Uncategorized

UNAKIKUMBUKA KITUO CHA WATOTO YATIMA CHA SIFA GROUP?

By  | 
Wakati nafanya harambee ya kuchangia vituo vitatu vya watoto yatima na chenyewe kilikuwemo kwenye list.Kituo hicho kipo Bunju mwishoo labda nikukumbushe kwa picha.
 Wakati nawatembelea ili kujua changamoto za kila kituo,kituo cha sifa pamoja na mahitaji muhimu ya kila siku ya watoto pia walikuwa wakihitaji eneo la kujenga kituo.Kituo hiki Sifa amekianzisha nyumbani kwao kwa wazazi wake ila hapatoshi kuhifadhi watoto alionao.
Baada ya kukamilisha michango na kuwasilisha vitu kwa vituo
vyote watu mbali mbali waliendelea kupiga simu kuomba kuelekezwa vituo watakavyopeleka misaada yao.
 Kuna siku nikaombwa list ya vituo vya watoto yatima pamoja na changamoto walizonazo kwani kuna mtu anataka kutoa msaada.Mie nikatoa pamoja na maelekezo na namba zao za simu.Mungu alivyo mwema Sifa ikapata mgeni aliyewapa kiwanja kikubwa cha eka 4.
 Dada Sifa pamoja na mama yake wakiwa wameenda kukabidhiwa eneo lao na wametinga tshirt za Dada Dina Cares.
 Eneo ni kubwa kuweza kujenga nyumba ya watoto kulala,shule,na watoto kuwa na eneo zuri la kucheza.
Wabarikiwe wote ambao wamekuwa wakimiminika vituoni kutoa misaada yao.Kituo cha Vetenary Temeke nacho kimepata eneo.Nitawatembelea tena na nitawapa maendeleo yao.Vituo hivi vimekuwa kama sehemu ya maisha yangu maana Sifa lazima tuongee mara kwa mara kwa simu kunipa maendeleo ya watoto kadhalika mama wa Temeke tunaongea sana na wanaendelea
vizuri.
 Wakati namalizia kupeleka misaada kwa watoto yatima nilitengeneza VIBUBU.Ofisini ninavyo viwili ambavyo watu wamekuwa wakidumbukiza pesa kidogo kidogo kwa ajili ya kusaidia watoto yatima.Jumamosi hii nitavifungua pesa nitakayoikuta nitanunua vitu kidogo kwa ajili ya watoto ntaenda Bunju kuwatembelea.
Hii ndio babari njema niliyowaletea kuhusu kituo cha watoto wa Sifa.Kuna changamoto ingine pia maana Sifa ananiambia tayari kiwanja kapata ujenzi itakuwaje?Nimemwambia anipe muda nitafakari nione mimi binafsi nitamsaidiaje wakati na yeye akiangalia namna atakavyopata pesa za kujenga kituo.Kama Mungu alivyoonyesha njia kiwanja kikaletwa na mtumishi wake na ujenzi pia hivyo hivyo ipo njia.Nipo kwenye kutafakari kwa sasa.

19 Comments

 1. Cute

  October 7, 2013 at 11:40 am

  Dina Dina Dina Dina… am speechless. LET GOD BE WITH YOU FOREVER AND FEVER

 2. Anonymous

  October 7, 2013 at 11:40 am

  Amen, sifa na utukufu tunamrudishia Mungu, Mungu awabariki wote waliotoa misaada sawasawa na KUMBUKUMBU LA TORATI 28:1-14, Dina mamii May almighty GOD bless you abountantly hii unafanya kutimiza maagizo ya Mungu soma KUTOKA 22:21-24, BARIKIWA SANA DEAR

 3. pulkeria

  October 7, 2013 at 4:41 pm

  Hongera sana dina,Mungu azidi kukubariki.

 4. Pulkeria Mtavangu

  October 7, 2013 at 4:45 pm

  Hongera sana dina,Mungu azidi kukubariki.

 5. Anonymous

  October 8, 2013 at 5:24 am

  Dada dina cares for sure,mungu akubariki sana na akuongezea rizki lukuki.
  Me loves u alot <3
  mie mwanaid.

 6. Anonymous

  October 8, 2013 at 6:02 am

  well done Dina. May God bless you my dear

 7. Anonymous

  October 8, 2013 at 6:35 am

  MUNGU akubariki sana Dina.

 8. Anonymous

  October 8, 2013 at 5:27 pm

  Mungu akubariki sana dada Dina….may He be your shepherd,usipungukiwe na kitu.

 9. Anonymous

  October 8, 2013 at 9:03 pm

  Tuko pamoja dina, nitakupigia ili nami niwe mmoja wa watakao toa msaada/mchango japo ni mdogo

 10. Anonymous

  October 9, 2013 at 7:10 am

  Neno la Mungu linasema atakae msaidia maskini umkopesha muumba wake so tegemeeni kulipwa zaidi na baba yetu muumba

 11. Anonymous

  October 9, 2013 at 8:54 am

  nimeishia tu kutoka machozi.. na mwili kunisisimka. ubarikiwe sana sana.

 12. dinamariesblog

  October 9, 2013 at 11:08 am

  Asanteni na nyie wadau kwa moyo wenu tupo pamoja naamini.

 13. Cymah Wandelt

  October 10, 2013 at 10:50 pm

  Mungu in mwema sana dadangu, Mungu akubariki sana tena sana, yaani nimekuwa Na ndoto ya kusaidia yatima tangu utotoni ukizingatia Mimi ni mmoja wao. Kila nikiona matunda yako nafatijika sana tena sana, dadangu Mungu akubariki sana tens sana. MACHOZI ya furaha ndiyo yanamiminika ubarikiwe mama.

 14. Anonymous

  October 13, 2013 at 11:33 pm

  mwili umenisisimika,ukiweka jina lako lakutuma pesa namie nitajitaid nitachangia hta kidgo nilicho nacho,mdau U.S.A

 15. กลูต้า

  November 4, 2013 at 4:16 am

  Neno la Mungu linasema atakae msaidia maskini umkopesha muumba wake so tegemeeni kulipwa zaidi na baba yetu muumba

 16. Anonymous

  November 20, 2013 at 11:18 am

  please dada dina mimi nipo arusha ila kama ungeweza kunielekeza hicho cha bunju kilipo ningefurahi sana kwani ni maeneo ya nyumbani kwangu,ili nikija dar nikawatembelee.

Leave a Reply