Uncategorized

MLO WA ASUBUHI KWA ANAYEPUNGUZA UZITO

By  | 
Wiki moja iliyopita nilisema ntakuwa nashare namna mbalimbali ya kuandaa ratiba ya mlo wa asubuhi,mchana na usiku.Tulianza na mlo wa asubuhi na nikapata maoni ya wale wanaotaka kupunguza uzito je wanaweza kuwa na ratiba ipi?Ifuatayo ni ratiba ya mlo wa asubuhi kwa mtu anaetaka kupunguza mwili/uzito.
JUMATATU
Mkate wa brauni
slesi 1 +siagi ya karanga
Yai 1 la kuchemsha
Kinywaji cha soya
Chungwa 1
JUMANNE 

Mhogo/kiazi/gimbi
kipande 1
Kachumbari-nyanya na
kitunguu na tango
Maziwa kikombe 1
Papai
 JUMATANO 
 Sandwich (mkate
brauni slesi 2,yai la kukaanga moja,nyanya kitunguu,hoho,tango)

Chai ya maziwa yenye
viungo


Tikiti maji

ALHAMISI
Chapati 1 ya unga wa
atta (roti-iliyochomwa bila mafuta)

Sausage 1
Kinywaji cha Soya
Parachichi

 

IJUMAA

Uji wa dona na maziwa/oats
na maziwa/all bran na maziwa(kula kimojawapo)
Tikitimaji

JUMAMOSI 
Supu ya
kuku/samaki/nyama
Chapati 1 ya unga wa
atta (roti-iliyochomwa bila mafuta)
Saladi ya matunda
JUMAPILI 
Skonzi za atta
+cheese/asali/siagi ya karanga

Salad ya mboga
mboga(nyanya,tango,kitunguu)
Maziwa kikombe 1

Nanasi

NOTE

·        
Maziwa yatakayotumika yawe yaliyoenguliwa mafuta
yaani skimmed milk,unaweza chemsha na kuondoa mafuta yatakayobaki juu au
ukatumia maziwa ya Cowbell.
·        
Matunda na mboga mboga zitumike za kwenye msimu,
mboga na matunda yanayoshauriwa zaidi kwa kupunguza uzito ni spinach, sukuma
wiki, lettuce,tango,nyanya,zabibu,chungwa,limao,parachichi,papai,apple,tikitimaji,cauliflower,broccoli,bilinganya,nyanyachungu,bamia,uyoga,zukini
na maharage mabichi.
·        
Tumia unga wa nafaka zisizokobolewa, dona-inga
wa mahindi mazima, atta-unga wa ngazo isiyokobolewa
·        
Roti jina
la aina ya chapatti ya Kihindi inayochomwa kwenye kikaango bila mafuta.
·        
Usile mayai kila siku, yana lehemu, mayai matatu
kwa wiki yanatosha
Kuna namna mbali mbali za kuandaa mlo wako wa asubuhi iwapo unafanya diet ili kupunguza uzito.Wataalamu wanasema sio vizuri kutokula kabisaa hasa mlo wa asubuhi kisa unataka kukonda.Kula ni muhimu ila unakula nini?Hii aametuandalia mdau Valeria Millinga.Ikipatikana ingine ntaweka pia

7 Comments

 1. Mama 2 (Mrs M)

  October 9, 2013 at 4:24 am

  Asante Dina! Ngoja nami nijaribu.

 2. Anonymous

  October 9, 2013 at 5:07 am

  Thanx Dina. Please naomba utuwekee full ratiba ili tujue lunch tutakula nini na dinner pia especial tulio maofisini coz kumaintain breakfast tuu haitasaidia kama lunch na dinner zitakuwa worse plz naomba tusaidie tena kwa hilo

 3. Anonymous

  October 9, 2013 at 6:56 pm

  Jamani Dina nifanyeje niongeze uzito?nakula wee lakini sigain hata kidogo kama kuna mlo wa kuongeza uzito plz plz dina uzito wangu ni mdogo mno.

 4. Anonymous

  October 18, 2013 at 10:18 am

  We anonymous wa 11:56 unautamani unene!!!!!!! Naomba usiutamani kabisa dada ni shida tupu kuanzia afya mpaka kimavazi

 5. Anonymous

  October 28, 2013 at 5:20 am

  Dina pls, embu tuwekee Milo yote ya mtu anayetaka kupungua, wa asubuhi tu hautoshi

 6. Anonymous

  November 3, 2013 at 8:04 am

  dada dina pole na majukumu..kunakipindi ulitengeneza nyele zako stail kama dreds flan hv ningependa kufahamu ulitengenezea wapii plss

 7. Anonymous

  November 14, 2013 at 9:11 am

  Asante sana dada ila naomba uweke yafull siku nzima maana wengine kama mimi hata nguo zakuvaa ni tabu, Mungu akubariki sana

Leave a Reply