Uncategorized

UKWELI KUHUSU BINTI ALIYETAKA KUTUPA MTOTO.

By  | 
Nilileta story ya huyu msichana wiki iliyopita kuwa baada ya kujifungua alikuwa anataka kumtupa mtoto au kumgawa kwa anayemtaka.Alisema yeye wazazi wamefariki na nyumbani alikuwa akiishi kwa dada aliyemfukuza kisa kupata ujauzito
Ukweli ni kwamba huyu msichana hakuwa na shida ya yoyote iwe ya hali wala mali.Familia yao inajiweza na amesoma Malaysia chuo.Ni kweli wazazi wake wote walifariki lakini waliachwa watoto wamesomeshwa.Dada zake wa wanafanya kazi na wanaishi kwao kwenye nyumba waliyoachiwa na baba na mama.
Yeye mwenyewe tu na akili yake ila akili zilipomkaa sawa aliwaita ndugu zake kumfata.
Dada yake anasema hakufukuzwa aliondoka nyumbani akaaga
anaenda hospital kwani mtoto hachezi tumboni.Akaulizwa apelekwe akakataa
akasema akipata tatizo atawataarifu ila waache aende mwenyewe.
Dada zake walipoelezwa taarifa hii walishangaa sana.Ila walikuja kumfata ndugu yao na kurudi nyumbani na mtoto.

20 Comments

 1. Mimi

  October 1, 2013 at 10:51 am

  Watakuwa walikuwa wanamsimanga wamempa stress kwann ndugu yao km wanamjar walimuacha anaenda hospital peke yake katika hali ile hapo hapo unakuta kuna family member mmoja akiumwa ukoo mzima wanachanganyikiwa mtu mzima atabembelezwa anywe dawa wakati uyu mwingine anaitaj msaada hapati…watu wabaya tuonane 2 njian lakin kuishi na ndugu wenye kipato kikubwa ila utu hawana n mtihan mkubwa nimepitia hiyo hali naelewa soo km akil iliamuwa basi n ndugu zake wamesababisha ad anataka kugawa mtoto wao walikuwa wap!!?kasoma nje Sawaaa kazi anayo!?

  • Anonymous

   October 4, 2013 at 6:10 am

   naungana na wewe mikono na miguu, kama kweli alikuwa na mazingira mazuri asingeweza kufanya hayo. wanajishaua tu kujitoa aibu, hivi kweli mjamzito aliekaribia kujifungua aseme mtoto hachezi tumboni mumuache aende hospitali peke yake??? mtoto akiwa hachezi kuna uwezekano mkubwa akawa amefariki kweli unawezaje kumuacha mdogo wako katika hali kama hiyo. mimi nashindwa kukubali maelezo yao kikamilifu hapa kuna jambo…

  • Anonymous

   October 16, 2013 at 8:14 pm

   Watoa mada hapo juu hamjakutana na mambo ya dunia ndio maana mnasema msemayo; mimba shurti umdekee alokupa ujauzito; embu uliza wenye experience ni wangapi wanapata family attention????

   Wenye waume wenyewe si wote wanasindikizwa hospitali sembuse mimba isojulikana baba???

   Suala ni kujikubali badala ya kulaumu ndugu; waweza jikuta unagombana na kila mtu ukiwa ni mtu wa lawama na kutegemea attention. Mfano kama ndugu zake ni waajiriwa watempeleka clinic kwa ruhusa gani?

  • Anonymous

   October 16, 2013 at 8:18 pm

   Kwa kumuangalia tu sioni kama alikuwa na bad time kwao…bado ana mvuto kabisa…she is so beautiful ukilinganisha a wazazi wengi waliochakaa na wako kwa waume zao….tusikimbilie kuhukumu jamani

 2. jackie malilo

  October 1, 2013 at 12:30 pm

  Kweli kichwa maji huyu mdada ajui kuna watu wanashida yawatt,ila hamkutaja umri wake namuona kama anaakili za kitoto tu.chamsingi amekubali hiyo hali basi inshallah mungu amkuzie

 3. Anonymous

  October 1, 2013 at 2:09 pm

  Sawa dina,ila kuna namna hapo kidogo bana! Katika hali yoyote huwezi kumuacha huyo bint ende mwenyewe hospitali. Hakuna cha kumuuliza,bali mnampeleka jmn! Vzr,tumemali na"happy ending"

 4. Anonymous

  October 2, 2013 at 7:11 am

  mhh!hao ndugu wa mashaka…mbona hawakuangaika kumtafuta alivyokua hajarudi nyumban?

 5. Anonymous

  October 2, 2013 at 7:35 am

  pana namna hapo lazma kwao walikua wanampa stress tu,ila nayeye na kusoma kote huko mbona anakua na maamuz ya kitoto sana

 6. Anonymous

  October 2, 2013 at 10:01 am

  Mmh pole yake jamani

 7. Anonymous

  October 2, 2013 at 11:09 am

  Me natafuta mtoto cpati wengine wanatupa. Moyo unaniuma sana.

  • Anonymous

   October 3, 2013 at 6:35 pm

   Pole mpz!!

 8. Anonymous

  October 2, 2013 at 12:28 pm

  Huwa siungi mkono vitendo vinavyokosa upendo, utu na visivyokubalika na Mungu kama kutupa mtoto n.k, kuna kila dalili kuwa ndugu walimuweka kwenye wakati mgumu, au TATIZO kubwa kuliko yote na ambalo huwakumba wengi MUHUSIKA mkuu (wa kiume)…je anajulikana na amehojiwa ? ,hao kwa asilimia tisini huchangia maamuzi yasiyo na utu kwa watoto wa kike pale wanapoanza kurudi nyuma mara tu wanapogundua ya kuwa" HARAKATI" zao zimezaa matunda (mimba)……na akili za binadamu zilivyo za ajabu….matokeo yanajulikana lakini unafanya unachofanya kwa kutegemea miujiza kwamba matokeo hayo yasitokee…..

 9. Anonymous

  October 2, 2013 at 5:35 pm

  katika nchi zilizoendelea kuna ugonjwa huwa ukiwapata baadhi ya wanawake (wachache) wanapojifungua -kizungu unaitwa postpartum depression – ni kama ugonjwa wa akili lakini hudumu kwa miaka michache na kisha kutoweka. ugonjwa huu hupelekea hao wamama kuwaumiza watoto waliowazaa hata kuwaua (ukiweza kugoogle habari za andrea yates – huyu mama alipatwa na huo ugonjwa na kuwaua watoto wake watano). Yaelekea huyu dada amepatwa na kitu kama hicho. Ndugu wanatakiwa kuwa karibu sana na kumsaidia kumwangalia mtoto kwa kipindi hiki. Mungu ambariki huyu dada aweze kulea mwanae.

  • Anonymous

   October 16, 2013 at 8:16 pm

   Au ni kifafa cha uzaz; wenye vifafa vya uzazi wengine wanakuwa vichaa kabisa. nimeshashuhudia wanawake wenye hilo tatizo. Ila sijuhi kama ni hilo ulilosema wewe

 10. Anonymous

  October 3, 2013 at 1:24 am

  mambo bi mdogo,kuna wanawake wengine huwa wanapata matatizo ya kichaa cha uzazi,(yaani mwanamke anachanganyikiwa baada ya kujifungua)

 11. Anonymous

  October 4, 2013 at 5:06 am

  PUNGUANI ASWA

 12. Anonymous

  October 4, 2013 at 5:08 am

  UCHIZI UO

 13. Anonymous

  October 5, 2013 at 2:28 am

  una lolote machoni unajifanya m2 mwenye maana kumbe mbulula 2 mwanamke gan mwenye status kama yako hapa mjini anaenda kubeba mimba za uzinzi eti role modal haha ha hata haipendez mama koku hufanan shoga miaka 30 unamuiga byonce?mwenzio yule alibeba baada ya kuolewa xaxa nakushangaa wew unamuiga zama ina huu?zama bdo mdgo we bibi unafanya ya watoto ..kazi kweli kweli unapenda kujidogosha wew?poyee we watu walikuona wa maana kumbe mashudu 2pu!ncha kali my foot!

 14. Anonymous

  October 7, 2013 at 6:22 am

  Jamani kuna ugonjwa unaitwa postpartum depression. Unawapata kina mama wengi baada ya kujifungua, na una dalili nyingi mojawapo ni kutomtaka mtoto. Mazonge yakizidi anaweza kujidhuru ye mwenyewe na hata kujiua. Ila utafiti umeonyesha kina mama wengi wenye kupata mazonge baada ya kujifungua ni mara chache sana kudhuru watoto wao, ila kuna ambao huua hata wana wao waliowazaa.

  Ugonjwa huu unawapata wamama wengi Ulaya na Marekani, na una tiba.

  Sijui hapa kwetu, pengine wengi tunaugua hatujijui au hatujulikani.

  Muulize aunt Sadaka anaweza kuzungumzia hili.

 15. Anonymous

  October 22, 2013 at 8:41 am

  Mmh pole zake

Leave a Reply