja bali ni kila cku toka nirudi kwangu January, 2013 amekuwa na mimi. Hindu Mungu akubariki sana Hindu unachotaka Mungu akupe. yani hadi natamani kila mtu amuone, nzuri zaidi mtoto wake NASRA (3.5 yrs) amekuwa faraja sana kwangu hata nikilala ucku nikaogopa anakuja kulala na me. we ushawahi kuona mtu mzima anaogopa alafu akimuona mtoto pembeni anapata faraja hofu inaondoka? basi ndivyo ilivyo kwangu, nikiwa na safari ninaogopa kudrive peke yangu basi ninamchukua NASRA anakaa na mimi kwenye gari yani ni company kwangu ya kutosha na ukinikuta bz. cwez kuelezea maneno ambayo wewe Dina utanielewa vizuri mwenzio ninaelezea mtu wa aina gani yaani hakuna maneno ya kumfanya mtu anielewe kilicho moyoni mwangu juu ya huyu dada (Hindu na mtoto wake Nasra). kweli ninawashukuru sana kuwepo kwao katika maisha yangu naamini ctawasahau milele thamani yao itaendelea kuwepo katika moyo wangu.

  Pia kwa wale wote waliokuwa pamoja na mimi katika kipindi hiki kigumu Mungu awabariki ninawapenda na kuthamini mlichonifanyia ni kikubwa sana kwangu cwezi kuwalipa bali Mungu mwenyewe anajua. Tarehe 27 th Oct, 2013 Mtaa wa Mkuranga KKKT Natarajia kumshukuru Mungu kwa kila jambo alilonitendea hadi kufikia hivi nilivyo sasa kwani naamini kama si yeye Mungu nisingefika hapa safari ni ngumu sana.

  Pia nikushukuru wewe kwa kunipa hii nafasi ya kuelezea haya maana wakati mwingine huwa ninatamani nipande pale twin tower au (burji alkhalifa) ghorofa refu kuliko yote then nishout kwa kuelezea na kuwataja wote wliogusa maisha yangu kwa namna ya pekeee kabisa. Mungu awabariki na kuwatunza.

  Ninaitwa Mama Washington Robert (Kaunga Amani)

  • Anonymous

   October 2, 2013 at 10:34 am

   Dada nmekufahamu…ww ni mtumishi wa halmashaur ya mkuranga…nshawah kuja ofcn ukanisaidia mawazo ya jinc ya kurud kazini…pole kwa matatizo..Mungu azidi kukupigania.

 8. Anonymous

  October 1, 2013 at 3:25 pm

  dina mimi bwana yani sijui nielezeje jamani haya maisha kweli ukimtegemea mungu kila jambo atakuvusha tu, dina mimi sintamsahau mama NORA MARIA SHUMA , jamani mungu amzidishie amjalie maisha marefu sana yani sijui alafu sina cha kumlipa zaidi mungu tu jamani huyu mama alinisaidia nilikuwa nimeshakwama chuoni kabisa mwaka wa mwsho sina kodi, nyumbani nakoishi maana nimepangsha arusha sina kodi sina chakula ndani fikiria nilikuwa na mtoto mdogo na house girls dina mwanaume amenitelekeza jamani jamani jamani yani nikikumbuka machozi yanaitoka jamani huwezi amini dina huyu nilikuwa simjui sijamzoea wala nini zaidi ya salamu basi lakini siku hiyo aliinita akaongea na mimi sana na mimi sikumficha japokuwa mimi ni mgumu sana kuelezea mambo yangu personal dina hata iweje sisemi nakufa na tai shingoni , basi yule mama jioni baada ya kutoka chuoni aliniita tukaenda nae mpaka kwake akaenda kunipa mchele,maharage,unga,mafuta,sukari,sabuni,maziwa ya mtt, pampares yani vyote hivyo ni stok kama ya miezi miwili dina, na hela ya kodi akanipa ya six month dina na nauli yakuendea chuoni maana firikia nilikuwa naamka saa kumi na moja sakini natemebea mpaka njiro na nyumban nilisahau mpaka chai nilikuwa napika ugal kama upo nakula asubuhi ni mpaka jion dina yani ww acha tu lakini jisi mungu aishivyo milele sikuwahi kupata suplmentary wala chohote hadi nikamaliza yule mama akinilea kwa hali na mali mwshoni hata hela ya joho alinipa yeye jaman jaman mm siwezi eleza mengi namwomba MUNGU tu amlinde mama NORA MARIA SHUMA.
  mimi naitwa mama aaron (patricia kambonyo)

 9. Anonymous

  October 1, 2013 at 6:42 pm

  Mwaka 2009 nikiwa mwanafunz wa diploma ya ualimu,nlipangiwa field mkoan rukwa wilaya ya nkasi.na sehem nliyokua nimepangiwa no mbali zaid name inabid usubir meli inayotoka Congo MV liemba ambayo upita Mara moja tu kwa wiki.wenzangu wote nilosafiri nao toka DSM walikua wameshaenda kwenye vituo vyao vya field maeneo ya karibu Mimi kwangu ilikua mbali kwenda.nakumbuka siku hiyo nikiwa mnyonge narudi guest niliyokua nmefikia na nilikaa apo kwa mda wa siku nne gari moja ilisimama pembeni yangu mama mmoja aliekua anaendesha gari iyo akaniuliza mbona no mnyonge sana.akaniambia niingie ndani ya gari. akanpeleka kwake na alinitunza Sana kama mtoto wake kwa ukarimu was hali ya juu.alinisaidia nikapangiwa shule ya apo apo wilayan name aliniambia nikae kwake mpaka nitakapoweza kujitegemea.
  Nikaja kujua kuwa kwa wakati ule alikua ni mkurugenzi wa wilaya ya nkasi.
  Alichoniambia no kwamba sikujui Mungu ndiye anaekujua nimeguswa tu nikusaidie.baadae aliamishiwa wilaya ya korogwe tanga.Mungu ambariki na amlinde na ampe kila jambo zuri analoliomba kwake. Sitakuja kusahau maisha yangu yotee

 10. Anonymous

  October 1, 2013 at 6:42 pm

  Sitasahau siku ambayo mke wangu amejifungua mtoto wetu wa kwanza kwa operation kesho yake naingia kazini nakuta nimepewa barua ya kuachishwa kazi!!! Kuuliza sababu Manager ananiambia ndivyo Director alivyoamua! hadi leo sipati jibu ilikuwa ni kwa nini, ni mwaka 2005 huo nakumbuka.
  Nikiwa kama niliechanganyikiwa hadi kuogopa kumjulisha mke wangu tukio hilo nikawa najitahidi kutafuta kazi kimya kimya na katika kipindi hicho rafiki yangu (alikuwa mteja wetu mzuri sana pale kazini) Fred Mdemu alinisaidia sana na kunitia nguvu sana katika maisha kweli sitamsahau na kila siku huwa namuombea kwa Mungu azidi kufanikiwa, alijitolea pesa yake utadhani mie ni nduguye wakati tulikutana tu tu kipindi cha miaka michache nikiwa nafanyakazi kwenye ile kampuni tata

 11. Anonymous

  October 2, 2013 at 6:54 am

  Sitasahau msaada niliopewa na rafiki yangu na mdogo wangu pia nilikuwa nasoma naye Chuo cha Utumishi wa Umma. Ilikuwa kipindi cha mitihani ya mwisho ya kumaliza Diploma. Mtihani wa mwisho ulikuwa mgumu sana lakini rafiki yangu huyo alisacrifice akanipa majibu yote maana kiukweli nilikuwa sina cha kujaza karibia maswali kumi na tano yalikuwa blanc, m ajibu yalipotoka nikafaulu. Kwa kweli nakukumbuka sana na pia nakushukuru mdogo wanagu na rafiki yangu Janeth Ussiri popote ulipo.

  • Anonymous

   October 2, 2013 at 11:04 am

   akinaJaneth AU nisem herufi J ni watu wazuri sana. Mimi pia nilikuwa na rafiki yangu anayeitwa JANETH. tulisoma wote shule flani maalum (special school). tupomaliza tukarudi DSM, yeye akiwa kwao mimi nilikuwa naishi na dadangu. baadaye wakati tunasubiri matokeo ya form six nilipata matatizo makubwa, na wakati huo dadangu alikuwa amesafiri Ulaya, shem lenyewe macho juu tumegombana na mawasiliano yote kwa dadangu yalikuwa kupitia yeye. nyumbani hapakaliki, na nikaugua gafla. Kwa kweli Janeth alinisaidia sana ikiwa ni pamoja na kunificha kwao (baba yake mkali alikuwa hataki wageni wasio rasmi), nikakaa kwao, ugonjwa uliponizidia nililazwa, huduma zote
   ikawa juu yake na matibabu juu, hili ni kubwa mana alikuwa ni tegemezi pia naishi kwa baba, hivyo alijinyima ili aweze kunisaidi mimi! jamani kiukweli namshukuru sana kwani nilipona maradhi yaliyokuwa yananisumbua na kufanikiwa kujiunga na chuo kikuu cha Dar. Kwa hapa nilipofikia, nadiriki kusema Janeth huyu amechangia kwa kiasi kikubwa kwa mimi kuweza kutimiza ndoto yangu kubwa ya elimu na ajira hii ambayo si haba..nalipa bills, simtegemei mtu, maisha yanasonga mbele. Mungu akubariki JANETH huko uliko. ni mwanamke mwema na nakuombea siku zote.

 12. Anonymous

  October 7, 2013 at 9:26 am

  sitasahau Mr Dominick Boniphace wakati tunasoma Sengerema yeye alikuwa F6 mie F2 msaada alionipa popote ulipo mungu akubariki

 13. Anonymous

  October 7, 2013 at 11:09 am

  sitakaa nikasahau katika maisha yangu yote baada ya kumaliza chuo nikaa sina hata kazi na hali yangu kifedha ikawa mbaya nikawa sina msaada wowote kutoka kwa ndugu jamaa au rafiki, kwani nilitamani hata kufanya kazi za ndani nilipwe hata mshahara wa elfu 20 ilimradi nipate mahitaji lkn kwa kudra za mungu sitamsahau dada wa rafiki yangu baada ya rafiki yangu kumweleza dada yake matatizo yangu akanisaidia kunitafutia kazi, mkoa aliokuwa anashi, kiukweli swala hili siwezi lisahau wala kusahau fadhila za dada huyu ambaye alikuwa hanijui wala hajawahi niona lkn alipoelezwa matatizo yangu na mdogo wake akanisaidia bila ya kinyongo ambapo leo naweza kuihudumia familia yangu, na kuonekana mbele za watu na nikaombwa msaada nikasaidia kwa kazi ambayo alinisaidia huyu dada,namshukuru na ni watu wachache sana katika dunia ya leo wenye moyo kama wake namuombea kwa mungu ampe maisha marefu yenye baraka tele si mwininge ni dada anaitwa Mwali kalolo anafanya kazi CRDB Mjini Morogoro.

 14. Anonymous

  October 8, 2013 at 1:33 am

  Cwezi kumsahau tunu ibrahim rehema kemmy na benadeta matalu msaada walionisaidia ctawasahau milele.mungu awape maisha marefu.

 15. Anonymous

  October 9, 2013 at 1:29 pm

  Ciwezi kumsahau bwana Katyega na kunitia nguvu baada ya kuachwa na mwanaume niliyeishi nae kwa miaka kumi na tano. Aliniacha vibaya sana, na kunisingizia mimi mchawi. Lakini Bwana Katyega anilifariji na kunitia moyo na kunisaidia hapa na pale. Sitamsahau huyu Bwana. Mungu atamzidishia kila alipopunguza.

 16. Anonymous

  October 14, 2013 at 9:10 pm

  Sitamsahau padre Gabriel Mshanga alinisaidia baada baba yangu kukataa kunipeleka shule kuanza masomo ya Secondary ilikuwa mwaka 1996, sikuwa nasali wala nyumbani kwetu hakuna aliekuwa anaenda kanisani. Ilitokea tu nikawa nimeenda kanisani na baada ya misa kuna roho nikaisikia inasema si umwambie padre kuhusu tatizo lako? Basi nikamweleza a-z lakini siku ile hakunijibu, jumapili iliyofuata nikaenda tena kanisani akaniuliza vipi kuhusu shule nilimwambia kama unaweza kunisaidia nisaidie coz baba hatanipeleka shule. Basi alinichukua akanipeleka shule na mpaka leo ninapoongea nina kazi yangu nzuri tu sitamsahau huyu baba jamani yeye ni mwanga katika maisha yangu.

 17. Anonymous

  October 19, 2013 at 5:47 pm

  Sitamsahau Sheikha Hilali
  Eee Mungu mbariki na mjaalie furaha ya moyo wake. Mpe mtoto atimize furaha yake. Ameen

  Huyu dada siwez kueleza zaiid lkn amenistir na bado anaendelea kunistr Mungu ambariki sana.

  Wanaume hii dunia wapo walokosa mioyo kabisa. Asante sana da Sheikha

 18. Kinego

  December 7, 2013 at 5:39 pm

  Mimi nakumbuka kuna mdada mmoja alinip nauli ya kupanda bodaboda ili ni2ahi ndege iaiache pal airport ya arusha..huyu mdada tulikutana kwenye daladala na foleni ilikuwa ya hatare..muda wa ndege kutake off nao ulikuwa umekaribia mfukoni cna kitu nikitarajia kwenda bank kuchukua pesa kidogo lakin ilikuwa too late..yani yule dada simjui hanijui akatoa akanisaidia..yani mm bado namkumbuka sana natamani kueudiaha fadhila lakin sijui pa kumpata..

Leave a Reply