Uncategorized

RATIBA YA KIFUNGUA KINYWA

By  | 
 Kuna wakati kwenye leo tena nilileta mjadala wa chakula.Mjadala wenyewe ni kuhusu kuweka ratiba ya chakula majumbani mwetu ili kuepuka kula aina moja ya chakula kila siku.Kwa kuanza tulianza na kifungua kinywa.Kina mama/dada waliandika ratiba za kifungua kinywa kwa wiki nzima na nikawa nasoma kila siku kwenye leo tena ili kupeana mawazo.Wapo mlioomba niweke kwenye blog lakini sikupata muda.Wiki hii nitaanza kushare zile chache ambazo bado ninazo.Baada ya hapo nitawaletea ratiba ya mlo wa mchana na usiku.Tulianza na kifungua kinywa kwa sababu tulisema ndio unatakiwa kuwa mlo mkubwa wa siku.
 
RATIBA YA KIFUNGUA KINYWA
Jumatatu
 Chai n chapati za kusukuma,maharage ya kuunga bila nazi,na mayai ya mboga mboga.
Matunda ya msimu yaliyopo au juisi freshy ya matunda.
 
Jumanne.
Chai na ndizi za kukaanga(mzuzu au bukoba) zilizoiva kidogo na tambi.
Matunda yaliyopo ya msimu au juisi freshy ya matunda.
 
Jumatano
Chai inaweza kwenda sambamba na supu ya mboga mboga,maandazi na chapati za maji.
Matunda ya msimu yaliyopo au juisi freshy.
 
Alhamisi
Uji wa ulezi wenye maziwa,viazi vitamu na mayai ya kuchemsha.
Matunda au juisi freshy
 
Ijumaa
Chai na kababu za mboga mboga,ndizi mshale za kuchemsha na kitunguu tu,na maharage.
Matunda au juisi visisahaulike.
 
Jumamosi

Supu ya samaki(sato)yenye viazi ulaya kidogo,ndizi kidogo na mboga mboga.Pia kunaweza kuwepo na chai na vitumbua kwa yule ambae hapendi supu ya samaki au ni lazima anywe chai.

Matunda au juisi
 
Jumapili
Supu ya kuku wa kienyeji
Matunda na juisi

 
*Ratiba hizi zilitoka kwa wasikilizaji wangu ili kupeana mawazo mapya.
*Unaweza kuhusisha vitafunwa kama magimbi,maboga,viazi vitamu,mihogo,mahindi ya kuchemsha n.k
*Matunda ya msimu yapo kila wakati inaweza kuwa maembe,peasi,chungwa,tikiti,papai n.k
*Chai inaweza kuwa ya rangi au maziwa.Bila kusahau viungo kuinogesha.Viungo kama tangawizi,mdalasini,mchai chai,iliki au tea masala ile ambayo imeshatengenezwa mchanganyiko wa viungo vingi.
 
 

18 Comments

 1. Anonymous

  September 30, 2013 at 9:44 pm

  Asante sana Dina kwa ratiba hii, inaonekana ni nzuri na kuhamasisha kuifuata, ila hofu yangu ni kwenye swala Zima la kuongeza uzito (kunenepa) tafadhali kama utaweza tujuze na hili je hii ratiba ni weight friendly? mana changamoto mojawapo inayotukabili wanawake ni swala la kuongeza uzito na nyamanyama za kizembe! Kingine ninachohofia kama una familia kubwa si rahisi kuwa na hii ratiba.

 2. Anonymous

  October 1, 2013 at 7:17 am

  Maisha sa hv yako very expensive dinner km. Unafamilia kubwa hutoweza kuifata,matunda yakutosha familia ya watu watano ni elfu kumi,tikit 4,hayo madogo dogo inafika total elfu kumi,hvy vikorombwezo bado nishat ya kupikia utajikuta asubuh unatumia elfu 30,bado mchana,usiku je?kwangu mwendo wa mkate mayai,au soseji jpili asubuh ndo napika vitu tofauti,mkiwa wachache ndo mtaweza,mi nina watu saba ndani mayai 14,mikate 2,na ninakipato cha kueleweka bt still inakuwa ngumu

  • Anonymous

   October 1, 2013 at 11:30 am

   Hata hivyo hongera sana maana hata hayo mayai 14 kwa siku tu ni mbinde.

 3. Anonymous

  October 1, 2013 at 7:57 am

  JAmani mbona siachi kuangalia picha ya kwanza hehehe! nataka hiyo juice, mkate ndodo hilo basi we acha tuu!

 4. jackie malilo

  October 1, 2013 at 12:35 pm

  Ni nzuri lkn ni watz wangapi wanaweza kuaford hii dina now maisha magumu mtu unapewa 10 ya kula ndio bajeti ya siku nzima na mko kama 6 hivi ndani itawezekana kweli mhh wengine watabaki kuviona kwenye blog mtazamo tu

 5. Anonymous

  October 1, 2013 at 3:09 pm

  ni nzuri ila kwa wafanya diet msijaribu huwezi kula ndizi,viazi, chapati au kababu na chai asubui kiafya ni big NO

 6. Anonymous

  October 1, 2013 at 4:24 pm

  Dina kile kitabu ulichosemaga cha mapishi vipi bado

 7. Anonymous

  October 1, 2013 at 5:10 pm

  Asante Dina huwa napata shida kupanga ratiba za chakula. Nasubiri kwa hamu hizo za vyakula vya mchana na jioni.

 8. Anonymous

  October 1, 2013 at 10:45 pm

  Hiyo ni Breakfast ya mtu asiyetaka kupungua, Breakfast nzuri ni Chai, mayai mawili ya kuchemsha au kukaanga, spinach nyanya na kipande kimoja cha mkate. Ukipenda kula tunda ni kipande tu na juice sio lazima. Hayo maandazi, chapati, na kadhalika vinaongeza uzito sio vitu vya kula mara kwa mara ukifuata ratiba hiyo mwezi tu utaona jinsi utakavyo futuka. Uji wa ulezi ndio kabisaa labda mara moja au mbili kwa mwezi

 9. Anonymous

  October 2, 2013 at 5:29 am

  Dina hiyo nzuri ila sasa mbona naona kama tutanenepa sana na sie wenye matumbo ndio itakuwa shida. Sasa tufanyeje? Tehetehetehe.

 10. Anonymous

  October 2, 2013 at 7:37 am

  Da Dina hii menu ya Alhamisi imeniacha hoi kidogo,yani Uji wa ulezi wenye maziwa,viazi vitamu na mayai ya kuchemsha,hapo si utatengeneza bomu la nyuklia kama by product?

 11. Anonymous

  October 2, 2013 at 10:30 am

  Hiyo ratiba ni nzuri kama una kipato kizur,kazini muda wa kuingia unaeleweka kuna kazi nyingine tunafanya muda wa kula ni wa kutafuta. Ukifika tu unampokea mwenzako hapo umetoka home alfajir.

 12. dinamariesblog

  October 2, 2013 at 10:41 am

  Idea hizi za mlo wa asubuhi zilitumwa kwangu na wasikilizaji wangu wa vipato mbali mbali.Hii nimenza zipo za aina nyingi tu.Muda unavyoenda ntazishare kama nilivyoahidi.Ukiona itakayokufaa utaitumia.Pia wale wa diet ntawatafutia za diet niwaekee.

 13. Anonymous

  October 2, 2013 at 4:36 pm

  Iyo cku ya alhamis daijeshen yake humo 2mbon cpat pcha.lilian wa kgambn

 14. Anonymous

  October 2, 2013 at 4:39 pm

  Hahaaha alhamis ongezea na mtindi badala ya juice.lilian masika wa kgmbn

 15. Anonymous

  October 4, 2013 at 4:22 pm

  ndio maana kupungua kazi

 16. Anonymous

  October 5, 2013 at 10:56 am

  Mimi nimeipenda mana mume wangu anapenda sana kula vizur. Thank u Dina for this.

 17. Anonymous

  October 8, 2013 at 4:13 pm

  aka mie ntakua nakandamiza ivo ivo wengine tunataka tunenepe atiiii

Leave a Reply