Uncategorized

BLOG YA MAPISHI KWA WALE MNAOTAKA KUONGEZA UJUZI JIKONI

By  | 
Tollyzkitchen Boresha Mapishi Nyumbani
Tollyzkitchen ni jiko linalofundisha juu ya chakula na mapishi.Jiko hili huendeshwa na Mtanzania katika Lugha ya kiswahili kwa ajili ya watumiaji wote wa lugha ya kiswahili.
Blog hii inaendeshwa na mwanadada Tolly Ben ambae huweka mapishi kwa njia ya video au picha na maandishi yanayokuelekeza namna ya kupika.
Hapa nitakuwekea moja ya pishi aliloliweka bloguni kwake huko.
 
NJEGERE ZA MAZIWA.
Njegere Ni chakula cha kawaida kabisa kwa watanzania wengi.Njegere huweza tumika kama sehem ya kifungua kinywa,kiungo cha supu ,kiungo cha saladi na hata kama sehem ya mlo mkuu .
Kuna Namna nyingi sana ya kupika na kuandaa njegere.Hii ni moja ya namna ya kuandaa njegere kama sehem ya mlo mkuu.
Kwenye pishi hili nimetumia Beef masala kama moja ya kiungo.Ingawa kiungo hiki ni maalum kwa nyama,kinaleta ladha nzuri sana kwenye Njegere.Kumbuka tu,Upishi ni sanaa,ubunifu lazima.Usikariri.

Mahitaji
Njegere ½ kilo
Nyanya 3 kubwa
Swaumu ½ kijiko cha chai
Beef Masala kijiko 1 cha chai
Nyanya ya Kopo vijiko 2 vya chai
Maziwa fresh kikombe 1 ½
Karoti Mbili,kata duara
Mafuta vijiko 4 vya chakula
Chumvi kwa ladha upendayo
Njia
1.Chemsha njegere adi ziive,ziwe laini na Maji yakauke.
2.Katika sufuria unga mafuta na kitunguu adi kitunguu kianze kubadilika rangi(usiache kikawa cha brown) ,Ongeza nyanya,nyanya ya kopo,chumvi,swaumu na beef masala.Kaanga adi nyanya na mafuta zitengene ndani ya sufuria.
3.Ongeza njegere na karoti ,kaanga kwa pamoja adi njegere na nyanya zishikane.Ongeza maziwa,chemsha uku unageuza mara kwa mara ili maziwa yasikatike na yasiungulie chini.Chemsha adi upate uzito unaopenda.Tayari kwa kula.

Tembelea .http://tollyzkitchen.wordpress.com/

Na ni website sio blog kama nilivyosema hapo awali.

3 Comments

 1. Anonymous

  November 8, 2013 at 10:51 am

  Afaadhali dina umemtoa huyu dada nami huwa namfatilia ana mapishi mazuri sana kina mama karibuni tollyz tuboreshe mapishi nyumabani , kwa kwelianajitahidi . Big up tolly .

 2. njoikiki mapunda

  March 7, 2014 at 10:26 am

  Hongera sana kwa kutuongezea ujuzi sisi wakinamama wa Kitanzania, naomba utuelekeze pia kutengeneza juice ya matunda rahisi kama ukwaju, ubuyu, rozera na matunda ya aina hiyo

 3. Anonymous

  July 7, 2014 at 7:49 am

  Asante nitapika duh tamu sana hii

Leave a Reply