Uncategorized

ANAITWA MWAZANI,ALINUSURIKA KATIKA AJALI ILIYOUA WANAMUZIKI WA BAND YA TAARABU YA 5 STARS MWAKA 2011.

By  | 
Tumemsikia Mwazani Said leo katika leo tena akituelezea namna alivyonusurika katika ajali ya gari iliyopelekea wasanii 13 ya band ya taarab ya 5stars kupoteza maisha.Ajali hiyo ilitokea tarehe 22 mwezi wa 3 mwaka 2011.Mwazani alisafiri na band kama mcheza show lakini yeye ilikuwa ni mara ya kwanza.Rafiki yake ambae alikufa kwenye band ndio alimwambia kuna kazi ya kucheza mikoani ambayo atatoka na pesa kidogo kuliko kukaa bure.
Wakasafiri na kuzuru mikoa mitano na yeye akafanya kazi yake ambayo alilipwa Tsh 100,000.Siku mbili kabla ya kurejea Dar wasanii waliopoteza maisha walikuwa wakiona vitu vya mauza uza.Msanii Issa Kijoti na mwimbaji mwingine wa kike walitokewa na mtu aliyevaa nguo nyeupe.Wakawaambia wenzao juu ya hilo wakawafanyia kisomo na dua ili waweze kukaa sawa.
Pia kulizuka ugomvi mkubwa ambao wasanii walikuwa wakigombana wao kwa wao mpaka Sheba Juma ambae ni marehemu alitaka kuondoka mwenyewe kurudi Dar.Lakini Ali J ambae yu hai alinusurika alisuluhisha ugomvi huo wakawa sawa.
Katika ajali hiyo wakiwa kwenye basi mwazani alikuwa amelala.Alikaa siti moja na marehemu Sheba Juma akamuomba wabadilishane siti ili yeye Mwazani alale maana alikuwa na usingizi.Alipolala alikuja kuzinduka baada ya siku 5 na kujikuta yupo hospital mkono umepooza na mguu umefanyiwa upasuaji na kuwekewa vyuma.Akamuuliza mama yake kumetokea nini mbona yupo hospital mama hakumjibu.Baba ndio akamletea gazeti akasoma na kuona kilichotokea na yule shosti wake aliyemuita wakacheze alipoteza maisha.

Baada ya ajali ile mpaka sasa mkono wake wa kushoto umepooza na mguu wa kushoto pia unavyuma bado.Walilipwa pesa ambazo yeye alizinunulia eneo kanyumba kadogo kakuishi.
 Wakati ananunua hapa sio yeye alikuja kununua.Kuna ndugu yake alikuja kupanunua lakini hakukuwa na choo.Ni mwaka sasa amekuwa akitumia choo cha jirani na kwa sasa amepigwa marufuku kutumia choo cha wenyewe.Baada ya kupigwa marufuku akarudi kwa baba yake ambae amepanga chumba na sebule.Baba na mama wanalala chumbani yeye analala sebuleni.
Sebule katika nyumba yake hiyo ambayo ipo Yombo dovya.
Huyu ndio jirani mwenye choo chake lakini amepigwa marufuku
Hapa ni chumbani kwake.

Kama ambavyo amesikika kwenye leo tena Mwazani anaomba kusaidiwa pesa ili aweze kujenga choo.Iwapo uliguswa na matatizo yake mchangie kwa namba 0759 789863 na 0657 795654.

32 Comments

 1. Anonymous

  October 2, 2013 at 7:29 am

  Amshukuru Mungu kwa kumnusuru ktk hyo ajar

  • Anonymous

   October 8, 2013 at 12:36 am

   Ajali sio ajar mdau

 2. Anonymous

  October 2, 2013 at 7:31 am

  Dina nshakaaa mkao wa kusikiza mapeema mpe sana pole kwa ajali. Jambo lingine hua naumia sana ninapoona mtu ni maskini hata kam sio maskini sana ila mazingira ya mtu anapoishi hua yananipa mawazo sana. Duuu tumetofautiana sana mungu awape nguvu wale wote wanaopambana na maisha yani huo ukuta nimeuwaziaaaa ukidondoka itakuaje? Ila ndo hvyo tena mungu ambariki

 3. Anonymous

  October 2, 2013 at 7:50 am

  Dinna!,
  Huyu Dada alikwa mwanamuziki? ama anaendelea na muziki? ama alikuwa mcheza show ama kuna nini kinaendelea? japo sijasikiliza kipindi , but nimeguswa na kitu. Kama huta jali tafadhali nisaidie maelezo kidogo na sasa anafanya nini?. Nitakushukuru.

  • Anonymous

   October 2, 2013 at 12:08 pm

   Alikuwa mcheza show

  • Anonymous

   October 4, 2013 at 11:58 am

   dia naona hujasoma maelezo ya Dina hapo juu anajieleza vizuri sana wala sidhan kama unahitaji maelezo mengine, soma kwa taratibu utaelewa, maelezo yamejitosheleza.

  • MIMI

   October 4, 2013 at 8:59 pm

   Watu wengine wavivu kusoma wazito kuelewa !post inajieleza victim alikuwa dancer uelew nini tena!!!!?me mwenyewe sikupata nafasi ya kumsikilizia radion mbona nimeelewa someni post yote acheni uvivu

 4. ahmed chaurembo

  October 2, 2013 at 8:45 am

  Inasikitisha sana Da dina Ile Ajali Iliyotokea, Imepoteza Mashujaa Wengi Katika Industry hii ya Taarabu. Mungu Awalaze Mahali Pema Peponi AMEN.

 5. Anonymous

  October 2, 2013 at 8:57 am

  Daaah, Maskini…pole sana kwake…

 6. Anonymous

  October 2, 2013 at 9:03 am

  Dah! inasikitisha sana. mungu amzidishie aweze kumlea huyo mtoto

 7. Anonymous

  October 2, 2013 at 9:15 am

  pole sana dada mwazan kwa matatzo

 8. Anonymous

  October 2, 2013 at 9:21 am

  duh hadi mwili umenisisimka mwili hadi huruma,mungu amsaidie

 9. SIMON BONIFACE

  October 2, 2013 at 9:40 am

  Simon wa Tabora, natoa pole zangu kwa huyo dada mwazan Mungu atamjalia tu kwani Mungu atakua na makusudi nae kufikia kumuweka hai mpaka sasa..!?

 10. Anonymous

  October 2, 2013 at 10:26 am

  Pole Mwazani, Mungu alikunusru kwa makusudi ili umtumikie, hivyo tumia nafasi hii kumtukuza na kulitngaza jina lake!

  • BIG DAVIS

   October 2, 2013 at 6:31 pm

   Hongera wana leo tena Anastahili kusaidiwa

  • BIG DAVIS

   October 2, 2013 at 6:32 pm

   HONGERA LEO TENA KWA KUTUJUZA MPENI POLE HUYO DADA

 11. Anonymous

  October 2, 2013 at 1:02 pm

  nimemsikiliza dada mwazani leo kwenye leo tena,very sad story,lkn dina irene uwoya si ana kipindi cha kukarabati nyumba? Muunganishe bac na huyo dada maana anakidhi vigezo asilimia mia.

  • Anonymous

   October 4, 2013 at 12:01 pm

   exactly, hawa ndo watu wa kusaidiwa na THE PARADISE ya Irene Uwoya, maana mna uhakika kabisa kuwa wanahitaji msaada tena wa haraka, please Dinna msaidie kuongea na Irene ili akipata hizo pesa kwa mpesa au tigo pesa zimsaidie kwa matumizi yake mengine coz am sure ana mahitaji mengi sana basic.

 12. Anonymous

  October 2, 2013 at 6:11 pm

  JAmaniii polee sanaa mwazanii nimesikiliza roho imeniuma sanaa pole mungu atakujaalia! Inshaallah!.PILI AOGWA

 13. Anonymous

  October 2, 2013 at 9:23 pm

  Dina mdogo wangu mi nina wazo kama tunataka kumsaidia huyo mwazani na mtoto wake,ufanye tadhimini ya kukarabati nyumba yake pamoja na choo halafu tumchangie kidogo tulicho nacho ili angalau apate sehemu nzuri ya kukaa yeye na mtoto wake,ni wazo tu Dina linaweza kupokelewa au kuachwa!

 14. Anonymous

  October 3, 2013 at 9:33 am

  Huruma na inauma sana jamani

 15. Anonymous

  October 3, 2013 at 10:18 am

  Pole sana dada!Dina huyo dada afanye tathimini ya ukarabati wa nyumba yake na choo na bafu ili tumchangie afanye marekebisho apate malazi mazuri na mtoto wake!mungu atamfanyia wepesi atapata maisha mazuri tu Mungu anamakusudi yakumuacha hai hadi alipo sasa.

 16. Thea

  October 3, 2013 at 11:20 am

  Dina Naungana na mdau hapo juu, kutokana na hali ya nyumba ya Mwazani, anahitaji si choo tu, bali pia ukarabati wa kicho kibanda chake kisije kuwaangukia usiku. Kwa hiyo Dina kwa sasa misaada ilenge hizo kaz mbili, CHOO na UKARABATI. Nipo tayari kuchangia. Thea.

 17. Moi Haisule

  October 4, 2013 at 5:52 am

  Watu
  hatuna huruma jamani,kama huyu mwanaume aliye mpa uja uzito na
  kumkimbia,dhambi yake ni kubwa sana!pole sana dada kwa yote mungu
  atakusaidia ucjali wala nini!

 18. Anonymous

  October 4, 2013 at 7:53 am

  Pole sana ndugu yetu, ni kweli alivyosema mdau hapo juu kuwa ana vigezo vyote vya kusaidiwa na dada Irene Uwoya katika suala la nyumba.ili michango mingine imsaidie kwa kufanya mambo mengine ili aweze kujikimu katika maisha yake na mwanae mpendwa. Ni wazo tu wapendwa

 19. Anonymous

  October 4, 2013 at 9:14 am

  Dash kiukweli inauma sana pole sana my love mwazani by JESCA HAULE CUTE BAB

 20. Anonymous

  October 4, 2013 at 12:03 pm

  pole sana mamie , Mungu anakupenda sana ndo maana kakupa uhai mpaka leo hii maana ni wengi walipoteza maisha ktk ile ajali, pia hongera kwa kukumbuka hata kununua sehemu ya kuishi. Mungu atakuponya na kukufanya mzima kama mwanzo na ukaendelea na maisha yako kama kawaida,

 21. Anonymous

  October 4, 2013 at 2:57 pm

  Michango ungepokea wewe Dina, akipokea yeye haitatumika kama ilivyokusudiwa

 22. Anonymous

  October 4, 2013 at 9:12 pm

  Mungu amsaidie jaman, Dina thx much kwa kaz nzur. Pendo Kyando

 23. ELIUD SAMWEL

  October 6, 2013 at 12:44 am

  Naamini tukiungana wanaleotena wote tutamsaidia dada etu

 24. ELIUD SAMWEL

  October 6, 2013 at 12:44 am

  Naamini tukiungana wanaleotena wote tutamsaidia dada etu

 25. Dominic Anthony

  October 7, 2013 at 5:13 pm

  pole mwayego

Leave a Reply